Wachezaji na mashabiki wa timu ya Magereza wakishangilia baada ya kuivua ubingwa kwa wanaume timu ya Jeshi stars na kutwaa ubingwa wa Taifa wa Volleyball
Michuano ya klabu bingwa mpira wa wavu Tanzania imemalizikamchana huu huku ikishuhudiwa timu ya Jeshi Stars(wanaume) ikivuliwa ubingwa baada ya kufungwa seti 3 -2 na timu ya Magereza ya Dar es salaam katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Hindu mandal mjini Moshi.
Kwa upande wa wanawake timu ya Jeshi Stars waliibuka mabingwa baada ya kuifunga timu ya Magereza kwa seti 3-0 mchezo uliokuwa na ushindani kwa timu hizo huku zikipishana kwa pointi chache katika kila seti.
Katika fainali hiyo kwa upande wa wanaume timu ya Jeshi Stars ndio walikuwa wa kwanza kuongoza katika seti ya kwanza baada ya kushinda kwa pointi 25-22 huku seti ya pili magereza wakiibuka washindi kwa pointi 25-16.
Kwa upande wa wanawake timu ya Jeshi Stars waliibuka mabingwa baada ya kuifunga timu ya Magereza kwa seti 3-0 mchezo uliokuwa na ushindani kwa timu hizo huku zikipishana kwa pointi chache katika kila seti.
Katika fainali hiyo kwa upande wa wanaume timu ya Jeshi Stars ndio walikuwa wa kwanza kuongoza katika seti ya kwanza baada ya kushinda kwa pointi 25-22 huku seti ya pili magereza wakiibuka washindi kwa pointi 25-16.
Katika seti ya 3 Jeshi Stars tena waliibuka washindi kwa pointi 25 kwa 23 huku Magereza wakishinda seti ya 4 kwa seti 25 kwa 18 ambapo katika seti ya mwisho kwa mujibu wa sheria za mpira wa wavu huwa inamalizika kwa pointi 15,timu ya Magereza iliibuka mshindi kwa pointi 15 kwa 12 za jeshi stars.
Kwa matokeo hayo timu ya Magereza ndio mabingwa wapya wa michuano ya klabu bingwa Tanzania ,nafasi ya pili ikishikiliwa na Jeshi Stars huku timu ya Mzinga kutoka Mrogoo ikishika nafasi ya 3.
Kwa upande wa wanawake timu ya Jeshi ndio wametangazwa mabingwa,nafasi ya pili ikishikiliwa na timu ya Magereza huku timu ya chuo cha KCM kikishika nafasi ya tatu.
Mshindi wa kwanza katika fainali hizo alikabidhiwa kikombe huku timu za chuo kikuu kishiriki cha stadi za biashara na ushirika (MUCCOB’s) na timu ya KCM Collage zikikabidhiwa zawadi ya mpira.
Mchezaji bora katika michuano hiyo alikuwa ni Aritidius Doto wa chuo Ushirika huku Kelvin Mwasha wa timu ya Magereza Dar es salaam akinyakua zawadi ya mshambuliaji bora.
Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi mgeni rasmi katika fainali hizo Katibu tawala miundo mbinu mkoa Kilimanjaro, Hassam Mpendeyeko alipongeza jitihada za chama cha mpira wa Wavu nchini TAVA za kuendeleza mchezo huo .
Taswila hizi za hindu mandal Moshi. Zimenikumbusha mbali sana.. Hongera sana Edwin masinga na Lameck Mashindano kwa mafanikio ya timu zenu zote zilizofanya kweli.
ReplyDeleteVolleyball ina nafasi ya kuwa mchezo maarufu katika Tanzania, kama ilivyokuwa miaka ya 90.Najisikia fahari sana kuwa mmoja kati ya wanajamii ya VB.