Mzee Michuzi,
Ninamajonzi mazito baada ya kuporwa begi ambalo niliweka ndani ya Gari yangu tarehe 23.05.2010, Nikiwa njiani kuelekea Gongo la Mboto ambako naishi, mke wangu ambaye ni mjamzito alijisikia vibaya kutokana na AC akashusha kioo na kupata hewa toka nje.
Kabla sekunde haijapita alijitokea kijana akawa kama anapita akaingiza mikono ndani ya gari na kuchukua begi lililo na fedha, Vitambulisho vya kazi, Insurance Card, na hata kadi za kliniki za mke wangu.Baada ya kurudi kufualitilia nilitajiwa jina la huyo kijana kuwa ni “Chege” Ni kijana anayefahamika na kila mtu anayeishi hapa mataa ya chan’gombe.
Nilienda kituo cha polisi wakaniuliza amevaa t-sheti gani?Mara baada ya kutaja rangi ya t-shirt walinitajia kuwa anaitwa Chege. Si hivyo tuu, jana nimeripoti tena kwa mwenyekiti wa Sungusungu hapa mataa ya chang’ombe na tukaenda tena kituo cha polisi, kesi ikafunguliwa, na wakatoa RB ya kuniwezesha kumkamata.Sasa cha ajabu ni kwamba huyo kijana amefanya matukio mengi sana, na Polisi wanajua hilo na wamesha wahi kumfunga.“ Kwa mahojiano na Polisi wa kituoni hapo yalijitokeza haya”
1. Polisi, Sisi huyo kijana tunamfahamu, anapatikana Keko mwanga eneo maalumu linaitwa „KEKO MWANGA” na tulisha wahi mfunga ila RAISI Kikwete akatoa msamaha na kijana akatoka na yupo tena barabarani ana kwapua.
2. Alisha wahi waibia hata wake za mawaziri na wabunge dola za kimarekani
Mzee Michuzi na wqadau mimi nifanyeje?
Mdau Benno

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

 1. AnonymousMay 25, 2010

  Hivi uwajibikaji wa Polisi unamuhusu nini JK?Suala la Parole linategemea maoni ya wasimamizi wa magereza labda hili ndio la kuangalia zaidi jinsi gani ya kuboresha parole kwa watuhumiwa wa mauaji na vibaka ila sioni sababu ya kumuingiza JK katika kadhia hii nzima.Kwani hata kabla yake yalikuwepo haya na mengi mengineyo mbona hamkuwahi kusema?Twajua huu ni wakati wa kampeni, suala la wizi ni suala la kushughulikia jamii ikishirikiana na polisi na vyema kuanzishwa mifumo ya kuwasaidia wafungwa wawapo magerezani kwa kuwasomesha na kuwapa changamoto za kujiendeleza kimaisha wakiwa katika majela na huu mfumo wa jela wa wakoloni tuuwache kwani hautusaidii kamwe!Jela ziwepo ila ziwe vituo vya mafunzo, na zianzishwe senta za kuwapa ushauri nasaha wale wanaotoka majela na kuwaanda wawe raia wema
  Tutaishi kwa amani na raha mustarehe
  Khamis Hassan Batanyaga

  ReplyDelete
 2. AnonymousMay 25, 2010

  Pole sana mzee, inaelekea huyo chege ni maarufu hapo, cha kufanya nenda hapo maeneo yake huyo jamaa(chege) na watu wako kama wawili walio fiti, chukua chege tia kwenye gari nenda nae mitaa unayoijua msulubu vizuuuri, hatorudia tena huyo, analindwa hata polisi inawezekana wanapata mgao!

  ReplyDelete
 3. Mtoto wa CoastMay 25, 2010

  Pole kwa yaliyokupata.

  Tuache kutafuta vihalalisho au visingizio.

  Yaani kwa vile Rais alitoa msamaha (nadhani wala si kwake pekee); je ndiyo iwe tiketi kuwa akifanya kosa asichukuliwe hatua?

  Wewe saidiana na askari wa aina zote wanaojua kazi zao na kujituma wakiwemo 'Polisi Raia' mumsogeze kwenye haki atashughulikiwa tu ipaswavyo!

