Benki ya CRDB kupitia Akaunti yake ya Tanzanite mahususi kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi, inapenda kuwajulisha watanzania wote wanaoishi Marekani kuwa itashiriki kwenye mkutano maalumu uliondaliwa na Watanzania waishio Marekani (Diaspora Council of Tanzanians in America- DICOTA).
Timu ya CRDB itawasili Minneapolis, Minesotta tarehe 29/06/2010 na kushiriki katika mkutano huo utakaofanyika Marriot Hotel tarehe (1st July to 4July 2010).
Tunapenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha kuwa katika mkutano huu shughuli kubwa tutayo endesha ni kufungua akaunti za Tanzanite kwa watanzania wote kuanzia tarehe 30/0602010 mpaka 05/06/2010.Sambamba nahili kujisajili kupata huduma za kibenki kupitia mtandao(online banking),kujisajili kupata kadi ya visa na maelezo yote kuhusu kupata huduma za kibenki zinazotolewa.
TARATIBU RAHISI ZA KUFUNGUA AKAUNTI.
Habari nzuri zaidi nikwamba zoezi zima lakufungua akaunti limerahisishwa kama ifuatavyo;
1. Kwawale watakao fungua akaunti wataweza kupewa namba za akaunti zaoPapo kwa hapo.
2. Utaweza kuanza kutumia huduma za kibenki kupitia mtandao (online Banking)siku inayofuata baada ya kufungua akaunti.
3. Utapatiwa kadi ya visa watapata ndani ya siku 15 za kazi kupitia anuani yako uliosajili kwenye form ya ufunguzi akaunti.
4. kwamtu asiye na resient permit/Visa atatakiwa kutoa wadhamini wawili walioko Tanzania.
MASHARTI NAFUU YA KUFUNGUA AKAUNTI.
Masharti ya kufungua akaunti ni kama ifuatavyo;
1. Picha mbili za paspoti,
2. kivuli cha hati ya kusafiria,
3. kujaza fomu ya maombi ya Akaunti ya Tanzanite na kianzio kisicho chini ya USD 50.
UJIO WA CRDB BANK NORTH CAROLINE (DARHUM/RALE) NA COLUMBUS OHIO
Pia tunapenda kuwafahamisha Watanzania waishio North Caroline (Durhum/Rale) na Columbus Ohio tutatembelea miji hiyo baada ya mkutano, ratiba kamili na wapi tutakuwa,lini, mtafahamishwa muda simrefu.
Kumbuka “Mtu kwao” jiwekee akiba yako nyumbani na upate faida zaida ya akiba yako,kwani ukiwa na Tanzanite akaunti mbali na faida lukuki vile vile unaweza kuwekeza kwenye soko lahisa na mfuko wa umoja (UTT) na utaweza kuwekeza kwenye soko la hisa la Dar es salaam kupitia wakala maalum alieteuliwa na Benki.
Kwa mawasiliano unaweza kutufikia kwa namba
651-354-8792

The Mission is impossible, wapelekeeni wa UK.
ReplyDeleteMdau Ohio
Mheshimiwa Mithupu hawa CRDB pia waangalie kwa watanzania waishio NEWYORK na WASHIGTON DC pia, wanaweza kuhitaji huduma hii. Cha msingi ni kuwasiliana na Balozi zetu za washington DC na Umoja wa mataifa ili waangalie uwezekano wa kuwasaidia watanzania waishio maeneo hayo. Naamini njia hii itawasaidia wengi wanaohitaji huduma za kibenki za nyumbani. Imekuwa desturi kwa watanzania wengi kutumia VISA kadi za benki za nje wawapo likizo nyumbani Tanzania na kuendelea kuzinufaisha benki hizo. Kumbe ilikuwa ni kutumia VISA kadi ya benki kama vile CRDB na inakuwa unachangia maendelea ya nyumbani. Kwani kukua kwa CRDB wadogo zetu wengi watapata ajira na huduma za kijamii zitaimalika nk.
