JK, Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. William Lukuvi wakiingia katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo jioni kabla JK hajaongea na wazee.

JK na viongozi wengine wakiwaamkia wazee kabla ya kuwahutubia
Semaaa...usiogope seeemaaaaaa....wazee wanaimba

"....ndio mwanetu... semaaaaa..!"
JK akihutubia taifa leo kupitia mkutano wake na wazee wa mkoa wa Dar es salaam leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. Kulia nia Makamu wa Rais Dr.Ali mohamed Shein na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam William Lukuvi
sehemu ya wazee wakimsikiliza kijana wao leo
JK akitoa pointi
Sehemu ya umati wa wazee wa jiji la Dar wakimsikiliza JK.
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 44 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2010

    Nategemea TUCTA nao watatoa msimamo wao kesho.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2010

    Hao ni wazee ikimaanisha wa watanzania wote, vyama vyote na wasio na vyama au ni waze wa CCM ? Anasubiri maji yamfike shingoni ndiyo aongee ? Na kisa cha kuleta mkuu wa majeshi na wa Polisi ni kumtishia nyau mtu mziam au ni kitu gani ? Kweli sasa sinema imefikia patamu.

    ReplyDelete
  3. Advocate JashaMay 03, 2010

    Mjomba Kweli wazee wanapashwa kuheshimiwa.Nafikiri ingelikua vizuri kama ukamwaga cheche chuo kikuu au vio vikuu.Huko watakusikiliza kwa makini na kukupima au kizipima cheche zako.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2010

    TUCTA endeleeni na mgomo
    maendeleo hayaletwi na bla bla za CMM nchi zote duniani zinagomea serikari zao pale zinapovurunda
    lakini si mgomo pekee ndiyo dawa
    cha msingi msichague tena CMM mwaka huu

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2010

    Ankal naomba usibane comments za watu,inakuwa haina maana unaweka maada/habari halafu watu wanapochangia unakuwa bias bila kujali huyo mtu ametumia muda wake wa kuandika na kuwasilisha maoni yake. Tanzania haiwezi kujengwa kama tukiwa waoga ankal. Baada ya kusema hayo maoni yangu ni kama ifuatavyo;

    Izingatiwe kuwa wakati wabunge wanalipwa mamilioni ya fedha kwa mwezi, wafanyakazi wengine hususani watumishi wa umma kama walimu, wauguzi, maaskari nk wengi wao wanalipwa kima cha chini ambacho ni chini hata ya fedha anazolipwa mbunge kwa siku moja. Inasikitisha sana kuona kiongozi wa nchi anatangaza kwamba suala la wafanyakazi kuongezewa mishahara yao halitatekelezwa kikamilifu kutokana na visingizio mbalimbali. Hii ni ishara ya matabaka katika taifa, kwani wakati wabunge wanajiongezea wenyewe kipato na kupata mapato ya kiwango cha kufuru ukilinganisha na hali ya taifa; wabunge hao hao wanashindwa kuibana serikali kutekeleza ahadi zake. Baadhi ya wabunge wamegeuka kama wenye shibe wanaosahau wenye njaa.
    Nachukua fursa hii kuhamasisha wananchi kuitaka serikali kuweka rasmi wazi kwa umma, kiwango cha mishahara na posho wanacholipwa watumishi wakuu wa serikali wakiwemo viongozi wa kisiasa. Kadhalika, tunaitaka serikali iweke wazi ripoti ya Tume ya Ntukamazima ambayo iliteuliwa mwaka 2006 na kukamilisha kazi yake mwaka 2007 ya kupendekeza nyongeza ya viwango na maslahi ya wafanyakazi. Hii itawezesha watanzania kuwianisha vizuri mapato ya kada zote za wafanyakazi na kuunganisha nguvu katika kuhakikisha mapendekezo ya ripoti hiyo na matakwa ya umma kuhusu uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi nchini yanatekelezwa.

