Mhandisi Jenkis Matumbo wa Mkoa wa Kigoma(kushoto) akimwonesha Rais Jakaya Mrisho Kikwete mitambo mipya ya kufua umeme inayozalisha umeme unaosambazwa katika maeneo mbalimbali Mkoani humo na kumaliza kabisa tatizo la umeme katika mji wa Kigoma na viunga vyake.Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa TANESCO mhandisi William Mhando.Wapili kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja. Mhandisi wa mkoa wa TANESCO Kigoma Jenkins Matumbo akimwonesha jinsi mitambo mipya ya kuzalisha umeme unavyofanya kazi katika chumba maalum cha kuongozea mitambo hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2010

    Tusidanganyane ili tupeane kura kiurahisi. Mkoa wa Kigoma unajumuisha wilaya ya Kigoma Mjini, Kigoma vijijini, Kasulu na Kibondo. Kama umeme unapatikana Kigoma mjini haina maana kuwa matatizo ya umeme mkoani Kigoma yamekwisha kwani kasulu, Kibondo na Kigoma vijijini ni giza totorooooooooooooooooooo.
    Tusiingize siasa kwenye kila kitu ... ama kweli huko ndiko kwenye wadanganyika.
    After all unahitajika umeme wa grid na siyo majenereta yanayokula mafuta kiasi hicho.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2010

    mimi nazani wazee wameshindwa kazi uko ma officini waachiwe vijana !!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2010

    acha kulia ujinga wewe,zito mwenyewe amekubali hiyo ni atuwa kubwa sana kwa mkoa wa kigoma,pemba wametumia umeme wa majenerata maisha yote,juzi hata mwezi bado ndo wamepata umeme wa gridi ya taifa,acheni kulalamika kitu watz,kwenye pongezi hatuna budi kusifia.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2010

    Kikwete amkuna Zitto

    MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amemsifu na kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Kigoma.

    Zitto alitoa pongezi hizo jana alipozungumza baada ya kupewa nafasi ya kusalimia wapiga kura wa jimbo hilo wakati Rais Kikwete alipofungua Sekondari ya Nyarubanda kwa ushirikiano wa Serikali pamoja na nguvu za wananchi.

    Mbunge huyo alisema katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi wa nchi, Rais Kikwete amefanya mambo makubwa kwa Mkoa wa Kigoma ambayo hayajawahi kufanywa na viongozi waliomtangulia.

    “Hapa si mkutano wangu, nimepewa niwasalimie kidogo, lakini napenda kumshukuru Rais Kikwete kwa kazi nzuri aliyofanya kwa Mkoa wa Kigoma, ambayo haikuwahi kufanywa na kiongozi yeyote aliyemtangulia na ameonesha kuujali Mkoa,” alisema Zitto.

    Alisema akiwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ataendelea kumuunga mkono Rais Kikwete katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi wa jimbo lake na mkoa kwa jumla, hasa ile ambayo imo katika ahadi za Serikali.

    Mbunge huyo machachari aliitaja baadhi ya miradi iliyofanikishwa katika kipindi hiki cha kwanza cha Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Kikwete kuwa ni barabara mbili za Mwandiga –Manyovu yenye urefu wa kilometa 60 inayopita jimboni mwake ambayo itagharimu zaidi ya Sh bilioni 65, na ya Kigoma – Kidahwe yenye urefu wa kilometa 37 itakayogharimu karibu Sh bilioni 39.

    Barabara zote hizo mbili zinajengwa kwa fedha za Serikali, hali ambayo Zitto alisema inaonesha kuwa Serikali imeanza kuujali Mkoa wa Kigoma.

    Mbali ya hilo, Serikali inatarajia kuupa mkoa huo umeme wa uhakika na leo Rais Kikwete atazindua jenereta tano za kufua umeme ambao utakidhi mahitaji ya mkoa na kuzalisha megawati za ziada.

    Rais Kikwete alisema yuko tayari kuadhibiwa na wananchi wa Kigoma kwa maagizo yake ya kuutaka uongozi wa Mkoa kuzuia ujenzi wa makazi katika vilima vinavyozunguka bandari ya Kigoma na kusema hatajali kama atanyimwa kura kwa hilo.

    Akizungumza na viongozi wa Mkoa juzi, Rais alisema hawezi kukubali kuona bandari ya Kigoma inadidimia kwa kuogopa kulaumiwa na watu wachache.

    Alibainisha kuwa bandari hiyo ni muhimu kwa maisha ya wananchi wa Kigoma na ukanda mzima wa Nchi za Maziwa Makuu na kwamba Serikali iko imara, kuhakikisha bandari hiyo inafanya kazi kwa ufanisi na kwa maslahi ya mkoa kiuchumi na Taifa kwa jumla.

    Alisema akiwa mkoani hapa mwaka 2007, alitembelea bandari hiyo na kuona athari za kupungua kwa kina cha maji kutokana na kujaa mchanga katika eneo la kuegeshea meli, ambao asili yake ni kutoka kwenye makazi ya watu waliojenga milimani na kusababisha mmomonyoko wa udongo.

    Serikali kwa mujibu wa Rais, imetoa fedha na tayari kazi ya kuchimba ili kuongeza kina inaendelea na ni bora kuzuia na kulaumiwa sasa, kuliko kuacha na mazingira ya bandari hiyo yakaendelea kuharibika.

    Awali, akitoa taarifa kwa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Joseph Simbakalia, alisema agizo la Rais mwaka 2007 la kuongeza kina cha bandari hiyo limetekelezwa, na kazi hiyo inaendelea na inatarajia kukamilika Septemba mwaka huu.

    Simbakalia alisema sambamba na hilo, uongozi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, imechukua hatua za kusimamisha ujenzi katika milima ya mji huo ambao ni chanzo cha kuingiza mchanga ziwani kutokana na mmomonyoko. Katika tukio lingine, wananchi wa Kijiji cha Kiganza, Kigoma Vijijini juzi jioni walisimamisha msafara wa Rais, wakitaka kupewa ufumbuzi wa kero yao ya fidia ya mazao kutokana na ujenzi wa barabara ya Mwandiga - Manyovu kwa kiwango cha lami.

    Wananchi hao walitanda barabarani ghafla baada ya magari ya ulinzi ya kiongozi huyo yakiongozwa na gari la Polisi kupita, walisimamisha msafara huo hali iliyomlazimu Rais Kikwete na msafara wake kusikiliza kilio cha wananchi hao.

    Kutokana na madai yao ya fidia, Rais Kikwete aliwaomba wasaidizi wake kwenye msafara huo akiwamo Naibu Waziri wa Miundombinu, Hezekiah Chibulunje, kutoa ufafanuzi wa jambo hilo na kukiri kuwapo madai hayo na kwamba yanafanyiwa kazi baada ya fedha zilizokuwapo awali za fidia kwisha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2010

    zitto mbona keshanunuliwa na CCM ,huko upinzani yeye ni kenge tu aliye kwenye msafara wa mamba na hata kukimbilia ujerumani eti anasoma ni potezapoteza tu ili watz mmsahau kwa makeke yake hatimaye ktk siasa za upinzani na baadaye arejee CCM. haka kajamaa watz hamkajui tu yani njaa kali.
    ALAFU NA WEWE MICHUZI HUO UNAZI WAKO WA CCM SOMETIME UNATUBOA USIWEKE NA HII SASA

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2010

    zito zamani bwana siku hizi ndo walewale!! uchaguzi una mambo halloo "chama chetu cha mapinduzi chajenga njiiiiiiii"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...