Leo, Ijumaa, Aprili 9, 2010, takriban saa 9:05 alfajiri, kumetokea tetemeko dogo la ardhi ambalo kwa makisio yangu lilikuwa kwenye kipimo cha 0.05 cha Richter.
Nikiwa kwenye hoteli ya Aquiline, ghorofa ya 5, nilikuwa ninafanya kazi kwa ajili ya maandalizi ya maonesho ya Lighting Rural Tanzania Competition 2010 (tembelea tovuti ya Rural Energy Agency - http://www.rea.go.tz), kwani leo baadaye majaji 10 wa kimataifa watawatembelea washiriki wote wa shindano hili muhimu (mimi nikiwa mmojawapo, nikiwa mwakilishi wa FOPAD... Foundation for Promoting People's Awareness and Development ... http://www.fopadtz.org/viewpage.php?page_id=3), ili kuweza kuwapata washindi 10 kati ya 39 (jumla walikuwa 81, kwenye mchujo wa kwanza, wakabaki 40 kwenye mchujo wa pili, hatimaye wakabakia washiriki 39).
Hicho kipimo cha Richter ni makisio yangu tu, lakini wenzangu waliokuwa ghorofa ya 5 walisema walishuhudia mtikisiko mkubwa zaidi. Hata hivyo, nilichokishuhudia kilinitosha kurukwa na akili na kupata kiwewe, kama si wazimu wa muda, huku nikikurupuka kukimbia chini kabisa kwenye ngazi, mkononi nimechukua simu zangu mbili za kiganjani (Zain na Tigo), miwani ya kusomea, ufunguo wa chumba, na nimevaa viatu BILA SOKSI, kana kwamba vitu hivyo ndivyo vilivyokuwa muhimu zaidi maishani mwangu! Msahafu uliokuwapo kwenye sanduku langu NILIUSAHAU! Je, imani yangu ni ndogo kabisa?
Sikumbuki kama nilikumbuka kuomba dua, walau hata kusema Allahu Akbar, wala La Illaha Illallah! Astghafirullah! Mola anisamehe!
ILIKUWA TAFRANI!
Mpaka sasa sijalala, sijiamini tena kulala. Nilipofika chini niliwakuta akinadada waliopo zamu usiku wa leo pamoja na mdau mwenzetu, ambaye yeye alikuwa ghorofa ya saba, na alishuka ngazi hizo kwa kasi kubwa zaidi yangu.
Sasa najiuliza: Haya majengo ya ghorofa yamejengwa kwa kuzingatia viwango vinavyokidhi kinga dhidi ya maafa kama vile matetemeko ya ardhi, angalau kudhibiti ukubwa wa maafa pindi yanapotokea?
Kwa mawasiliano, 0715-019119 au 0786-019019.
SILALI! NAKESHA!
Simuombei mtu yeyote akumbane na hali niliyokutana nayo, kwani kama una moyo dhaifu unaweza kupatwa na ama kiharusi au mshtuko wa moyo na kuaga dunia papo hapo. Watu wengi walikuwa wamelala, mpaka sasa hawana habari ya kilichotokea.
Alhamdulillah! Mungu kweli ni Mkubwa! Asante Mungu kwa kutunusuru!
La Illah Illahllah, Muhammad Rasullulah!
Mimi mdau wako,

Aziz Mongi, safarini Arusha.
We Aziizi acha woga wa kitoto, siku yako ikifika utasalimu amri tu kwa GIBRIL.
ReplyDeleteSasa je lingekutokea ukiwa kwenye kiota kimojawapo cha maraha hapo A-Town na changudoa mkononi si ungehamia Maka kabisa.
Sasa ndio ujue kuwa Mungu yupo kweli na huo ni ushuhuda mdogo tu. Yale mambo "mengine" achana nayo na uimarishe ibada.
What are you really trying to say?? Tetemeko? Maonesho? kipimo cha Richter? Viwango vya majengo? Simu mbili? au mawasiliano yako?
