ASSALAM ALEIKUM ANKAL
NIMEJITOKEZA TENA WAUNGWANA, INFWACT NINATATIZO KUBWA NAOMBA MSAADA WENU.
NIMEJITOKEZA TENA WAUNGWANA, INFWACT NINATATIZO KUBWA NAOMBA MSAADA WENU.
MIMI NI SINGLE PARENT NA NINA KIJANA WANGU WA MIAKA 8, MARA KWA MARA ANAKUA NA KIKOHOZI KIKAVU AMBACHO HUPOTEA KWA KIPINDI FULANI, WENGI WAMEKUA WANA SEMA KWAMBA ANASUMBULIWA NA KIMEO!!!!.
NADHANI HATA WEWE BWANA MICHUZI UNAKIJUA, WAKANIAMBIA NIMWANGALIE KWA NDANI YA MDOMO, KWELI NIKAMUONA ANA KITU KIREFU KAMA MOYO WA KUKU KWA NDANI, HIKI NDICHO KIMEO a.k.a KILIMI. WAKANISHAURI NIKIKATE PALE MTAA WA UDOE KARIAKOO.
KWA KWELI NIMESITA MAANA MADAKTARI WANASEMA KWAMBA KUNA MADHARA KUFANYA HIVYO, SIJUI MADHARA GANI ILA WANASEMA KUNAUWEZEKANO WA KUVUJA DAMU SANA NA INAWEZA PELEKEA KIFO, ( HAPO NDO KHOFU YANGU)
DAKTARI NILIEMFUATA NI JIRANI YANGU MSOMI HASA, ILA MY WIFE YAKE AKANISHAURI PIA NIMKATE MAANA HATA YEYE WANAE ALIWAKATA BILA MZEE KUJUA NA MAMBO NI SHWARI. NAULIZA MABINGWA NA WAJUVI WA MAMBO YA TIBA YAFUATAYO
1. NIKWELI KIMEO (KILIMI) HUSABABISHA KUKOHOA??
2. NIKWELI KWAMBA KIKIPEA BILA KUKATWA KINAPASUKA NA MTU AWEZA POTEZA MAISHA??
3. NIKWELI TIBA NI KUKATA??
4. WAPI WANAKATA KITAALAM KAMA INAJUZU??
AHSANTENI WAJAMENI
MZEE WA BUNJU
1. NIKWELI KIMEO (KILIMI) HUSABABISHA KUKOHOA??
2. NIKWELI KWAMBA KIKIPEA BILA KUKATWA KINAPASUKA NA MTU AWEZA POTEZA MAISHA??
3. NIKWELI TIBA NI KUKATA??
4. WAPI WANAKATA KITAALAM KAMA INAJUZU??
AHSANTENI WAJAMENI
MZEE WA BUNJU
Ddugu yangu nakushauri usimkate mtoto wako kilimi, kwani hakuna ushahidi wowote wa kitiba ambao unaonyesha kwamba kikohozi kinasababishwa na kimeo kuvimba. Pengine mwanao anasumbuliwa na kikohozi kinachosababishwa na allergy ambacho huenda na kurudi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Au kinasabbaishwa na nyinginezo ambayo kwa kumuona dakitari na kupewa antibiotics kinaweza kukoma kabisaa. Ni bora ukamuone mtaalamu wa magonjwa ya watoto kuliko kurisk kumkata mwanao kilimi na pengine apatwe na hayo uliotahadharishwa. Nafikiri tabia ya kuwakata watu vilimi inatokana na dhana ile ile ya waafrika wengi pale tunapopatwa na tatizo la kitiba la kwanza tunatafuta alternatives ambazo si sahihi kama vile ramli, mganga wa jadi, babu na bibi wanafikiri vipi, fulani alipougua pia alifanya vipi na kama hivyo, badala ya kwenda hospitali kwanza.
ReplyDeletela kushangaza ni kuwa kilimi tunakatana huko kwetu tu (Tanzania) na sehemu nyinginezo hakuna suala kama hilo. Laajabu ni kwamba kabla ya kukatwa kilimi kila kikohozi kinanasibishwa na kilimi, kilimi kikishakatwa na kikitokea kikohozi kingine hatuna kisingizio kingine au hakuna cha kukata tena, inatubidi tuende hospitali au tuwavike wenetu hirizi!
mpeleke mwanao hospitali moja inaitwa "Ekenywa" kamuone Dr. Ole (ndio mwenye hospitali). Yeye ni mtaalamu wa ENT (Ear, Nose and Throat) (Masikio, Pua na Koo).
