
Tunashukuru MUNGU kwa kila jema alilotujaalia mpaka muda huu, pumzi ya uhai ndio kitu kikubwa kuliko vyote. Milima na mabonde, vizingiti na mito, maziwa bahari kwa uwezo wake tu tutavuka.
Miaka 5 ya urafiki na miaka 5 ya ndoa. 5+5 = Jumla 10
Tumeshakuwa kama kaka na dada, more than friends
Mimi nahesabu bado miaka 35 nifikie malengo kama ile anivessary nilioipost juzi; Itimie miaka 40 au ikibidi hata 50
MUNGU BARIKI
Ijumaa tutakuwa Zhong Hua kama kawaida tutasherehekea hapo, na yoyote atakae penda kuja kujumuika na sisi anakaribishwa. Machozi Band itaunguruma kama kawaida.
Miaka 5 ya urafiki na miaka 5 ya ndoa. 5+5 = Jumla 10
Tumeshakuwa kama kaka na dada, more than friends
Mimi nahesabu bado miaka 35 nifikie malengo kama ile anivessary nilioipost juzi; Itimie miaka 40 au ikibidi hata 50
MUNGU BARIKI
Ijumaa tutakuwa Zhong Hua kama kawaida tutasherehekea hapo, na yoyote atakae penda kuja kujumuika na sisi anakaribishwa. Machozi Band itaunguruma kama kawaida.
Wadau Lady JD & Gadna G. Habash
------------------------------------------
Globu ya Jamii inatoa pongezi za dhati kwa Lady JD na Gadna G. Habash kwa kusherehekea siku hii na kama walivyoomba wao wenyewe inawatakia watimize ya kusherehekea miaka 40 ama 50 wakiwa vijeba pamoja. Nyie ni mfano wa kuigwa kwa vijana kwa kuonesha urafiki na mapenzi kuwa ni kitu kimoja, kushirikiana katika mihangaiko yote kwa pamoja kama mlivyoapa siku ile ambayo nilibahatika kuwa mpiga picha pekee, na kuwa pamoja katika shida na raha kiasi ya kufurahisha. Ni wachache wako kama nyinyi, japo Jide ni Chelse na Gadna ni Bwawa la Maini mwenzangu. Libeneke oye!
-Michuzi
Duh, Ebwana eeh, hiyo harusi ilifungwa na nani, maana hilo vazi la Jay Dee sitegemei kama liliingia kanisani au msikitini !!!
ReplyDeletedu kivazi
ReplyDeletesio kila harusi lazima ifungwe kanisani au msikitini
ReplyDeleteMtajiju !! wambea nyie ....
ReplyDeletenyie mmeolewa ay mmeowa ?
wivu tu !!
mnahangaika na dunia
mdau
kkoo
Hicho kivazi cha bi harusi mie hoi!
ReplyDeleteThatwhy hii harusi ilifungiwa baharini mungu wangu kivazi noma mtoto alitoka ile mbaya kudadadeki walitisha.
ReplyDeleteAnyway wamependeza mungu awape maisha mazuri tunasubiri miaka 15 mingine ijayo mashallah. Kiukweli walipendeza.
MUM
Gadna Habash alimpenda JD kama alivyo na si kinginecho. Na wanamachi.
ReplyDeleteKIVAZI ..hoiii! hongereni lakini
ReplyDeletehilo vazi sijui.....
ReplyDeleteMIJITU MINGINE HUMU NDANI INA ROHO MBAYA KAMA MASHETANI!!MNASHINDWA KUWAPA HONGERA MMNAENDA KWENYE MAVAZI,ACHENI ROHO MBAYA JAMANI..JIDE NA GADNER HONGERENI SANA NAWAPENDA NA NITAENDELEA KUWAPENDA NA MUNGU AWABARIKI SANAAAAA!!!MLIPENDEZA KWA KWELI.....MDAU NORWAY
ReplyDeleteRoho mbaya unayo wewe Anno wa Fri May 14, 01:18:00 PM, kuita watoto wa wenzio mijitu! Koma!Kila mtu anawaza na kusema tofauti!Ubinadamu utakuwa wapi sasa?
ReplyDeleteHe he wenzangu tuwape hongera, kwani kivazi kinataabu gani?