    Mdau Ughaibuni

    ReplyDelete
  6. Inasikitisha kuona kwamba madai ya wafanyakazi yamefikia sikio ambalo haliko tayari kuyasikiliza madai yao. hoja ya Mh. Rais ni nyepesi na kwa maoni yangu hazijajibu maswali ya msingi ya wafanyakazi. Rais alipashwa kuwaambia watanzania kwamba hiko kima cha chini kinachodaiwa na wafanyakazi ndani yake kina kodi ya mapato ambayo ni asilimia karibu 33%. kwahiyo kwa kadilio la juu ni kama shilingi 3.3 trilion ndo gharama za mishahara za wafanyakazi wa sekta ya umma. lakini vile vile wafanyakazi wamependekeza njia mbadala ya kuongeza mapato ya serikali na kupunguza matumizi ili serikali iweze kujenga uwezo wa kulipa mishahara inayo kidhi hali ya maisha. serikali hili wanachelea kulifanyia kazi ama kwa makusudi au kwa sababu ambazo si wazi kwa mtu wa pembeni.

    vile vile nimesononeshwa na jinsi mh. rais alivyoligeuza swala hili la kisiasa ilikupata uungwaji mkono na wazee wa chama wakati madai ya waafanyakazi ni ya msingi, yanahoja na kwaajiri ya afya ya maendeleo ya nchi yetu.

    Niseme kwamba tulikuwa na chaguo mwaka 2005 lakini wazanzibari wakalitupa. Mwisho, salamu alyhekhum kwa watanzania wote mnaolipwa mshahara kima cha chini.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2010

    Naombeni msaada wa tafsiri za maneno yafuatayo katika darubini ya Tanzania:
    1) Mzee
    2) Kijana
    3) Kijiji
    4) Mji
    5) Haki

    Natanguliza shukrani kwa wadau wote watakaojikoza katika kusaidia.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2010

    Kweli JK ni msanii aliyebobea...kwanini amekimbilia kuongea na wazee wasiojua kitu na kuwamimbia wafanyakazi.kwani wazee ndio waliogoma?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2010

    Poleni sana wafanyakazi, ndo hali halisi. Inauma sana,kulichukulia/kulielezea swala hili kirahisi namna hiyo bila kujibu hoja ya msingi na mzizi hasa wa tatizo lenyewe kama vile maisha/mishahara duni ya mfanyakazi wa serikalini na pia makato makubwa ya kodi.
    Jifarijini na kibwagizo hiki.

    http://www.eastafricantube.com/media/25390/Wagosi_Wa_Kaya_-_Maumivu_Ya_Miaka_Kumi/

    Mdau

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 04, 2010

    Vipi hao wazee waaoshagilia ni wale waliokuwa wafanyakazi wa East Africa wameshalipwa mafao yao? kama hata wao hawajalipwa, basi hao waaoshangilia wanafanya kufuru mabazo malipo yake sijui itakuwa wapi.Ni sawa pegie madai ya TUCTA hayatekelezeki kwa asilimia mia lakii nadhani President katumia lugha ya vitisho mno, leo hii wakulima nao wakijitokeza na madai itakuwaje?
    TUCTA ombeni kuonana na President achaneni na Kapuya, ni vizuri mkaenda Ikulu moja kwa moja badala ya kuongea na Kapuya, hana uwezo kwa nafasi yake kuwasaidia.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 04, 2010

    Laiti JK angelijua madhara ya kauli zake kama hizi kamwe asingesimama na kuongea kauli kama hizi za kuchefua wafanyakazi mbele ya hao wazee ambao wengi wanaishi kwa kutegemea mafao na misaada ya watoto wao ambao ndo wafanyakazi hao wanaotishiwa wasigome. Kulikua na haja gani kuwaeleza wazee haya kama kweli suala lipo kwenye mazungumzo?.
    Hivi hajui hao wafanyakazi ndio wanaomweka yeye ofisini na kuwahudumia hao anaodhni ndo wanakura za kutosheleza kumpa ushindi katika uchaguzi mkuu?.

    Hajui kuwa dhama za utawala wa kimra zimepitwa na wakati na kuwa wafanyakazi hawapaswi kutishiwa kama watoto??
    Hajui hata hiyo dola anayoitegemea kulinda Serikali yake na kukabili mgomo wa wafanyakazi nayo inaundwa na hao hao wafanyakazi anaojaribu kuwatishia nyau?.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 04, 2010

    Kikwete ni chaguo la nani vile? Wafanyakazi msichague mbunge yeyote wa Chama cha Mafisadi

