cheki sehemu ya hili gemu kupitia http://www.bongoline.com/
paparazzi wa kimataifa wanaoongozana na timu ya Brazil wakirekodi taswira ya jinsi kina ras makunja wakimnasa kijana aliyevamia uwanja wakati wa gemu na kwenda kumkubatia Kaka
"...Unajifanya fara sio? basi sisi ni mafara zaidi yako. haya twendeeee..."

kina ras makunja wakiwa wamempa kijana huyo 'no-smoking' wakimtoa nje (kunradhi taswira si nzuri sana kwani mpiga picha wetu alikuwa upande wa pili wa uwanja)

Huko uwanjani Kaka na wenzie wakifurahia bao la nne huku
nahodha shadrack nsajigwa (shoto) na mwenzie wakirudi kati

wadau wakishuhudia pambano
wadau wa Globu ya Jamii walikuwepo kibao
Wanja la neshno halikujaa kihiiiivyo...
hapa ni VIP B ambapo kwa laki unusu mambo yalikuwa hivi...
Kaka akihojiwa na TV ya Brazil wakati wa mapumziko
wanja lilivyokuwa wakati wa gemu
Mabeki wa Taifa Stars wakimsindikiza Ramos anapoingia ndani ya 18
Kipa anapimwa na kujikuta anapigwa bao kirahisi kabisa
Kipa wa Taifa Stars na mabeki wake hawana hamu...

Tanzania yavunja mwiko waliouweka Brazil
Dakika 87 Taifa stars yapata goli tamu. Haijawa kutokea. Maana toka Oktoba 2009 Brazil haijawahi kuvujisha goli. Mshambuliaji Jabir Azizi wa Taifa Stars anaunganisha kwa kichwa kona na golikipa wa Brazil Gomez anadaka hewa na Tanzania kupata goli.

Dakika ya 91 Raminez afunga bao la tano kwa Brazil. Brazil 5 Tanzania 1.
Mpira umekwisha Brazil 5 Tanzania 1.

Mdau
Jijini London.
----------------------------------------------
DAKIKA YA 29 YA KIPINDI CHA PILI KAKA
ANAFUNGA BAO LA 4 KWA KIFUA
BAADA YA RAMIREZ KUIPATIA BRAZIL BAO LA 3 KIASI CHA DAKIKA 8 BAADA YA MAPUMZIKO. ALIITOKA NGOME YA TAIFA STARS KABLA YA KUMPELEKA KIPA MWARAMI UPANDE WA PILI WA UWANJA.
GOLI INGEKUWA 4-1 KAMA NGASSA ASINGEPATA KIGUGUMIZI AKIWA YEYE NA NYAVU NDANI YA SITA.
DAH! KATIKATI YA GEMU ANATOKEA MSHABIKI ANAYEINGIA UWANJANI MKUKU NA KWENDA KUMKUMBATIA KAKA. ANADAKWA NA KINA RAS MAKUNJA MARA MOJA NA KUPELEKWA WANAKOKUJUA
Habari Kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 52 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2010

    Asante Ankal. Vipi hali ya uwanja, nyomi kibao au? Unaweza kutupatia kavideo kidogo pia?

    Thanks,

    Mdau wa Canada.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2010

    Du Midhupu hapo ni sawa na Duma anacheza na kitoto cha swala japo hata kila. Nategemea bao ntingi zaidi kwa kuwa ni sherehe ya kumuaga kocha maximo na kumkaribisha mrithi wake raia wa Denmak. Hongerenisana wanetu kwa kupigwa walau bao hizo kabla na baada ya kipindi cha kwanza

    ReplyDelete
  3. UNCLE MICHUZI....KAMA TUNAANGALIA GLOB YAKO, VILE VILE INA MAANA KUWA TUNAWEZA KUANGALIA HII MECHI - INAONYESHWA ONLINE...KWA HIYO HAKUNA HAJA YA KUPOSTI HIVI VITU UNAVYOPOST - SUBURI MPAKA MWISHO THEN POST MATOKEO. AU UNASEMAJE UNCLE??

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2010

    marisha n gasa(comentator voice)

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2010

    TAZAMA LIVE MECHI YA MPIRA KUPITIA
    WWW.ATDHE.NET TZA VS BRZ

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2010

    Dakika ya 75 Kaka anapokea krosi murua toka upande kwa kulia mwa uwanja na kufunga bao la 4 kwa Brazil.

