Dear bro Michuzi Hope this mail meets you in good health and spirit
Naomba msaada kaka mimi ni mjasiriamali ambaye nimejitahidi na hatimaye nimeweza kununua kausafiri kadogo.
Siku ya jumatano 28 April nikiwa maeneo ya barabara mkwepu karibu na ofisi za sensa nilidondosha rimoti ya hiyo gari ambayo kwa bahati mbaya sikujua kwani niliingia kwenye stationery kwa kipindi kifupi kuulizia kitu fulani na niliacha mtu kwenye gari(sikuzima gari) hivyo nilivyorudi tuliendelea na safari bila ya kujua kama nilikua nimeshaidondosha.
Kaka naomba unitolee tangazo kwenye glob yetu ya jamii ili kama kuna mtu ameiokota aweze kunirudishia kwani nimepata usumbufu mkubwa sana Kwa yoyote atakayekua ameiokota naomba anijulishe kwa namba hizo:
0719 729182 au 0713 021 052 -Dada Happy
Thanks and best Regards

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2010

    mdau hebu fafanua,remote ya nini? kuna gari zina remote za dvd/cd player,remote ya gari ipi?au unamaanisha FOB?ulishukaje na FOB ukaacha funguo?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2010

    Matusi huwa mnayatafuta wenyewe wakati mwingine.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2010

    Uliingia Stationery? Stationery ndio wapi ?





    Mzee wa Ununio

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2010

    Unazungumzia keyless car remote au? Na kama ni hiyo kwanini utembee nayo peke yake bila kuiweka kwenye keyholder yako. Hata kama gari mnashare na kila mtu ana ufunguo wake ni lazima basi uwe na keyless remote mbili...ili isiwe kila ukitaka kumwachia gari mwenzako basi keyless remote uitoe kwenye ufunguo..Mimi najua wanauzaga mbilimbili kama walikuuzia moja wamekula...kama huna nyingine unaweza kununua nyingie ambazo nadhani ni universal na kuiprogram upya sio lazima upeleke gari kwa fundi wakatengeneze the whole thing again...

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2010

    Nafikiri unaweza kuchukua hatua zaidi kwa kutoa tangazo katika mtaa uliopotezea, bandika matangazo katika eneo hilo na kuahidi zawadi kidogo.

    Mtaa wa Mansfield unaoungana na huo wa Mkwepu una wezi wa vifaa vya magari wengi kupindukia sasa kama mmoja alivuka mpaka na kufika eneo hilo anaweza kukusaidia kwani wao hujichukulia wenyewe na hakuna anayethubutu kuwataja mtaani hapo, sembuse akipata cha kuokota?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...