.jpg)
.jpg)

By Edward ALEX MkweLELE
The first Tanzanian president and father of the nation, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere will be declared saint on June 1, 2010 in Namugongo, Uganda as part of the celebrations to mark this year's Martyrs' Day. Heads of states of African countries and Nyerere's widow Maria Gabriel Magige will attend.
President of Uganda, Yoweri Museveni supported the campaign to have Nyerere recognised as a saint. The campaign began in January 2006, when Rome accepted the request from Bishop Musoma of Northern Tanzania Diocese.
Meanwhile, preparations for the celebrations are in high gear. Fr. Dennis Ssebuggwawo, the shrine rector, said the programme at the Catholic Shrine will begin with a nine-day Novena (reciting of prayers) from May 26 to June 2.
Ssebuggwawo said Moroto diocese will host this year's celebrations under the theme "I am with you always, yes to the end of the time (Mathew 28:20)".
Twenty-two Uganda martyrs were murdered at the Catholic shrines between 1885 and 1886.
Bado sijajua kwanini hizi sherehe zifanyikie Uganda!!!
ReplyDeleteMICHUZI BABU YANGU GAVE ME HASHEEM SABITI MOBILE NUMBERS I WANTS TO ATEND THIS SAINTSHOODS OF FATHER OF NATIONS, NYERERE WERE MY MODEL AND ARE STILL ON MY HEARTS EVERY DAYS OF OUR LIVES. HE ARE GOOD TO MANY PEOPLES OF THE WORLDS NO MATTER TODAY IS SAINTSHOODS, PLEASE I WANTS HASHEEM HIS WEALTHYNESS THE BILLIONAIRE OF EAST AND CENTRAL AFRICANS UNDER 24 YEAR OF AGES TO WIRE ME ONLY 2000 USD SOTHAT I COULDN`T GO TO UGANDA FOR SAINTS TOO. OK MICHUZI GOOD DAYS AND I HOPES TO TALIKING TO HASHEEM HELP ME GOD.
ReplyDeleteHii haijakaa sawa kabisa,nakubali kafanya mambo mengi mazuri,ila hii ya kutaka kumpa usaint???...mmhhhhhhhhhh si sahihi..
ReplyDeleteWe ma-saints unajua wanatakiwa kuwa wazungu tu au watu usio wajua? We acha utaratibu wa kumpa usaint ufate mkondo wake, kama atapewa, atapewa kama hapewi hapewi taabu iko wapi?
ReplyDeleteKwanza unawajua masaints wooote na walifanya nini ktk maisha yao hadi wateuliwe kuwa ma saints?
Tehe hehe..!! saint Nyerere, saint Rugambwa, saint Massawe, st. Fisi, st Nyahongo, st Sengondo, st. Marwa & st.Mthangi haya ndio majina ya kibantu.
ReplyDeleteThe Kalija
KWANINI SHERERE YA KUWA MWANAHERI ISIFANYIKE KWENYE NCHI YETU TANZANIA?
ReplyDeleteMHESHIMIWA MICHUZI, NAOMBA KUWAKILISHA...
Mke na watoto wa Mtakatifu huitwa nani?
ReplyDeletePia ankal, hebu tuanikie vigezo vyote vilivyotumika kupitisha uamuzi huo mzito sana, narudia tena, MZITO SANA!
Hivi huyo Hasheem anakula msondo ama vipi??? Naona huyo jamaa huwa anamtegeshea kinoma.
ReplyDeletekwa utakatifu upi huo??
ReplyDeleteHivi we Nalitolela, utaacha lini jamani Kiinglish chako kibovu. Kwa nini unapenda kuji-expose lakini? Unatu-bore, tumia kiswahili tu!
ReplyDeleteThe Man Created and instigated the classes in Tanzania.
ReplyDeleteWamjini na Washamba,
He transfer all regional authorities and centralised only in Dar es Salaam, and this has been going on till today, in turn the system paralyzed regional development. All this was under experimentation of UJIMA na UJAMAA Policy.
He rounded up innocent people and throw them on vijiji vya Ujamaa, using army and authotarian force, which in turn colapse the agriculture sectors in our country which was the backbone of economy of this country.
We had surplus in agricultural sector in 60's and early 70's, but once VIJIJI vya ujamaa vilipoanza, thats was all gone, ukilima na tractor wewe ni bepari, lazima ulime na JEMBE na wenzako, tena kwa nguvu za kijeshi, kwenye sehemu ambazo umeme hamna, maji ya tabu, barabara hakuna, KUNGEKUA NA UFANISI HAPO?
