





Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Duh!! Halafu kesho kazini?
ReplyDeleteNakumbuka kulikuwa na ule msemo kuwa Jumatatu na Jumanne sehemu za kazi ni kuzungumzia wikiendi iliyopita, JUMATANO ndio kazi, Alhamis na Ijumaa ni kujiandaa na wikiendi. Sasa kama na Jumatano (ambayo ndio siku pekee ambayo yasemekana tulikuwa ukifanya kazi imechukuliwa na Bills) sijui tunaelekea wapi.
Kwanza pole kwa wale walopata mshituko kutokana na tukio hili na tunamshukuru Mungu kuwanusuru ndugu zetu na pengine janga ambalo tungekuwa tunazungumza vingine kwa sasa.
ReplyDeleteNashawishika kuuliza Je hapa Nyumbani TZ kuna utaratibu wa kukagua vifaa vinavyotumia umeme baada ya muda gani ili kuonyesha vinatakiwa kufanyiwa ukarabati(service) ndani/baada ya muda gani? au tunatumia tu vyombo hivi mpk vikilipuka kama hivi ndo tunajua vimezeeka?Hii ikiwa kwenye majumba yetu na majumba ya starehe, Je kuna mamlaka yeyote inayohusika na jambo hili?
Na Je kuna busara gani katika swala la askari Polisi kuwa na nguo za kiraia huku wakiwa na silaha zinazo onekana kama ninavyo ona hapo pichani? je hii haituweki katika hatari yeyote ya kiusalama?
Askari polisi kutovaa uniform na kukamata SMG haipendezi hata kidogo.
ReplyDeleteKwa nini wasivae uniform iwe kama wamejitambulisha?Likishika jambazi hapo na silaha za moto tutajuaje nani jambazi na nani askari?
(US Blogger)
Watu kumbe mnaogopa kufa, lakin hamugopi kumkera mungu, Huo ulikuwa ukumbusho kwenu msijisahau kila siku Club.
ReplyDeleteWachina watatumaliza nchi zima wapate pa kuhamia!Wanetu maziwa yenye kimikali, sie wenyewe TV zenye kulipuka na vingine hatujui wanatuwekea kwenye nini!
ReplyDeleteSijui hata tujipatie ushauri gani? Used electronics yale yale, kuacha kuangalia Luninga hatuwezi!
yaani wabongo kaazi kweli kweli , yaani bado wanataka kurudi ndani na kuendelea ? yaani siamini, wanajali sana sterehe kuliko maisha yao , wewe ushaona kuna moto umefanikiwa kuzimwa kwanini usiende kulala kwako ? bado unataka kurudi , je lingekuwa bomu dogo limelipuka sasa bomu kubwa linafatia ? hehehehe mungu atawasidia na akili zenu..
ReplyDeletemdau
USA
sasa hao askari na vipensi jamani tutawatofautisha vipi na majambazi? kweli ukisimamishwa na hao si utakimbia tu wakupige wasingizie wewe ni jambazi ulikuwa unawakimbia!!!
ReplyDeletepolisi hawataki kuchafua uniform zao, tabu kuzifua, yaani kaazi kweli kweli.. mimi nitafurahi na polisi IKIBINAFSISHWA....
ReplyDeleteBONGO TAMBARALE....
Naifu hapo juu umenichekesha kweli , eti kama kuna utaratibu bongo wa kuangalia vifaa vya umeme muda hadi muda ,, hehehehe AFYA ZAO HAWAANGALII MUDA KWA MUDA WATAANGALIA VITU VYA UMEME..!!!
ReplyDeletekaazi kweli kweli...
kila mtu alikuwa akihuDHunika, tanzania darasa bovu kiswahili tunafeli hata kiingilishi pia!
ReplyDeleteWadau wote mnaolishikia bango suala la Uniform kwa polisi mpo sahihi 100%. Hapo kuna hatari kuu mbili, moja kwa raia na ingine kwa polisi wenyewe.