    Nsajigwa, Gigi, Hamoud, wanatolewa nafasi zao kuchukuliwa na Jabir Aziz, Salum Kanoni, Naftali. Mpira dakika ya 80 Brazil 4 Tanzania 0.
    Mdau
    jijini London.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2010

    lol.. arent these brazilians ashamed to celebrate a goal against tazmania..

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2010

    Ha ha ha ha ha ha ha ha!!Mimi kama mzawa nina uchungu sana,lkn ndyo mchezo.Kinachonifurahisha ni huyo mzalendo alikwenda kum-hug kaka,cjui alikua anawaza nini,ha ha ha ha ha ha ha ha ha!!Kaaaaaaaazi kwl-kwl!

    Mkulima-Kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2010

    Angalau mumetuonesha mnamacho. Hongereni kwa kabao kamoja pia hongera kipa kwa kufungwa na wachezaji wenye majina

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 07, 2010

    SIJAWAHI KUONA KIPYA HOVYO KAMA HUYU WA TAIFA STARS. KAFUNGISHA MAGOLI 4 KATI YA 5. HOVYO SANA. ARRRGGHH!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 07, 2010

    Tanzania yavunja mwiko waliouweka Brazil, dakika 87 Taifa stars yapata goli tamu.

    Haijawa kutokea, maana toka Oktoba 2009 Brazil haijawahi kuvujisha goli, Jabir Aziz wa Tanzania anaunganisha kwa kichwa kona na golikipa wa Brazil Gomez anadaka hewa na Tanzania kupata goli.

    Dakika ya 91 Raminez afunga bao la tano kwa Brazil. Brazil 5 Tanzania 1.
    Mpira umekwisha Brazil 5 Tanzania 1.


    Mdau
    Jijini London.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 07, 2010

    tunaomba picha ya mdau aliemkumbatia kaka

    Kamau oyeeeeeee

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 07, 2010

    Mpira umeisha hongereni taifa stars kwa kufungwa 5 kwa 1 kwe2 mnabaki washindi tu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 07, 2010

    kipa kimeo, timu imecheza vizuri ila bado sijajua tulikuwa tunacheza formation gani

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 07, 2010

    This is exactly what Uncle Kamau of Kenya said recently in his article has attracted a lot of critisism! I bet the money that was spent on the Brazillian team could have been used to feed the hungry for about a week or so!! Or may be to renovate those "round-abouts" of mithupu in daressalama! This was like asking a math teacher to compete with a girl or a boy of 2 years in algebra!! Tutafika lakini duuu!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 07, 2010

    Naona Uwanja umeshindwa kujaa. Big game like this ina maana demand ilikuwa high. But hiyo high price ya ticket imefanya watu wengi wasiingie uwanjani. Wangeweka bei ya wastani na uwanja ungejaa na wangepata faida kubwa.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 07, 2010

    Ankal, hayo matangazo hapo uwanjani inakuwaje? Mbona sijawahi kuyaona bongo?

    Watu ni kama kiasi gani kwa makadirio ya haraka haraka?

    Mdau wa Canada.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 07, 2010

    WEWE unaejiita KILO, acha kujifanya unafundisha watu kazi. Kama unaiona endelea kuangalia.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 07, 2010

    Mkuu wa wilaya ya nanihii, waonaje uongee na waziri wa michezo, muwashitaki Eurosport kwa kutangaza mpira wa Brazil na Taifa Stars kwa kuweka bendera ya Brazil pekee bila ya bendera ya Tanzania. Je huu sio ubaguzi?? Au ndio kusema hakuna bendera za tanzania huko waliko??? Balozi wa Tanzania UK fuatilia issue hii.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 07, 2010

    KIPA WETU ALIKUWA KAMA PAMBO TU KUKAMILISHA IDADI YA WACHEZAJI 11.ZERO KABISAA.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 07, 2010

    Sio mbaya afadhali tumepata bao moja la kufutia machozi,hata hivyo vijana wamechoka jana walipiga gemu tafu na RWANDA sio mchezo kucheza mechi mbili katika masaa 24.ZIMBABWE hawakupata hata goli moja go TZ go STARS you made it.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 07, 2010

    kaka nakupongeza kwa kazi nzuri ya kutupasha habari. naomba uniwekee swali langu maana nimeulizwa hili swali nikagundua kuwa ni zuri kuchemsha bongo. pundamilia ni mweusi anamistari myeupe? au ni Mweupe ana mistari myeusi? natakuliza shukurani kwa wadau wataonipatia jibu la swali langu.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 07, 2010

