WAKAZI wa mji wa Unguja wakijipatia mahitaji ya vitu vya nyumbani katika mnada wa marikiti darajani, tafauti na zamani katika mnadfa huu vilikuwa vikuuzwa vitu vikongwe.
WACHUKUZI wa mizigo wakiwa na rumbesa ya mzigo wakikatisha katika mitaa ya Darajani Unguja, uchukuzi wa namna hii unaweza kuleta madhara kwao kutokana na kutoona kinachotokea nyuma yao.
ASKARI wa Usalama barabarani akiwa na Pikipiki ambayo ameikamata kwa makosa ya barabara akiikokota kuipeleka Kituo cha Polisi Malindi, kama alivyokutwa na mpiga akikatisha mitaa ya Darajani.
WANANCHI wakiwa wanaangalia ajali iliotokea katika barabara ya Michezani, mpanda baskeli aliigonga daladala kwa nyuma baada ya kusimama kwa hafla mbele yake, mpanda maskeli huyu ameumia na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu anayeshughulikia Fedha na Uchumi Dk. Mwinyihaji Makame akitoa muhtasari wa mwelekeo wa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Zanzibar. Picha na Othman Mapara wa Globu ya Jamii, Zenji





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kweli kuna tofauti kubwa kati ya bara na visiwani.Mfano hiyo lumbesa bara unakuta ni mtu mmoja anayehangaika nayo toka shule ya Uhuru hadi karume tena bila wasiwasi zenji watu wawili bado wanahenya kuifikisha mtaa wa pili,hahahahaha.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2010

    Huyo Asakali wa Usalama barabarani sio kwamba anakokota pikipiki aliyoikamata hata,bali anatoka sokoni darani kununua kitowewo na kukiwaisha nyumbani!kama ilivyo kawaida ya wanzazibar wanaume ndio waokwenda sokoni! sio akina mama.
    na mara nyingi ikifika saa 4 asubuhi wanaume wengi utoroka makazini na kwenda sokoni

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2010

    ww Mbigiri hao wanaokokota lumbesa ni wabongo na sio wazenj

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2010

    Kaka Michuzi Tunashukuru kwa kutuletea habari mchanganyiko toka upande wa visiwani wa nchi yetu. Hii ni muhimu sana na tunataka itokee mara kwa mara,

    Unajua visiwani pako kivyakevyake.Hawa jamaa kweli huwa wanatoroka kazini kabla ya muda wa saa za kazi. Hili swala naomba lipewe mada yake lenyewe,
    Mfano: Wakazi wa visiwani huingia kazini wakiwa wamechelwa sana, then kabla ya saa saba mchana huenda kumwomba Mwenyezi Mungu Msikitini; then wanarudi kazini baada ya dk chake kisha kutoweka kwenye kahawa na kashata.
    Ila Zenji kuna fleva zake kama kule Forodhani enzi hizo; unapata pweza, samaki fresh, nk,nk pale kwa disco Bwawani, taarabu na mavari ya ki-mwinyi-mwinyi, dala dala zao, na mambo ya Msheha...viko poa kabisa;

    wape salamu zangu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...