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 04, 2010

    Hali ya maisha ya mtanzania wa kawaida bado inasikitisha, ni miaka karibu 50 ya uhuru imepita , lakini ni uhuru wa maneno mtanzania bado hajawa huru, demokrasia ya mtanzia ni ya kibabe bado hakuna demokrasia halisi.
    Pamoja na rais kutoa mkwara lakini hapo moyo unamdunda kwa hofu kubwa! Je wafanyakazi wote wakigoma kweli matokeo yatakuwa ni vipi katika nchi! Nchi itapoteza mabilioni kwa siku na kwamaana hiyo serikali itabidi kuwa shut down. Serikali itaumia na wananchi zaidi watakosa huduma na itachukua miaka kupata wafanyakazi wenye uzoefu ili kuziba mapengo. Ametoa matisho lakini moyoni mwake hana amani kwani itakuwa ni mchafuko wa hali ya juu katika nchi na tutaendelea kujididimiza katika umaskini wa hali ya juu.
    Kauli ya mheshimiwa Kikwete ni ya kibabe na kiimla ndani yake inabidi awafikirie wafanyakazi wa serikalini upya. Gharama za maisha ni za juu mno Tanzania kila siku bidhaa zinapanda bei na haziwiani na kipato cha mtanzania, ndo maana tatizo la rushwa kuanzia ngazi ya chini halitakaa kwamwe liishe kwani wafanyakazi wanatafuta kipato cha ziada ili kuweza kukidhi ugumu wa maisha, mshahara hautoshi jamani, wafanyakazi wahurumiwe. Inaumiza sana ndugu zangu wananchi. Hapo wafanyakazi wa serikali wameachwa njia panda wapo katika wakati mgumu sana.
    Niishie hapa naomba ankal usiweke maoni haya kapuni kwani hichi chombo ni cha wanyonge na hii ni sehemu ya kutoa yale yaliyo moyoni kwa mnyonge.
    Asante sana kwa kunipa nafasi hii kutoa maoni yangu. Asubuhi njema
    Dau USA

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 04, 2010

    Kwa kweli naona jamaa alikuwa anatumia muda mwingi kumtishia Mgaya badala ya kudili na tatizo, huyu JK naona hizi kauli zake zitatupeleka pabaya. Hata wale wazee waliokuwa wanashangilia sikujua walikuwa wapapongeza nini pale, naomba niungane na mdau mmoja wa hapo juu hivi wazee wa daresalam ndo wafanyakazi wa nchi hii?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 04, 2010

    ha ha... Tumeacha Afadhali tumechagua Potelea Mbali!

    Rais anahutubia akinukuu maneno ya khanga! "Ukubwa Jalala"; "Akutukanaye.....".

    Badala ya kutupa data, percentages, hard facts yeye anatupa stori... hivi anafikiria Tanzania ya leo ndio ya kupelekwa kiholela namna hii?

    Mpo wapi viongozi wa kweli? Mnasubiri nini? Mpaka siku tuchapwe kama walimu wa Katerero? Kwa lipi hasa? Laki moja kwa mwezi?

    Ooooh tulipoingia kima cha chini kilikuwa 65,000/= sasa hivi 100,000/= kaona kafanya makubwaaa bila kucheki inflation rate ipo wapi? Laki moja unafanya nini? Laki moja haimtoshi mkewe kupata kitenge cha Wax Original kama anavyovaa na kukishona halafu anataka wenzie walee watoto wao, walipe kodi ya makazi na kula hapo hapo?

    Sitashangaa Rais atakapong'ang'ania madaraka baada ya miaka mitano ijayo kuisha, Katiba itabadilishwa maana haonyeshi yupo tayari kuacha nafasi yake... laiti angekuwa tayari basi angeweka mazingira mazuri japo ya kustaafia maana miaka hii 5 iliyopita hakuna lolote zaidi ya Safari, Safari, Safari, Safari!

    ~ Ahsante!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 04, 2010

    Mnashangaa nini? Kweli kila mtu na akili zake,Kazungumza na Wazee wa Dar ni kwa niaba ya Taifa zima imeelezwa na watu wameelewa, mgomo ni haki lakini ni suluhusho la mwisho ikiwa majadiliano yamevunjika sasa hata majadiliano hayajaisha mgomo wa nini? Kwa kuwa una njia nyingi za kujikimu
    GOMA UONE

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 04, 2010

    Duu kazi kweli kweli, dawa wafanyakazi na wakulima woteee msiwachaguwe viongozi wa CCM mwezi wa OCTOBER.