  ReplyDelete
 4. AnonymousMay 25, 2010

  dawa ni kibiriti tu akionekana!!!!

  ReplyDelete
 5. AnonymousMay 25, 2010

  Kaka Michuzi, mimi nadhani watanzania sasa inabidi tuchukuwe responsibility kwa jamii tuliyoitengenea wenyewe badala ya kumlaumu JK kwa kila kitu. Sasa hata vibaka tunamlaumu Rais? Acheni hizo!!

  ReplyDelete
 6. NDUGU YANGU MI NAKUSHAURI KITU KIMOJA, MUHIMU ZAIDI NI KUPATA HIZO NYARAKA ZAKO, WE TUMIA UJANJA NENDA KIJIWENI KWAKE IKIWEZEKANA TOA KITU KIDOGO KWA WASHIKAJI ZAKE UTAPATA NYARAKA ZAKO (LAKINI SI PESA, UKIJIFANYA KUFUATA MFUMO WA SHERIA ITAKULA KWAKO, ATACHOMA MOTO VITU VYAKO KUPOTEZA USHAHIDI. USIAMINI MFUMO HUU WA SHERIA AMBAO UMEOZA, KAMA POLISI WANAMJUA MPAKA SHATI ANALOVAA KWA NINI WASIMKAMATE? JK ASILAUMIWE KWANI MSAMAHA UKO KISHERIA NA HUTOLEWA KWA USHAURI WA MAAFISA WA MAGEREZA, RAIS HAWEZI KUFATILIA MIENENDO YA TABIA ZA MAELFU YA WAFUNGWA KUONA KAMA WAMEJIREKEBISHA

  ReplyDelete
 7. AnonymousMay 25, 2010

  Olease tafuta utaratibu wa mob justice, maana correctional services haimtosh huyu kijana, ameishakuwa sugu.

  ReplyDelete
 8. AnonymousMay 25, 2010

  KAMA VIPI WEWE CHUKUA TU SHERIA MKONONI ILI UKOMESHE KABISA HUYU KIBAKA.

  UARABUNI ANAKATWA MKONO.

  ReplyDelete
 9. AnonymousMay 25, 2010

  Pole kwa yaliyokusibu, achana na Chege songa mbele na wakati mwingine uwe mwangalifu.

  ReplyDelete
 10. AnonymousMay 25, 2010

  MBONA HAPO CHANG'OMBE KUNA KITUO CHA MAFUTA KARIBU TU. NUNUA MAFUTA LITA TANO NA KIBIRITI, KAMATA HUYU CHEGE, MWAGIA MAFUTA, BIGA KIRIBITI. UKIBAKA WAKE UTAISHIA HAPO HAPO.

  ReplyDelete
 11. AnonymousMay 25, 2010

  Sasa hao polisi kuzumzia matukio aliyoyafanya huyo kijana na kusema kuwa aliwaibia hadi mawaziri ndo wana maana gani? wanachotakiwa kufanya ni kuanza ufuatiliaji wa huyo kijana ili qasiendelee na usumbufu kama vipi wampoteze tu,so waanza kusema maneno ya kumkatisha tamaa mzee wa wa2,fanyeni kazi kama vp waachie wananchi wafanye kazi yao....

  ReplyDelete
 12. AnonymousMay 25, 2010

  Nafikiri polisi wanachokitafuta kwa huyu Chege ni wananchi kutoa hukumu ya kifo cha kipigo cha wananchi wenye hasira.

  Kazi ya polisi ukiacha kusimamia sheria ni pamoja na kukamata wahalifu na kuwafikisha mahakamani. Sasa kama wao hawawezi hiyo kazi ni bora watafute mashamba wakalime waachie watu hilo zoezi.

  Mdau uliyeibiwa pole sana ila kama utaweza kuingia kahasara kidogo ka kuwapelekea supu hapo polisi basi watashughulikia, ukiona hivyo ujue wananjaa, na kwa kuwa wameshamjua muhalifu basi wanataka Rushwa tu ndiyo watekeleze majukumu yao. Nafikiri kuna haja ya raia wema kutembea na vya moto sasa, maana tuliowakabidhi watulinde wanashindwa majukumu yao.