    I like this wamechangamshwa haswa...Ni kama wamefungwa ni 5-0 jana moja leo manne kesho mwende kwenye kambi mjue nini la kufanya. Mukae muangalie video mjue wapi mlitakiwa kuchacharika. Hata hivyo mmejitahidi 4-0 tu ...Mmmekazana sanaaaaaaana tu.....Nilikua naogopa ingekua 8-0

    Maoni yangu kwa game liamke TZ walipeni vizuri hao wachezaji waweze kutunza familia yao na kufanya soccer kuwa profession yao bila hivyo hatutaenda popote..na kmama mmeshawalipa basi muengeze b'se it is not enough

    kama watu wana hizi hela why don't own a team na kumake sure unawatunza na kuwafanyisha mazoezi kila siku? Bila mazoezi na kuwa na makocha wakila aina tutabakia kukimbia uwanjani tu.

    sijui timu ya taifa inaundwaje TZ laini mimi ningetaka iwe ya msimu tu hao wachezaji wawe na vilabu vyao ila siku ikitokea mechi za kuwakilisha nchi ndio wakusanywe the best of the best... Na iwe kila mwaka ni kuchaguliwa upya, hufanyi vizuri unapisha wengine ...Hiyo itawasaidia wawe wanacompetition na kujitahidi zaidi. mambo ya kuwa na permanent timu ya taifa sio mazuri...

    Halafu tujaribu kuwa na makocha wengi tu...kocha mkuu hawezi kujua kila kitu...Huku wenzetu wana specialized wanakocha wa viungo, kocha wa kushoot, kocha wakuofundisha jinsi ya kuokoa, therapist, psychologist, nutritionist, and dietitian ..utakuta hapo wengine wakwetu walilumanga sima kubwa mchana ya ugali halafu wameingia kucheza kandana hapo mweeee ngoma hiyo....polepole tutafika bila ubishi


    nawapongeza walioandaa hii timu kuja kucheza najua kuna watu waliolalamika wee lakini ndio wa kwanza kustream live online kwa freee..Mnajijua wote...muone aibu...kama uliudhika sana msingebother hata kuangalia hiyo game tungewaelewa lakini kumbemaneno mengi kutaka kuona ikoje mmekua wakwanza...agalia link hii , angalia na link hii sigh.....

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 07, 2010

    NYIE ACHENI NYIE!! SI MCHEZO SIE WANDENGEREKO KUCHEZA NA MABINGWA WA DUNIA, HAYO MAGOLI 5 MBONA MADOGO!

    ILIBIDI KWANZA WACHEZAJI WETU WAPEWE SIKU NZIMA YA KUWASHANGAA WACHEZAJI WA BRAZIL NA KUONGEA NAO ILI KUONDOA WAHKA, KISHA NDIO MECHI INGECHEZWA. WALLAHI NAKWAMBIA HATA NINGEKUWA MIE NISINGECHEZA NINGEBAKI KUWASHANGAA WACHEZAJI WA BRAZIL KAMA KAKA AMBAYE MIE NI FAN WAKE! nahisi golikipa wetu yeye alikuwa anawashangaa tu hao wachezaji wa brazil wala msimlaumu!

    PAMOJA NA KUFUNGWA LAKINI CHENGA TUMEWALA NA SISI SIKU MOJA TUTAWASIMULIA WAJUKUU ZETU KUWA TULICHEZA NA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL ILIYOCHUKUA KOMBE LA DUNIA MWAKA 201O!

    HAO KINA KAMAU NA WENZAO WAKAFIE MBELE MECHI IMECHEZWA, NA SIKU IMETOKA HIYOO IMEBAKI HISTORIA half london wameshindwa kuwaita hata ma Landlord wao (watasha) wakafanye hata mazoezi tu kwa kina lord delamere!!