    JK na watu wake wanatakiwa kujipanga vizuri, mpaka sasa wanaendelea kuchemshaa.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 04, 2010

    Wadau, mimi langu ni dogo sana kuhusu Huyu Mr. President.
    Amepataje muda wa kwenda kuzungumza na wazee anakosa muda wa kukutana na Viongozi wa TUCTA???????????.
    Haya maneno ya vitisho ndo huwa wanayutumia viongozi wa vyuo kipindi cha migomo na bado wanazuoni wanagoma.
    nathani kwasababu huwa wale upeo wao ni mkubwa japo wanachi huwa wanakuwa wanashindwa kuwaelewa na kuwaona sio watii.
    Sasa limekuja pabaya ambapo watu wamegawanyika sana wafanyakazi wengi ni waoga and sithani kama TUCTA watafikia lengo kwa Jinsi watanzania tulivyo.
    Nimeshiriki sana kwenye Migomo nchi hii Tangu Secondary mpaka chuoni bado kazini tu na yote ilifanikiwa kwa kiasi flani but huu nawasiwasi nao sana maana najua vile viongozi watakavyobanwa wasisikike kabisa kutoa msimamo kwa wanachama wao.
    Mr. President ametumia Jazba sana katika kujadili mambo mazito kama haya and kwa nchi za wenzetu huyu bwana ndo ungekuwa mwisho wake kuiona ikulu.
    Sijui Tanzania itapata uhuru lini katika utumwa huu wa mawazo.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 04, 2010

    BINAFSI KIKWETE NIMEMUELEWA VIBAYA SANA. JAPO MAMBO MENGI ALIKUWA ANAONGEA YAPO LOGICAL ILA APPROACH YAKE SIYO KAMA RAIS WA NCHI. HIVI ANGEKUWA ANAJITOKEZA KAMA JANA KUDHUNGUMZIA MASUALA YA UFISADI SI INGEWATISHA KIDOGO MAFISADI?. BINAFSI SIKUMCHAGUA KIKWETE NA SITOMCHAGUA HATA WATANZANIA WOOTE WAKIAHIDI KUMCHAGUA.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 04, 2010

    Hao wazee wastaafu wanaoshangilia na kufurahi wanatunzwa na hao watoto wao wafanyakazi lawama kibao pindi wasipopewa chochote wa watoto. Sijui hata hapo walipo hata nauli ya kurudia makwao walikotoka kama wanayo wanacheka tu. Mhe. Wafikilie wafanyakazi hali mbaya jamani!!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 04, 2010

    Hivi hawa wazee....yaaani...aaaah! kwani wanaishi kwa support gani? wale wa afrika mashariki waliwakilishwa.Bonge la changa la macho! tumempima mjomba. Ila PAYE inaniuma! Daaah sasa tunafanyaje? Mgaya badilisha jina usiitwe rais wa TUCTA labda matusi yangepoa....yaani yale yale ya square root, sikuelewa somo kabisa!

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 04, 2010

    Kikwwete ni Msanii na hata hao Wazee wanaomsikiliza Mimi nawashangaa kwani wameenda hapo kwa ushabiki wa CCM pia hata maji ya kunywa hawakupata. Isitoshe JK katika hotuba yake ameelezea tu et Wafanyakazi wanadi mishara mbona jambo la msingi kuhusu kodi hakuzungumza au haoni kuwa ni mzigo mzito kwa Wafanyakazi?

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 04, 2010

    Ni bahati mbaya sana Mkuu alikuwa anamzungumzia mtu na sio tatizo, hotuba ilikaa kitaarabu taarabu badala ya kuonyesha the way forward. Vitisho vingi kwa watu wanaodai haki yao ila likija suala la Richmond, EPA kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 04, 2010

    kwani wanaofanyakazi ni wazee,mbona jk kaishiwa sana,angewaita wafanyakazi na sio wazee kimsingi ambao hata selikari inawapunja hata mafao yao,wanakufa njaa tu,halafu eti wanaenda kumsikiliza mwenzao ambae hawafikirii kabisa,acha usanii,nchi hii ni ya wote,na wafanyakazi ndio wafuja jasho kwa kodi zao ili yeye apate kusafiri nje kwa kodi zetu.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 04, 2010