  Kama mdau alivyopendekeza hapo juu, kwa kuwa una RB basi nenda kachukue Polisi kituo kingine wamkamate Chege, japo wao sheria zao ni lazima kituo cha eneo la tukio kiwe na taarifa. Vinginevyo kama mnaweza kasheshe maana ni lazima atakuwa na group lake basi mzukieni mumpeleke msitu wa PANDE ninyi wenyewe

  ReplyDelete
 13. AnonymousMay 25, 2010

  Pole mwenzetu, lakini hiyo ndiyo tanzania yetu. Sasa kama aloiba mamilioni ni jana tu kafungwa miaka miwili unataka kibaka apewe miaka mingapi?

  Nadhani ungelihangaika ukampata na kumuomba akurudishie documents zako na za mkeo mambo yaishe, pesa sahau hapo.

  Tanzania, tanzania nakupenda kwa moyo wote!

  ReplyDelete
 14. AnonymousMay 25, 2010

  pole sana ndugu yangu. yani umenitonesha kidonda. hao polisi hawana msaada wowote ndugu yangu chamuhimu ni uweze pata lose report tu. vijana wa keko mwanga ni balaaa. nimezaliwa huko yani ni balaa. ulivyopokonya wewe ndivyo nilivyopokonya tarehe 26/2/2010 na nikaenda kulipoti polisi cha kushangaza wakanijibu hatuwezi kukusaidi kwani huyo mtu simjui jina lake. nilipokonya mkoba wenye pesa taslimu laki saba simu 3, kadi ya gari na document nyingi. Pole sana na nakuomba usipoteze muda wako hao polisi hawafai hata kidogo, wamewekwa hapo ni sehemu yao ya kula rushwa tu. by Atuganile

  ReplyDelete
 15. AnonymousMay 25, 2010

  Hii imenikumbusha utotoni kule kwetu zanzibar, kulikuwa na kijana akiitwa kimbunga, naam ni kimbunga yaani alikuwa anafahamika mpaka ikulu. huyu jamaa akikupita tu inabidi uangalie mifuko yako, sio utani alikuwa ni mwizi wa ustadi wa juu kweli kweli, jela ilikuwa jambo la kawaida kwake.

  Pia kulikuwepo na mwengine huyu ni muhindi, naam ni muhindi, huyu mpaka alikuwa anasema gari ya polisi ni taxi zake na jela ni hoteli yake.

  Hawa walikuwa wafungwe maisha kutokana na vitendo vyao vya wizi, lakini serikali na mfumo mzima wa sheria nchini unawaangusha rai wema.

  Taymour
  UK

  ReplyDelete
 16. AnonymousMay 25, 2010

  kwa haraka haraka nadhani unao uwezo wa kumiliki bastola. Mtafute chege m-miminie njugu kadhaa basi, hatokwapua tena.

  ReplyDelete
 17. AnonymousMay 25, 2010

  Yaani Chege bado unaiba hadi leo??hadi unatoka kwenye vyombo vya habari!! nilisikia uliacha wizi...tumesoma wote Shule ya msingi Keko Mwanga na shule ya sekondari jioni pale chuo cha ualimu chang'ombe.Ukaacha shule kungali mapema, form two! madawa ya kulevya yamekuponza Chege!! ulianza bange mapema ukashindwa kui-control imekuzingua !!!nasikia ulikua unaiba hadi ndala nyumbani kwenu!! najua hii msg itakufikia kupitia kwa Kaka yako (simtaji jina) na atakwambia nani kaituma!Nimeshaongea naye kwa simu..Chegendo unatafuta kifo...unawaibia hadi wake za mawaziri!!Mama yako ameshakukana, Sijui utazikwa na nani! Nauona Mwisho wako Chege...kundi la wananchi wenye hasira wanakufukuza...tena si wale wa barabarani unakoiba simu, ni wale jirani kabisa na unapokaa, na hadi ndugu zako wamo katika kundi hilo la wananchi wenye hasira!! Habari zitazagaa kuhusu kifo chako keko zote tano (Keko magurumbasi, keko toroli, keko mwanga, keko magereza na keko machungwa)
  Kundi la wananchi wenye hasira Chegendo ndiyo watakaohitimisha safari yako ya uhalifu hapa duniani!!!

