Na Mohammed Mhina,
wa Jeshi la Polisi

DAR ES SALAAM IJUMAA APRILI 02, 2010. Jeshi la Polisi nchini kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani kimewaonya vikali madereva wote watakaoendesha magari yao kwa uzembe na kusababishwa ajali kuwa watafutiwa leseni na kufikishwa mahakamani kwa kutumia sheria za SUMATRA.

Hayo yamebainishwa na Kamanda mpya wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamisna Msaidizi Mwandamizi (ACP) Mohammed Mpinga, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam kubainisha mikakati walioiweka katika kupambana na ajali za barabarani hasa katika kipindi hiki cha siku kuu za pasaka.

Kamanda Mpinga amesema kuwa wakati wa siku zote hizi watu wengi watakua na pilikapilika za hapa na pale na wengine kutumia siku hiyo kwenda katika kumbi mbalimbali za burudani kwa ajili ya kunywa pombe na kulewa kupita kiasi.

Amesema kuwa Askari wote wa kikosi hicho hawatapunzika na watakuwa kazini kuhakikisha kuwa hakuna Dereva ama mtumiaji mwingine wa barabara atakayeendesha vunja taratibu na sheria za ulama barabarani na hata kusababisha ajali kwa uzembe ama kutokana na vitendo vya ulevi.

Kamanda Mpinga amewataka Madereva na watumiaji wengine wa barabara wakiwemo waendesha bajaji, pikipiki, baiskeli, maguta, mikokoteni na wale waendao kwa miguu, kujidhari na kujiepusha na vitendo vyovyote vitakavyopelekea ajali.

“Tunawataka pia Madereva wote wa mabasi yaendayo mikoani, na wale wanaofanya safari zao kati ya mkoa mmoja na mwingine, kuacha kabisa kwenda mwendo wa kasi ama kuendesha magari hayo wakiwa wamelewa ili kuepusha ajali”. Alisema Kamanda huyo mpya wa kikosi cha Usalama Barabarani nchini.

Kamanda Mpinga amewataka Makondakta na mawakala wa mabasi hayo, wasiruhusu basi kujaa kupita uwezo wake na kwamba yeyote atakayekaidi na kukiuka maagizo hayo atachukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine watakaoiga.

Aidha Kamanda Mpinga pia amewaomba abiria na wananchi kwa ujumla kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za siri na za haraka pale wanapoona ukiukwaji wa makusudi wa sheria na kanuni za usalama barabarani, kwani nia ya kila abiria ni kufika salama kule anakokwenda na sio kuishia njiani kwa kusababishiwa majeraha ama kufariki kutokana na ajali za barabarani.

Amesema Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani kwa kushirikiana na makachero wa Polisi na wale wenye sale za kawaida, watatawanywa katika maeneo mbalimbali kuhakikisha kuwa ajali za barabarani hasa katika kipindi hiki cha mfululizo wa siku hizi za mapumziko zinakoma.

Amesema tayari Makamanda wa Polisi wa Mikoa na vikosi hapa nchini wameagizwa kuhakikiksha kuwa wanawasimamia kwa karibu askari wote waliochini yao ili kuwadhibiti madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuona kwamba havileti madhara ama kusababisha kero na usumbufu kwa watu wengine.

Uwegeshaji wa magari usiozingatia taratibu ama kupakia abiria pasipo na kituo, hasa kwa mabasi ya miji mikubwa, ni mambo ambayo hayatapewa nafasi kabisa katika kipindi hiki.

Amewaomba wananchi na abiria kutosita kupiga simu kwa kutumia namba 0732 928723 au kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutumia simu zao za viganjani kwenda kwenye namba 0767 750198 ili Polisi wachukue hatua.

Naye Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ACP Abdallah Mssika, amewa kumbusha wananchi kutokuacha nyumba zao ama mali nyingine pasipo na uangalizi wa kutosha ama kuacha milango wazi ama kuwaachia watoto wadogo ili kuepuka wezi kutumia nafasi hii kwa kuiba.

Amewakumbusha pia wazazi na walezi kutowaacha watoto ama vijana wao kwenda matembezini ama kwenda kuogelea kwenye fukwe za maziwa na bahari pasipo uangalizi wa watu wazima ili kuepuka watoto hao kuzama na kufa maji ama kunasa kwenye matope.

