CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR
Sanduku la Posta 146, Zanzibar - Tanzania
Simu: +255 24 2230724/2233337
Nukushi: +255 24 2233337
Barua pepe: registrar@suza.ac.tz
Tovuti: www.suza.ac.tz
Taasisi ya Elimu Endelevu ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) inatangaza nafasi za masomo ya IT Essential (Computer Hardware, Software na Networking).

Mwanafunzi atakayemaliza na kufaulu masomo hayo ambayo ni ya kimataifa atapata cheti kutoka CISCO Network Academy pamoja na kile cha Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Masomo yataanza tarehe 12 Aprili, 2010 na yataendelea kwa muda wa miezi mitatu (3). Muda wa masomo ni saa 8.00 mchana.

Sifa za Muombaji:
o Awe anaweza kusoma na kufahamu lugha ya Kiingereza.
o Awe anaelewa kutumia kompyuta pamoja na kutumia Internet.

Fomu za kujiunga na masomo haya zinapatikana katika Afisi ya Msarifu wa Chuo iliyopo katika Kampasi ya Vuga.

Pia Chuo kinawatangazia wale wote walioomba masomo ya Basic Librarianship kuwa masomo hayo yataanza tarehe 12 Aprili, 2010 na wanatakiwa wafike Chuo kukamilisha taratibu za masomo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ahsante kwa hili tangazo. Mimi nilikuwa natafuta mahali pa kusoma hii cisco.

    Ninachotaka kujuwa ni
    1.bei ya kozi hii.
    2. Niko bara jee mnaweza kunipatia mahali pa malazi?
    3. kama ndio ni kwa kiasi gani?
    4. kozi inaanza saa nane mchana, jee ni kwa masaa mangapi?
    5. kozi ni kwa miezi mitatu jee ni kwa siku ngapi katika wiki?

    ahsante sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...