ReplyDeleteRoho mbaya na tena chafu unayo wewe ambaye unaona ni kitu chema kwa vile uko huko Norway na unawaona wa huko wakikaa na chupi tupu unadhani ndiyo kuendelea. Ngoja na siku hiyo utakayorudi Bongo hala watoto zako wakaye chupi tupu mbele ya Baba yako ndipo utajua. halafu nyie ndiyo mnapotosha watu. Watu wengine Bwana, YAANI KUKAA NORWAY ANAONA AMEMALIZA NA KUDHARAU TAMADUNI ZA KWAO.
ReplyDeleteWacha sisi tuwafunde walio wa kwetu waendane na Utanzania.
Au unataka ktutangazia kuwa uko Norway?? ACHA USHAMBA.
hongereni sana!
ReplyDeletemiakamitano mnastahili pongezi maana mmevumilia maneno ya watu.
je, mna watoto wangapi???
Namuona Vivian Tillya kwa mbali,RIP my former school mate!
ReplyDeleteJide na Gadner nawafagilia sana tu mpo juu zaidi nawapenda ninyi ni hustlers..Gadner take care of Judith she is an a gold try never to loose her.
May God give u "till death do us apart or forever life"
mavazi kitu gani wewe kwani siyameletwa na mkoloni tuu, asili ya vazi la mwafrika ni kufunika baadhi tu ya viungo vya mwili,so hilo vazi la Jide ni poa kabisaa. By the way J n G hongereni saana
ReplyDeleteHa! Kitovu nje mpaka siku ya Harusi jamani! It is completely diaphanous! What are you JD?
ReplyDeleteMi kinachonifanya hata nisitoe comment zangu kwa jaydee ni tabia yake ya kutopenda kukosolewa ninaimani kuwa hata annony wa 11:37 itakuwa ni yeye mwenyewe anaejibu.so simuelewi maana kila mtu anamapungufu na nilazima uyakubali pale mtu anapojaribu kukueleza mapungufu hayo.Vilevile usipende watu wanaokusifu tu hata kama kunabaya umefanya maana kule kwenye blog yako ndio watu wanavyokusifia wengine unaona kabisa hii ni unafiki so jaribu kuwa makini na watu hao labda nikupe ujanja mmoja wa kuweza kuwajua watu hao,weka tukio tu la kijinga ambalo hata wewe mwenyewe umeona ni ujinga then wawekee wadau wako wa comment from that utajua wapi wanafiki na wapi ndio wanaokupenda kweli.Hongereni sana ila hiyo nguo haikustahili tafrija yako.Wakati wa Mungu Mpe Mungu na wakati wa ujinga mpe shetani.
ReplyDeletebimkora!!!!!
vipi watoto mbona hawajasema
ReplyDeletemdau hapo juu mwenye roho mbaya kama shetani ni wewe kwani we ulijuaje kama shetani ana roho mbaya kama si shoga ako ukomeeee chukua time kuleee
ReplyDeletemdau iraq
mmependeza
ReplyDeletehahahaha nicheke mie
ReplyDeletekweli gadner na jide mlitia aibu ndo maana hamkutaka ata picha zenu zionekane,sidhani ata kama mna baraka za mungu
Hii ndoa ata ikidumu milele sidhani kama itakua na baraka
Mmh hongera dada JD na Gadna, lakini mke na mume mkianza kuzoeana kama dada na kaka si ishara nzuri, jitahidi mume wako kila siku umfanye mpenzi, umuenzi na wala zio kumzoea. penzi likiwa jipya kila siku mnakuwa hamchokani.
ReplyDeleteHongereni sana.
Jamani mmependeza sana. Mimi nina miaka 35 ya ndoa na nina hakika na nyinyi mtafikisha tu. Mungu awabariki. Maisha ya ndoa ni kama gari unapoiendesha barabarani unakutana na mashimo mara unakutana na barabara imenyooka ila gari huikimbii na kuiacha iende yenyewe.
ReplyDeletejamani, naomba niseme hivi na naomba nieleweke hivi, kama mmeamua kutopata mtoto sasa pateni mtoto jamani, ila kama ni mipango ya Mungu basi. ila hongereni sana
ReplyDeleteWabongo, bwana. Kwani watoto lazima? Mmafanya watoto lazima na kuwanyanyapaa mpaka ambao Mungu mwenye kaamua wawe hivyo. Unyanyapaa wenu unafanya mpaka akina dada wengine wanaiba watoto. Unyanyapaa wenu unafanya mpaka wengine wanajiua. Unyanyapaa wenu unafanya ndoa zinavunjika.
