Mshambuliaji wa timu ya Mwanza (kati) akijaribu kuwatoka wachezaji wa timu ya Arusha katika mchezo uliochezwa leo uwanja wa Uhuru jijini Dar.wadau wa TBL wakifuatilia kwa makini mtanange wa leo kati ya Arusha na Mwanza,ambapo Arusha imeweza kusonga mbele kwa hatua ya nusu fainali mara baada ya kuitungua timu ya Mwanza kwa mikwaju ya penati 6-5.


Mwanza wakiandika bao la pili dhidi ya Arusha katika mtanange uliomalizika jioni hii katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.mchezo ulikuwa ni mkali na wakuvutia kwa timu zote mbili huku kila mmoja akiwa na hamu ya kusonga mbele.

Golikipa wa timu ya Mwanza akiusindikiza kwa macho mpira ulioingia moja kwa moja wavuni mara baada ya kupigwa na mchezaji wa Arusha,Bakati Kibodeko na kufanya matokeo yawe ni 2-2 mpaka dakika tisini zilivyogota na hatimae kuamriwa kupigwa kwa penati tano tano ambazo zilipigwa .
beki hasifiwagi.
wachezaji wa timu ya Arusha wakishangilia ushindi walioupata leo dhidi ya timu ya Mwanza baada ya kupata ushindi wa mabao 6 - 5 (penati) katika mtanange uliomalizika jioni hii ndani ya dimba la Uhuru a.k.a shambani kwa bibi.matokeo hayo yameifanya timu ya arusha kusonga mbele kwa hatua nyingine ya nusu fainali ambapo watacheza na timu ya Singida ambao wameweza kuwatoa katika mashindano hayo timu ya Temeke kwa mabao 3-2 katika mchezo wa awali uliochezwa leo hii katika uwanja huo huo wa Uhuru.
Timu ya Arusha ikipiga dua mara baada ya mchezo kumalizika leo shambani kwa bibi.kesho kuna mechi zingine kali ambapo timu ya Ilala itamenyana na Iringa na baadae timu ya Kilimanjaro itamenyana na Lindi katika hatua hiyo ya robo fainali ya Kili Taifa Cup.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2010

    Tatizo mpira wa Tanzania umeshakuwa Islamised mno, Utaona mara dua mara wachezaji wamelishwa yamini mara sijui arbadili imesomwa, Yaani vituko vitupu mwisho ya yote huwa kupigwa bao tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2010

    wacha chuki wewe mtoa comment wa kwanza....huoni wachezaji hata wa bongo na ulaya wanaweka alama ya msalaba kila leo zaidi ya waislam.Inaonekana una chuki na dini ya kiislam unataka kuona watu wanaomba kikristo tu lakini hutaki kuona waislam pia wana exercise rights zao.U r just a hater.Michuzi usinibanie hii comment.Watu wengine wanauzi sana.Sweden.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2010

    Mtowa maoni wa mwanzo, hebu toka hapa! unaangalia mechi gani wewe? unaishi kwenye pango gani hata huoni yanayotokea duniani?

    Wachezaji mpira sehemu zote duniani wanaonekana wakibusu viwanja kabla ya kuanza kucheza, wanafanya alama ya cross na wengine wanavua jazi na kuonyesha fulana za ndani zenye maneno kama jesus, jusus loves you, i belong to jessu na mengineyo, jee hiyo unasemaje?

    Wacha chuki binafsi, kutafuta kulaumu watu au dini nyengine kwa matatizo yako ni ujinga wa mwisho.

    Eti tanzania mpira umeshuka, twambie ni lini mpira wa tanzania ulipokuwa juu? ni mwaka gani tanzania walicheza katika kombe la dunia? mwaka gani tanzania walishinda kombe la afrika? ni lini mara ya mwisho kusikia jina la mchezaji wa kitanzania akisifika na kujulikana duniani kote kwa uhodari wake? nchi tele za kiafrika zina watoto wao wanacheza mpira wa kulipwa katika ligi kubwa duniani na ni maarufu na wanajulikana, ni mwaka gani tanzania tulikuwa na wachezaji kama hao?

    Wewe baki tu na chuki zako, ukweli ukatae.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2010

    Kwani hiyo timu ya Arusha ni ya waislam watupu? Inasikitisha sana kuona vituko kama hivi dini mkafanye huko misikitini.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2010

    wewe mdau wa Tue May 25, 03:39:00 PM, hivi kumbe inauma sana ukiona waislamu wanaomba kwa mola wao enhe? lakini ni sawa wakiristu wakiomba au vipi?

    Naona unauliza suali kama wapo wakiristu katika hiyo timu kuna aliyelazimishwa kuinua mikono hapo?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2010

    anon wa Tue May 25, 03:39:00 PM, fumbua macho uelimike, wacha chuki hizo? wachezaji kuomba au kushukuru mungu wanaemuamini ni jambo la kawaida kwenye futiboli duniani kote. sasa kwa nini waislamu wasifanye uwanjani wafanyavyo wenye dini nyengine?

    Hivi wewe hapo ulipo unapata nafasi ya kuona mechi za nje? hivi hujawahi kuona wachezaji wakibusu misalaba yao au kufanya ishara ya cross kwenye mechi?

    Unauliza kama hiyo timu ni ya waislamu peke yao, jawabu huenda ni ndio na kama wako wasiowaislamu labda wako dhaifu na imani zao na ndio wakaona waungane na waislamu katika kuomba kwa dini yao, sioni bastola kwenye kichwa cha mtu yeyote kwenye picha, kwa hivyo ni uhakika hawakulazimishwa na mtu kuungana na kuomba dua.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 25, 2010

    aste aste jamani, punguzeni jazba! kwanza mumeaje kama wanaomba dua kiislamu hapo? jee ni kwa sababu wameinua migkono? mbona hamuoni kama wengine wamepiga goti? kwani waislamu au ni wakiristu ndio wanaomba kwa kupiga magoti, tena kuna mmoja amefunga mikono (viganja vyake). Sisemi kama hawa ni waislamu au wakiristu ninachosema ni kuwa msiruke tu na kuanza kucritise watu bila kujua details zote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...