Na Mohammed Mhina,
wa Jeshi la Polisi
DAR ES SALAAM IJUMAA APRILI 9, 2010.
Wataalamu na Wakuu wa Vitengo vya Kuzuia na Kupambana na Biashara haramu ya dawa za kulevya kwa nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika, watakutana Jijini Dar es Salaam kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na usafirishaji wa mihadarati Barani Afrika.
Msemaji Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini ASP Advera Senso, amesema kuwa, mkutano huo wa siku mbili utafunguliwa na Mkurugenzi wa Operesheni wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Paul Chagonja Jumatatu ijayo Aprili 12, 2010.
Amesema mkutano huo ambao utafanyikwe kwenye Hoteli ya Regency Park Mikocheni Jijini Dar es Salaam, utafunguliwa Saa 2.15 asubuhi.
Amesema kuwa pamoja na wajumbe wan chi za Maziwa Makuu na pembe ya Afrika, mkutano huo utahudhuriwa na wataalamu kutoka nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, nchi za Jumuiya za Falme za Kiarabu UAE na Pakistan.
Amezitaja nchi na mashirika ya Kimataifa yatakayohudhuria katika mkutano huo kuwa ni Nigeria, Ghana, na Makao Makuu ya Shirikisho la Polisi wa Kimataifa INTERPOL kutoka nchini Lyon Ufaransa na Nairobi inayohudumia nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika.
Nchi za maziwa makuu zitakazoshiriki katika mkutano huo ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya, Shelisheli, Sudani, Djiout, Eritrea, na wenyeji Tanzania.
Huo ni mkutano wa kwanza wa wataalam kufanyika kwa nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika na unafuatia azimio namba mbili la wakuu wa vitengo wa madawa ya kulevya kutoka nchi washiriki uliofanyika Cairo nchini Misri mwezi Julai mwaka jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. wananiwekea kiwingu tu,nitauza na kuvuta raha ya dunia, hii dunia sijui ni nini,madem,pombke,club yaani starehe zote wananiwekea usiku zinakatazwa,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...