Ankal tunashukuru sana kwa jitihada zako za kutukutanisha na
kutuhabarisha. Nina tatizo kidogo nilikuwa naomba uniwekee kwenye blog
yetu ili wadau wanisaidie. Huenda
inawezekana akawepo mmoja wetu anayejua jinsi ya kupata taarifa ninazohitaji. Natafuta link ambayo inaweza kunisaidia kupata makusanyo ya kodi kwa kila mwezi au robo mwaka kuanzia mwaka 2000/2,
2002/3,
2003/4,
2004/5,
2005/6,
2006/7,
2007/8,
2008/9,
2009/10.
Kama kuna mtu anajua tafadhali naomba anisaidie. Kabla ya kuomba nisaidiwe nimejaribu kutafuta kwenye internet bila mafanikio kwa kadri nilivyokuwa nahitaji. Taarifa hizi ningezipata TRA lakini kwenye website yao kuna taarifa mbili tofauti; mosi, ni makusanyo ya kodi kimkoa (about us/tax regions) halafu pili ni takwimu za makusanyo ya kodi (tax informations/statistics). Ukijaribu kuchambua takwimu zao utagundua kwamba taarifa za kimkoa kwenye vyanzo
vyote viwili zinatofautiana. Na kingine ni kwamba taarifa zao zina
zinaishia 2008/9 (kwa maana ya June 2008). Mimi nahitaji takwimu hadi
March 2010.

Wadau, natanguliza shukurani.

Mdau K. Martin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. sema study yako inahusu nini tunaweza kukupa ushauri incase of missing data. unafanya study ya mahusiano kati ya kodi na nini???

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu nashukuru sana.

    Study yangu inahusu mahusiano ya makusanyo ya kodi (revenue collections) na mtikisiko wa kifedha duniani (global financial and economic crisis) kwa Tanzania.

    Email yangu ni kaburu.martin@gmail.com

    Shukrani.

    ReplyDelete
  3. Mzeeee, mimi nitakuandikia ka introdakisheni kidogo.
    ............................
    There is a big correlation between Tanzania revenue collection and the global finacnical and economic crisis. When there is a global financial crisis, collecting revenue is always difficult, people are broke, companies are broke too, some even going into adminstration or liquidity. In other words, if there is a global financial crisis, less amount of revenue is collected it doesn't matter what part of the world you are.

    Mkulima namba moja

    ReplyDelete
  4. Piga simu makao makuu ama waandikie

    http://www.tra.go.tz/index.php?option=com_contact&task=view&contact_id=1&Itemid=3

    They ought to have the stats even if they are not published online.

    Waambie mapema if you are looking for nominal numbers or if you want the numbers to be factored for inflation or both ili muelewane mapema.

    Wakisema wanataka kitu kidogo ili wakukusanyie takwimu usishangae sana, Bongo tambarare.

    Good luck!

    (US Blogger)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...