  ReplyDelete
 18. AnonymousMay 25, 2010

  Nadhani kuna baadhi ya watu mmemwelewa jamaa vibaya. Yeye hamlaumu JK ila anaeleza yale aliyoeleweza na Polisi. Pili anazungumzia kuibia hadi kwa wake za mawaziri which implies huyu jamaa ni popular. Sasa nini kinachomfanya anakuwa so popular kiasi hicho na hatua hazichukuliwi?. Kama unaenda kwa polisi unayeyushwa? Inabidi uende wapi sasa?. Msiba kwa mwenzio ila ukiwa kwako u can understand huyu jamaa anamaanisha nini?. Huzuni mtupu bongo

  ReplyDelete
 19. AnonymousMay 25, 2010

  Swala la vibaka ni wewe mtu kutoa street justice. Kama mdau alivyo kuambia nenda na jamaa wa kukodi, beba Chege peleka unakojua wewe, BONDA na NONDO magoti yote. Hapo utakuwa umepunguzia hata watu wengine kero za huyu jamaa. Usitegemee polisi wakusaidie. Sana sana watakuomba mafuba na utapoteza muda wako bure na vitu vyako usivipate. Na hata Chege asipotoa vitu hatakusahau maishani kwake. Hiyo diyo dawa pekee kaka.

  ReplyDelete
 20. We unaesema 'Achana na Chege songa....'' Yaani bado unataka tukae mitaani bila uhuru kwa kumuachia Chege aendelee tu kusumbua mitaani?????

  Kibiriti tu.... Nadhani hayajakukuta.... INAUMA!!!!

  ReplyDelete
 21. AnonymousMay 25, 2010

  Pole sana. Hayo ndiyo matokeo ya kuwa na nchi inayoongozwa na wahuni. Uhuni katika ngazi zote, ndiyo sababu mtu kama huyo anakuwa nje wakati anajulikana na alishawahi kukamatwa. Wanasema mvunja nchi ni mwananchi, na kwa hiyo pia mjenga nchi ni mwananchi. Tuamue kusuka ama kunyoa, Oktoba tuondoe wahuni na uhuni utaisha. Tukiamua kuendelea nao tuache kufikiri kutakuwa na mabadiliko. Hayadondoki kutoka mbinguni, tunayaleta wenyewe, tukiamua.

  ReplyDelete
 22. AnonymousMay 25, 2010

  Pole sana kaka yangu, umenikumbusha mabli sana pale rafiki yangu anayekuwa anaishi Salasala aliingiliwa na majambazi na mimi nilipoibiwa vitu vingi kwenye gari. Ukweli wenyewe tuliishiwa kuombwa hela kila siku na polisi eti kuwasaidia katika upelelezi. Ilikuwa mbaya zaidi pale tulipogundua kumbe baadhi ya SMS za vitisho zilizokuwa zinatumwa zilikuwa zinatoka kwa huyo mpelelezi kutoka pale kituo cha Kunduchi. Yaani ndipo nilipoamini kuwa Polisi ndiyo wezi kuliko hata hao majambazi kwani wakageuza mradi kutuma SMS za vitisho na kisha ukiwapa taarifa wanataka mkutano alafu wakuombe hela za kusaidia upelelezi.

  Kwa upande mwangine naamini hizo nyaraka ni muhimu kwako, pls usipoteze muda kwa hao polisi. jaribu kupata watu wa vijiwena na uwaombe wakuunganishe na huyo jamaa ili akurudushie na uwezi amini kazi yote hiyo inaweza fanywa kwa TShs. 10,000 - 20,000. Na baada ya hapo ndo waweza kuchukua njia mbadala kuhadabisha huyo Chenge. Tafuta vijibaba vilivyoshiba viliwi vimkamate na kumpa mzigo wa kiutu uzima na wamfire basi baada ya hapo lazima ashike adabu.