ReplyDeleteWatoto anatoa Mungu. Si vizuri kumuuliza mtu kwa nini hana watoto - whether kaamua yeye mwenyewe au kwa mpango wa Mungu. Watoto ni matokeo tu. Hakuna anayepata watoto kwa bidii yake mwenyewe.
Mhh. Naona hii picha ndio ilikuwa nzuri/afadhali kuliko zote. Nina wasiwasi na mapenzi ya Gadna kwa huyu dada. Hivi unayempenda unaweza kumruhusu akae uchi kiasi hicho? Na ni msajili yupi wa ndoa mliyekwenda kumwonyesha mwili. Mwanamke shurti ujisetiri maungo yako. Mimi kusema kweli namshauri JiDe sasa amekuwa mtu mzima hebu ajitahidi kuwa wa heshima, mwogope MUNGU. Mambo mengine yanaweza kuleta laana kwenye familia ukaanza kutafuta mchawi. Hayo ni maoni yangu michuzi ukitupa kwenye kapu sawa tu,lakini huyo rafiki/shemeji yako inabidi abadilike.
ReplyDeletekwa hilo vazi la jide kama ilikuwa ni shughuli ilyohudhuliwa na vijana pekee pasipo kuwepo wazazi au watu wazima wenye maadili na viongozi wa dini sawa. maisha mema wanandoa
ReplyDeletekama kaka na dada?wats this?
ReplyDeletehaya we. . .hata wazungu wenyewe hua havai hivyo kwa harusi, angalau wale wanaotunza heshima zao...
ReplyDeletehalafu mbona hatuwaoni kina kaka kutembea vifua wazi kuonyesha six packs zao?
HUYO LADY D NAEYE KWANI YUKO KWENYE HESABU YA MWANAMKE..MIMI SIONI KAMA MWANAMKE...MNAPOTEZA NGUVU TU KUPIGA MAKELELE
ReplyDeletevijana mmependeza sana muugu awabariki, kijana siyo kila kinachofanywa na wazungu tuige, kwa sisi wamatumbi haipendezi kusherehekeya vitu visivyo na faida yaelekeya huna uhakika nandoa yenu samahani saka kama nitakukera hela uliyotumiya kwa garama ya sherehe ugelisaidiya ndugu au jamaa wenye kuhitaji msaada au unaweza kusaidiya wagonjwa wasiyomudu garama za matibabu hivyo ndivyo wanavyofanya hao wazungu tunaowaiga mambo yaliyopitwa na wakati hivi sasa hata watoto wadogo huko ulaya husherehekeya siku ya kuzalili kwa kuchangisha kwa kusaidiya watoto wezao kupata matibabu ,elimu ,na majanga mbali mbali ,
ReplyDeleteWatu wengine bwana watoto wakuwapi watoto wako wapi...kama wanao si wangesema jamani? Watu wengine wameletwa hapa duniani sio kulea mtoto mmoja bali wengi...Sas huwezi jua kama wakiwa na wakwao hawataweza kufanya wanayoyafanya na hiyo yote ni mipango ya Mungu...
ReplyDeleteWaacheni siku ikifika kamawameandikiwa kupata mtoto watapata....
nachukia sana rafiki yangu huku wameoana mwaka jana sasa hivi nyumbani kwao huko tanzania kila siku ni kuwa bado tu ..Agrrrrrr..Jamani wenzenu wanalipa kwanza madeni ya hela wazizotumia kuwaleta huku...Nyie mmekuja kwenye harusi na kusherekea mlizania hela zilitoka wapi...Wanamalengio yao...Na sio kuolewa tu basoi mtoto ...
INABIDI TUBADILIKE ...na alivyovyaa kwa harusi yake is non of your business...Kwani nguo za kimasai zikoje...Si hapo ni kuwa rangi ilikua nyeupe tu....Mimi wla simjui huyu mwimbaji lakini hey mwacheni afurahie harusi yake...Mnaosema haina baraka kwa Mungu nyie ni nani...Toeni boriti na msizoee kuhukumu watu msije mkahukumiwa...sorry too long but I need to vent...
Hongera na Mungu awajalie na kuwazidishia maisha mema