Hivi leo tumerithi hizi siasa na hizi class, ndio tunaona washamba purely WASHAMBA na wamjini wa WAMJINI, na ndio wenye kuchukua madaraka, na hata vile utaona wabunge, mawaziri kwao Dar is everything, yote haya ni SIASA ya NYERERE, wamerithi toka kwa baba wa Taifa, he was really baba wa Taifa, in turn created struggle for power, kwa hiyo ni DOMO(SIASA) tu, vipi utachukusanya SIMBA utaweka kwenye SENG'ENGE MOJA(DAR), si itakua kujionyesha tu nani mbabe zaidi, kwa hiyo kusahau yale majukumu yao kisiasa! sasa hili DOMO tumerithi BIG TIME, agree with me or NOT, thats the fact.
Jengine KUDUMASHA elimu kwa ujumla, the effects of that educational system which was set backwards inatufanya sote sisi hata kizazi chetu kuwa na elimu duni, ambayo haiko Competitive na ya wenzetu kama waganda, wakenya na hata wazimbabwe, tunastruggle kwenye unforgiving international scene. Hii ni OBVIOUS today.
Ameingiza siasa hata kwenye sector za Teknologia na biashara, katibu kata kuwa manager wa bank, mtoa vibali vya vibiashara na mgawaji wa bidhaa za biashara???(wapi na wapi) taifisha kila kitu(UPORAJI), na kuwapa watu ambao wamefail kuendeleza hivyo viwanda, mabank na biashara ambazo zilikua zinafanya vizuri kipindi hicho, kabla ya hizi siasa.
amewacopy wachina but he failed miserably to understand UJAMAA on its context, ameemphasized too much UJAMAA, UJAMAA, UJAMAA, bila kuzingatia DERIVATIVES za MAENDELEO and how to.
ameshindwa kuelewa katika jamii yoyote hata kama hao WACHINA kuna walichonacho na wasio nacho, distribution ya WEALTH, ipo kwenye cut off of TAXES na siyo KUPORA MALI YA WATU, yeye bahati mbaya amechukua DOMO(SIASA NYINGI), na KUWARITHI KAUNDA SUTI, kama MAO.. LOL..lakini hili hakulifahamu.
Alikua anaongoza kwa IRON FEAST, kuwazamisha kina KAMBONA, na wengine kama munatofautiana kisiasa, he was totally INTOLERABLE on debate, which should have been healthier in any socieity kuwa na opposition of view of anything.
Jengine zaidi baya ambalo tulikuwa nalo enzi zake, na hivi sasa ni, hatuelewi A FINE LINE between CHAMA TAWALA na UTAWALA kwa ujumla wa NCHI, katika nyanja zote, kwa mfano, matenganisho ya kifedha baina ya Matumizi ya CHAMA TAWALA, na MAJUKUMU YA KISERIKALI, hakuna maelekezo au ufafanuzi juu ya hili, na wamekusudia kufanya hivyo na iwe hivyo DAIMA ili kukaa madarakani, LAKINI NDUGU ZANGU HILI NI MUHIMU SANA kuwa CLARIFIED, with regular REPORTS in terms of FINANCE ya CHAMA PEKEE, siyo kutubabaisha, utamuona waziri au balozi anakuja huku kwa fedha za WALIPA KODI, ya wananchi wote kufungua kata YA NCHI ZA NJE(aka matawi ya CCM). Ndugu zangu hizi ndio siasa tulizozirithi.
Naomba proper DISCUSSION na REFUTATION ya hayo niliyoyasema na siyo matusi, na BLIND FOLLOWING AND NOW WARSHIPING,
Shukrani.
