Hiyo ilikuwa siku moja kabla ya uchaguzi 1995, tukiwa airport Songea ili kuwahi mkutano wa mwisho Dar es Salaam pale Jangwani. Anayempiga MWalimu Konozzzz ni kaka Saidi Msonda wakati huo akiwa mwandishi wa Uhuru na Mzalendo na sasa yuko Umoja wa Mataifa huko Sudan, nyuma ni kaka Kenan Mhaiki aliekuwa pilot wa ndege tuliyokuwa tunasafiria.
Shoto ni mdau John Kitime mleta taswira hii ambaye wakati huo alikuwa fundi mitambo wa vipaza sauti vya kampeni ya Mwalimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2010

    Du! Kumbe kuna watu walimzoea mwalimu kiasi hiki!

    Kitime naye kumbe katoka mbali?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2010

    jamani! Mwalimu kumbe alikuwa na watu aliowapenda na kuwa nao karibu namna hii, nimeipenda hii picha, na nawahauri wenye nayo waitunze kwa ajili ya kumbukumbu, mwalimu was a simple and a good friend, hadi pozi la kuwekewa mkono begani, yeye hakujikweza pamoja na kuwa baba wa taifa. Mfano wa kuigwa, Mungu ampe raha ya milele.

    ReplyDelete
  3. Haji DrogbaMay 13, 2010

    DU!KWELI TUNAKUKUMBUKA JULIUS,WATANZANIA WAKO TUNAKULILIA MPAKA LEO,MBELE YAKO NYUMA YETU MWALIMU ULIETUACHIA UTAJIRI WA HEKIMA NA BUSARA,HAKIKA ALIPANGALO MOLA HALIPINGIKI ILIOBAKI TUMWACHIA YEYE.MUNGU AKULAZE PAHALA PANAPOFAA JULIUS WETU MTU WA WATU.AMEN

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 13, 2010

    YEAH ! HII NI KUMBUKUMBU NZURI SANA KWA MTU MASHUHURI KAMA HUYU JULIUS NYERERE.Mzushi

    ReplyDelete
  5. Lakini kama watu wanashangaa kumuona Mwalimu akiwa friendly yaonesha kuwa friendly haikuwa kitu cha kawaida kwake.

    Na kwa vile wakati wa utawaala wake kulikuwa hakuna uhuru wa kupata na kutoa habari yathibitisha kuwa hakuwa friendly.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2010

    Jamani asante sana Mdau uliyepost hii photo. Imefanya siku yangu iwe nzuri. Nilikuwa na stress zangu za kazi, lakini nikaona ngoja nifungue blog ya jamii, maana ndo njia yangu pia ya ku-relax. Lakini kwa kweli nimefarijiwa sana na hii picha, mungu akubariki michuzi kwa kazi nzuri. Na hongera kwa kuwa na network na watu wengi, ndo mana unaweza kupata picha kama hizi. Kitime tafadhari share with us na nyingine ulizo nazo (za mwalimu).

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2010

    acheni kusifia ujinga,mwalimu japo alituunganisha,lakini yeye ndo chanzo cha umasikini tanzania,aliondoka madarakani uchumi hoi,watu mlo mmoja kwa siku,tena ugali wa njano,kupanga mstari ka sukari,alafu baadae akatuchagulia mkapa kwa lazima akaja kutuchukulia madini yenu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2010

    We anoy wa Mat 13,11:11:00 AM ni mtu wa ajabu sana hivi hujui kwamba hakuna mtu aliekuwa na upendo na nchi yake na watu wake kama J.K.Nyerere nakushangaa kuandika kitu kama hichi hata nyie wazanzibari vitu vingi mnafaidika kwa sababu ya sera za Mwalimu na Karume kama unabisha nitafute nikupe shile .
    Pole sana.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2010

    Kila mtu anamapungufu yake lakini tupime kulinganisha na mema yake

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2010

    Nadhani hii picha ndio ilompatia kazi Umoja wa Mataifa mdau. Kwani Ukiiweka tu mwisho wa CV basi umepita!...tehe tehe tehee

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 13, 2010

    photo of the month...so blessings n touching i miss yu nyerere!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 13, 2010

    mdau hapo juu nakuunga miguu watu wengine bendera fata upepo tuu nyerere nyerere wala hamjui alifanya nini mie nilikula ugali wa njano mswaki tunapigia majivu au mkaa tukaogea sabuni ya mbuni wee yani hiki kidingi sikifagilii katu watu misifa tuu kusifia uongo mbona bado nchi inajikongoja maskini duniani kwa kipi haswa ni maji umeme au barabara??? sijaona bado

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 13, 2010

    jamani huyu pilot kenan mhaiki mbona anaatajika sana yani hata kwenye picha mtu una intoruduce kulia halafu kushota lakin michuzi ume introuduce kulia halafu umemrukia ken. hah ha ha..

    nadhani ken alikuwa kiungo muhimu sana huyu jamaa ndo maana bado ana zari serikalini.
    hongera zake, bongo yetu ndo ilivyo.
    mdau kutoka los angeles u.s.a

    ReplyDelete
  14. Aidha utavuna ulichopanda au ulichopandiwa.Ndio maana hadi leo mafisadi wa EPA,KIWIRA,RADAR NA RICHMOND bado wanaitwa mashujaa wa Taifa hili???!!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 14, 2010

    Hongera Saidi.
    Huyo annon wa May 13 1:22 anahitaji kuelimishwa. Point of correction. Kazi za UN [international posts] zinapatikana on competitive basis siyo njia nyingine-hakuna michoro short cut etc. Lazima uqualify hata kama wewe ni mechanic, driver, secretary or engineer you have to compete in the global market. Saidi amefanya hivyo na sasa anapeta-Mwacheni katoka mbali huyu na wenye kumuonea wivu wajinyonge.

    Kwa waandishi wa habari kukutana na viongozi ni part and parcel of the job but mpaka ukumbuke kupiga picha kama hii is a plus-mara nyingi muda unakosekana.

    Saidi, I wish you more Luck in Elgeneina-border with Chad-You do a good job and Kemal should see this man! GREAT PIX I'm jealous big time and you know who's writing this right?

    ReplyDelete
  16. Hata mimi simfagilii hata kidogo huyo mzee na sera zake zilizotufanya kuwa maskini mpaka tuliko. Anyway Mungu amlaze mahali pema PEPONI, by double M

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...