Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim, Bi. Sabetha Mwambenja, katikati akimkabidhi kitanda cha kujifungulia Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Betha Swai kushoto, huku Mkurugenzi wa PSI Tanzania Mary Mwanjelwa akishuhudia. Benki hiyo imetoa msaada wa vitanda nane vyenye thamani ya sh. milioni 8.5.kwa Hospitali za Mkoa wa Mbeya.




Benki ya Exim imetoa vitanda nane vya kujifungulia wanawake wajawazito katika mkoa wa Mbeya.

Akikabidhi vitanda hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 8.5 Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini dare s Salaam, Mkuregenzi Mkuu wa benki hiyo, Sabetha Mwambenja alisema benki yake inatoa vitanda hivyo ikiwa ni jitihada zake za kuboresha maisha ya wanawake na Watanzania wote kwa ujumla.

“Tunatambua umuhimu wa afya za akina mama na ndiyo maana tumeguswa na tatizo hili mkoani Mbeya na kuamua kushirikiana na Mkoa ili kuboresha afya za akina mama,”
Benki yake alisema iko mkoani Mbeya hivyo msaada huo ni muhimu sana katika kuhakikisha kwamba wakazi wa Mbeya wanapata huduma bora za afya.


“Tutaendelea kushirikiana kila mara si kwa Mbeya peke yake ila hata kwa maeneo mbalimbali ya nchi lengo ni kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata huduma bora za afa.

Naye katibu tawala mkoa wa Mbeya, Bertha Swai, akipokea msaada huo alisema kwamba msaada huo ni muhimu sana kwa hospitali za mkoa wake kutokana na mahitaji ya vitanda hivyo.
Alisema vitanda hivyo vitagawiwa kwa Wilaya nane za Mkoa wa Mbeya.


Alisema kwa wastani katika mkoa wake kitanda kimoja kinatumika kwa akina mama 20 na kwamba kwa mwezi mmoja kitanda kimoja kinaweza kutumiwa na akina mama 9000 wakati kwa mwaka wastani wa akina 72,000 wanatumia kitanda kimoja.

“Hivyo mnaona ni jinsi gani msaada huu kutoka Exim ulivyo muhimu sana kwetu” alisema
Alisema serikali inafarijika inapoona sekta binafsi ikijiendesha kwa tija na hatimaye kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma za jamii.


Aliipongeza benki ya Exim kwa msaada huo na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano wake.
Benki ya Exim ni miongoni mwa benki zinazokua kwa kasi ikiwa na matawi 18 nchini kote inatoa huduma mbalimbali za kibeki, ikiwa na kitengo maalum cha mikopo ya wanawake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2010

    Jamani watanzania mlio na nyadhifa mbalimbali kwenye nchi yetu hii ya unamjua nani upate huduma hii, tukumbuke nyumbani kama hawa wenzetu wakina MWA...... wanavyokumbuka kwao. Hivi unafikiri watu wote wenye nyadhifa wanaotoka sehemu tofauti tofauti kama wakina chachamarwamwita, kina Nyuuraa masawe na shimbonyi namchichaa,kina Rutananihii, kina rwechunaniihii..., kina masanja, kina chamaki nchanga, kina shemananihii, kina shinanihii....., wale wa mwisho wa reli, na woootee.....si tungekuwa mbali jamani...!!!!Tuache ubadhilifu na ufisadi kwa ajili ya maisha yetu ya sasa, Tujenge nchi yetu kwa ajili ya watoto na wajukuu zetu hapo baadae wakati sisi tutakapokuwa majivu.....Thats a piece of advice for you all...!!!

    ReplyDelete
  2. Mpalang'ombeJune 08, 2010

    Mimi hoja yangu ni hawa donors. Huu mchezo wa kuandika "donated by XXX" nafikiri ungeisha. Suala la donation liwe subjected na "tax benefit", Kama donor anahitaji kutangaza anaweza weka lebel tu ya kampuni yake kwenye kifaa kilichotolewa hayo ni matangazo tosha kuwa wana mkono wao.

    The biggest benefit huwa ni pale wanapopata publicity at a time of event. Haya mambo ya kuandika donated by sound like hawa jamaa wanajitolea kweli wakati indirectly wana-understate profit zao na wakibanwa wanasema walitumia kutolea misaada,

    TRA hili waliangalie kuwa kampuni isiruhusiwe kutoa msaada na kujumuisha katika tax deductable expenses while they get free ride on advertisement at the expense of tax payer.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2010

    ndaga kikolo!!
    thanks its gud unapokumbuka ulipotoka ktk njia ya aina yake!!
    stay blessed

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...