ReplyDeleteHuyu daktari atakupatia tiba ya mwanao, he is really good in that.
Hospitali iko mwembechai (usijali location), unapita njia iliyoko ubavuni mwa kituo cha mafuta halafu unaenda mbele (keeping right) utaikuta hospitali mkono wako wa kushoto.
Nawasilisha!
Kwako Single Parent - nimeguswa sana na maelezo ya tatizo la kijana wako wa miaka 8, nikaona nisipoteze muda katika kukupa ushauri.
ReplyDeleteMimi si daktari wa binadamu bali ni kuwa nilipata uzoefu huo baada ya kijana wangu kufikwa na tatizo kama la mwanao, akatibiwa na kupona kabisa.
Chonde chonde usithubutu kukikata hicho kimeo kwa mwanao. kinachotokea ni kuwa hicho kiungo huwa kinapata 'infection' ndio sababu ya kuumuka na kuwa na size tofauti na ile ya kawaida.
Mpeleke mwanao kwa dakatari wa kawaida 'General Practitioner' atamtibu kijana wako kwa hizi dawa za hospitalini.
Pole single parent
tafdhali tuwasiliane 0755029182 au 0655029182 nina dawa, na kwa yeyote yule mwenye tatizo tuwasiliane nina dawa nyingi tu
ReplyDeleteau ingia http:///mujydebubyz.ning.com utanipata
sio utani naweza kukusaidia
Ndugu yangu waliotangulia wote wametoa ushauri bora tena bora sana, mimi sina cha kuongezea ila wameacha kukushauri jambo moja kuwa ukishapata hiyo tiba urudi kwa huyo daktari jirani yako na umwambie kuwa wanawe wamekatwa kimeo ili nae ajue kwani wewe umebabaika ulipojua kuwa watoto wa dkatari nao pia wamekatwa kimeo.
ReplyDeleteTumia asali na tangawizi mbichi, yaani unasaga/grate tngawizi mbichi, kisha unakamua ile juice yake bila kuchanganya na maji unapata kijiko kimoja ambayo utachanganya na asali kijiko kimoja.
ReplyDeleteMpe mtoto wako mchanganyiko huo wa asali na tangawizi, inshaallah kikohozi kitaondoka.
Ila tafuta asali safi huko idara ya misitu na nyuki/maliasili, usinunue sukari ya kuchemshwa mitaani.
Mimi nilishauriwa kukata kimeo nikiwa mtu mzima, Nilikuwa Bunda nilikuwa karibu nife. Usithubutu kufanya hivyo. Kimeo kikiwa hivyo ina maana mtoto ana maambukizi mwilini. Kazi yake ni kupambana na infections hizo hivyo ukikitoa, umemwondolea kinga yake. Mpeleke hospitali wataona kiini inawezekana anahitaji antibiotics au kama mdau alivyoshauri labda ni virus kama mafua, hivyo tangawizi na asali na limau ni dawa tosha sana pamoja na vicks kwenya kifua. Usisikie ya waganga wa kienyeji hatari!!!!
ReplyDeleteKaka tunashukuru sana kwa kuomba msaada huo wa ushauri japo tupo wengi lakini tunaweza kukupa ushauri unaofaa au usio faa ni wewe wa kuuchuja.
ReplyDeleteMimi ni mmoja wa watu ambao wagumu kuamini juu ya tiba ya kimeo kuwa ni kukata. Leo nilibahatika kupata wasaa na kupita pale Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wanapofanya maonesho yao ya miaka 10. Banda la kwabnza kuingia linahusiana na Tiba ya hicho Kimeo.
Hakika majibu na maelezo niliyopata pale katu sikushauri umkate huyo mtoto KIMEO. Harakaraha ni kuwa TIBA IPO FIKA HOPSPITALI ZINAZOELEWEKA hata muhimbili nenda.
Pia mama aliyekuwa ananieleza anasema Kimeo nisehemu au kiungo muhimu sana kwa uzalishaji wa chembechembe nyeupe ambazo hutoa kinga sana kwa magonjwa. Mtu hufa baada ya kukatwa hicho kutokana na eneo kuwa ndo kiwanda.
Hata hivyo nikaambiwa kuwa ni nyenzo mmoja wapo ya kutolea sauti.
NILITHIBITISHIWA KUWA TIBA IPO NA KATU MTOTO AU MTU MZIMA ASIKATE KIMEO. DAKTARI ATAKAE KUSHAURI KUKATA KIMEO SI DAJTARI NI MGANGA WA KIENYEJI.
