Na Mohammed Mhina na Athumani Mtasha, wa Jeshi la Polisi
DAR ES SALAAM IJUMAA APRILI 09, 2010.


Mtoto wa Malkia wa Uholanzi, Her Royal Highness Princess Maxima, amesema kuwa nchi yake itaendelea kutoa misaada ya kitabibu kwa Jeshi la Polisi nchini Tanzania na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Princess Maxima, alitoa ahadi hiyo jana jioni, wakati akizungumza kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika Makao Makuu ya Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.


Princess Maxima, ambaye pia ujenzi wa wodi ya watoto, maabara ya kisasa ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali na kliniki ya ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (CTC).


Amesema kuwa lengo la misaada hiyo ni kuleta matumaini zaidi kwa askari na watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama vya hapa nchini kwa kujali afya zao kwa kuboresha huduma za tiba kwa magonjwa ya Kifua Kikuu na Ukimwi.


Amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kusimamia kwa karibu shughuli za ujenzi na ukarabati wa majengo ya Hospitali hiyo Kuu ya Jeshi na nyingine zilizopo katika mikoa mbalimbali na vyuo vya Polisi hapa nchini.


Kabla ya mkutano wa hadhara Pricenss Maxima, alikutana na kufanya mazungumzo na kikundi cha kutoa huduma wagonjwa majumbani kwa watu walioathirika na ukimwi na kifua kikuu.


Awali Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Lawrence Masha amesema kuwa Serikali ya Uholanzi kupitia Shirika la Maendeleo linalohudumia miradi ya Afya kwa nchi za Afrika, Farm Access International (PAI) tayari imegharimia ukarabati wa Zahanati 26 zikiwemo 13 za Jeshi la Polisi na nyingine 13 za Magereza.


Amesema kuwa hadi kufikia mwaka 2011 kila mkoa utakuwa na na Hospitali moja kwa Jeshi la Polisi na nyingine kwa Jeshia la Magereza zenye viwango vya kisasa na huduma za magonjwa ya ukimwi na Kifua Kikuu.


Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema amesema kuwa mbali na ukarabati uliofanyika katika Hospitali Kuu ya Kikosi cha Afya Jijini Dar es Salaam pia umefanyika ukarabati wa zahanati za Polisi zilizopo katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, CCP Mkoani Kilimanjaro, Arusha, Tabora, Dodoma na Zanzibar.


Princess Maxima ambaye amefuatana na ujumbe wa watu 30 kutoka idara na wizara mbalimbali za nchini Uholanzi wakiwemo waandishi wa Shirika la Habari la Uholanzi NOVA yupo hapa nchini kwa ziara ya kiserikali.


Naye Mkuu wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi hapa nchini Naibu Kamishna (DCP) Neven Mashayo amesema kuwa zaidi ya ukarabati wa majengo, mpango huo pia unalenga katika kuinua na kujenga uwezo kwa watendaji wa afya katika Hospitali za jeshi la Polisi ili zitoe huduma bora kama inavyotarajiwa.


Amesema ukarabati huo umeshaghalimu zaidi ya shilingi milioni 700 na kwa sasa kitakacho fuata ni kuanzisha kitengo cha X-RAY na Kitengo cha huduma za tiba ya Ukimwi VCT na maabara ya kisasa ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali yakiwemo ya Kifua Kikuu (TB).


Serikali ya Uhalanzi pia imefanya ukarabati katika Jengo la Kiliniki kwa akina mama walioathirika na virusi vya HIV pamoja na kujenga sehemu maalumu ya uteketezaji wa taka ngumu na laini zitokanazo na Hospitali hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. MAXIMA SI MTOTO WA MALKIA WA UHOLANZI BALI NI MKWE WA MALKIA.YEYE NI MKE WA PRINCE WILLEM ALEXANDER VAN ORANJE AMBAYE NI MTOTO WA MALKIA BEATRIX VAN ORANJE. MAXIMA ANATOKEA ARGENTINA. AMEOLEWA 2001. KABLA YA HAPO ALIKUA ANAISHI NA KUFANYA KAZI KATIKA BENKI MOJA JIJINI NEW YORK.

    ReplyDelete
  2. MAXIMA SIO MTOTO WA MALKIA WA UHOLANZI BALI NI MKE WA MTOTO WAKE.
    MDAU
    KISIJU PWANI

    ReplyDelete
  3. Ndio maana Mkapa anawaponda waandishi wa bongo,yaani wao ni no research.
    Kabembe.

    ReplyDelete
  4. Hii nchi siasa zao zikoje? Mkwe ma alkia anasafiri kiserikali na anatoa misaada ya kiserilari? Nielewesheni hapo kidogo wakuu!!!
    Nanjilinji!!

    ReplyDelete
  5. NAONA BADO MPO NYUMA KATIKA HABARI NI BORA KABLA YA KUTOA HABARI UFATILIE ILI KUWAJUWA WAHUSIKA WA HABARI HIYO

    NAJARIBU KURUDIA TENA KUELEIMISHA JAMII KWA UPOTOSHO WA MHUSIKA ALIEFIKISHA HABARI HII

    HUYO SIO MTOTO WA MALKIA HUYO NI MKE WA MTOTO WA MALKIA WA UHOLANZI

    JINA LAKE NI MAXIMA ANATOKEA NCHI YA ARGENTINA ALIOLEWA NA PRINCE ALEXANDER MWAKA 2001

    MALKIA WA NCHI YA UHOLANZI NI BEATRIX AMABE MTOTO WAKE ANAITWA ALEXANDER NDIO AMEMUOA HUYO MAXIMA

    SISI AMABAO TUPO HUKU TUNAJUWA VIZURI HISTORIA YA HAO WATU

    NAOMBA UNIFIKISHIE HUU UJUMBE ILI KUELEMISHA JAMII SIO KUPOTOSHA JAMII

    KESHO MTOTO WA ANKAL AKIJA KUULIZWA NI NANI MTOTO WA MALKIA WA UHOLANZI ATASEMA MAXIMA NA WAKATI SI KWELI

    MAXIMA NI MKE WA MTOTO WA MALKIA WA UHOLANZI.

    NA HIYO FAMILIA YA MALKIA BEATRIX NDIO WAMILIKI WA NDEGE ZA ROYAL DUTCH KLM.....THANKS.
    mdau uholanzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...