Tunashukuru MUNGU kwa kila jema alilotujaalia mpaka muda huu, pumzi ya uhai ndio kitu kikubwa kuliko vyote. Milima na mabonde, vizingiti na mito, maziwa bahari kwa uwezo wake tu tutavuka.

Miaka 5 ya urafiki na miaka 5 ya ndoa. 5+5 = Jumla 10
Tumeshakuwa kama kaka na dada, more than friends
Mimi nahesabu bado miaka 35 nifikie malengo kama ile anivessary nilioipost juzi; Itimie miaka 40 au ikibidi hata 50
MUNGU BARIKI
Ijumaa tutakuwa Zhong Hua kama kawaida tutasherehekea hapo, na yoyote atakae penda kuja kujumuika na sisi anakaribishwa. Machozi Band itaunguruma kama kawaida.
Wadau Lady JD & Gadna G. Habash
------------------------------------------
Globu ya Jamii inatoa pongezi za dhati kwa Lady JD na Gadna G. Habash kwa kusherehekea siku hii na kama walivyoomba wao wenyewe inawatakia watimize ya kusherehekea miaka 40 ama 50 wakiwa vijeba pamoja. Nyie ni mfano wa kuigwa kwa vijana kwa kuonesha urafiki na mapenzi kuwa ni kitu kimoja, kushirikiana katika mihangaiko yote kwa pamoja kama mlivyoapa siku ile ambayo nilibahatika kuwa mpiga picha pekee, na kuwa pamoja katika shida na raha kiasi ya kufurahisha. Ni wachache wako kama nyinyi, japo Jide ni Chelse na Gadna ni Bwawa la Maini mwenzangu. Libeneke oye!
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2010

    Duh, Ebwana eeh, hiyo harusi ilifungwa na nani, maana hilo vazi la Jay Dee sitegemei kama liliingia kanisani au msikitini !!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2010

    du kivazi

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2010

    sio kila harusi lazima ifungwe kanisani au msikitini

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 14, 2010

    Mtajiju !! wambea nyie ....

    nyie mmeolewa ay mmeowa ?

    wivu tu !!
    mnahangaika na dunia

    mdau
    kkoo

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 14, 2010

    Hicho kivazi cha bi harusi mie hoi!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 14, 2010

    Thatwhy hii harusi ilifungiwa baharini mungu wangu kivazi noma mtoto alitoka ile mbaya kudadadeki walitisha.

    Anyway wamependeza mungu awape maisha mazuri tunasubiri miaka 15 mingine ijayo mashallah. Kiukweli walipendeza.

    MUM

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 14, 2010

    Gadna Habash alimpenda JD kama alivyo na si kinginecho. Na wanamachi.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 14, 2010

    KIVAZI ..hoiii! hongereni lakini

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 14, 2010

    hilo vazi sijui.....

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 14, 2010

    MIJITU MINGINE HUMU NDANI INA ROHO MBAYA KAMA MASHETANI!!MNASHINDWA KUWAPA HONGERA MMNAENDA KWENYE MAVAZI,ACHENI ROHO MBAYA JAMANI..JIDE NA GADNER HONGERENI SANA NAWAPENDA NA NITAENDELEA KUWAPENDA NA MUNGU AWABARIKI SANAAAAA!!!MLIPENDEZA KWA KWELI.....MDAU NORWAY

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 14, 2010

    Roho mbaya unayo wewe Anno wa Fri May 14, 01:18:00 PM, kuita watoto wa wenzio mijitu! Koma!Kila mtu anawaza na kusema tofauti!Ubinadamu utakuwa wapi sasa?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 14, 2010

    He he wenzangu tuwape hongera, kwani kivazi kinataabu gani?

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 14, 2010

    Roho mbaya na tena chafu unayo wewe ambaye unaona ni kitu chema kwa vile uko huko Norway na unawaona wa huko wakikaa na chupi tupu unadhani ndiyo kuendelea. Ngoja na siku hiyo utakayorudi Bongo hala watoto zako wakaye chupi tupu mbele ya Baba yako ndipo utajua. halafu nyie ndiyo mnapotosha watu. Watu wengine Bwana, YAANI KUKAA NORWAY ANAONA AMEMALIZA NA KUDHARAU TAMADUNI ZA KWAO.
    Wacha sisi tuwafunde walio wa kwetu waendane na Utanzania.
    Au unataka ktutangazia kuwa uko Norway?? ACHA USHAMBA.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 14, 2010

    hongereni sana!
    miakamitano mnastahili pongezi maana mmevumilia maneno ya watu.
    je, mna watoto wangapi???

