Nimesoma kwenye Glogu ya jamii kuhusu huyo mdau anayehitaji msaada wa kubadilishiwa injini ya gari yake kwenda gesi. Ni rahisi. Mwambie aende pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.
Akifika pale aulizie iliko BICO garage. Ipo upande wa pili wa mama Lishe unapoelekea Changanyikeni ukishapita Hill Park au jengo la shule ya Biashara na Utawala. Pale wanaweza kumbadilishia injini yake.
Asante
Mdau wa Glogu ya Jamii
Faraja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Mdau wasiliana na mtu mmoja anaitwa Onesmo Nathan kutoka kampuni ya Triangle Tanzania wapo Kariakoo simu 0754 599777 hawa ndo wanahusika pamoja na jamaa wa Chuo Kikuu.

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi, Mdau Faraja kajitahidi sana kutoa msaada, ila kuna masahihisho kidogo.
    Ni kweli anaweza kupata msaada pale BICO ya UDSM, na haitakuwa na ulazima kwake kubadili mfumo wa utumiaji mafuta badala ya gas, ila anaweza kuelekezwa jinsi na mahali pakupata gas kwa matumizi ya gari lake. Huduma hii ipo hapa Dar sasa.
    BICO haipo huko alipopaelekeza, bali ipo kule engineering. Kwa urahisi, inabidi aingie kupitia pale gate-maji.
    Mdau

    ReplyDelete
  3. Jamani ndugu zangu watanzania hakuna gari linalotumia gesi hapa duniani tatizo ni jina tuu ambalo linalotumika huku Marekani instead of Petroleum we call it Gas hususan hapa Marekani na Canada. Natumaini ujumbe umefika........john.....D.C

    ReplyDelete
  4. Mdau John wa DC, siamini hata kidogo kama uko hapa Marekani na unasema kuwa hakuna gari inayotumia gesi. Kwa taarifa yako kuna magari kibao yanatumia gesi(Compressed Natural Gas-CNG). Na hata kuna dump truck zilikuwa zinatumia propane hapa hapa Marekani.Ndugu yangu fanya utafiti kabla ya kubisha. Mdau USA

    ReplyDelete
  5. Wewe madau wa D.C wenzio huku bongo tumeshaanza kutumia gas kwenye magari. Namfahamu mtu aliyewekewa mfumo huo wa gas, inaitwa CNG (Compressed Natural Gas)na inapatikana PanAfrican ambako kuna kituo cha kujaza gesi hiyo pale ofisi zao za Ubungo na BICO garage iliyopo njia ya kwenda changanyikeni ndio walifunga hiyo system.
    Bongo tambarareeeeeee na gesi yetu wa songosongo!!!

    ReplyDelete
  6. We John wa D.C hizo gari zipo kakaa..Wala usibishe hadharani labda wewe hujagundua bado,huku nilipo mimi algeria ndo mchezo wao,gari ikija wanaibadilisha fasta fasta inakwenda kwenye kutumia gas,maana gas huku ni kama maji.We kalaghabaho....watakucheka wenzio!!

    ReplyDelete
  7. SASA WEWE JOHN WA DC NDO HUJUI. DUNIA SASA INA MAGARI YANAYOTUMIA GESI NA HAPA TANZANIA TAYARI KUNA KITUO CHA KUJAZA GESI (YA SONGOSONGO nadhani KWENYE MAGARI YANAYOTUMIA NISHATI HIYO. UKIENDA PALE KUWEKA NISHATI UNAUZIWA KIASI CHA GESI UNAYOTAKA KATIKA KIPIMO CHA KILOGRAMU TOFAUTI NA KWENYE WESE (AU HUKO KWENYE GESI YENU) TUNAKO/MNAKOTUMIA LITA/GALON WHATEVER. An eye opener for you BRO.

    Mdau Chiggs, Deslam

    ReplyDelete
  8. John naomba kutofautiana na wewe katika hili, mimi nipo kwenye kijimji kidogo tu huku NY, mabasi ya hapa kwetu yanatumia Gas, mkuu kukaa Marekani kwote umeshundwa kugundua kwamba kuna magari yanayotumia none-liquid gas? Umetuabisha watu tulioko ughaibuni, mwana punguza box ukae na watu ujifunze. Naamini una mtandao nyumbani kwako jaribu hata kutembelea Wikipedia itakusaidia.
    Mdau, US.

