Home
Unlabelled
burudani ya enzi hizo...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Nchi inajaribu kuhakikisha kila mtu anaongea KISWAHILI wewe ndo kwanza unafagilia jinsi ulivyosoma ENGLISH!!!???. taaaaaaabu kwelikweli!!!
ReplyDeleteHii nimeipenda, nimekumbuka mbali sana. pia Tintin, Snow, Captain Huddock. Then Astericks... wakati umeenda wapi?. Kwa Tanzania Chakumbanga, Harakati za Pimbi, Ndumlakuwili, kipepe. Lakini nakubaliana na utafiti kwamba usomaji unapungua.
ReplyDeleteIka
Kaka si utani lazima jamii ikushukuru kwa hii blog inayotukumbusha enzi zile za zamani.Wasiokuwepo nzi hizo watadhihaki lakini lazima tukubali hii blog inatukumbushia jamani.Spear ni kweli alitufunza wengi.Wakati huo hatukuwa na TV na viodeo au hata hizi mobile phones na i-phones za sikuhizi.
ReplyDeletejamani nyie vijana wa leo lazima tukubali kuwa kuwa YOU CANNOT DENY THE HISTORY.Also you cannot say no to somebodies experience.
Mungu mbariki Issa Michuzi na pia wale wooooote watoao mimchango yao katika hii blog.
Ndugu yangu kweli wewe mtungu nilikua naulizia sana kuhusu magazeti haya.spear na zolo.boom.bila kusahau Film Tanzania. ya Faraji Katarambula.Na mengineyo.Fukua hazina hiyo tukumbushe zamani.KC OTHMAN IN LONDON
ReplyDeleteHapo ni Lance Spearman na Captain Victor we acha ilikuwa kosa kukosa toleo la kila wiki. Mheshmiwa Katalambula akaanzisha Film Tanzania ambapo tulimwona Mzee Kipara Live baada ya kuwa tunamsikia kwenye michezo ya redio tu
ReplyDeleteHuyo 'Spear' alitokea kule Nigeria,tena basi tulikuwa tukipata majarida hayo kila wiki na tukisubiri kwa hamu kubwa...ahh enzi hizo huzipati tena yakhe...good old days!!!
ReplyDeleteNa za yule Freddy Sengo mpelelezi mashuhuri hebu tutafutie
ReplyDeleteWewe anon. Thu May 13, 11:21:00 PM, nadhani umeelewa vibaya (sina ubaya katika hili). Ni sawa tuzungumze Kiswahili, lakini katika hii dunia ya leo ni sawa kweli kukiweka Kiingereza kapuni? Unaweza kuzuia kwa nguvu zako zote mwanao au wanao wasijifunze Kiingereza bali Kiswahili pekee (labda pia na kiluga)?
ReplyDeletewewe ano wa kwanza ninafikiri umesoma lakini hujui english. na kama hujui hiyo lugha shule ziko nyingi zinazo fundisha english hapa nchini. jua kwamba wakenya, waganda etc wanaajiriwa hapa tanzania na makampuni ya kigeni kwasababu watanzania hawajui english. kujua lugha tofauti hakuna ubsya. siku hizi hata wachina wanajifunza english na lugha nyingine ili waweze kufanya biashara nchi za nje. anyway soon watanzia wengi watajua kingereza vizuri na wataweza kushindana na hao foreigners. do something don't be left out.
ReplyDeleteMichuzi umenikumbusha mbali sana enzi hizo, my favorite was gazeti gani sijui hadithi ilikua ya Lawalawa Tabora, aliyechanganya barua kwa mume na kwa mpenzi! that was a smash for me! Pia hadithi ya Diana Kiboko, msichana mzuri sana, badae kitabu chake kikatoka mwandishi Kajubi Mukajanga-the best!
ReplyDeleteKweli kienglish ndiyo chenyewe si kufagilia tu, nipo nje mwaka wa pili kimasomo, yaani wanafunzi toka sudan , yemen na nyinginezo ambao atufagilii kienglish nchini kwetu, ni matatizo sana, wenzetu wanigeria hawatumii nguvu kusoma na wanafanya vizuri class, sisi tunasumbuka kukariri tu, wasudan na wengine wanaanza kujifunza english toka A to Z atleast mie ninacho cha secondary, sikulazimishwa kujifunza lugha kwanza, kiinglish kiachwe na kiendelezwe, wanaotaka kukiondoa wanakijua vizuri, mnataka tusain mikataba tusiyoielewa?
ReplyDeleteBillions of blue blistering bunnacos!!!!!!
ReplyDeleteWewe ng'ang'ania KISWAHILI wakati umekumbatia UTANDAWAZI halafu nini kitatokea, utaachwa solemba ubaki na uswahili wako, ni ushamba kudhani Kiswahili kinaweza kuwa mbadala wa Kiingereza katika hali ya Ulimwengu kwa sasa, Watanzania wanatakiwa kujifunza si tu Kiingereza bali pia lugha kubwa za dunia ambazo zimesheheni maarifa na teknolojia ili tupate maendeleo. Mpaka leo ukienda Urusi au Cuba ukiwa na nia ya kujifunza taaluma fulani unatakiwa kwanza ujifunze lugha itakayotumika kukufikishia ujumbe. Taabu iko wapi au una wivu wewe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHAO WANAO JIDAI KUFAGILIA KISWAHILI MBONA NACHO HAMKIJUI MNAFELI! HEBU SOMA WANAO TUMA MAONI UONE MAKOSA YA MATAMSHI YANAYOANDIKWA, MANEANO KAMA HUDHUNI HUANDIKWA HUZUNI, DHAHABU ZAHABU MPIRA MPILA NA MENGINEO MENGI TU NA HALI HII IPO MPAKA KWA VIONGOZI NA WASOMI WETU! HATA HAO WAINGEREZA WALIPOKUJA HAPA WALIJIFUNZA KISWAHILI NA NILAZIMA MTU UJUE LUGHA MBILI ZA KIMATAIFA HII HAINA UBISHI LABDA TU KAMA ULIKIMBIA DARASA UKAENDA KUKAA BANDARINI UKISUBIRI MELI KUZAMIA, LAKINI NAKO UKIFANIKIWA LAZIMA UTAJIKUTA UNAJIFUNZA LUGHA YA HUKO UENDAKO HILI HALINA UBISHI PIA.
