Amani akiwajibika vilivyo
Mwimbaji maarufu nchi Kenya, Amani kwa mara nyingine tena aliwafurahisha wapenzi wa muziki jijini London baada ya kuangusha shoo moja matata sana. Amani ambaye yupo nchini uingereza kwa ziara ya mwezi mmoja, alifanya show yake ya tatu katika ukumbi wa Club Africa iliyopo Canning Town, London. Show hiyo ilionekana kumefana sana kwani wapenzi wengi walionekana kuridhika na minenguo na kipaji cha uimbaji cha mwanadada huyo. Mwandishi wa wa Blog ya TZ-ONE, Ally Muhdin alipowahoji wapenzi wa nyimbo za mwanadada huyo, walisema kuwa sauti ya mwanadada huyo na mashahiri ya nyimbo zake zimewafanya waridhike na tamasha hilo. Vilevile unenguwaji wa mwanadada huyo umewaridhisha sana
Wanablog maarufu jijini London, Bi. Jestina George na mhariri wa blog ya TZ-ONE Ally Muhdin wakiwa katika tamasha Amani lililofanyika Club Africa, London
Amani katikati akiwa na Jesse Malongo kulia na Bi Rahma Lupatu
Kulia mdau wa CCM shina la London Abdallah Mdidi na Bw. Pazi wakiwa kwenye tamasha la Amani
wadau wakipata taswirazz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Heko wana-diaspora tunawaona

    ReplyDelete
  2. Great vocal! Ila hizo beats za wakenya zinanikumbusha wali maharage na jua la bongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...