Ya Kaizari tumwachie Kaizari na ya Mussa apewe Mussa,huu ni uamuzi wa kiroho wa kanisa Katoliki na haufanywi juu juu tu bali kuna taratibu na sheria zake tena ni za kiroho zaidi kwa hiyo sidhani kama tuna uhalali wa kuhoji ndio au hapana kwani taratibu hizi za kikatoliki hazijaanza leo na hata hao watakatifu wengine [Amani yake Bwana iwe nao,nasi pia] walipitia mchakato huo huo hivyo haimaanishi wote tunalazimishwa tumwite au kuamini yeye ni mtakatifu la hasha bali ni kikanisa na wale wenye imani katika hilo,tuwe makini katika hili na kuheshimu imani za wengine, jina lake Kristu lihidimiwe
ReplyDeletewho cares, all i know, wale wajanja zaidi yake ndio mafisadi mpaka leo, mafisadi hawa walimtumia huyu jamaa, alichojali yeye ni madaraka tu,wenzake wanaiba mpaka leo, tanzania leo haina demokrasia isipokuwa chukua chako mapema. mali zote za wananchi aliwapa ccm kwa mfano jumba la ccm dodoma,uwanja mpira dom. huku nilipo hakuna hata mmoja ninayefanya nae kazi au jirani ambae anajua huu jamaa sasa ni mtakatifu au alikuwa rais. usa
ReplyDeleteastaghafirulah
ReplyDeleteis this a joke? najua baba wa taifa alikuwa anasali sana pale st peters lakini kuwa saint? mmmh au kuna mengi tusiyojua, michuzi tufahamishe kwa kirefu, ni miujiza gani baba wa taifa kafanya? nami basi nitaanza kumwobma nilikuwa sijajua ni mkubwa kiasi gani hata akiwa hatupo nae duniani.
ReplyDeletena wewe PETER NALITOLELA?? kwenye mambo muhimu usiingize utani kama unamtaka hashim mwombe tu kwa kivyako usitumie post ya baba wa taifa. By the way your english is very bad, please get a hold of Mpalang'ombe im sure he will give you tips on how to write proper english. I grew up in tz also but look at my english, its simple but clear. Get it together bro.
hii ni hongera kwetu sote watanzania! Ni heshima kubwa sana and i dont care what anybody else think HE DESERVES THIS!
ReplyDeleteHongera zaidi kwa Mama Maria na wanafamilia wote.
Mungu awabarkiki,
Mdau in NY.
ndio maana tunaambiwa tutumie kiswahili.... kwa kiinglish hicho hapo juu safari bado ndefu wazawa
ReplyDeleteWhy this "sherehe" zifanyikie Uganda? The answer is simple: It never ocured to most Tanzanians that Nyerere is infact a saint, if not a deceased who deserves sainthood. Another reason is simple also: Is it a surprise that some Tanzanians will object to this idea! Who doesn't know the 'character' that defines most Tanzanians? It takes education, formal education for one to realise that Nyerere is/was a saint. Again, EDUCATION.
ReplyDeleteNi kweli alitenda mambo mengi mazuri nilikuwa najiuliza kuhusu yale matambiko wakati wa kupigania uhuru yanakaaje. Mwenyewe alikuwa anatoa hotuba na akaongelea mambo hayo.
ReplyDeleteDuh! Kwa kweli sijamuelewa kabisa huyo Peter Nalitolela hapo juu. Hicho alichokiandika ni kiingereza au Kinyakyusa!
ReplyDeletemh hizi imani hizi?!na kwanini iwe uganda?
ReplyDeleteSAINT=mtakatifu au mwenye-heri?haya 2 yanafafana kiinglish?
Weweee unaujua usaint!!! wala msikiti au kanisa hulijui!!! wayahudi walikuwa wanachambua KITABU na wakamuua YESU!!. Mshukuru Mungu tu anakupa punzi ya bure ufanye fujo!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteNIMEAMINI YA KUWA NABII HAKUBALIKI NYUMBANI, NA NAITHIBITISHA KUPITIA WACHANGIAJI HAPO JUU..
ReplyDeleteKAMA HAMTAKI AWE SAINT KAWEKENI PINGAMIZI ROME KTK MJI WA VATICAN YALLIPO MAKAO MAKUU YA KANISA KATOLIKI..LOL!
Why Uganda and not homeland?
ReplyDeletemdau wa 24:00 PM
ReplyDeletenaungana moja kwa moja na wewe manake hii mtu nasemaga kila siku simfagilii ng'oo kwa kippi?! kaacha nchi imedodaa full masikini halafu watu wanammwagia misifa inashangaza sana ni basi tu bendera fata upepo na huo u st marys mie mh anyway labda utaleta maendeleo nchini
lakini si ameshafariki jamani au?
ReplyDeleteAmbaye hayupo na lake halipo no matter what he /she has done!
Enway ni mambo ya kiimani zaidi ngoja tuone....