ReplyDeleteUUMZUNGUMZIAPO SPEAR LAZIMA UMKUMBUKE NA ZORRO.
Nakumbuka enzi hizo mnaazimana haya majarida ya picha na kusema kweli sio tu kuelewa lugha lakini yalikuwa pia yanazoesha tabia ya kusoma. Hao wanaofagilia Kiswahili juu ya lugha ya Kiingereza au yeyote nyingine wataje basi ni vitabu vingapi vilivyoandikwa na Eric Shogongo tuseme na je wameyasoma yote? Hoja sio lugha, hoja utamaduni wa kusoma. Kwa msomi yeyote kadri unavyojua lugha nyingi ndio unavyojijengea nafasi nzuri ya kujiendeleza katika maisha ya sasa. Kiswahili hakifi leo wala kesho, haileti maana ku treat lugha yetu kama it is facing extinction. Watanzania tuwe na tabia ya kuhoji vitu sio kukubali mtakayoambia na waendesha mambo.
ReplyDeletemimi sichangii ila naenda kuiba kwenye storage ya baba. nadhani nitayakuta nami nipate huo uhondo mliokuwa-ga nao mwaka 47. then was then bwana!
ReplyDeleteMichuzi umenikumbusha mbali sana maana mie binafsi Mzee alikuwa na jitihada kubwa ya kutununulia magazeti kila aina hasa hizi Comics Beezer,Dandy,Beeno, Topaz, Archie halafu kuna kitabu cha hadithi za Kipelelezi za kina Willy Gamba
ReplyDeleteDuuh! What a nostalgie.. Lance Spearman and Captain Victor on the move (dRU)
ReplyDeleteWee anonymous wa Fri May 14, 09:43:00 AM, unaowarekebisha wenzio kiswahili, Aliyekwambia HUDHUNI ni kiswahili sanifu nani?? Huzuni ndio sahihi kwa taarifa yako. Ebo!
ReplyDeleteDu Mithupu , mie leo nina umri wa miaka 53 lakini hii picha inanirudisha nilipokuwa darasa la 4 hadi la saba,Chang'ombe.
ReplyDeleteUkikosa toleo la "Spear" miaka hiyo na mwenziwe " Zolo" ilikuwa huli wala hulali mpaka umelipata.
Miaka hiyo ni 1965-1970.
Lilikuwa burudani tosha kabisa na gazeti dada na hilio lilikuwa "Fearless Fang", jamaa la kibantu la miraba minne.
EE bwana kumbe utoto wetu ulikuwa mtamu.
jamani kweli mmenikumbusha mbali sisi haya magazeti ya Tintin na Novels tulikuwa tuna ya pata pale maeneo ya mnara wa DTV kulikuwa kuna duka flan lina supply. Dooooh long time! thanks Michuzi umetukumbusha mbali
ReplyDeletewadau, miaka gani hii? Mbona sikumbuki mimi? Au ni kwa vijana wa zamani tu?
ReplyDeletewe mdau wa12:50PM
ReplyDeletemwenzio amepatia sana tuuu ni HUDHUNI na sio huzuni acha kunyumbulisha mambo we ndiyo umeboronga
fisadi kiwembe
Aloo, anony mmoja hapo juu - Spear alitokea Nigeria???? He was Kenyan, mazee! Anyway, nakumbuka tukiwa sekondari kule Mkuu, Rombo, inasemekana baada ya franchise hiyo kufa, Spear alikuja ingia maisha ya shida sana na eti akawa mwizi wa magari enzi zile kule Tarakea, Mkuu, Loitoktok, Taveta etc, akiiba tokea Nairobi na Mombasa na kupitisha kuingia Tanzania katika sehemu hizo.
ReplyDeleteBTW, kuna character mmoja wa ki Jemz Bondi hivi yuko online akitokea hukohuko Kenya - mmemuona?
Kwa wale msiojua. Mtunzi wa mpelelezi Willy Gamba alikuwa Rais mstaafu wa Tanzania Commerce, Industrial and Agricultural Association, mzee Evans Musiba. It was a good book jamani.
ReplyDeleteNi huzuni sio hudhuni (hudhuni sio neno la Kiswahili, unless linamaanisha zana ya kijambazi).
ReplyDeleteWe nayejiita fisadi kiwembe ni kweli ni fisadi wa mawazo kiduuchu!!! Ha ha ha haaaa, HUDHUNI? Kiswahili gani! "xxxxx''''@@@@xcnchwiiii!!!
ReplyDeleteJuu ya yote, Mkuu umenikumbusha mbali sana. Spear?? Yaani haya magazeti tulikuwa tunaazimana kila wiki, usipolisoma wewe sio mjanja.
Guys, sorry to write in English. I am writing from Germany and am originally from India. In my youth, i have had chance to read lots of books on Lance Spearman, and was very great fan of those books. Lance Spearman, Captain Victor, Lemmy (the cunning boy who helped Lance), his girlfriend (was it Sonia?), etc.. I also remember there were two different actors playing Lance Spearman..
ReplyDeleteAny idea if one gets these comics to read again anywhere?