mshambuliaji wa timu ya Lindi,Ally Mohamed "Gaucho" (10) akijaribu kutaka kumtoka beki wa timu ya Kilimanjaro,Emmanuel Lugano huku akisaidiwa na Raphael Mhanga katika mtanange uliopigwa jioni hii katika uwanja wa Uhuru.Lindi imefanikiwa kusonga mbele kwa hatua ya nusu fainali mara baada ya kutandika timu ya Kilimanjaro mabao 3-1.magoli ya Lindi yalifungwa na Ally Mohamed "Gaucho" (26),Aman George (34 kwa mkwaju wa penati) na Omar Matwiko alimalizia kwa goli la tatu.huku kwa upande wa Kilimanjaro goli lilifungwa na Magogo Mgaya.mshambuliaji wa kusoto wa timu ya Lindi,Abdallatif Abdallah akijaribu kumtoka beki wa timu ya Kilimanjaro,Crispian Linze katika mchezo uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Lindi imeifunga Kilimanjaro mabao 3 - 1 na kufanikiwa kusonga mbele kwa hatua ya nusu fainali itakayochezwa siku ya alhamisi mei,28 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.
kipa wa Kilimanjaro,Emmanuel Mseja akiondoa hatari iliyokuwa imekuja langoni mwake
mshambuliaji wa Kilimanjaro,Ismail Athuman (14) akijaribu kutaka kumtoka kipa wa Lindi,Mohamed Dihile.lakini kutokana na umahiri wa golikipa huyo aliweza kuuondoa katika hatari mpira huo.
wachezaji wa timu ya Ilala,Cosmas Aloyce (2) na kapten wa timu hiyo,Samuel Ngassa (8) wakimpongeza golikipa wa timu yao Juma Abdul (1) mara baada ya kufuta penati mbili katika mchezo uliochezwa leo mchana katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Ilala imeweza kusonga mbele kwa hatua ya nusu fainali mara baada ya kuitoa timu ya Iringa kwa mikwaju ya penati 5 - 3.kwa ushindi huu wa leo Ilala itambenyana na Lindi katika hatua ya nusu fainali hapo Mei 28.
uleeeee nyavuni.kipa wa Ilala Juma Abdul akiusindikiza kwa macho mpira ulipoingia wavuni.
Kocha wa Ilala,Jamhuri Kihwelo "Julio" (kulia) akitoa darasa wa wachezaji wake.
Athuman Iddy Chuji wa Iringa akiwania mpira wa juu na beki wa Ilala,Shaban Sunza katika mchezo uliopigwa mchana wa leo katika uwanja wa Uhuru.Ilala Imeweza kusonga mbele kwa hatua ya nusu fainali baada ya kufunga Iringa kwa mikwaju ya penati 5 - 3.
mshambuliaji wa kushoto wa timu ya Iringa,Brington Mponzi (15) akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Ilala,George Minja (kushoto/15) na Shaban Sunza katika mchezo uliochezwa mchana wa leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar.Ilala imeshindwa kwa mikwaju ya penati 5 -3 dhidi ya Iringa.kesho kutakua na mchezo wa hatua ya kwanza ya nusu fainali kati ya timu Arusha na Singida utakaochezwa katika uwanja Uhuru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Patrick Tsere (DC wa zamani Ilala)May 25, 2010

    Ilala Oyee. Julio Oyee. Najua mtashinda tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2010

    huyo kipa wa Ilala nini hicho kafunga kwenye mkono, ama kweli mja haachi asili. Mtoto kilo tatu hirizi kilo tano.... halafu oooh.. mwanangu haongezeki uzito.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2010

    Duhhhh!!!!! Hiyo mkononi(karibu nabega) mwa kipa wa ilala ni the "ndubazz" ya kuokoa penalt?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2010

    Labda alipewa na kamati ya Ufundi jamani si unajua tena kamati za ufundi za bongo sharti degree kutoka bwagamoyo!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 26, 2010

    Ankal kuna kawimbo ka zamani ebu tutafutie tujikumbushe enzi ""UKIMWONA CHOGO HAPA SEMBULI ATIA GOLI!!!""

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...