    Hadithi za sungura, akaenda wee akakuta shimo, akatumbukia akakuta kisima, akaja panya mkubwa kama tembo akammeza sungura, sungura akafa hapohapo na hadithi yangu imeishia hapohapo!! Ni propaganda na hoja nyepesi za kumshambulia Mgaya, angejadili hoja, aache usanii. Atazame Thailand wazee wa mashati mekundu, natamani Mungu angewapa roho hiyo watanzania kwa uwezo wa roho mtakatifu kwani ni waoga na kweli hawatagoma lakini watu wataendelea kufa Mwananyamala na wao watakwenda kutibiwa ulaya. Wajitahidi basi kutumia sanduku la kura Oktoba. Mungu wasaidie watanzania waweze kubadilika.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 04, 2010

    hotuba kama hii ya jana hutegemei kuisikia kwa Rais wa nchi, hivi kweli ilikuwa hotuba au maneno ya jazba yenye kuleta hasira kwa wasikilizaji badala ya muafaka. Nadhani kama kuna neno naweza kulitumia ni Raisi amekosea this time na si kidogo sana, dharau na lugha iliyotumika sio ya busara hata kidogo wafanyakazi ni wajibu wetu kuelewa na kuchukua maamuzi sahihi

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 04, 2010

    Mhe. Rais, Asituone kuwa wote ni HAMNAZO! Angetoa a SCIENTIFIC RESPONSE ya HOJA za TUCTA. Issue ni kuwa hali ya uchumi ni ngumu kwa mtanzania wa kima cha chini. Chukua mfano kwa mahitaji ya kawaida kwa huyo wa kima cha chini.

    i. Usafiri wa Daladala (250*2*30)=15,000/-;
    ii. Kodi ya Chumba (Mabondeni/Mbali ya Mji) - (20,000*2)= 40,000/-;
    iii. Mlo wa mchana (1,000*30)= 30,000/-;
    iv. Nyumbani (Mlo kwa mama na mtoto 1)- (2,000*30)= 60,000/-;
    v. Nishati/Umeme = 15,000;
    vi. Huduma ya Maji =15,000;

    Hapo jumla ni Tshs. 175,000/- hujaumwa wala hujampeleka mtoto shule.

    Kwa hiyo cha msingi hapo ni kumuwezesha huyo wa kima cha chini angalau aweze kuishi (kusurvive) suala la akiba (savings) hapo ni NDOTO.

    Hivyo Mhe. Rais, anabidi atambue ya kwamba ISHU hapa siyo Kima cha chini cha laki 315,000/- kama anavyosema yeye suala ni KUJENGA UCHUMI utakaoweza kuwawezesha watanzania walio wengi ili kuweza kutekeleza Ilani ya Chama.

    Sula la wafanyakazi kudai Sh.315,000/- kama kima cha chini ambacho kwa mujibu wa Mhe. Rais. ni sawa na kiasi cha Trillion 6.0 kwa mwaka; ambako makadirio pekee ya Pato la Taifa kwa mwaka 2010/11 kama alivyosema mwenyewe ni Trillion 5.7. Ni sawa kuwa na nakisi (deficit) ya Bilioni 300 hivi bila kuzingatia mahitaji mengine ya Taifa. Suala hapa ni kuwa yeye amedai kuwa na Wafanyakazi 350,000 wa sekta ya umma.

    kwa mahesabu ya haraka haraka (logical thinking) ukisema kuwa unawalipa hao wafanyakazi wastani wa milioni 1 kwa mwezi (hii ikijumuisha na michango ya mashirika ya kijamii-social services ya mwajiri)kwa wafanyakazi hao kwa mwaka ni sawa na kusema unahitaji Trilion 4.2 kwa mwaka (350,000*1,000,000*12) na siyo kadirio la Trilioni 6.0 kama alivyosema Mhe. (WENYE TAKWIMU SAHIHI MNAWEZA KUCHANGIA).

    Katika hilo, Serikali inachukua Kodi (PAYE) tuchukulie wastani wa Asilimia 15 ni sawa na Bilioni 630. Hivyo kiasi kamili Serikali inachotakiwa kulipa ni kama Trilioni 3.6.

    Hiyo Trilion 3.6 ukiiangalia kwa mapana yake (Multiplier effect) yake ni kuwa hao wafanyakazi wataweza kuajiri watu wengine, kuwatumia Ndg. zao wa vijijini, kuongezeka kwa uwezo wao wa kununua (purchasing power) n.k.

    Tathmini yote ya hapo juu haijaangalia Upande wa sekta binafsi ambao nao unamchango mkubwa tu katika kodi hususan kodi ya mapato ya PAYE.