    Aliyedata

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 07, 2010

    Tumefungwa lakini cha moto walikiona, wameondoka na kanzu mbili, moja kapewa Felipe Melo, ingine kapewa Bastos...hahaha, Mgosi mbaya sana aisee...ila Maximo sub zake alifanya mbofu mbofu na pia Ngassa na Mgosi kwanini wananyimana pass? Ngassa kakosa magoli matatu ya ubwete...lah salalaaah!!!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 07, 2010

    mdau wa pundamilia mbavu zangu zinauma sana loo

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 07, 2010

    mtangazaji alisema ni ajabu kwani hawa jamaa hawajafungwa goli lolote tokea Novemba mwaka jana. poleni na hongera

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 07, 2010

    Mechi hii ilikuwa sherehe ya mwisho ya kumuaga MAXIMO, kocha gani asiyeambilika, heri aende zake kwao. Kipa gani anamuweka angekuwa KASEJA hayo magoli 4 aliyofungwa kipa MWARAMI kwa KASEJA ingekuwa chakula tu. Karibu kocha mpya wa Denmark ulete maendeleao.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 07, 2010

    Asante michuzi!!!

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 07, 2010

    Namuunga Mkono Mdau anayemtaja Juma Kaseja. Sijui kwa nini Maximo alikataa kumtumia huyu Kipa namba Moja kwa sasa.

    Chuki binafsi siyo nzuri michezoni.

    Karibu Kocha mpya -Denmark

    Golikipa mzuri angeweza kubadili matokeo japo goli mbili

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 07, 2010

    WADAU HEBU MUANGALIENI BEKI WETU MWENYE JEZI NAMBA 5 MGONGONI MAMBO ALIYOYAFANYA UWANJANI.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 08, 2010

    nauliza kipa,kaokotwa wapi huyu?

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 08, 2010

    Big up Taifa stars. Hongereni sana. Taifa stars hoyeeeeeeeeee!!
    Mmeifunga Brazil!!!! Hilo goli moja tu linatosha kuwapeleka mbali sana. Goli hilo litaingia kwenye kitabu cha Guiness maana nchi changa kwenye mpira kama Tanzania kuifunga nchi kongwe kama Brazil??? unkle Mithupu, huyo kijana aliyepachika goli wavuni anione nimemtayarishia zawadi nono. Email yangu ni mnayani@yahoo.com, number yangu ya simu ni 0754267114. Napatika DSM mwananyamala. Kazi nafanyia Stanbic DSM branch. Hii ni kali ya mwaka.
    Mdau wa bongo

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 08, 2010

    sasa tunataka wale wachawi watolewe adharani tuwaone mabao tumekula but tumejitahidi kipa katuangusha

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 08, 2010

    MICHUZI BORA UNGEKAA WEWE KIPA

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 08, 2010

    Hili bao tamu sana, kwa kweli vijana wetu wanastahili pongezi manake hawa Brazil wamechanjiwa.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 08, 2010

    Kipa wetu alikua pazia tu golini. Jamaa kila wakilenga goli badi nyavu.maximo makipa wako wamekuzingua. kipa gani lile

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 08, 2010

    Bora wangeweka shati golini ikajulikana moja. Maana huyo golikipa hamna chochote kazi kujishika kiuno tu.

    Au alikuwa anaona ujiko kufungwa na akina Kaka ili kesho akawatambie makipa wenzake mtaani kuwa ni yeye tu anayeweza kufungwa na akina Kaka.

    Aibu sana, ila vijana kati walicheza vizuri.Hongera zao

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 08, 2010

    INGEKUWA MASHINDANO YA BIA TUNGEWASHINDA TUU;

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 08, 2010

    Namuunga mkono Kamau. Nasikia hata Rais alikuwepo. Anaacha watu wanakufa njaa na wengine hawana madawa hospitalini anaenda kuangalia mpira? MMh sijui. Baba Amina au baba mwanakombo kaacha watoto nyumbani wana njaa; yeye kaenda mpirani!! ya leo kali

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 08, 2010

    Taifa Stars wangefuata ushauri waliopwewa; wangeomba 'special request' kuwa waruhusiwe kuwa na makipa wawili kwa wakati mmoja wakilinda lango, pengine ingesaidia kupunguza deficit ya magoli.

    Brazil wamewaachia tu hao waTZ, maana sitaki kuamini kuwa Rwanda ni bora kuliko Brazil; si TZ ilishindwa kuifunga hata goli moja Rwanda hapo juzi? Sasa imewezaje kuifunga Brazil?

    Tuseme tu kuwa huu mchezo ulikuwa ni wa kuwapasha misuli moto waBrazil kwa ajili ya kombe la Dunia, kwa gharama za Tanzania. Sasa Brazil ikaona ngoja iwafurahishe kidogo waTZ kwa kuwaachia hiko kigoli. Situmai kuwa kuna walioshangilia baada ya waTZ kufunga hilo goli.

