Waziri wa fedha na Uchumi Mustafa Mkulo (katikati) akisisitiza jambo jana jijini Dar es salaam kwa viongozi wa Hoteli ya Bahari Beach ambayo inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni mara baada ya kukamilika ukarabati wake.Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa Hotel hiyo Gerald Schravan(kushoto kwa mh) na Mkurugenzi Mtendaji Abdalah Hiblo(kulia kwa mh.).
Waziri wa fedha na Uchumi Mustafa Mkulo (kulia) akimwonyesha kitu jana jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Bahari Beach Hotel Abdalah Hiblo( kushoto) . Waziri huyo alikwenda Hoteli hapo kwa niaba ya Rais Kikwete ili kujionea hatua ya ukarabati ilikwishafikiwa mara baada ya Hoteli hiyo kubinafishwa kwa Mwekezaji kutoka Libya.
Waziri wa fedha na Uchumi Mustafa Mkulo (katikati) akiongea jana jijini Dar es salaam kwa viongozi wa Hoteli ya Bahari Beach ambayo inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake.Wengineni Mkurugenzi Mkuu wa Hotel hiyo Gerald Schravan(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji Abdalah Hiblo(kushoto).
Picha na Tinganya Vincent- MAELEZO



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Naomba kuuliza, hivi Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji nani anaripoti kwa mwenzie na nini tofauti ya majukumu yao?? Asante.

    Mwajiriwa

    ReplyDelete
  2. Muwekezaji katoka LIBYA.. sasa KILAJI baridi na ile KITU MOTO vitakuwapo kweli??
    Huo ndo mwanzo wa kukimbiza wageni then hotel ifungwe tena!!

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza juu, ngoja tusaidiane ndugu yangu.

    Mkurugenzi Mkuu (the name goes by itself) ni ofisa wa kampuni ambaye wakurugenzi wote wanaripoti. Ni kiongozi mkuu wa kampuni kiutendaji. Kwa lugha ya bibi anaitwa Managing Director kwa miundo mingi ya makampuni huyu anaripoti kwa bodi.

    ReplyDelete
  4. KITIMOTO KIPO HOTELI ZA DUBAI ITAKUWA HIYO YA DAR? MBONA KEMPINSKI YA WAARABU LAKINI KIPO.

    ReplyDelete
  5. Yaani, hata kukarabati hoteli ni lazima rais afike kukagua? Kazi hiyo ingefanywa na Meya au Waziri wa Utalii. hata si hadhi kwa Makamu wa Rais kuifanya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...