ReplyDeletePole sana Aziz. Tunashukuru Mungu amewanusuru na Janga hilo baya mno sana sana. By the way tetememeko limekuchanganya kweli kweli mana umeongelea kama mambo kumi na mbili kwa wakati mmoja. Ooh! mara tamasha, Mara FODAP,mra majaji, mara walikuwa 10 sasa 39 sijui 81, Mara Zain,"thumni" sijui tigo, mara hapo hapo unataka tukufanyie tathmini kama Imani yako ni haba.......! Kweli tetemeko limekuchanganya kabisaaaaaaaa.......! Pole sana Aziz...1
ReplyDeleteNakushauri leo jioni mkimaliza Tamasha usiende Cocktail Party wewe nenda zako hotelini uoge maji ya vugu vugu pata msosi baada ya saa nzima ivi ukalale. Akili yako itatulia kama kawaida. Naomba dua tetemeko lisitukumbe hata sie tulioko mbali. Amen Nagira.
Mongi pole kwa yaliyokukuta, ila kwa kweli umenivunja mbavu zako, kwa story ulivyoipanga.
ReplyDeleteArusha na sehemu kubwa ya kaskazini ya TZ iko katika ukanda wa mtetemeko wa bonde la ufa. Kwa mujibu wa tovuti ya European-Mediterranean Seismological Centre, tetemeko hilo limetokea 02:57:41 hours (a.m.) (saa 9 kasoro dakika 3 usiku)9 April 2010 ni kiwango chake ni 4.7 katika mizani ya Richter na ilidumu kwa sekunde zisizozidi 10. Ilipiga kilomita 10 chini ya ardhi na episenta yake ni kiasi cha kilomita 170 kus/magh ya Arusha. Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wetu.
ReplyDeleteHii story kiboko.. unazungumzia tetemeko.. unazungumzia.. ghorofa refu.. unazungumzia.. mashindano na majaji... unazungumzia simu za mkononi... au?
ReplyDeleteAfu umekadiriaje hicho kipimo? una uzoefu gani wa matetemeko.. pengine ungetueleza kwa kirefu... du! Some Stories
TOTAL CONFUSED.POLE SANA
ReplyDeleteAsamehewe bure,alikurupuka kuandika haya yote akiwa bado kachanganyikiwa na tetemo,maana ni madudu tu(Simu zangu mbili??)Mengi yaliyomo hayatusaidii wasomaji.
ReplyDeleteAnko pole ila umetumia vipimo vya kichina kujua ukubwa wa tetemeko.
ReplyDeleteWewe Aziz wa UDSM miaka ya themanini?
ReplyDeleteHii story kama alivyosema mdau ina vikorokocho vingi mno kiasi huwezi kuamini ujumbe maalumu anaoutoa aziz! Labda uJaribu kufupisha useme majengo arusha hayana kiwango kizuri cha ujenzi - lakini uisimamie kauli yako hiyo.
duuuuuuuh we kiboko!
ReplyDeletehiyo style mpya ya matangazo yaliyo ktk mfumo wa story eh?
Kaka Aziz wewe mtu wa burudani mkubwa, nimekukubali.
ReplyDeleteIt's hilarious the way he put down his story.
ReplyDeleteAcheni kumsema huyu...hii imenichekesha sana
ReplyDeletePole nakumbuka Arusha tulikua tunamatetemeko sana nikiwa naishi huko...
Lakini ukishasikia haya matetemeko ya simu hizi yanayochopoka kila siku bikla mpango mimi ningejikuta nimeruka dirisha...
Pole Aziz.
ReplyDeleteStyle yako ya kusimulia matukio nimeipenda.
(US Blogger)
Labda nikusahihishe kuhusu vipimo vya tetemeko. Makadirio yako yako very wrong. tetemeko ili uweze kulisikia mtikisiko labda vipimo vya richerscale viwe zaidi ya 3 na umbali kutoka epicenter usiwe mkubwa na depth iwe ndoko. Kwa faida yake tetemeko lililotokea AR lilikuwa na vipimo vifuatavyo:
ReplyDeleteEarthquake Details
Magnitude 4.9
Date-Time Thursday, April 08, 2010 at 23:57:41 UTC
Friday, April 09, 2010 at 02:57:41 AM at epicenter
Time of Earthquake in other Time Zones
Location 4.106°S, 35.306°E
Depth 10 km (6.2 miles) set by location program
Region TANZANIA
Distances 170 km (105 miles) WSW of Arusha, Tanzania
Si unaona ulivyokosea richerscale 0.005 na ilikuwa 4.9 sijui hiyo na error au mistake.