ReplyDeleteMzee, hiyo inaitwa North Carolina na miji ile Durham na Raleigh.
ReplyDeleteKwanini msiwe high tech kikweli tukafungua tu online????..Hivi mnazania ni wote tutakuja kwenye huo mkutano wa CCM huko Minesota? Kama manataka soko kweli basi mjiachie online tufungue kwa wakati wetu....Watakao fika kwenye huo mkutano ni hardly 2% ya watanzania wote wanaioshi huku....Mimi nitoke Seattle niende Minnesoata kwenye mkutano????!!!!
ReplyDeleteRemember watu unaowataka kuingia kwenye benk yako wako kwenye nchi yenye soko huria...Kuna options kibao hivyo unatakiwa uwabembeleze sana ...ingekua mimi ningewapa hata free account to join or no minimum to join for the first year...
Customer is the King why do you forget that....???
Kinda Crap is this?! Why should I pay $50 to open an account while I can get a free Checking and Savings account at Chase/Bank of America and all other banks. To be honest, I opened an account with chase and I was even given free $100 just to open an account. I added a direct deposit through my job and got another $100. Mnadhania tuko bongo hapa? Stop hustling us, like the other dude said, you gotta beg for our business and not hustle us. Nyie akili hamna kabisa, BENKI GANI INATAKA PASSPORT SIZE, mambo ni digital hapa. If you have your id you are good to go, why should I run to walgreen and take a picture just because I wanna open an account. Nikija bongo I will continue using my credit cards kama kamaida and not pay a dime to your lousy bank. Eti unaweza kulog in online the next day, wtf?? Eti unapewa account namba hapo hapo, who said that was a hard thing to do. What is the differance does it make? Nyie mnacheza makida makida(I'm sorry natumia misemo ya kizamani) How will I get in touch with you guys tu assist me with my banking, how will I make a deposit. Kasusura akiiba hela Je? Mna liability insurance? Kwendenu zenu!!tryna hustle some hustlers, get your grind on!
ReplyDeleteCrdb baada ya kuona wameshindwa ku operate UK ,wamekimbilia USA,Watanzania wenzangu wa USA ni vyama kuwauliza nini kilichofanya tanzanite uk ikafa?Ni bora kuwauliza maswali ili kwamba msijiingize ikawa taabu,mfano mtajaza form vizuri ila card kuzipata ni shughuli ,will take 2-4 month kuzipata mbali na hiyo internet banking ni taabu ,kuna vitu vingi waliboronga UK,gharama za ku run Tanzanite ni kubwa kila mwezi wanakata pesa ,ukiamaisha kwenda kwenye acc nyingine wanakata,pia ikifika mwisho wa mwaka wanakata service fee ya kuwa na card .Tupo ulimwengu wa kwanza waambieni wajibu hayo maswali,UK wanadai haijafa ila ukipiga ubalozini hawafahamu agent ni nani.Kimei kuwa mkweli hawa unawao watuma ni tax payer ,kwa kifupi haya makampuni wanakuja kufanya shopping tu,hakuna na nilongolongo kabisa,Michuzi lusha hii.
ReplyDeleteHata Ukerewe walishindwa, eti mteja maximum amount allowed for account hold should not exceed pound sterling 10,000(yes ten thousand), ina maana mteja akiwa na zaidi ya equivalent ya tshs millioni ishirini benki inaogopa, mwe makubwa benki za kitanzania hazitaweza kupata wateja ktk diaspora.
ReplyDeleteNdugu zetu wa CRDB ninaomba majibu ya swali hili.
