Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Shamsi Mwangunga akimkakabidhi Restituta Joseph zawadi ya pesa taslim shilingi laki tatu baada ya kutwaa nafasi ya kwanza katika mbio za km 21 mkoani Arusha maalum kwa kuhamasisha jamii nchini kote kuendeleza vita dhidi ya adui wa taifa Malaria, kulia alieshikilia bahasha ya zawadi ya Laki 2 ni Mary Naali mshindi wa Pili na Neema Emanueli mshindi wa tatu Laki moja na Nusu.
mshindi wa kwanza Restituta Joseph akimalizia mbio za km 21 maalum kwa kuendeleza kupinga adui wa taifa Malaria (Tigo Ngorongoro Run half Marathon) zilizofanyika mkoani Arusha Karatu kwa lengo la kuunga mkono kampeni ya muheshimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Kikwete ya "Maleria haikubaliki" aliyoizindua mapema mwaka huu. Mbio hizo zilidhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo pamoja na Pepsi

Mshindi wa Pili Mery Naali akimalizia mbio za km 21 maalum kwa kuendeleza kupinga adui wa taifa Malaria (Tigo Ngorongoro Run half Marathon) zilizofanyika mkoani Arusha Karatu kwa lengo la kuunga mkono kampeni ya muheshimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Kikwete ya "Maleria haikubaliki" aliyoizindua mapema mwaka huu. Mbio hizo zilidhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo pamoja na Pepsi
Mshindi wa tatu Neema Emanuel akimalizia mbio za km 21
Kikundi maalum cha mkoani Arusha cha wairaq wakiwa na Timu ya Tigo Thumni walioshikilia gitaa wakitumbuiza kisha kuonyesha ishara ya kuikataa malaria kwa kusema Malaria haikubaliki wakati wa hafla maalum mara baada ya kumalizika kwa mbio za km 21 maalum kuunga mkono kampeni ya muheshimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Kikwete ya "Maleria haikubaliki" aliyoizindua mapema mwaka huu. Mbio hizo zilidhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo pamoja na Pepsi
Wanariadha 137 wavulana na wasichana 98 wakianza rasmi mbio za km 21 maalum kwa kuhamasisha jamii nchini kote kuendeleza vita dhidi ya adui wa taifa Malaria, mbio zinazojulikana kama Tigo Ngorongoro Run half Marathon) zilizofanyika mkoani Arusha Karatu kwa lengo la kuunga mkono kampeni ya muheshimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Kikwete ya "Maleria haikubaliki" aliyoizindua mapema mwaka huu. Mbio hizo zilidhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo pamoja na Pepsi

===============================

Serikali yawapongeza wawekezaji binafsi pamoja na wadau wa utalii Karatu Arusha kwa kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na kuendeleza harakati za kutokomeza Malaria kwa kudhamini mashindano maalumu ya riadha ya kilometa 21 yaliyofanyika Ngorongoro maalum kwa kuhamasisha jamii nchini kote kusema Malaria Haikubaliki kupitia michezo

akihutubia wananchi Wazizri kiongozo wa Serikali ya mapimduzi ya Zanzibar Mh Shamsi vuai Nahodha alisema " ninaomba niwashukuru na niwapongeze Tigo, Pepsi, Exim Bank, Zara Tours na wengine wote kwa uamuzi wenu wa kuunga mkono kampeni ya kuitokomeza malaria.

Najua wote tunafahamu mapema mwaka huu mheshimiwa raisi alizindua kampeni maalum ya Zinduka Malaria kaikubaliki" akiwa na dhamira ya kuagiza kuwa malaria itokomezwe

pia tufahamu Tanzania, mtu mmoja anakufa kwa malaria kila baada ya dakika 10 hivyo ninasababu ya kuwashukuru wadau, wadhamini na wanariadha wote kwa kushiriki katika mchezo huu wenye lengo la kuboresha Afya pamoja na kutoa elimu maalum jinsi ya kuitokomeza malaria

Pia ninaendelea kutoa wito nchi nzima tusiishie hapa, tufanye kama walivyofanya wenzetu wa karatu na wafadhili waendelee kuunga mkono jitihada hizo za wananchi.

Nae Ofisa Mauzo wa Kanda ya Kaskazini wa Tigo Joseph Mutalemwa alisema "Tigo Tanzani tumekuwa wadhami wakuu wa Tigo Ngorongoro Half Marathon (Race Against Malaria) kwa mfululizo wa miaka miwili sasa tukiwa na imani ya kwamba tunagusa sehemu mbili muhimu katika jamii ambazo ni muhimu kwa wateja wetu tunaowategemea

Kwanza kupitia udhamini huu tunahamasisha harakati za kutokomeza malaria ambayo yanaathari kubwa sana kwa kuoneza vifo vya wakina mama na watoto nchini pili tunaimarisha afya za washiriki wote wanaotoka sehemu mbalimbali nchini kushiriki mchezo huu.

Hivyo basi faida ya udhamini wetu kwenye Tigo Ngongoro Marathon kwa wananchi tunaowalenga ni kubwa sana na ndio maana tunaendelea kudhamini kila mwaka, ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuendeleza mashindano kila mwaka yaendelee kuwa na matokea na muelekeo mzuri zaidi

kwa upande wake muwakilishi wa WellShare International ambao ndio waratibu wa NGORONGORO MARATHON Bi. Jolene Mullins alisema "NGORONGORO MARATHON was initiated by WellShare International (formerly Minnesota International Health Volunteers (MIHV)) in 2008. WellShare International is a US-based non-governmental organization (NGO) funded by the United States Agency for International Development (USAID) and working in collaboration with the Government of Tanzania's Ministry of Health and Social Welfare and the Karatu District Council.

Through the support of the Tanzania Olympic Committee, attendance has grown from the first half marathon in 2008, to more than 250 international marathoners from East Africa, Somalia and the United States in 2009. The course, from the gates of Ngorongoro Crater to the center of Karatu Town, not only highlights the malaria pandemic but also the beauty of the northern circuit.

The time is now to focus the world on the health and development of Tanzania and the marathon provides us with a unique opportunity to make a difference.

In 2010, WellShare International is proud to have a TIGO as our primary sponsor again and we welcome the support of local and national members of the private sector including the Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA), the Karatu District Council, Zara Tours/Highview Hotel, A to Z Textiles, Exim Bank, Bougainvillea Lodge, Jubilee Tyres, Karatu Quality Garage, Octagon Hotel and FAME Medical.

Be a part of Tanzania's future, join us to make a difference!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ankal,

    Ingesaidia zaidi kama ungeweka na muda waliotumia hawa washindi.Muda ni data nyeti katika mashindano, ankal mbona unakuwa kama sio mwanaspoti?

    Asante kwa habari na hongereni washindi.

    (US Blogger)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...