Kwa mujibu wa 'gazeti' la Sun la nchini Uingereza, ile Safina ya Nuhu ambayo Waktristo na wasomaji wa Biblia wameisoma au kusimuliwa inasemekana ipo nchini Uturuki kwenye umbali wa futi 13,000 katika mlima mmoja nchini humo.

Kikundi cha Wainjilisti na Wavumbuzi wa Mambo ya Kale (archeologist) kutoka China na Uturuki wamesema kuwa wameyapata mabaki ya vipande vya mbao katika Mlima Ararat ulioko Mashariki mwa Ururuki.

Wavumbuzi hao wanasemakuwa kipimo cha kung'amua umri wa vitu kwa kitaalam, 'carbon dating' kinathibitisha kuwa mabaki hayo yana umri wa miaka 4,800 - muda ambao unashabihiana na muda unaosomeka katika vitabu vya dini na historia kuwa ndipo safina hiyo ilipoelea juu ya maji.

Mmojawapo wa wachambuzi hao, Dk. Yeung, amekanusha taarifa kuwa inawezekana hayo ni mabaki ya shughuli za kibinadamu wa hivi karibuni kwa kusema kuwa shughuli za kibinadamu hazijathibitika kuwepo katika eneo hilo lenye mwinuko wa futi zipatazo 11, 000.
Habari Zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mdau, Very interesting. Nakujulisha kuwa maelezo ya Safina ya Nabii Nuhu yako pia katika Kurani Takatifu. In fact, Sura ya saba ya Quran Tukufu inaitwa Sura ya (Nabii) Nuhu. Thanks for sharing the info. Mdau wa Vitabu Vitakatifu.

    ReplyDelete
  2. CORRECTION!!!!!Smahani sana.......
    Mimi ndiye niliyeposti comments ya kwanza. Sura ya Nuhu SIYO ya Saba katika Kurani Tukufu: Sura ya Nabii Nuhu ni ya 71 katika Qurani Tukufu. To err is human...Mdau wa Vitabu Vitakatifu.

    ReplyDelete
  3. Afadhali ulivyo sahihisha maana Qur ani haitakiwi kupungwa wala kuzidisha Kuh hiyo historia ya Nabii Nukhu radhi ya llah ng anhuu ni historia nziti na yenye mvuto mkubwa nawakia kila kheri wagunduzi soon tutapata ukweli wa kila jambo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...