Ankal baada ya kuisoma hii post mwanzo hadi mwisho na kupitia maoni yote ya watu nimeona ni bora niiweke sawa hii post yako. Kwanza sio kweli kwamba Mwl. Nyerere atatangazwa mtakatifu tarehe 1 June pale Namugongo, Uganda. Ukweli ni kwamba baada ya maombi ya Askofu wa Musoma kukubaliwa na Vatican(sio Rome)kuomba mchakato wa kumtangaza Mwl. Nyerere kua Mtakatifu, kuna taratibu ambazo Vatican walizitoa ili ziweze ama kuthibitisha kwamba Mwalimu anastahili ama hastaili kutangazwa mwenye heri kisha mtakatifu.Hivyo siku hiyo ni kwamba Mwakilishi toka Vatican atatangaza petition for Beatificatin, the next (after years) itakua ni canonization. Mojawapo ya vigezo hivyo (vya kukubaliwa hiyo petition for beatification) ni miujiza (takribani 3 au 5)aliyoitenda akiwa hai au amekufa, pindi jina lake litakapotumika kumuomba ( muujiza ni kufanya kitu ambacho kwa uwezo wa kibinadamu kamwe hakiwezekaniki). Sasa baada ya kukubaliwa kuendesha huo mchakato kanisa katoliki hukusanya matukio na habari zote za maisha aliyokua akiishi Mwalimu. Mojawapo ya miujiza iliyokusnywa ni kutoka kwa Rais Museveni alielezea jinsi mwalimu alivyoweza kuleta amani Burundi. Fanyeni mapitio ya namna Warundi walivyomkataa mwalimu baada ya kamati ya kina Museveni kushindwa kusuluhisha mgogoro huo na jinsi Mwalimu alivyoweza kuumaliza kabisa na kuleta amani Burundi.
ReplyDeleteUwezo wa kipekee wa Mwalimu pale alipopigana na kuondoa Quota system kwenye soko la Dunia kitendo ambacho Wabrazil na kahawa yao walimchukulia Mwalimu kama mwokozi wao.Ni kiongozi gani leo anaweza akalifanya hili? Ukizingatia pesa nyingi madalali wa Ulaya walivyokua wakikusanya kwa kutoa quota certificates kwa mazao ya kilimo toka nchi zetu hizi huku wao wakicontrol supply ya mazao husika kwenye soko la dunia ilikua si rahisi kuondoa uo mfumo na makampuni mengi ya udalali huo yalikufa baada ya kufutwa huo mfumo.
Ujasiri usio wa kawaida wa kusema waziwazi kwenye majukwaa ya kimataifa kutaka ukombozi wa Afrika toka kwa makaburu,wareno n.k na kulitekeleza kwa vitendo,nani leo anaweza kutekeleza kwa vitendo haya? Pia kitu kingine ambacho sisi hatukielewi hasa watoa maoni wengine ni kwamba sera ya ujamaa na kujitegemea iliyozungumzwa kwenye Azimio la Arusha haikuwa na maana ya Tanzania ifuate siasa za China au ukomunisti. Hili la ujamaa na kujitegemea kama lingefanikiwa( kwa kuungwa mkono)leo hii bajeti yetu isingetegemeea wafadhili,wala tusingejua maana ya wafadhili au wahisani na kamwe tusingekua na maneno kama mkukuta. Yale maadili yaliyopo kwenye azimio la Arusha mengine hata Barack Obama anayafanya leo kwa vitendo kwa hupitisha sheria ya bima ya Afya kwa wote.Leo hii tunalalamika nchi imeutwa ni kwa sababu viongozi maadili yameshuka, no patriotism any more, maslahi binafsi kwanza.
Kuhusu ni kwanini shughuli hiyo inafanyika Uganda ni kwamba pale Namugongo pana historia kubwa sana kwa Kanisa Katoliki soma hapa utaona mashahidi ambao walitangazwa wenyeheri kisha wakatatifu baada ya mapitio ya maisha yao na matendo yao mahala walipozikwa au toka kwa watu walioomba kupitia kwao. Ningeandika mengi kuuhusu hatua za awali zilivyofanikiwa kufikia hata kufanikisha hatua ya petion for beatification kufikiwa maana viginevyo hii hatua isingefikiwa kama Mwalimu angekua hastahili. Wenye imani tuendelee kuomba ili hizo hatua zipite na canonization hatimaye na sie tuweze kuimba Santa Nyerere, ola pronobis....
Anno wa Tue May 25, 09:24:00 PM Almost 15 paragraphs tuta-duscuss nini? Condens!
ReplyDeleteMichuzi huyo Anno wa Wed May 26, 03:58:00 PM anafanya hapa paonekane kuna wenye brain wanapita.