Hata hivyo Kamanda Mssika amesma kuwa tayari Makamanda wote nchini, wameagizwa kuhakikisha wanaweka ulinzi wa kutosha katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu na kufanya doria katika maeneo mbalimbali katika himaya zao ili kudumisha usalama wa wananchi pamoja na mali zao hasa katika kipindi hiki cha mapunziko ya muda mrefu.

Amesema Jeshi la Polisi limejipanga vema kuhakikisha kuwa Wananchi wanasherehekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu.

Lakini pia Kamanda Mssika ametoa angalizo na tahadhali kwa wazazi na walezi kutowaachia watoto wadogo kwenda katika kumbi za sinema zisizo rasmi na kuangalia picha zisizo na maadili kwani picha hizo zinachangia kwa kiasi kikubwa katika mmomonyoko wa maadili kwa vija wetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. HAPA KINACHOTAKIWA NI MATENDO TUU HAYA MAMBO YA KUONYANA NI YA KAWAIDA SANA NA WATU WAMESHAZOEA. KINACHOTAKIWA ITOLEWE MIFANO YA HIZO ADHABU NA IWE ENDELEVU MAANA POLISI WANA TABIA YA KUZIMA MOTO TUU KUKIWA NA MATUKIO FULANI HALAFU BAADA YA MUDA HALI WANASAHAU NA HALI INAJIRUDIA ..

    mZOZAJI

    ReplyDelete
  2. Serikali yetu iwe na priorities. Hakuna kitu kinachoniuzi kama kuwasikia viongozi wakisema wewe unataka tuwe kama Ulaya huko wameendelea. Hizi ni kauli za kuhalalisha uzembe, Badala ya kung'ang'ania mradi wa vitambulisho wangeanza na ku-digitalize driving licence.

    Na kila gari lazima lisajiliwe na kujulikana dereva wake ni nani. Likifanya uzembe wowote ule namba zikipatikana moja kwa moja dereva anajulikana na hakuna nini wala nini ni kulifuta barabara kwa kipindi chote atakachokuwa amefungiwa leseni. Vinginevyo aweke bima ya nani ataliendesha.

    Huu mtindo wa kuazimana magari ukome. Leseni zitolewe baada ya mtu kufaulu Computer based theory test baada ya hapo afaulu piapractical test ambayo itarekodiwa na CCTV na kuwekwa kwa muda mwaka mmoja incase itaoneka dereva alitumia rushwa kupass-practical basi mkanda utakuwepo kama ushahidi. Tukiweza hilo kazi ya kufutia watu leseni itakuwa rahisi sana, na traffic wasiruhusiwe kuadhibu watu bila kidhibiti yaani wanarecord kama ni overspeed na ku-print evidence from speed recording device ili kupunguza Rushwa.

    Barabara kuu zifungwe CCTV zitakazokuwa na uwezo wa kurecord speed pamoja na namba ya gari. Wajenge nguzo kubwa kuzuia vandalism wazikinge na umeme.

    Nafikiri hii itakuwa ni investment nzuri sana katika kulinda maisha ya raia. TATIZO KUBWA HATUNA VIONGOZI WENYE UCHU WA MAENDELEO BALI UCHU WA KUJILIMBIKIZIA HATA KAMA WAMEVIMBIWA(RUSHWA, RUSHWA, RUSHWA-MDUDU HUYU ANAANGAMIZA MAENDELEO YETU).

    Ningekuwa nina madaraka, ningetumia wataalam waliopo nje ya nchi kutransform waliopo nyumbani polepole hata kwa miaka kumi then tuatakuwa tumejenga jamii ianyotii sheria. Favouratism & nepotism should be discouraged ata all costs ili kufikia haya.

    ReplyDelete
  3. roho zote zinazopotea kwa ajali za barabarani ni uzembe wa madereva na serikali yetu !
    umekuwa upuuzi mtupu, kila siku kuona ajali tu ! tumechoka kupoteza wapendwa wetu kwa ajali !
    serikali ingilieni kati swala hili kwa nguvu za ukweli na si upumbavu tu mnaousema hadharani . tumechoka na maneno yenu .
    SUMATRA kitu gani bwana, wekeni traffic lights katikati ya mji kuzuia mwendo kasi wa magari na zebra lazima ziwepo. kuwe na kikosi maalamu cha polisi kudili na madereva waovu .
    ama kwa mabasi ya mikoani abiria msikubari kupelekwa kwa mwendo kasi, mtieni dereva makofi akileta uzembe, tuache uwoga.