    Hivyo USHAURI wa BURE kwa Mhe. Rais na waandaji/Washauri wake wa karibu kuwa, unapotoa Hotuba ya Jazba ya namna hiyo ni vyema ukaitoa kwa uchambuzi wa KINA na KITAALAMU hususan unpojibu hoja ya msingikama hiyo.

    Kwa mtazamo wangumHe. Rais. hapo umetumia JAZBA na siyo Busara katika kujibu swal la msingi kama hilo.

    MDAU.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 04, 2010

    kazi ipo na hizi TAARABU za upwani-upwani!!!

    aisee JK usijisahau hivo ndugu,wewe ni mtu tu kama sie wengine sawa?sasa unapoita hao wazee ambao ndo sie tunawalisha badala ya kuongea na wasomi/wafanyakazi wenyewe na lako lilikua na KUMTUSI MGAYA tukuiteje wewe?

    personal attacks

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 04, 2010

    Kama kuna hotuba mbaya zilizowai kutolewa na rais wa nchi hii basi aishindi hii. inashangaza kabisa rais kuja mbele ya wananchi wake wanaoitwa wazee na kuanza kufoka!! na hao wazee masikini kwa kutojua walifanyalo wakaanza kushangilia hoja nyepesi kabisa zilizokuwa zikitolewa na kikwete. mimi nafikili kikwete anacheza na wafanyakazi.wafanyakazi ndio wanaomfanya yeye na serikali yake wawe hivyo walivyo. hivi ni kweli rais ameshindwa kwa upeo wake kuona hoja ya msingi ya wafanyakazi? kazi ipo wana ccm.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 04, 2010

    kwa kweli Kikwete kapotea hivi hao waliokuwa wanaomshangilia walipewa nini akili zikaruka , watanzania wa sasa si wazamani tunajua mbivu na mbichi . na maneno mengi tena kama ya waimba taaarabu hayajengi nchi. Ama kweli yalikosekana Matarumbeta tu jana maanake dar siku Hizi wanasutana kwa matarumbeta.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 04, 2010

    TANZANIA HAITAKAA INDELEE KAMA RAISI WA NCHI ANAWATISHIA WAFANYAKAZI BADALA YA KUSILIZA KILIO CHAO, HUU NDIO UJINGA UNATURUDISHA NYUMA.WATANZANIA AAMKENI UCHAGUZI UNAKUJA BADILISHENI VIONGOZI WENU.NJIA PEKEE NI KUPIGA KURA.NCHI ZA WENZETU ZIMEENDELEA KWA KUWA VIONGOZI WANAWASILIKIZA WANANCHI. MANENO KAMA HAYO YA KIKWETE ANGEKUWA RAHISI WA MAREKANI INGEKUWA BALAA HUKU WANANCHI WANATAKA WASIKILIZWE SHIDA ZAO.
    JK AMEONYNYESHA NI JINSI GANI VIONGOZI WA AFRICA WANAENDESHA NCHI ZAO

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 04, 2010

    Shikamoo Hon President Jakaya,

    Mimi Mtanzania,niliye wai kufanya kazi na wizara fulani kwa mda nakuacha, kwa sasa niko Sweden na shule yangu ni nzuri,infact Phd in international Trade,

    Hivyo basi, kwa maelezo ya jana umechemka tena sana. Watumishi ndo watekelezaji wakuu wa ilani ya CCM,iweje uwaone hawafai kiasi hicho,

    Dunian kote hakuna shirika/au taasisi iliyofanikiwa bila kuona rasilimali kama mtaji wa kutosha kuleta mafanikio, Iweje leo uwadharau kiasi, We ni nani?

    Wewe ni rahisi,uko hapo kwa Kipindi na unaweza ukatolewa tu! Unaposema mtumishi wa umma na mlinzi anayekulinda yupo, tafadhli be sensintive.

    Sitakulaumu sana, nataka niongelee juu ya washauri wako na wasaidizi wako na mkurugenzi wa Mawasiliano,

    Nyinyi hamfai ndo mnasababisha president wetu anachafua jina lake, hamumwambii ukweli bali mnachonganisha,
    Kimsingi watumishi wana haki, japo mshahara wanao itaji haiwezekani lakini nao wanaitaji majadiliano yenye tija kwao.