ReplyDeleteMimi nina akaunti yangu CRDB. Niliwahi poteza kadi yangu Dar es salaam na nikaingizwa kwenye taratibu za mwaka 47 za kibenki za hapo bongo. Nilipokwenda ku-deposit pesa pale CRDB na kumweleza teller kwamba sina kadi yangu ya kwamba nimei-misplace nilipokua nahamia kwenye nyumba nyingine huyo teller akaniambia utaratibu uliopo ni kwamba ninapaswa kwenda CENTRAL POLICE na kuwaambia waniandikie maelekezo kwamba nimeipoteza hiyo kadi, halafu nipeleke kidhibitisho from CENTRAL, ndipo wao wa CRDB ndio wataangalia kama watanipa kadi nyingine au la. Nilishusha pumzi halafu nikasikitika sana.
Kesho yake nikafunga safari kwenda CENTRAL. Jamaa wa CENTRAL wakasema hawana karatasi, meaning that walikua wanataka hongo. Nikashusha pumzi tena na kusikitika kwa mara ya pili.
Kwa kutumia experience yangu kwa taratibu za kibenki za miaka ya 47 za kibongo ndio maana nimekuja wachapa swali humu wahusika wa CRDB. Mnapowashurutisha watanzania waishio nje kufungua akaunti wakati muna conflicting and dated procedures za kibenki, na bila kufikiria taratibu/sheria za nchi nyingine kama Marekani nafikiri mtakuwa mnawaweka watanzania hawa pahala pabaya. Mwenye akaunti ya CRDB akipoteza kadi yake Marekani halafu akawa safarini bongo na akataka kuchukua pesa yake na mkaishia kumweka kwenye longolongo la kuleta barua kutoka CENTRAL POLICE ya Marekani wakati huko Marekani hamna CENTRAL; Na wala huko Marekani hawana utaratibu wa kuenda polisi kuomba wakuandikie barua kwamba umepoteza kadi yako; Nafikiri mtakua mnawaweka hawa raia katika pahala pabaya sana. Badilisheni taratibu zenu ziendane na wakati. Harmonize your banking regulations kwanza ili ziendane na international banking procedures. Then ndio mje US kuwashurutisha watu waweke pesa zao kwenye benki zenu. Ninazungumza from my personal experience, hakuna jungu hapa.
wewe mtu wa seattle kumbuka hao wenzako bado wana operate kama Tanzania wewe unaleta mambo ya Mtoni. Kama huwezi kuja basi umekosa kama ulikuwa na nia kufungua akaunti bongo. Kama huna nia poa, watapat watu wengine. Hivyo ndio tunavyoenda kibongo bongo.
ReplyDeleteI commend your action of expanding your business to Tanzanians living in US,but I am still skeptical with your services in general,your online banking still doesn't let customers to access their accounts via online contrary to what you tell us.Also In this era in which people like to shop online to buy whatever they want from any part of this world,your bank isn't yet paypal friendly.To end, please make really changes in your bank because it doesn't seem to be ready of what it tells us.
ReplyDeleteLO!kwa hizo dissapointment nilizosoma hapo juu basi sitaki kabisaa kufungua hiyo acc,i was looking foward to do so buti have changed my mind already.
ReplyDeleteasanteni kwa kutushirikisha nimepata kujua kinachoendelea,hel no!!!
Duh!, asanteni wadau mliotoa maexperience yenu, i guess i will stick to my free checking and saving account with CHASE. Good luck CRDB.
ReplyDeleteLOL I was excited to open an account wakija ohio but hizo comments zimenitisha. Inabidi nitulize boli kwanza nisiingie kichwa kichwa and loose my money.
ReplyDeletewabongo inabidi mtoe usauri wa wafanye nini siyo kuponda tu any way kuhusu maendeleo tumewakabidhi balozi wetu mshindwe wenyewe.
ReplyDeleteHata mimi siwezi kabisa kufungua akaunti na hawa CRDB yaani maelezo ya wadau wengine wa juu yamenifumbua macho. Unajua hizi kampuni za Bongo zinafanya biashara kwenye nchi za watu kibongobongo ambapo kule mteja ni mtumwa na sio mfalme. Halafu pia tumieni tovuti mbalimbali kujitangaza baada ya kuboresha huduma zenu
ReplyDelete