Beki wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 kutoka Kenya, Milton Milimo (kulia), akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa timu ya Ngorongoro Heroes, Jukumu Kibanda, wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika leo jioni kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar. Ngorongoro Heroes ilishinda bao 4-3
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes, wakipongezana leo baada ya kuibanjua Kenya kwa mabao 4-3 katika mchezo wao uliofanyika jioni hii katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar. Endapo Ngorongoro Heroes itafanikiwa kuifunga Malawi katika mchezo huo itakutana na timu ya vijana ya Ivory Coast katika mchezo utakaopigwa mwezi Julai na kama itashinda katika mchezo wake dhidi ya Ivory Coast basi timu ya Tanzania itatinga moja kwa moja katika fainali za michuano hiyo huko Libya. Mshambuliaji wa timu ya Vijana ya Tanzania, Ngorongoro Heroes,
Abuu Ubwa (kulia) akimtoka beki wa Kenya, Edwin Simiyu.
Kocha Mkuu wa Yanga, Kostadic Papic (kulia) akiwa na msaidizi wake, Medic Momcilo 'moma' wakifuatilia mchezo wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania 'Ngorongoro Heroes' inayojiandaa na mchezo wake na timu ya Malawi utakaopigwa Aprili 17 katika mjini wa Lilongwe wa kufuzu fainali za Afrika za vijana wa umri chini ya miaka 20 ambapo fainali zake zitakazofanyika Libya. katika Mchezo wa leo Ngorongoro Heroes imeshinda 4-3.

Kikosi kamili cha Ngorongoro Heroes leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwanza Hongereni Vijana kwa ushindi, Je ma Kocha wa Timu zengine za Ligi ya Tanzania Bara walikuwepo? kama hawakuwepo alikuwa tu huyo wa Yanga inaonesha kabisa Nchi yetu bado haitizami Vijana kama inavyotakiwa. Nilienda Visiwani Kwa wenzetu ZNZ angalau wanajitahidi wanamashindano ya vijana na wanawapa nafasi kwenye timu zao za Ligi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...