ReplyDelete1. Tukianzia kwa wananchi wenyewe ni kweli kabisa inakuwa vigumu kutambua kuwa anayekusimamisha ni polisi halali au jambazi anataka kukupora na hivyo kukuweka katika mtihani mgumu sana, mfani ni yule Tax driver aliyeuwawa kule kimara suka baada ya kusimamishwa na polisi wasiokuwa na uniform akadhani ni majambazi na hivyo kukanyaga mafuta huku polisi nao wakidhani jambazi na kummiminia risasi na kumuua. Kitambulisho pekee cha polisi kwa raia ni uniform zao, na si vinginevyo
2. upande wa polisi wao pia wanakuwa katika risk kubwa hasa pale inapotokea kuwa wanapambana na majambazi na kuomba msaada either wa helicopter au polisi wengine ambao hawafahamiani nao na hivyo kufanya tukio kuwa gumu kwa wasaidizi kwani hawajui jambazi na polisi ni yupi. Pia hapo wanaonekana hawana hata bullet proof kitu ambacho kinaweka maisha yao katika risk kubwa sana
Sikatai askari kanzu ni muhimu hasa pale wanapofuatilia jambo na wao wasigundulike na mfuatiliwa lakini hawa wawe na silaha zilizofichwa kama bastola na wakati huo huo kikosi cha polisi wenye uniform na silaha kinakuwa alerted pindi vurugu ikianza.
Style hii ya kutokuwa na uniform inawafanya hawa polisi wakati mwingine kufanya ujambazi wao wenyewe kwa kuwa hakuna atakayejua kuwa ujamabazi umefanywa na polisi pia namba zao ambazo huvaliwa kwenye uniform zinakuwa haizjulikani.
Mimi ningekuwa waziri wa polisi au mkuu wa polisi basi taratibu kuu ingekuwa bila uniform haupo kazini, uniform ni lazima, mbona askari jeshi wanapigana vita huku wamevaa uniform?
Jamani Jamani!
ReplyDeleteHii mioto kwenye maukumbi ya Disko vipi jamani? MAISHA club nayo si iliungua siku za hivi karibuni tu?
Sio bure. Kuna mikono ya watu hapo.
Nawashauri waende NGENDE wakaangalie hilo
nauliza tu jee kisheria mbali na body gurds askari polisi au jeshi anaruhusiwa kuwa na smg au bastola uraiani akiwa hana magwanda yake?
ReplyDeleteJe utamtambuaje kama huyo ni askari/jeshi? si hapa tunawapa idea majambazi?
WABONGO BWANA....SASA WEWE UNAWEZA KUMILIKI CLUB BILICANAS HALAFU TENA UNANUNUA TV ZA CHINA....SASA CLUB INGEUNGUA UNGEPATA FAIDA GANI...SHULE MUHIMU SANA JAMANI....BONGO ZERO
ReplyDeletewewe mtoa maoni KILO hapo juu , akili zako ziko KILO moja nini ? una hakika gani kwamba tv zao zilikuwa feki ? uliwanunulia ? kwani tv original ndo hailipuki ?
ReplyDeletehuna cha kuongea nyamaza
nimekusamehe nilivyoona jina lako..
mdau
kariakoo
Najiulzia hivi hizo emergency exits zinakau openi au ndio yale yae zina fungwa na siku ya tukio watu wankua trapped?
ReplyDeleteHivi nyinyi mnaojidai kukandia kwanini hamuulizi kabla zaii ya kushambulia na kukandia?Eti polisi na nguo za kiraia.Hao kazi ya ni kuzunguka huku na huko kuangalia ulinzi wa raia,wanakuwa na Land rover 110,huwa hawavai uniforms,wao wanavaa kiraia.Sasa cha ajabu ni nini km walikuwa kwenye patrol na wakakuta tukio hapo?mbona wakienda kwenye maeneo mengine kwenye vurugu,au wanapoenda kupambana na uhalifu hamuulizi uniform?au kwakuwa ni Bills?au ndo hizo picha za mitaa mingine hamzipati.Acheni kujidai nyinyi..
ReplyDeletepoleni jamani ; ila sipati picha hilo sokombinde lake uwiiiiiiiiiii
ReplyDeleteWadau hao ni Askari wa Upelelezi na wako zamu! kwa kawaida wanaitwa PATROL! wakati wote wako na silaha, hawahitaji kurudi kituoni kuchukua silaha. Wepesi kureact kwenye tukio! Kwa taarifa tu, msipende kila kitu kucomment negatively!
ReplyDelete