    ReplyDelete
  9. Ndugu yangu hapo juu!! nani amekudanganya hakuna magari yanayotumia gas!! kuwa marekani sio kujua kula kitu. ngoja nikueleweshe basi uweze kupata picha. Gas ndio kwa american english inamaanisha mafuta ya gari lakini Gas ambayo anaongelea ndugu yetu hapa ni ya English ya UK ambayo aimaanishi mafuta ya gari. haya magari yapo mengi sana na hapa euro ndio yanazidi kuongezea.

    Mdau tokea Europe.

    ReplyDelete
  10. Musalia MudavadApril 15, 2010

    John wa Marekani hapo juu acha ushamba. Hapa Tanzania kwenyewe kuna jamaa wanaitwa Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC). Wao pamoja na shughuli nyingine wanabadilisha magari ya Petrol na Diesel kwenda kutumia gas tena ya Songosongo, kila maonesho ya sabasaba wanaonesha magari hayo, na hata ukienda ofisini kwao utayakuta. Kwahiyo sikweli kwamba kwa kuwa huko Marekani kama ulivyosema (sijui ni kweli) kuwa hakuna gari inatumia gesi basi dunia nzima ndio hakuna. Tembea uone, acha kung'ang'ania box, mambo yamebadilika ebo!

    Asanteni

    ReplyDelete
  11. Mdau Namba tatu unauhakika kuwa hakuna gari inayotumia gas duniani???

    ReplyDelete
  12. Mdau unaejihakikishia kuwa hakuna gari inayotumia Gas Duniani, kwa taarifa yako hapa Tanzania zipo. Tena ni Gas ya SONGOSONGO.Sijui huko ughaibuni kwenu maana wengine tuko tu huku TZ siku zote.Mpaka mnafikia kusema mtu haelewi tafsiri ya Gasoline!

    ReplyDelete
  13. Huyo jamaa mwenyewe mwenye gari mbona hasemi sasa ni wapi kafikia juu ya ushauri wote huu?

    Je amehakikisha kuwa gari yake haitumii petrol = GAS au GAS = gesi?

    Watu walimshauri awaulize walomtumia wanaposema gas wanamaanisha nini na wengine walimuomba akafungue mfuniko wa tangi lake la mafuta ajue kama ni petrol au la.
    Mbona yupo tu kimya, anaacha watu wanachambuana tu, hasemi chochote?

    Pili, Ninavyojua mimi ni kuwa kila gari hapo kwenye mfuniko wa mafuta pana maelezo ya ni mafuta gani gari inapaswa kutumia, je yeye kasoma pameandaikwa nini au hata apige picha alete hapa tumsaidie.

    Ninaomba mtoa hoja ajitokeze na kusema kafikia wapi juu ya suala hilo. Vinginevyo alikuwa anatuzingua tu.

    ReplyDelete
  14. Boksi limeanza kuleta balaa. Miji mingi ya Marekani utakuta mabasi yao ya public transport (UDA zao) yanatumia Compressed Natural Gas (CNG) na yanarembwa kabisa na usemi kama "Clean Air" au kitu kama hicho na maelezo kwamba linatumia CNG.
    Fungua macho utajionea.

    ReplyDelete
  15. wadau naomba kuuliza, Gas ikiwa compressed inakuwa katika fomu gani? liquid au gas?

    ReplyDelete
  16. Inakuwa in a Liquid State! Haiitaji tochi hiyo! Mmeenda shule gani?

    ReplyDelete
  17. Jama basi jama, Mdau wa DiiCii amekoma. ASANTENI WADAU KWA KUMSAIDIA, SIKU NYINGINE HATAKURUPUKA namna hii, nadhani ata-research kwanza. hahahahahahaaaaaaaaa, kujua kwingi

    Mdau chiggs, Deslam

    ReplyDelete
  18. Anony apr 16:
    Compressing gas means increasing pressure of a gas. This can be achieved by decreasing its volume. Kama umesoma Kemia au Phizikia utakumbuka PV=constant. Kwa maana nyingine ukiongeza Presha, ujazo unapungua na ukiongeza presha ya kutosha unaweza kupata kimiminika kutoka kwenye gesi. Kwa baadhi ya maada, unaweza kupata solids from gas.

    Chemical Engineer.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...