(By US Blogger)
Katika pitapita zangu katika maofisi mbalimbali ya Serikali na ofisi binafsi nimeona picha za Baba wa Taifa na Mh. JK zikibandikwa kutani.
Nilipata majibu yasiyolingana kutoka kwa wahusika kama hiyo ni sheria ama mapenzi binafsi kwa wahusika ama uzalendo.
Labda wadau wa libeneke munisaidie.
By US Blogger
USblogger11@gmail.com
Katika pitapita zangu katika maofisi mbalimbali ya Serikali na ofisi binafsi nimeona picha za Baba wa Taifa na Mh. JK zikibandikwa kutani.
Nilipata majibu yasiyolingana kutoka kwa wahusika kama hiyo ni sheria ama mapenzi binafsi kwa wahusika ama uzalendo.
Labda wadau wa libeneke munisaidie.
By US Blogger
USblogger11@gmail.com
Nafikiri ni ufisadi. Ile picha inauzwa ghali kweli na ni lazima uwe nayo kwenye duka zamani sijui siku hizi
ReplyDeleteUkoloni
ReplyDeleteUS Blogger wacha uzushi..hahaha
ReplyDeleteMashaka, nitakuandikia na kukufafanulia sheria, kanunu na taratibu zinazoongoza katika matumizi ta picha RASMI ya rais katika ofisi za umma.
ReplyDeleteNInavyojua hapa kwetu Tanzania katika ofisi za Umma ni Sheria kubandika picha ya rais na ya baba wa taifa, utaratibu huo umeainishwa kwa waraka wa serikali ambao siukumbuki, picha ya rais inatakiwa kuwekwa nyuma ya ukuta ambao amekaa kiongozi katika ofisi hiyo na picha ya baba wa taifa inatakiwa kutazamana na picha ya rais, kwa maana nyingine iwekwe opposite na picha ya rais
ReplyDeletesi hatuna na pesa za kununua izo picha hatuna...
ReplyDeletekazi kweli izi pesa za mtanzania,yani kodi tunalimwa ya kufa mtu,basi na mengine lazima pia tuyanunue.tule polisi???
khaaaa
Tuwapende viongozi wetu sio kuwasahau picha napenda kuziona ktk office na zipewe heshma inapendeza. tusipo zipenda nani atazipenda mimi na nyie tukizipenda wote watazipenda.
ReplyDeleteMambo ya picha za viongozi ukutani ni kutokana na historia ya mfumo wa zamani wa chama kushika hatamu, lakini siku hizi tungepigia kura hilo halina uzito wo wote.
ReplyDeleteWenzetu walioendelea sijaona picha za marais ukutani hata ofisi za serikali hakuna picha za marais