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 14, 2010

    Namuona Vivian Tillya kwa mbali,RIP my former school mate!

    Jide na Gadner nawafagilia sana tu mpo juu zaidi nawapenda ninyi ni hustlers..Gadner take care of Judith she is an a gold try never to loose her.

    May God give u "till death do us apart or forever life"

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 14, 2010

    mavazi kitu gani wewe kwani siyameletwa na mkoloni tuu, asili ya vazi la mwafrika ni kufunika baadhi tu ya viungo vya mwili,so hilo vazi la Jide ni poa kabisaa. By the way J n G hongereni saana

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 14, 2010

    Ha! Kitovu nje mpaka siku ya Harusi jamani! It is completely diaphanous! What are you JD?

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 14, 2010

    Mi kinachonifanya hata nisitoe comment zangu kwa jaydee ni tabia yake ya kutopenda kukosolewa ninaimani kuwa hata annony wa 11:37 itakuwa ni yeye mwenyewe anaejibu.so simuelewi maana kila mtu anamapungufu na nilazima uyakubali pale mtu anapojaribu kukueleza mapungufu hayo.Vilevile usipende watu wanaokusifu tu hata kama kunabaya umefanya maana kule kwenye blog yako ndio watu wanavyokusifia wengine unaona kabisa hii ni unafiki so jaribu kuwa makini na watu hao labda nikupe ujanja mmoja wa kuweza kuwajua watu hao,weka tukio tu la kijinga ambalo hata wewe mwenyewe umeona ni ujinga then wawekee wadau wako wa comment from that utajua wapi wanafiki na wapi ndio wanaokupenda kweli.Hongereni sana ila hiyo nguo haikustahili tafrija yako.Wakati wa Mungu Mpe Mungu na wakati wa ujinga mpe shetani.
    bimkora!!!!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 14, 2010

    vipi watoto mbona hawajasema

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 14, 2010

    mdau hapo juu mwenye roho mbaya kama shetani ni wewe kwani we ulijuaje kama shetani ana roho mbaya kama si shoga ako ukomeeee chukua time kuleee
    mdau iraq

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 14, 2010

    mmependeza

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 14, 2010

    hahahaha nicheke mie
    kweli gadner na jide mlitia aibu ndo maana hamkutaka ata picha zenu zionekane,sidhani ata kama mna baraka za mungu
    Hii ndoa ata ikidumu milele sidhani kama itakua na baraka

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 14, 2010

    Mmh hongera dada JD na Gadna, lakini mke na mume mkianza kuzoeana kama dada na kaka si ishara nzuri, jitahidi mume wako kila siku umfanye mpenzi, umuenzi na wala zio kumzoea. penzi likiwa jipya kila siku mnakuwa hamchokani.
    Hongereni sana.

    ReplyDelete
  24. ADILI NA NDUGUZEMay 14, 2010

    Jamani mmependeza sana. Mimi nina miaka 35 ya ndoa na nina hakika na nyinyi mtafikisha tu. Mungu awabariki. Maisha ya ndoa ni kama gari unapoiendesha barabarani unakutana na mashimo mara unakutana na barabara imenyooka ila gari huikimbii na kuiacha iende yenyewe.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 14, 2010

    jamani, naomba niseme hivi na naomba nieleweke hivi, kama mmeamua kutopata mtoto sasa pateni mtoto jamani, ila kama ni mipango ya Mungu basi. ila hongereni sana

    ReplyDelete
  26. KalikaliMay 14, 2010

    Wabongo, bwana. Kwani watoto lazima? Mmafanya watoto lazima na kuwanyanyapaa mpaka ambao Mungu mwenye kaamua wawe hivyo. Unyanyapaa wenu unafanya mpaka akina dada wengine wanaiba watoto. Unyanyapaa wenu unafanya mpaka wengine wanajiua. Unyanyapaa wenu unafanya ndoa zinavunjika.

