video ya Sean Kingston alipoongea na wanahabari leo hoteli ya Hilton jijini Dar

Maulid Baraka wa Kitenge (kulia) akiwa na bodigadi wa Sean Kingston leo
Msanii Sean Kingston (wa nne toka kulia) akighani mjoa ya nyimbo zake alipokutana na wanahabari hoteli ya Hilton jijini Dar mchana huu. Ameahidi makubwa kwenye shoo yake ya Jumamosi katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall ambako atafanya vitu vyake katika Kili Awards Winner's Concert. Kesho Ijumaa atakuwa mgeni maalumu kwenye utoaji wa tuzo za Kili Music Awards na atatoa tuzo kwa msanii bora wa reggae
Sean Kingston akiuza nyago na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL David Minja (shoto) na Meneja wa Kilaji cha Kilimanjaro George Kavishe Mchana huu hoteli ya Hilton.
ankal nae alikuwepo kuuza nyago na Sean Kingston.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2010

    ankal nimependa mwamvuli wako..

    ankal ukipata nafasi tena ya kuonana na sean tena mwambie afanye mazoezi..
    BP inamnyemelea

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2010

    Kijana mdogo kabisa lakini laaaah! Kazi ipo...........zoezi linahitajika hapa kukata mafuta hayo. Well, wazalendo wanasema ilimradi mkono unaingia kinywani.....ila afya muhimu kwanza.

    ReplyDelete
  3. ......WEWE BWANA KAVISHE WEWE, KWA NINI UNAONGEA KISWAHILI??, JAMAA ATATUELEWA VIPI WABONGO??....INABIDI MFUATE MFANO WA KUSAGA, NAKUMBUKA ALIPOKUJA SHAGGY AU 50CENT, JAMAA ALIKUWA ANAPANDA UMOMBO KAMA KAWA....

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 14, 2010

    ankal na yeye hakuwa nyuma.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 14, 2010

    Duh, yaani jamaa kaona bodyguard ndio jumlishatoa, supa staa wa bongo kajimulika kweli kweli.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 14, 2010

    Umbeya sasa, mtaanza ooh Kavishe hajui kidhungu, lakini mmeniudhisana kuninyima Invitation nyie sababu zenu wakti niko kwnye music industry.

    Bongo kweli kila kitu dili, huyu naye kapiga na body guary huku akiamini a bodyguard naye ni a celebrity .

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 14, 2010

    aloo ww anony hapo juu unaonyesha ni ginsi gani ww ni adui wa lugha yako na mshamba maana ww waona aibu kushusha kimatumbwi.shame on you hata kama upo jpn au swdn au dnk au holland lazima watumie lugha yao asili maana jamaa mgeni afu kaletwa na wenyeji na atagalamiwa kila kitu na wenyeji wake.weee nenda huko na ushamba wako huo mtumwa wa mawazo.africa kwa wa africa tu ukija africa lazima ufuate masharti

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 14, 2010

    Duh nilikua sijui kama kuna bado watu wanaona aibu kuongea lugha yao nyumbani kwao. wewe unadhani raisi wa urusi hajui kiingereza kwanini huwa anaongea kirusi akiwa na kina obama na brown? Ndiyo maana kuna wafasili ndiyo ulaji wao huo. Kiswahili ni moja kati ya Lugha 4 kubwa africa hivyo usione aibu kwa huyu mangi kutumia kiswahili.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 14, 2010

    yaani nimecheka leo kaka mithu, nivyosikiliza hiyo video, mimi ni mchagga lakini du, "FITAFINIO" KARIBUNI SANA,

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 14, 2010

    mmmmh jamani we mdau hao juu acha mbwembwe hakusema fitafinio alisema vitafunwa karibuni sana!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 14, 2010

    Eti nini? Fitafinio????

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 14, 2010

    kuna vitafunwa kidogo,kweli kiswahili kigumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...