Mwandishi hapo juu safi sana, umefafanua swala zima vizuri sana. Na unaonesha kwa kiasi flani kujua unachokizungumza. mimi kwa mtazamo wangu na kwa jinsi ulivoonesha kidogo baadhi ya watanzania wanakosa uelewa wa mambo na mbaya zaidi hawajiangaishi kujaribu kuutafuta huu undani, wanabakia kutokubaliana na jambo bila kulifahamu kiundani.
ReplyDeleteAnon wa Tarehe Tue May 25, 10:23:00 PM, Mie nilizani USA ndio wengi wa watu hawajui nini kinaendelea hata nchini mwao achilia mbali Afrika au tuseme Tanzania.
ReplyDeleteNa unaposema hamna mtu anajua nini kinaendlea kuhusu Nyerere wakati huo huo wewe unajua na uko USA sasa sijui ni nini kinakufanya uzanie wewe hauko USA na hakuna mtu mwengine ktk USA anayejua ila ww tu!!??
Nakubaliana na annon wa Wed May 26, 03:58:00 PM. Duh jamaa kaweka sawa mambo vizuri na sasa ninaamini ile kauli ya nabii hatambuliki kwao,wenzetu waganda wanatambua mazuri yake na wanamuhehimu,Afrika nzima inamuheshimu kwa sababu kipindi chake angeweza kuwa Dikteta kama watawala wenzake enzi zile. Sioni ajabu kwa Nyerere kufikia hapo, jamani anastahili kama hamkubaliani na hili anzeni kupingana na vitabu vinavyosema kwamba Nyerere ni miongoni nwa "Thinkers of 20th century" pia
ReplyDeleteasalaam aleykum,
ReplyDeletekwanza nimpongeze mchangiaji wa may26,03.58pm kwa kutuchambulia kwa uwazi mfumo mzima wa shughuli hii kwa sababu kama mtu hujui hayo ndio unatoa maoni kwa kutumia kichwa cha habari tu tena unaendelea kutoa duku duku lako ukidhani unachangia la maana kumbe unatukana ovyo bila sababu kwa vile hujui ajenda ikoje au inazungumzia nini.
mimi kwa mtazamo wangu iko haja ya kuzidi kumjadili mwalimu ili baadae kanisa katoliki limkubali au kumkataa kuwa mtakatifu kwa sababu anastahiki kufanyiwa mchakato huo kwa maoni yangu tena kupewa au kutopewa hayo hayako mikononi mwangu.
ninasema haya kwa sababu naelewa mchango wa mwalimu nyerere kwa taifa hali na mataifa mengi jirani ambayo leo yako huru kwa mchango mkubwa aliouonyesha katika uongozi wa kuyatetea mataifa hayo wakati hakuna taifa lolote duniani makubwa au madogo yaliyokuwa "front line" katika kuwatetea wasio na sauti na waliotawaliwa pia katika tanzania leo tuko salama na tunasonga mbele kwa mabadiliko tofauti na amani ndio imetutawala ingawa wengi sasa hivi ni wepesi kulaumu ujamaa na mifumo mingine iliyopita kuwa ndio vikwazo kwa maendeleo lakini ni vema tukakumbuka kuwa amani tumeiona haina thamani kitu ambacho kwa mawazo yangu ni bora nikawa na amani kuliko maendeleo yenye mauaji kama hawa majirani zetu ambao sote tunaweza tukakubaliana kuwa wameendelea kuliko sisi lakini kila baada ya muda wanauwana kwa maelfu.
sisemi kuwa tusiendelee ninachokisema kuwa sisi tumepiga hatua kuliko hawa tunaowaona wameendelea katika usalama kitu ambacho hatuwezi kukitia thamani.
mwisho nigependa kuweka wazi kuwa tanzania kwa muda mrefu hatutopata kiongozi muadilifu pengine tusipate tena mpaka kiama kwa sababu nimeshaona dalili na mifano ya viongozi waliopita waliopo sasa na wanaokuja kuwa kumpata kiongozi mwenye kujali watu hasa masikini na mwenye upendo na heshima,huruma na mcha mungu hamna wapo ambao wana afadhali tu lakini ubinafsi,choyo, majivuno,wizi,uongo,wapenda ngono,wasiotenda haki,wenye udini,ukabila,udugu "you name it" ndio tuliojaaliwa kwa sasa.
mungu tusaidie kwani watatuuwa hawa viumbe wako na nchi ndio wanaipeleka arijojo{washaimaliza}
mola umlaze pema mwalimu julius kambarage nyerere.
amen.
ahsanteni,
sheikh ahmed sultan omar.
panama canal, panama.