    Watoto anatoa Mungu. Si vizuri kumuuliza mtu kwa nini hana watoto - whether kaamua yeye mwenyewe au kwa mpango wa Mungu. Watoto ni matokeo tu. Hakuna anayepata watoto kwa bidii yake mwenyewe.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 14, 2010

    Mhh. Naona hii picha ndio ilikuwa nzuri/afadhali kuliko zote. Nina wasiwasi na mapenzi ya Gadna kwa huyu dada. Hivi unayempenda unaweza kumruhusu akae uchi kiasi hicho? Na ni msajili yupi wa ndoa mliyekwenda kumwonyesha mwili. Mwanamke shurti ujisetiri maungo yako. Mimi kusema kweli namshauri JiDe sasa amekuwa mtu mzima hebu ajitahidi kuwa wa heshima, mwogope MUNGU. Mambo mengine yanaweza kuleta laana kwenye familia ukaanza kutafuta mchawi. Hayo ni maoni yangu michuzi ukitupa kwenye kapu sawa tu,lakini huyo rafiki/shemeji yako inabidi abadilike.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 14, 2010

    kwa hilo vazi la jide kama ilikuwa ni shughuli ilyohudhuliwa na vijana pekee pasipo kuwepo wazazi au watu wazima wenye maadili na viongozi wa dini sawa. maisha mema wanandoa

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 14, 2010

    kama kaka na dada?wats this?

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 14, 2010

    haya we. . .hata wazungu wenyewe hua havai hivyo kwa harusi, angalau wale wanaotunza heshima zao...
    halafu mbona hatuwaoni kina kaka kutembea vifua wazi kuonyesha six packs zao?

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 14, 2010

    HUYO LADY D NAEYE KWANI YUKO KWENYE HESABU YA MWANAMKE..MIMI SIONI KAMA MWANAMKE...MNAPOTEZA NGUVU TU KUPIGA MAKELELE

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 14, 2010

    vijana mmependeza sana muugu awabariki, kijana siyo kila kinachofanywa na wazungu tuige, kwa sisi wamatumbi haipendezi kusherehekeya vitu visivyo na faida yaelekeya huna uhakika nandoa yenu samahani saka kama nitakukera hela uliyotumiya kwa garama ya sherehe ugelisaidiya ndugu au jamaa wenye kuhitaji msaada au unaweza kusaidiya wagonjwa wasiyomudu garama za matibabu hivyo ndivyo wanavyofanya hao wazungu tunaowaiga mambo yaliyopitwa na wakati hivi sasa hata watoto wadogo huko ulaya husherehekeya siku ya kuzalili kwa kuchangisha kwa kusaidiya watoto wezao kupata matibabu ,elimu ,na majanga mbali mbali ,

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 15, 2010

    Watu wengine bwana watoto wakuwapi watoto wako wapi...kama wanao si wangesema jamani? Watu wengine wameletwa hapa duniani sio kulea mtoto mmoja bali wengi...Sas huwezi jua kama wakiwa na wakwao hawataweza kufanya wanayoyafanya na hiyo yote ni mipango ya Mungu...
    Waacheni siku ikifika kamawameandikiwa kupata mtoto watapata....

    nachukia sana rafiki yangu huku wameoana mwaka jana sasa hivi nyumbani kwao huko tanzania kila siku ni kuwa bado tu ..Agrrrrrr..Jamani wenzenu wanalipa kwanza madeni ya hela wazizotumia kuwaleta huku...Nyie mmekuja kwenye harusi na kusherekea mlizania hela zilitoka wapi...Wanamalengio yao...Na sio kuolewa tu basoi mtoto ...

    INABIDI TUBADILIKE ...na alivyovyaa kwa harusi yake is non of your business...Kwani nguo za kimasai zikoje...Si hapo ni kuwa rangi ilikua nyeupe tu....Mimi wla simjui huyu mwimbaji lakini hey mwacheni afurahie harusi yake...Mnaosema haina baraka kwa Mungu nyie ni nani...Toeni boriti na msizoee kuhukumu watu msije mkahukumiwa...sorry too long but I need to vent...

    Hongera na Mungu awajalie na kuwazidishia maisha mema

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...