  ReplyDelete
 23. AnonymousMay 25, 2010

  we nenda hapo kijiweni usiende kwa shari mtafute then mwambie akuuzie vitu vyako maana havitamsaidia mtu yeyote mimi nilishawahi kusahau bahasha ya docs zangu then kesho yakenikalisaka lile daladala tukaelewana na walionisaidia kulisaka nikawalipa

  ReplyDelete
 24. AnonymousMay 25, 2010

  WEWE MUOMBE TENA KWA UPOLE SANA AKURUDISHIE NYARAKA ZAKO MUHIMU MWAMBIE PESA AKAE NAZO SI KITU ILA AKURUDISHIE NYARAKA ZAKO MUHUMI NASEMA HIVYO KWA KUWA MFUMO MZIMA WA SERIKALI NA UTAWALA WAKE NI MBOVU, NI KAMA WANACHEZA MADANGE SI KWELI KWELI. TUSIWALAUMU SANA HAWA VIJANA NI HALI HALISI YA MAISHA NDO INAPELEKA WAO KUWA HIVYO. UTAWALA MBOVU UZAA RAIA WABOVU. MUOMBE TU AKURUDISHIE VITU VYAKO WALA USIJISUMBUWE MAMBO YA KESI IKIWEZEKANA MPATIE PESA ZAIDI AKUPATIA VITU VYAKO MUHIMU. THAT IS THE ONLY WAY TO HANDLE THE MATTER, AND THIS IS DUE TO OUR ROTTEN SYSTEM OF GOVERNANCE.

  ReplyDelete
 25. We unaesema 'Achana na Chege songa....'' Yaani bado unataka tukae mitaani bila uhuru kwa kumuachia Chege aendelee tu kusumbua mitaani?????

  Kibiriti tu.... Nadhani hayajakukuta.... INAUMA!!!!

  ReplyDelete
 26. AnonymousMay 25, 2010

  wadau waliotoa comments za mob justice wanasahau kuwa ulimwengu mzima unapigania kuondoa hukumu ya kifo. Wapo chege wengi sana katika mazingira tofauti hususan serikalini, mbona sioni comments zenu huko mnataka kumgeuza mshikaki chege anyeendeshwa na njaa tu? washika dau pamoja na chege mnahitaji kupata neno.

  ReplyDelete
 27. AnonymousMay 25, 2010

  Kaka Michuzi na Wadau wengine hapa.Wa-Tanzania tumekuwa ni watu wa kulaumu mno wala hatujui chanzo cha matatizo wala hatutaki kuumiza vichwa vyetu kutatua matatizo.Kila kukicha ni kulaumu!Hivi tutafika?Nakushauri kaka yangu Michuzi kwa jinsi ulivyo na influence kwa jamii ianzishwe Michuzi Youth Social Iniative ambayo itakuwa ikisaidia kuwaondoa vijana katika lindi hili la ujambazi, madawa ya kulevya, wizi wa mkwapuo , Uhuhuni wa kina dada kujiuza na mengineyo mengi.Wajitokeze watu wapewe mafunzo ya jinsi ya kuwapa Ushauri Nasaha watu hawa kupitia mafunzo sahihi ya kidini na mafunzo mengine ya kijamii.Iwepo timu ya kujitolea kusaidia watu hwa na wengine katika jamii , tujenge nguvu kazi, Naamini hata JK atakuwa nawe au Kiongozi yoyote wa Kisiasa wa vyama vyetu kama CCM, CUF,CHADEMA na vinginevyo wahusishwe kwenye kampeni hii.
  Ukiangalia mzizi ya haya yote ni malezo ambayo si bora, hali mbaya za kimaisha katika jamii zetu, kutojituma.Kuna mdau anasemlaumu Chege kwa kuanza kutumia madawa ya kulevya toka form two ila hajaleta suluhisho la kumsaidia.Tuanzishe Rehabilitation centers kuwasaidia jamaa zetu
  Michuzi...MICHUZI YOUTH SOCIAL INITIATIVE AND OUTREACH PROGRAM!!!
  Khamis Hassan Batanyaga

  ReplyDelete
 28. KinyamkeraMay 25, 2010

  "Tanzania ni nchi ya amani na utulivu"- Haya ndiyo maneno ya wanaolindwa na secret services + FFU masaa 24 (Watawala)