    Leo hii,Mkurugenzi in a months anaweza aingize more than ten million,mbunge over 20 millions lakini secretary wake tu 200,000 ameweka na allowance, maisha yake hayafananii Ps wa Director? Ni utumishi gani huo?



    Watu smart always wanafanya vitu smart, na watu ovyo always wanafanya vitu ovyo. Wasaidizi wako na washauri wako kuna uwezekano mkubwa kufanya vitu ovyo,ni ushauri wa bure tu, Watu wenye tabia chafu kuwa ikulu ni dhahili dhamira yao ni Kufanya uchafu,mambo ya msingi hawatampelekea ukweli. Tafadhali naiomba tume ya maadili kuweka kipengele cha maisha na mwenendo kiujumla ya mtumishi yoyote anaye enda Ikulu awe ametakasika kila eneo na ni makini Kumsaidia president. Haya yanayotekea ni dalili za kuzungukwa na watu wachafu wa tabia na mienendo mibovu.

    Leo taifa kama Tanzania halina watumishi. Dr,Walimu,IT,Lecturer alafu unamshauri rahisi aseme "ambaye hatosheki na mshahara aache aende kwingine, yeye amebaki hapa kwa sababu ni nyumbani na heri kwa Mtanzania kabwela aliyeko huko Uparen MVUNGWAMA kwani atapata huduma.

    Siseme walipwe hiyo wanayotaka, nasisitiza kuwa Kuheshimiana ni jambo la msingi katika maendeleo ya Taifa. Rweyemamu awajibike kwa kudhalilsha heshima ya Rahisi. Wewe rahisi ana tatizo na watumishi anaenda kuhutubia wazee wa Dar tena wengi wao wacheza bao na karata hapo kariokoo! ndo wafanyakazi hao? TUGHE.TUCTA wakitana kuonana na rahisi wanaambiwa yuko busy,Mda alioenda kuropoka tu na Wazee hao basi angehutubia nchi nzima mambo mengine ya msingi. So what ameshusha hekima yake? najua wafadhaina wake hapo ikulu wamefurai kwa hasira ya rahisi lakini ni aibu kwa Taifa na Bara la Afrika.

    Dr Matungwa

    ReplyDelete
  33. Wale wazee waliokuwa wanashangilia jana wameshapata PESHENI zao? au Ndo kufurahia tisheti za njano? kweli Bongo ya wabongo haina wenye bongo

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 04, 2010

    jamani hawa si wale wazee waliolala pale daraja la salender asubuhiii kuzuia magari yasipite hadi kieleweke leo hii wamekuwa wanafiki ati wamejifanya kusahau ghafla mmelogwa kweli nyinyi ovyo sana

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 04, 2010

    Hi michuzi,
    Pole kwa Kazi ngumu, basi leo hata post maoni yangu haya! Maana nimejaribu mara kwa mara kutuma news zangu kutoka huku china naona huna time nazo hasa zile za Masanja na madawa.

    Langu ni President Jakaya Mrisho,
    La jana ni aibu,anawadhalilisha watalaamu wake kama wamechokwa. Ebu tafakari kama wakigoma tu hata halmashauri 30 atapata wapi watu competent kujaza nafasi hizo? Anasema wakitaka waache wapo watu wengi wanatafuta kazi?

    Lkn yote Kurugenzi yake ya Mawasiliano haiko makini(Rweyemamu)huwezi kumuandalia hadhara hiyo na kutoa hotuba hiyo pale,

    Washauri na wanausalama wake,hawako makini kumuelekeza President na kumpa taarifa sahihi,

    Napendekeza kuanzia mfagiaji wa ikulu hadi juu, Kabla ya kufanya Kazi pale basi tume ya Maadili,PCCB,Commissioner Right,Usalama wafanye kazi ya Kupitia historia na mienendo yao ili wapeleke watu makini pale, Mtu kama ana tabia za ovyo hata kwenye familia ujue na mambo yake ni ovyo uovyo huo ataingia nao ikulu matakeo IKULU inakuwa ya ovyo.

    La jana ni wasaidizi na watumishi wa ikulu ovyo wamelisababisha. Raisi ameongea bila data wala fact.

    Umakini katika utumishi wa umma utawezesha mafanikio makubwa ya maisha ya Mtanzania. Na Raisi akiwa na watu makini pembeni basi maamuzi na matendo yake yatakuwa makini.

    Tafadhali nyinyi watu wa ikulu msilewe allowance hizo na kuwa busy na ya Dunia mkasau Wantazania wenzenu.