    ReplyDelete
  42. Pablo ShemgoloJune 08, 2010

    oooh the lovely Taifa stars, you did well but you also looked like a sheep without a sherperd for mr maximo seemed to be sided with his own national team at the moment. But big up, the progress are coming.

    ReplyDelete
  43. AnonymousJune 08, 2010

    yeah nadhani kipa wetu alikuwa ovyo, otherwise ongereni taifa stars...ingekuwa mnakipa mzuri matokeo yangekuwa 2-1 au 3-1.

    ReplyDelete
  44. AnonymousJune 08, 2010

    HII MECHI KIPA WETU NDO KAHARIBU. YAANI JAMAA WAKILENGA TU GOLINI LAZIMA IWE GOLI.KHRAAAAAA

    ReplyDelete
  45. AnonymousJune 08, 2010

    Huyo kaka aliyeingia uwanjani sawa amekosea ila ni shauku ya kutaka kumshika kaka....Usifanye utani na shauku bwana...Huyo ndio mwenye mapenzi ya kweli na Kaka....

    Kwa niaba ya wananchi wengine naomba huyu kaka asihukumiwe vibaya...Kwani sidhani kama alikuwa anania mbaya....Wamsamehe tuu jamani....

    ReplyDelete
  46. AnonymousJune 08, 2010

    Kipa kulikuwa hamna huyu hastahili kuwa Tanzania one

    ReplyDelete
  47. AnonymousJune 08, 2010

    Ukiangalia takwimu za mechi kama ilivyoratibiwa na ESPN inaonekana hivi.Kwa mtizamo huo ni wazi Stars walijitahidi kufika langoni kwa brazil mara nyingi.Hii pia inaoneshwa na uwingi wa saves kwa brazil na pia kona.umiliki tu wa mpira ndo walituzidi.Tulijitahidi sana.takwimu zaonesha
    Scoring Summary
    Tanzania Brazil
    Jabir Aziz (86) Robinho (10)
    Robinho (33)
    Ramires (53)
    Kaká (76)
    Ramires (90)

    Match Stats
    Tanzania Brazil
    Shots (on Goal) 18(9) 20(7)
    Fouls 13 15
    Corner Kicks 7 6
    Offsides 6 4
    Time of Possession 39% 61%
    Yellow Cards 0 1
    Red Cards 0 0
    Saves 2 8

    Match Information
    Stadium: National Main Stadium
    Attendance: 35,000
    Match Time: 15:00 GMT

    ReplyDelete
  48. AnonymousJune 08, 2010

    yani huyo kipa wa taifa stars ni ovyo kuliko makipa wote duniani ameachia magoli kirahisi sana hata wale makipa wa shule za msingi wanaweza kuokoa goli la 4 na la 5 wala haikuwa lazima wafunge huyo kipa hafaiiiiiiiiiiii full mdebwedoo

    ReplyDelete
  49. AnonymousJune 08, 2010

    tatizo ilikua waliokuja uwanjani hawakuwa washangiliaji hata kidogo

    ni wenye pesa zao tu na mabosi,maana naona watu waliingia na suti na tai zao na mokasi lol

    nimempenda uyo jamaa alomkumbatia KAKA,jina lake tafadhali!!

    ReplyDelete
  50. AnonymousJune 08, 2010

    Kwa heri Maximo ila umetuchosha, kocha gani huna first eleven for four years, nani alidaka Misri akapigwa tano ukaambiwa mchukue kaseja ukakataa umeweka pazia lako limepigwa tano tena kauze matikiti cruzerio, CV yako ilikuwa picha uliyopigwa na Ronaldo.Anway we scored one.

    ReplyDelete
  51. AnonymousJune 08, 2010

    jamani taifa stars siyo kaseja wala ngasa na ndio sababu kocha wa timu ya taifa ya brazil enzi hizo alikataa katakata kumchukua Romario na pamoja na rais wa brazil kushinikiza na bado Brazil ikachukua kombe la dunia;

    Hivi huyu kaseja alifungwa goli ngapi hivi karibuni na Alhoodod ya Misri? Alifungwa ngapi na Enyimba?

    ReplyDelete
  52. AnonymousJune 08, 2010

    Ivi TFF wanalipi la kujitetea kwa kuwavalisha wachezaji wtu jezi ambazo haziwakilishi taswira ya nchi au ndo kamati ya ufundi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...