Mwanamuziki maarufu toka nchini Marekani,Sean Kingston akiwa na Mkurugenzi wa masoko wa TBL,David Minja (kulia) pamoja na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe (pili kushoto) wakitokea ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere usiku huu.
Mwanamuziki maarufu toka nchini Marekani,Sean Kingston (pili kulia) akiongozana na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe (kati) kutelekea katika gari iliyokuwa imeandaliwa rasmi kwaajili yake wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere usiku huu.
Sean Kingston akiingia katika gari lililokuwa limeandaliwa kwa ajili yake.
baadhi ya wanamuziki walioongozana na Sean Kingston wakielekea katika usafiri walioandaliwa.baadi ya wadau waliofika katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha JK Nyerere kwaajili ya kumpokea Mwanamuziki wa Kimarekani mwenye asili ya Jamaica,Sean Kingstone pamoja na timu yake ambao wamewasili usiku huu na ndege ya shirika la KLM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2010

    Kwamba kutoka na mito ya shingo mpaka nje ni Style, Ubrazamen au Ushamba, Hebu nisaidieni, maana huyu jamaa namlinganisha na wale wanaotembea na blue tooth peace kwenye masikio yao hata kama hawaongie na simu!!!!
    MTAJIJU!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2010

    Mi naona BP tu kwa huyu kijana. aonyeshe mfano mzuri kwa watu wa huko, kwa kuanza zoezi kali. Jamaa bado mdogo sana huyu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 13, 2010

    Nimezoea kuona Joseph kusaga ndio anawaleta wanamuziki ila haya tena naona na watu wengine wa bia nao wanajitahidi.

    Wakina dada msijirushe tu kwa huyu jamaa wanamuziki huwa hawana mpango. Mtaachwa salenda (kama bado ipo).

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 13, 2010

    WATANZANIA TUMEROGWA! TUNAPENDA SANA BURUDANI NA STAREHE KULIKO UZALISHAJI MALI NA SHGHULI ZA MAENDELEO. KILA SIKU TUNASIKIA MATANGAZO YA MATAMASHA, MASHEREHE, UTOAJI TUZO, WANAMUZIKI WA NJE KUALIKWA...SIO KWA WAJASIRIAMALI,WASOMI AU WANASAYANSI WAGUNDUZI, MADAKTARI BINGWA N.K..BALI KWA WANAMUZIKI, WANAMICHEZO, WASANII NA VITU KAMA HIVYO. VIPI UWEKEZAJI HUU WA MAKAMPUNI KAMA HAYA UNGELENGA ZAIDI HUDUMA ZA JAMII, ELIMU, AFYA, SEKTA ZA KIUCHUMI KAMA KILIMO, VIWANDA, BIASHARA..PIGA HESABU FEDHA UNAZOTUMIA KUNYWA POMBE, KUJIRUSHA KWENYE KUMBI ZA STAREHE KILA W/END NA SIKUKUU, KUCHANGIA MASHEREHE KAMA HARUSI MPAKA KITCHEN PARTY, IMAGINE HELA HIYO UNGEWEKEZA AU KU-SAVE, UKAJIONGEZEA ELIMU, UKAFUNGUA BIASHARA N.K NA KILA MTZ ANGEKUWA NA MTAZAMO HUO!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 13, 2010

    annon 8:49am,,,izo ni akili za mtu binafsi na mtazamo wake.watu tumejisahau sana na izi starehe kila kukicha shindano sijui la suruali la nchi gani!!
    kheee muwe na kiasi mjiendeleze wandugu na jamaa zenu kule vijijini

    uwa sielewi kabisa hii tabia "mpya"

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2010

    cheki huyo baunsa upande wa kulia, ndio mkubwa kuliko mabaunsa wote tanzania lakini kwa sean kingston yuko kama piriton, kazi kubeba minondo bila msosi...tehetehetehe

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2010

    tehe tehe tehhe uwiiiiii, jamani mbavu zanguuu zinauma kwa kucheka, BAUNSA KAMA PIRITON !!! yaani raha kweli humu MICHUZI , tunasahau matatizo kwa muda tukiingia humu....na pia nimecheka huyo mwanamuziki alivokuwa kibopa ( mnene ) jamani afanye mazoezi atapendeza zaidi

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2010

    ha ha ha,maoni mbavu sina,eti kama Piriton,huyo ndo baunsa wetu jamani mwacheni,
    Na hao warembo ndo wazuri kweli ha ha,Hapa kwetu mtu lazima ajichubue au poda mpaka ukuchani,ndo awe mzuri,Stay Black Stay Beauty,Wenzenu Ulaya wanapambana na Solarium,watu wanataka kuwa wabrown,watazame masuper starz wa Bongo-walipoanza sanaa walikua weusi tii na wazuri sasa mpaka wanatia kinyaa,

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2010

    Uwelewa wa jambo ni kitu bora katika maisha ya kila siku ya mwanadamu,hakuna mtu yoyote hapa duniani asiye penda starehe.unafanya starehe wanasave hela zao kwa maendeleo yao.Pia wameenda shule vilevile na maisha ya mtu hayapangwi na mtu mwingine.TBL big sana katika tamasha lenu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2010

    hahahaaa mbavuuuuuu zangu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...