Bwana acheni uzungu wenu! hii kitu kimeo ipo, sana tu! watu wengi wamepita pale UDOWE na wote mpaka leo sijasikia kuna mtu kafa kwa sababu ya kukatwa, vizuri ni kwamba kabla ya kukata wanamtizama mgonjwa na kama hahitaji kukatwa wanamwambia na hawamkati. Nakumbuka mdogo wangu alikuwa hivyo hivyo anasumbuliwa kuumwa umwa hovyo na kukohoa kila siku mpaka Daktari mwenyewe akasema huyu anakimeo ndo akamshauri mama ampeleke pale na akampeleka akapona mpaka leo anadunda. na kwanza si kama wanakikata chote ni kincha tu na siku mbili au tatu utamwona mtoto mzima.
ReplyDeleteHii kitu ipo ingekuwa inamadhara toka miaka hiyo serikali hawajaiona wakawafungia?!
Ndugu,
ReplyDeleteMi nitaakupa uzoefu wangu. Nilipokuwa mtoto nakumbuka nilikuwa nakohoa sana, kikohozi fulani kinakuwa na ladha ya "metallic" kooni mwa anayekohoa kutokana na kimeo kuwa kirefu na hivyo kutekenya tekenya koo mara kwa mara.
Nilikuwa kijijini Mbeya kwa babu na bibi, wazazi wangu wote walikuwa masomoni Uingereza. Nilikuwa na umri wa miaka minne tu. Siku moja bibi alinichukua na kunipeleka kwa mganga wa kienyeji hapo kijijini. Huyu ni wale waganga wa tiba mbadala (kama doctor Ndodi) sio waganga wa ramli na uchawi.
Alinipa dawa fulani ya mitishamba halafu nikakatwa kimeo. Haikuuma sana. Na wala sikupata matatizo yote. Yaani suala la kuumwa au kukaribia kufa baada ya operesheni hiyo halikuwepo kabisa.
Huo ndio uzoefu wangu kuhusu kimeo. Nilikuwa na miaka minne wakati huo. Sijui kwa mtoto wa miaka 8 kama itakuwa nongwa.
Fuatilia ushauri wa watu hapo juu. Nakumbuka baba yangu nikiwa mdogo alikwatwa hii kitu na bado aliendelea kukohoa tu.....Hivyo sidhani hiyo ndio solution....
ReplyDeleteKam huyo alivyosema baada ya kukwatwa kikohozi kikirdi huna jibu na huna cha kusingizia..
hata mimi nilikatwa KIMEO kwa kumbakumba long time yaani,sasa ukae na kimeo cha kazi gani..ila inabidi ukatwa ukiwa bado mtoto mdogo.Unazani kwanini wanaita KIMEO,ila ka unaogopa usimfanyie mwanao,kimeo kama JANDO tu!! wengine wanaishi na magovi...
ReplyDeleteAnony uliyesema watu waache uzungu wao nakubaliana nawe mia kwa mia. Nikiwa mdogo babu yangu alikuwa an shughulikia stizo hilo hakuna mtu aliyekufa. Ilikuwa akiniita na kunituma dukani kununua wembe (enzi hizo Perma Sharp au chapa mamba siyo hizi za kwenu topaz )najua kazi yake. Tatizo kwa sasa kila cha mzungu ni kizuri
ReplyDeleteEbana eee!! mtu akiwa na hicho kimeo ndio huwa anakuwa kingàngànizi na kitu, dah mm ndio nimejuwa leo kumbe afdhali umkate ili asiwe kingàngànizi na kitu.
ReplyDeletePamoja na ushauri uliotolewa kuwa mzuri, sidhani kama nimechelewa sana na ushauri wangu ambao ninauzoefu nao kupitia kwa rafiku yangu ambaye kwa sasa kapona kabisa. Yeye amesumbuliwa na kikohozi kikavu tangu akiwa form six hadi kamaliza chuo. Amekunywa dawa za kila aina na ametumia kila gharama hata ikafikia kwenda kupima ngoma nayo hakuwa nayo. Mwisho wa siku akashauriwa kienyeji kuwa anunue asali ya nyuki wa dogo awe anaichanganya na yai moja la kienyeji anakunywa asubuhi na jion. Inakuwa ngumu kumeza kwa jinsi ule ute ute ulivyo lakini alipona ndani ya wiki 2 tu! Epuka madawa ya viwandani pasopokuwa na ulazima. Ni hayo tu
ReplyDeleteMdau Dar