
Nyerere Prof. Issa Shivji akitoa tamko rasmi la Tamasha hilo.
KIMBEMBE CHAJA KUANZIA
TAREHE 12 - 15 APRILI PALE NKRUMAH HALL
Ankal, we ushalisoma Azimio la Arusha? usikose basi mjadala mpana na
wa kina umeandaliwa na KIGODA CHA TAALUMA CHA MWALIMU NYERERE cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Mwalimu Julius Nyerere Professorial Chair in Pan-African Studies).
wa kina umeandaliwa na KIGODA CHA TAALUMA CHA MWALIMU NYERERE cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Mwalimu Julius Nyerere Professorial Chair in Pan-African Studies).
Safari hii Mgeni Rasmi ni Mtoto wa aliyekuwa
raisi wa kwanza wa Ghana Dr. Kwame Nkrumah anaitwa Mh. Bi. Samia
Nkrumah ni Mbunge kule Ghana.
raisi wa kwanza wa Ghana Dr. Kwame Nkrumah anaitwa Mh. Bi. Samia
Nkrumah ni Mbunge kule Ghana.
tuna ngojea clip kwa hamu, ni matumaini globu ya jamii itakaribishwa kufanya kazi kwa ajili ya jamii nzima iliyotapakaa kote ulimwenguni.
ReplyDeleteMdau
Ughaibuni ktk Dayaspora
Arusha Declaration = Uonevu wa wananchi kwa kuwa mali zao zilipokonywa kwa nguvu na Nyerere. Sioni sababu yoyote ya kusherehekea hapa. Njaa ilianza muda si mfupi kwa kuwa uchumi ulisimama papo hapo na makampuni yakapunguza uzalishaji kwa kuwa viongozi walikuwa hawjui kuendesha biashara na pesa na wasomi wakakimbia nchi. Mwanzo wa umasikini wetu ulianza hapa. Wananchi wa leo, hatudanganywi tena.
ReplyDeletenakubaliana na mdau hapo juu,azimio la arusha ndo liloiuwa tz,na umasikini ukawa wa hli ya juu,hapa pia ndipo kenya ikatuwacha,watanzania wakawa mafukara,uchumi ukadidimia,ujama ndo umeiuwa tz na kufanya wengi wao kuwa mambumbumbu,brazo mzee ruksa,uliweza kubadilisha uchumi wa nchi kwa kipindi kifupi mno,kutoka kupanga line kununua sukari mpaka uchumi ulosimama.
ReplyDeleteanonymous Sun Apr 11, 03:49:00 AM
ReplyDeleteUnaongea usichokifahamu. Je umelisoma Azimio la Arusha? Ndiyo, yapo makosa yalifanyika katika utekelezaji wake na makosa hayo Mwalimu mwenyewe aliyakili na kutoa kijitabu cha TUJISAHIHISHE. Na akalitaja kosa kubwa miongoni mwayo kuwa ni ukosefu wa menejimenti nzuri. Makosa hayo yaweza kusahihishwa kwani mpaka leo tunaogelea katika bahari ya makosa yaleyale.
Sasa hoja si Azimio la Arusha, kosa ni utekelezaji wake. Bila Azimio la Arusha Tanzania isingekuwa na UTAIFA na huo ndio ukweli. Hivyo basi amani tunayojivunia isingekuwepo. Azimio linatufaa sasa zaidi ya wakati wowote katika historia ya nchi yetu. Ongeeni 'objectively' na si kulalama tu.
SI KWELI AZIMIO LA ARUSHA LILIKUWA LINAONEA WANANCHI NA LILINYANG'ANYA MALI ZA WANANCHI. 1967 MWANANCHI GANI ALIKUWA NA MALI YA KUNYANG'ANYWA? WALIONYANG'ANYWA MALI WALIKUWA WAGENI WENGI WAO WAKIWA WATU WA ULAYA LA ASIA NA WALIOJILIMBIKIZA MALI HIZI YA HATA KULIPA KODI SAHIHI KWA VILE HAKUKUWA NA UTARATIBU WA KUKUSANYA KODI SAWASAWA WAKATI WA UKOLONI, WAFANYA BIASHARA WAKUBWA WA ENZI HIZI WALIFANYA BIASHARA HUKO MAPORINI NA VIJIJINI YA BILA HATA SERIKALI KUU KUJUWA KUWA WAKO WANAFANYA BIASHARA NA KUJILIMBIKIZA UTAJIRI MKUBWA YA BILA KULIPA KODI NA KUWALIPA MIASHARASAHIHI WAFANYA KAZI WAO NA HII ILIPELEKEA WAO KUWA MATAJIRI WA KUTISHA, KAMA WALIFANYA SASA KWA NINI BAADA YA AZIMIO LA ARUSHA HAWAKUBAKI KUFANYA BIASHARA SAHIHI WAKILIPA KODI? NI KWA VILE SERIKALI ILIKUWA IMEAMUKA NA HAKUKUWA NA MWANYA TENA WA WAO KUNYONYA. SOMA VIZURI AZIMIO LA ARUSHA NA UTALIONA UZURI WAO, HAMNA HATA SEHEMU MOJA INAYOSISITIZA SERIKALI KUNYANG'ANYA MALI ZA MTU. LILIKUWA NI LA LAZIMA KWA WAKATI ULE ILI KUSUKUMA NCHI MBELE, NA KUTOKANA NA HILO WATU WENGI WALIONA NA HALI NZURI SASA WAMETOKANA NA HILO. NAJUWA WATOTO WADOGO WATASEMA SI KWELI KWA VILE WAMESHAKUTA WAZEE WAO WANA HALI NZURI AMBAYO ILITOKANA NA AZIMIO LA ARUSHA, IKIWA PAMOJA NA WAZEEE WAO KUSOMA BURE NA KUJENGA CAPITAL AMBAYO WATOTOWAO SASA INAWASAIDIA, KUIBUKA KWA WAFANYAKAZI NA WAFANYABIASHARA WAZAWA AMBAO BAADA YA AZIMIO LA ARUSHA WALIWEZA KWENDA BENKI YA KIZALENDO NA KUPATA HUDUMA YA PESA KWA BIASHARA ZAO KITU AMBACHO KABLA HAKIKUWEPO. SOMENI VIZURI AZIMIO LA ARUSHA KABLA YA KU-NEGATIVE, LISOME KAMA LILIVYOKUSUDIA NA SI KAMA WATU WALIVYOLITEKELEZA, KAMA WALITEKELEZA KINYUME NI UPUNGUFU WAO NA SI WA AZIMIO LA ARUSHA.
ReplyDelete