    ReplyDelete
  4. Wadau wa 1 na 2 hapo juu, mmeni-touch sana. Haya maonyo tumeiyasikia kila kabla ya sikukuu lakini hakuna mabadiliko yoyote. Wala hakuna mkakati wowote mpya kwenye hao maneno yake. Inasikitisha kuwa watu wenye uwezo na mawazo mazuri kama mdau namba 2 hapo juu hawako kwenye hizi nafasi. Tatizo liko kwenye mfumo wa mafunzo ya udereva, utoaji leseni, hali ya mbovu ya baadhi ya magari, na zaidi sheria kutokumika. Wasimamizi wa sheria wameshindwa kabisa. Tushughulikie mzizi wa tatizo kama tunataka kufanikiwa. Kutoa maonyo ambayo hayana maana kabla ya Pasaka, Krismas, Idd nk nk haina maana yoyote kama hakuna ufuatiliaji wowote.

    ReplyDelete
  5. all this is jus crap talk,wen will the minister and his cohorts resign? how many mo peeps are suppose to die b4 sumthin serious is done? sisi watanzania tunatia aibu. its jus pathetic

    ReplyDelete
  6. aaa MDAU HAO JUU MBONA KAMA HUIJUI BONGO YAANI UNACHOZUNGUMZA KINGEWEZA KUTEKELEZEKA AAH MAMBO INGEKUWA MSWANO, LAKINI POLITICS ZETU ZA HAPA BONGO,

    CCTV ZIKINUNULIWA, KWANZA SI UNAKUMBUKA ULE MRADI WA KUFUNGA CCTV KATIKA JIJI LA BONGO? ULIISHIA WAPI-WAMEFUNGA MAJUMBANI KWAO.

    HAYO MAGARI NI YA WAKUBWA NA WANATAKA KULIPWA BIMA, WE NIAMBIE NANI HUWA ANADAI BIMA AKIPATA AJALI YA BASI? HAKUNA ZAIDI YA MWENYE BASI ANACHUKUA CHAKE NA ANACHEZA MAGUMASHI IMETOKA NA BASI LILILOPATA JALI LINATENGENEZWA LINARUDI NDANI YA BARABARA.

    NI HAYO MACHACHE TU MENGINE KESHO

    ReplyDelete
  7. Suluhishi la ajali za barabarani ni:
    1-Kila gari lazima kuwa na bima(liability or full- coverage),hii itasaidia bima ya dereva anaesababisha ajali kulipa gharama zote na malipo kwenda juu kwa miaka kadhaa.

    2.Leseni za udereva zote lazima ziwe na link ya kitambulisho ,maana either unakitambulisho au hiyo D/L yako ndio kiambulisho maana information zako zote zinatakiwa kuwepo humo.

    3.Magari yote yanasajiliwa kwa kitambulisho au D/L,kama ni dereva basi lazima information zote zake ziwe kwenye hilo gari la kazi yake.

    4.Wanaopata ajali lazima wajue haki zao,ni lazima utafute mwanasheria(wanasheria huwa ni bure maana wanapata malipo baada ya kesi-kesi hizi ni ushindi tu) kulishitaki hilo gari ikiwa umeomba msaada(lift) au hata kama ni la biashara kama daladala.

    Nchi za wenzetu ukipata ajali ya gari hata kama maumivu ni kidogo unalipwa mapesa mengi sana,hivyo hakuna dereva anaeleta uzembe maana bima inapanda,au hata kufungiwa kuendesha gari.

    5.Police wote wawe na kazi ya kuangalia usalama wa raia na magari,police wapewe uwezo wa kutoa tiketi kwa makosa ya magari.

    6.Kuwepo na ukaguzi wa magari kila mwaka.

    Nadhani yapo mengi ila haya yatapunguza sana ajali.

    ReplyDelete
  8. hizo polojo tupu hapa raiaa wanaendelea kutolewa roho na hao madereva wazembe au walevi.sasa nisikilizeni kwa makini wekeni vizuizi barabara zote kuu za hapa mjini kila dereva anapigwa alcohool testi.kama kalamba mbege leseni mpokonye na faini juu.afuu uone kama hawa madereva hawatokua wanaacha mausafiri yao nyumbani wakiwa wanaenda bar na kwingineko kune maulevi yao.

    ni hayo tu

    mdau ubungo NHC

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...