Mjomba Michuzi,
Kuna jambo nataka tuwashirikishe wadau ili ikiwezekana tuwaombe wahusika kama si kuwashiknikiza. Jambo lenyewe ni hawa ndege wazuri waliokuwa wakilipendezesha jiji letu la Dar kwa miaka lukuki.
Kuna jambo nataka tuwashirikishe wadau ili ikiwezekana tuwaombe wahusika kama si kuwashiknikiza. Jambo lenyewe ni hawa ndege wazuri waliokuwa wakilipendezesha jiji letu la Dar kwa miaka lukuki.
Ndege hao walikuwa maarufu sana katika mitaa ya kuanzia Ikulu,Luthuli,Ohio,Mirambo, Makumbusho na sehemu jirani na maeneo hayo, ndege hao si wengine bali ni Tausi. Lakini siku za hivi karibuni kumetokea wimbi la kubadilisha sura ya Jiji hivyo kuongezaka kwa kasi ya ujenzi wa maghorofa kumeondoa uoto wa asili ambao ulikuwa ni makazi ya ndege hao wazuri,hivyo kutishia kutoweka kwao.
Ombi langu kwako Mjomba kwa kutumia nafasi yako katika jamii jaribu kuwasiliana na idara zinazohusika iwe ni Ikulu, JIJI au Maliasili ili ndege hao waliobaki waweze kuhamishiwa katika viunga vya chuo kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya mlimani huko bado kuna maeneo mazuri kwa ustawi wa ndege hao,pia kuwapo kwao hapo kutaongeza ubora wa eneo husika na kuwa kivutio tosha kwa Jiji letu. Mjomba najua ujumbe utafika.
Wasalam,
Mdau wa mazingira,
Mapesa,E
Wasalam,
Mdau wa mazingira,
Mapesa,E
NAUNGA MKONO HOJA!!!!!
ReplyDeleteMTOA HOJA UNA AKILI SANA. HOJA YAKO IMEPITA, KAZI KWA MICHU...
ReplyDeleteTick tick!! Mapesa, wewe genius ndugu yangu.
ReplyDeleteNaunga Mkono Hoja. Sijui kama jiji hili lina watendaji wanaofanya kazi kadri ya mafunzo waliyoyapata. Katikati ya jiji kumejaa, kwanini wanaendelea kutoa vibari vya ujenzi? Kwa hali ilivyo lazima tausi waathilike.
ReplyDeleteMtoa hoja nimekupenda.....ingawa inaelekea unapenda sana PESA lakini ni dhahiri una akili ....yani umeeleza tatizo na kutoa solution.....BIG UP!
ReplyDeletebadala yake wamejaa wale kunguru wa zanzibar wezi walafi wachafuzi wa mazingira ustaarabu sifuri na jinsi walivyo wengi hope ndo wangekuwa wale kina tausi hii mikitu iko ovyo sana huachi kitu nje haooo weshajaa
ReplyDeleteTungefanya hivyo mdau lakini na huko nako tuna mpango wa kurundika maghorofa bila kuimarisha miundombinu kama mifumo ya majitaka.
ReplyDeleteKama unapenda ndege tu burudika na kunguru wa Zenji wapo kibao.
Huu ndio ubunifu tunaoupigia kelele kila siku, na sio mitindio kibao iliyop JIJI, mi nakumbuka wakati tuko pale IFM walikuwa wanasogea mpaka maeneo yale walikuwa wanapendeza sana !! Wasiwasi wangu huko chuo watu watawakamata na kuuza nje rasilimali za taifa, fisadi kila mahali kaka !!
ReplyDeleteWewe anon. Thu May 13, 09:49:00 PM umefulia, jamaa ametoa hoja ya ukweli na waungwana wanachangia kiustaarabu ila wewe umeona ni lazima ujambe wakati wa maakuli, namna gani???? Tausi waende mlimani, na mlimani padhibitiwe, sio kila kitu kigeuzwe kuwa tangible cash. Hapa ndipo tunapotambua kinaga ubaga busara za viongozi wenye mamlaka husika. Lakini wakati huo huo, wale nyumbu wa Ikulu wameliwa na Rais gani?
ReplyDeleteNAUNGA MKONO HOJA 100%....Ankal naomba upeleke hili wazo kwa Wahusika! Mie nimekulia pale SEA VIEW, pale penye Ghorofa Refu kupita yote,(enzi hizo) juu palikua pana Tangazo la Biashara la "AIR INDIA" TAUSI walikua wanafika mpaka kwetu na ni wengi! siku hizi wanaishia OCEAN RD HOSP.
ReplyDeleteWazo zuri pia kawa hawa ndege wataweza kuenea sehemu nyingine!