Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Maendeleo Dr. Komba (Mwenye mwamvuli) akijiandaa kumlaki Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samuel Sitta Chuo Kikuu cha University of Dar es salaam kampasi ya Mlimani leo kabla ya kuzindua rasmi mpango wa KUREJESHA MAADILI KWA WATUMISHI WA UMMA kwa lugha ya wenzetu Public Integrity Restoration Initiative (PIRI). Mpango unaanza na vijana 4000 wanaomaliza vyuo vikuu vya umma. Changamoto aliyoitoa ni kwamba mpango huu uenee vyuo binafsi, vya kati vinavyotoa vyeti na diploma maana huko pia kuna wahitimu wengi, lakini pia uenee kwa wote, hasa waliopo kwenye utumishi hivi sasa inapasa elimu hii ya maadili ya utumishi wa umma iwafikie.
Mh. Sitta akilakiwa
Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Yunus Mgaya akimuongoza Mgeni rasmi kuelekea ukumbini.
Waigizaji katika igizo la 'Maadili Company' lililomvutia mno mgeni rasmi kiasi
cha kukialika kundi hili la vijana wa Chuo kwenda mjengoni Dodoma ili waheshimiwa nao wapate ujumbe uliomo kwenye igizo.
Mh. Sitta akichati na wanafunzi wa UDSM
Mh. Sitta Katika picha ya pamoja na wanafunzi na wahadhiri baada ya uzinduzi







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...