  Ukitaka kujua kuwa Tanzania inaelekea pabaya angalia vijana wasiokuwa na ajira. Nchi yoyote ile haiwezi kupita ikijitapa kuwa imetulia kama 95% ya wananchi wake hawana ajira na hapohapo hakuna juhudi zozote za maana za kuondoa tatizo hilo. Mimi binafsi ninawashukuru sana wazazi wangu kuniandalia mazingira mazuri ya ajira kwa kunipa kibano kikali hasa nilipokuwa nakataa kwenda shule ama kupata habari nimefanya uhalifu. Kuna kipindi nilipelekwa dingi mdogo ilinibidi nijifunze kuiba kwa ajili ya njaa japo haikuwa hulka yangu na niliokolewa kabla haijawa too late. Wizi unaanzaje?

  steps toward wizi
  1. Maisha magumu na hakuna wa kukusaidia zaidi ya wewe mwenyewe

  2. Unaona kitu mtu kasahau, unachukua na kuficha ukisubiri kama litasanuka au la, siku tatu zimepita kimya unatafuta mteja unauza na kupata hela unaenda nunu pipi

  3. Hela zikiisha unaanza piga mahesabu tena ya kuchukua kitakachochukulika. Mwishowe unaungana na kundi la wenzio unawapa stori wanakwambia mbona siye ndiyo zetu hizo

  4. Mnaanza kutupita sehemu za watu na kuanza kukwapua wakati wenyewe hawapo, stage hii ikiisha, mnaanza kutumia nguvu huku mmeshajifunza kuvuta bangi. Ikifikia hapa mnaanza kutafuta mbinu za kutumia nguvu na kunyang'anya vya watu "armed robery"


  Chanzo ni nini hasa?, jibu ni moja tu KUKATA TAMAA ya maisha na mafanikio kwa njia za halali, hasa pale unapomuona mtu unayejua ni mbumbumbu ameyapatia maisha kwa kubebwa na nduguye aliye serikalini anayetoa ajira. Pia unapomuona mtu aliyekuwa akisoma kwa juhudi mpaka kufika chuo kikuu, anakaa kijiweni na kaka zako waliokimbia umande na kuamua kusubiria ugali wa nyumbani tu.

  Nini Kifanyike?:
  Kupata viongozi wasiokuwa na ubinafsi, yaani wasiosahau walipotoka kimaisha na kujivika ule uhusika wa mtu kutojua atakula nini leo wala kesho. Tukiwapata hawa watu wanao-connect na maisha halisi basi watakuwa na huruma na rasilimali ndogo tulizo nazo na kuzipanga kwa uadilifu mkubwa sana ili kupunguza umasikini. Viongozi ambao watakuwa kila siku akifika ofisini anawaza leo nifanye nini kwa ajili kuondoa kero fulani siyo afanye dili gani la yeye kuondoka na mamilioni. Viongozi ambao hawatakuwa wanaoneana aibu pindi mmoja wao anaopoonesha kuwapaka matope kwa ubinafsi na uroho wake. Viongozi ambao watakuwa tayari sehemu ya mishahara yao ipunguzwe ili ilitumike kuwalipa watu wengine na siyo kujilimbikizia wao. Viongozi ambao kila siku watakuwa wanajiuliza jana nilifanya nini kilichobadili maisha watanzania ya leo kuwa bora zaidi ya maisha ya jana?.

  Ajira ajira ajira ajira:
  Kama hatutaweza kuwafanya wananchi kuwa na ajira either ya kujiajiri au kuajiliwa basi tutarajie kuzalisha CHEGENDO (Vibaka, majambazi, wezi etc) kwa ongezeko la asilimia 30% kila mwaka.

  AMANI NA UTULIVU WETU HAVIWEZI KUDUMU KAMA SERIKALI INAJITOA KATIKA SUALA ZIMA LA KUKUZA AJIRA KWA VITENDO SIYO KWA MANENO YA JUKWAANI NA BUNGENI KISHA WANAJISIFIA KUWA SWALI UMELIJIBU VIZURI KWELI.