    Tafadhili kurugenzi ya mawasiliano,wanausalama, washauri wa Raisi mpe taarifa sahihi sio mnamuingiza mjini.

    Mdau China.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 04, 2010

    Hv mshkaji atatudanganya hadi lini? Eti mshahara ukifika 315,000 kwa mwezi ni sawa na tilioni 6.8 which more than mapato yetu! Mbaya zaidi anasema wafanyakazi wa serikali ni kama 350,000 hv, sasa wadau emu changieni 315,000*350,000*12 kweli ni sawa na tilioni 6.8!!!??!!

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 04, 2010

    Chondechonde JK Next time tuachie muda wetu ni bora tumuangalie PRETA kuliko kukusikiliza, ita wazee wako hukohuko kimyakimya, tafadhari sana.

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 04, 2010

    Majumuisho ya maoni haya yote ni " Mchimba kaburi kaingia mwenyewe",mkubwa anamalizwa na ushauri potovu, hiki ni kipidi sensitive wenzake wamemzunguka yeye bila kujua anatoa hotuba zinazomjengea uadui na wanachi ili wanaotaka madaraka wachukue, sasa tayari, kurudisha picha nzuri haiwezekani, hotuba hii imemaliza kila kitu, sijui itakuwaje maskini, watu wajanja kweli kweli, wamemaliza kazi kiualaiiiiiiiiiiiini.

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 04, 2010

    WATAJIJU... HAO WANAODAI MISHAHARA MBONA NA HOUSEGIRL NA HOUSEBOY WAO WANA-WANAWANENGA MISHAHARA YAO HIVYO.. MKUKI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU.

    WEWE UNAEDAI WABUNGE NK UMEKATAZWA KUGOMBEA???

    ABOVE ALL I LOVE LUKUVU SANA SIJUI WHY... MICHUZI TUMA SALAM

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 04, 2010

    Aiseeh......! Hivi wale EPA, RICHMOND, IPTL na......wengineoo ......na kule Bandarini walikoongeza mkataba juu ya mkataba, hivi hawa ndio wapiga kura wa kweli.....maana Mjomba kimyaaaa...hata kununa !!! haya bwana, si umesema nisikupigie, sawa nimesikia na Ahsante.

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 04, 2010

    .....Mbayuwayu akapaaaaaaaaa.... blah blahahh blaaah.....mbayuwayuuuuuuuuuuuuuu akapaaa weeeeeeee........ mbayuwayuuu huyuuuuuuuu.... blahhh blaaahhh blaaah..... Mbayuwayu akajulikana alikuwa fisadi ......... blah blah blahh

    ReplyDelete
  42. MZALENDO.May 04, 2010

    This is pathetic, raisi wa nchi anaona mambo yamemzidi kimo ndio anaamua kuviita vijizee vya watu na kuvipa soda na msosi halafu anapata watu wa kumshangilia. Katika hiyo hotuba yake mbona hajajibu madai ya TUCTA kwamba serikali inatenga mabilioni (5.6 bilioni TShs) kwa ajili ya marupurupu na kugharimia safari za viongozi? Mbona hajajibu tuhuma zilizotolewa na TUCTA kwamba serikali yake inafuja fedha za umma kwa matumizi yasiyo ya lazima ya kununua mashangingi kila mwaka, fedha ambazo aidha zingetumika kuwaongezea kipato watumishi wa umma au kuboresha maisha duni ya watanzania. Lakini mitanzania imeshazoea kuishi kwenye ufukara ndio maana CCM itachaguliwa tena na itaendela kuongoza. Sijui tumelogwa!!!

    PS. Michuzi isiiminyie comment yangu.

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 04, 2010

    nimecheka sana mdau wa mbayuwayu mbavu zangu zinauma lool!!

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 05, 2010

    PLEASE MR PRESIDENT,
    KUWA MUUNGWANA,WAOMBE RADHI WAFANYAKAZI KWA STYLE YOYOTE ILE.KWELI HOTUBA YAKO ILIKUA THE WORSE OF ALL NILIZOWAHI KUSIKIA KUTOKA KWA WATU MAKINI.MIMI SI MFANYAKAZI ILA NIMEONA AIBU MNO(WENZETU WA JIRANI WANAOJUA KISWAHILI WANATUCHEKA)-UMEONGEA KISWAHILI MNO!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...