Na Tiganya Vincent, Dar es salam.
Wizara ya Fedha na Uchumi imesema kuwa iko katika mipango ya kuandaa utaratibu utakaorahisha ufunguaji wa akaunti kwa wananchi wengi hasa wale wanaoishi vijijini ili wajenge utaratibu wa kuhifadhi fedha.
Hatua hiyo inalenga kuwa na viwango ambavyo wananchi wengi wataweza kumudu huduma za kufungua akaunti katika benki mbalimbali hapa nchini.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo wakati wa mazungumzo maalum na Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na ambaye ni Binti Malkia Maxima wa Uholanzi.
Alisema kuwa benki nyingi zilizopo hapa nchini zinatoa gharama za ufunguaji wa akaunti ziko juu ukilinganisha na pato halisi la Mtanzania hali inayowafanya wengi wasindwe kabisa kuweka fedha zao katika Asasi hizo.
Mkulo aliongeza kuwa kiwango kimefanya baadhi ya Benki zinatoa huduma hapa nchini kuonekana kuwa ni maalum kwa ajili matajiri jambo ambalo sio sahihi. "Wananchi wengi wanashindwa kuweka fedha zao benki kwa sababu kiwango cha kianzio hakiwiani na fedha wanazopata kwa siku..hivyo kama kiwango kingekuwa cha chini wananchi wengi wangejitokeza kuwa fedha zao" alisema Mkulo.
Vilevile alisema kuwa Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kuwawezesha wananchi wa vijijini kunufaika na huduma za fedha. Aidha alisema kuwa hivi huduma za utumaji fedha kwa njia rahisi zimeimarika ambapo kila Kampuni karibu nyingi za Simu zimekuwa zikisaidia kusafirisha fedha kutoka kwa mtumaji hadi kwa mlengwa kwa haraka zaidi.
Mkulo alisema inakadiriwa karibu watu milioni 10 wanamiliki simu za mikononi jambo ambalo linarahisha utumiaji na upokea wa fedha kwa wakazi wa vijijini. Kwa mujibu wa Mkulo ni asilimia 7 ya Watanzania wanaopata huduma za Kibenki ikiwemo vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS)
mimi nataka kujua ni kwa nini nikiweka akiba yangu bank hapa tanzania badala ya kupata interest huwa nakatwa mimi kila mwezi. hata kama sikufanya transaction yeyote zaidi ya kuingiza pesa zaidi kwenye account yangu kwa mwezi mzima. hii inakuwaje kuwaje?
ReplyDeleteMawazo yote yapo jimboni tu.
ReplyDeleteLini Maxima kawa malkia? au sikuhizi Princess maana yake malkia? Ninavyojua mama mkwe wake ndio malkia wa uholanzi
ReplyDeleteMichuzi fanya uchunguzi kabla ya kuweka habari..malikia wa Uholanzi Maxima..hahahaha..aibu.
ReplyDeleteMichuzi huyo Ni Princess Maxima sasa sijui kwa kiswahili atakuwa Malkia?
ReplyDeletemwana malkia!!!!!
ReplyDeleteKwa kiswahili fasaha ataitwa mkaza sultan
ReplyDeleteAnkal mbona unaharibu jamii kwa kutoa majina yasiyo sahihi unapotosha jamii
ReplyDeletemimi ndio yule mdau wa uholanzi huyo sio bint malkia
huyo ni mke wa mtoto wa malkia jina lake ni maxima
na malkia wa nchi hii anaitwa beatrix.familia hiyo ya malkia beatrix ndio wamiliki wa ndege za royal dutch....KLM
mdau nawakilisha