  Ningekuwa JK baraza la mawaziri lijalo niweka wizara nane tu na kuchagua mawaziri wasiopungua kumi na mbili tu toka miongoni mwa watanzania wajasiliamali wa maendeleo bila kujali itikadi zao siyo wahudhuriaji (Makada wa Chama). Na yeyote anayeonekana kulala anatupwa muda wowote bila notice, Na uwaziri huo wanapewa kwa mikataba ya mwaka mmoja mmoja kuongezewa kutatokana na nini umefanya kinachooneka ndani ya mwaka huo mmoja.

  Tunaweza kuwasaidia akina Chege na polisi wavivu kwa style hii tu na si kufanya ziara za kisiasa, hasa kwa wingi kwa mwaka unaoishia na "0" au "5"

  ReplyDelete
 29. AnonymousMay 25, 2010

  tatizo ni rushwa, hao wafungwa wanaopewa msamaha ndugu zao huwa wanahonga magereza na si kweli msamaha unapewa kulingana na makosa uliyofanya
  mimi ninaushahidi tosha kuna jamaa alifungwa miaka 15 kwa kumbaka mtoo wa shule ya msingi na akapewa msamaha wa raisi na mwingine alifungwa kwa kukodisha bunduki iliyokuwa ikifanyika ktk uhalifu alipewa msamaha

  ReplyDelete
 30. Rais makini anapaswa kuhakikisha jina lake halitumiki vibaya.Mnaweza kuzunguka huko na kule kuepusha lawama kwa JK lakini ukweli unabaki kuwa laiti msamaha wake kwa Chege usingetolewa 'kimakosa' angalau mhalifu mmoja (Chege) asingekuwa uraiani muda huu.Bottom line ni rushwa iliyokithiri katika Tanzania yetu.Si busara kusema "hata huko nyuma hayo yalikuwepo" kwani hata Ukimwi na Malaria vilikuwepo miaka nenda miaka rudi na tunaendelea na mapambano.Two wrongs do not make a right.
  Uchaguzi or not,rushwa inaendelea kuitafuna nchi yetu,na la kusikitisha ni hii misguided defence kwa mamlaka inayopaswa kuwa mstari wa mbele kukabiliana na rushwa.Hivi sio JK huyu anayetetewa hapa alotuambia mwaka 2006 kuwa anawafahamu wala rushwa na anawapa muda wajirekebishe?Hiyo deadline ina-expire lini?Au ni indefinite?Hivi miongoni wa hao wala rushwa alosema anawajua miongoni mwao sio hao walio-engineer parole ya Chege?
  Is it possible kuwa aliyeturoga kishakufa?

  ReplyDelete
 31. AnonymousMay 25, 2010

  Tatizo lingine ni pale hela yetu inavyoshuka thamani. Ukiwa na laki tano tu lakima umeme mfuko mkubwa. Huwezi kuiweka kabisa kwenye wallet yako ukaikalia kwenye gari.

  Chege chege wee rudisha documents za watu. Mama wa watu atajifungua vipi?

  ReplyDelete
 32. AnonymousMay 26, 2010

  Mdau uliyeibiwa naona unasumbuka bure kumtafuta CHEGE wakati ni kitu rahisi , ukitaka kumpata mtafute Mh. TEMBA atakuchukua mpaka kwa Fella ndipo anaposhinda kutwa nzima ukimkosa nenda manzese TIP TOP Family ulizia MADEA au TUNDAMAN watakwambia wapi alipo. au wasubiri TMK wakiwa kwenye show unaweza kumpata. na wewe CHEGE kuimba kote na album zote ulizouza bado unakwapua kwapua tu ?. shauri yako kibiriti kinakusubiri.
  mdau Pakacha UK

  ReplyDelete
 33. AnonymousMay 26, 2010

  tafuta wenzake Chege watume wakaongee nae akurudishie vitu vyako pesa achukue au kama hakukuwa na pesa mlipe na akupe begi lenye vitambulisho vyake, kushinda unaenda polisi kutoa habari haitakusaidia kwanza unapoteza muda polisi wenyewew wanamwogopa Chege.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...