Meneja wa Tawi la NMB Namanga Bi. Stella Thambikeni (katikati) akimkabidhi sehemu ya mipira 20 mwenyekiti wa shule za sekondari mkoa wa Arusha, Bw. Charles Msangi katika hafla fupi iliyofanyika katika shule ya sekondari Longido,kushoto ni mwakilishi wa NMB kanda ya kaskazini, Ramadhani Mvumo.
Picha na Habari na
Woinde Shizza wa Globu ya Jamii, A-Taun
Benki ya NMB kanda ya kaskazini ,imekabidhi mipira 20 kwa ajili ya mashindano ya michezo ya shule za sekondari (UMISETA)yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mei 31 mwaka huu,mkoani hapa.
Msaada huo umekabidhiwa katika shule ya sekondari Longido kwa niaba ya shule 180 za sekondari mkoani hapa,ambayo itatumika katika michezo hiyo kwa ajili ya maandalizi ya kupata timu ya mkoa na baadae timu ya kanda, itakayowakilisha katika mashindano ya kitaifa yatakayofanyika mkoani pwani.
Akikabidhi msaada huo kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa shule za sekondari mkoa, Bw. Charles Msangi, Meneja wa NMB tawi la Namanga Bi. Stella Thambikeni alisema kuwa NMB imetoa msaada huo kwa kutambua na kuthamini umuhimu wa michenzo nchini,na kwamba NMB ndio wadhamini pekee wa mpira wa miguu katika mashindano hayo kwa shule za sekondari.
''NMB inaamini kwamba ili kupata wachezaji wazuri wa ngazi ya taifa ni lazima waanze kuandaliwa kwa ubora toka ngazi ya chini watakao iwakilisha taifa vyema kwenye michuano mbalimbali''alisema Thambikeni.
Kwa upande wa mkuu wa shule hiyo,pamoja na kuishukuru NMB kwa kuthamini na kuchangia michezo mashuleni,ameiomba benki hiyo kuendelea kutoa msaada kwa kadri inavyo pata faida ,na alitumia fursa hiyo kuwahimiza wanafunzi kufungua akaunti katika benki hiyo kwa kiasi kidogo wanachopata kutoka kwa wazazi wao ili waendelee kunufaike na faida zitakazopatikana .
Bw. Msangi aliyataka mabenk mengine , taasisi za fedha kuiga mfano wa NMB katika kutambua umuhimu wa kuchangia michezo ili kujenga na kuimarisha afya za wanafunzi hao sanjari na kupata wachezaji bora na wenye vipaji watakao weza kuliwakailisha taifa katika michezo mbalimbali.
Michezo ya UMISETA inatarajiwa kuanza mkoani Arusha Mei 31 mwaka huu na kumalizika juni 2 ,ambayo itajumuisha shule zote za sekondari mkoni hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2010

    jamani wameshindwa hata kujaza upepo mpira mmoja tu wakukabidhiana ? au ndo upepo ulikuwa haupo katika bajeti ?

    bongo tambarare kaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2010

    Lugha iliyotumika ni kali kweli kweli, eti "wamwaga...", kumbe wamedondosha tu. Mi nilidhani ni bonge la tafu, kumbe ni kuchukua advantage ya hao wasaidiwa kutojituma. Wangejituma leo hii wangedondoshewa ufadhili wa miaka kadhaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...