Uongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM , Tawi la Moscow Urusi unawatangazia vijana wote walioko Urusi , kuwa sherehe za ugawaji KADI ZA UVCCM kwa Wanachama wapya Zitafanyika tarehe 30/5/2010 kuanzia saa 16:00 hadi 19:00, Ukumbi wa Mikutano block 6, Mikluho Maklaya Mjini MOSCOW

Pia sherehe hizo zitaambatana na Hafra ya Kuwaaga Vijana watiifu wa CCM wanaomaliza Masomo yao Mwaka 2010 kutoka katika Vyuo Mbalimbali hapa Urusi.

Uongozi wa Jumuiya ya Vijana Tawi, Unapenda kuwakumbusha kuwa, MWISHO wa kupokea Form,ada ya uanachama (50rub) na Picha Mbili ni Tarehe 28/5/2010. Kwa wale ambao hawajakamilisha zoezi hili , wasiliana na:-

1. Katibu wa UVCCM tawi la Moscow - Ndg. Mbarouk .M.O (+79268071127)

2.Katibu wa Fedha na Uchumi UVCCM tawi - Ndg. Octavian Nyalali. (+79258241202).

Mikakati ya Sherehe hiyo imekamilika na wageni na Viongozi mbalimbali wamealikwa kuhudhuria sherehe hiyo.

Aksanten!!
Kidumu chama cha Mapinduzi!!!!
Imetolewa na Uongozi UVCCM
TAWI LA MOSCOW URUSI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2010

    Kama tangazo lako liko sahihi,basi vijana wooooooote wanaoishi urusi ni wana ccm.Kama wapo vijana ambao ni wanachama wa vyama vingine vya siasa basi tangazo lako lina kasoro.Rekebisha lugha nyakati zijazo na uelewe kuwa kila kimiminika siyo maji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...