Kwa heshima na taadhima naomba niwakilishe kilio chetu Watanzania dhidi ya jamaa zetu hawa (kina Kamau). Sio siri kwamba jamaa wame dominate njia za anga katika ukanda huu wa Mashariki na Kati ya Afrika. Japo hilo linanikera lakini naomba nisilifanye hoja kwa siku ya leo. Sasa kumbe hoja kwa leo ni nini basi! Hawa jamaa wamekuwa na dharau kubwa sana kwa route ya Dar-NRB-Dar ama vice versa, ubaya sana ukiwa una connect kwenda kwenye destination nyingine. Kwa leo sitaongelea ukiwa unakwenda mbali, wacha nijikite hapa ndani ya Jumuia.
Jamaa, wanakukatia ndege ya kutoka Kampala saa 10 usiku, meaning kwamba unafika Jomo Kenyatta Airport saa 11 alfajiri. Ukifika tu, kitu cha kwanza kukutana nacho ni kwamba flight ya kwenda Dar imekuwa delayed mpaka saa sita mchana ama saa nane. Usumbufu unakuja kuwa Entebbe ulitakiwa ucheck in saa 9 usiku, na kama ulikuwa Kampala ina maana ulitoka saa 8 usiku. Waweza fikiria mateso ambayo hawa jamaa wanaku subject, umetoka saa 8 usiku Kampala, unafika Nairobi saa 11 alfajiri, unazubaa mpaka saa 8 mchana ndio ufike tena Dar (si bora ungepanda mabasi ya Scandnavia kama bado yapo?)
Route ya Kigali ni balaa zaidi, unacheck in saa 5 usiku, mnaondoka Kigali saa 7 usiku, mnaelekea Bujumbura, hapo wanazuga mpaka saa 9 usiku. Mnatoka tena Bujumbura na kufika Nairobi saa 10:30 alfajiri na kukuta tangazo lile lile la kusubiri mpaka saa sita/nane mchana. Kiukweli tabia hii inachosha na kukera. Niandikapo niko Jomo Kenyatta Airport kutokea Kigali na yamenikuta haya (anyway kwa sababu za kiitifaki usiweke email yangu upenuni).
Wito wangu kwa Watanzania ni kwamba hawa jamaa wameshatudharau kwa kiasi kikubwa, wanafanya wanachotaka, sijui Mh. Makatta na lile Shirika letu la ninhii wana mpango gani, maana tumechoka kiburi cha hawa kina Kimau.Jamaa zetu wa Precision ile deal yao ina kupata na kukosa, sitaki kufanya uchambuzi huo kwa leo (na hata hivyo sio National flag carrier ile, ni basi tu tunawalaumu bure kina Shirima).
Sasa bana nirushie hiki kilio changu. Mimi wacha nizame online nione kama naweza pata grounds za kuwa sue hawa Watani wetu (japo wanachimba mkwara sijui na Warsaw Convention na sijui madudu gani).
Siku njema.
Mdau Mzalendo.

Tumia ethiopia airlines mimi walisha nilaza Lusaka kisa eti wameleta ndege ndogo...
ReplyDeleteSalaam wadau,pole kaka kwa yaliyokukuta ila nasema kheri yako wewe maan mimi nilipatwa na kisanga kama hicho kufikaka saa kumi na mbili alfajiri na kupangiwa ndege ya saa sita mchana na baada yakufika saa sita nikaambiwa ndege itachelewa so itakuwa saa nane,mbaya zaidi ilipofika saa nane nikaambiwa ndege imejaa sasa nikawauliza walinipatia vp tiketi wakati wanajua ndege imejaa?na unapotaka kujua kulikoni unaambiwa watizedi mna kiswahili kirefu.
ReplyDeletewatanzania tujutahidi tuwe na vyetu ndio heshima itakuwepo
WABONGO BWANA....SASA MNALALAMIKA NINI??NYINYI WENYEWE SI MMESHINDWA KU MANAGE NDEGE YENU YA ATC...NDIYO FAIDA YAKE HIYO....NA BADOO...MMEKALIA WIZI TU...WAKENYA WAJANJA NDIYO MAANA NI MAMENEJA WA MABENKI NA SEHEMU KIBAO, UTADHANI WABONGO HAMJASOMA
ReplyDeleteComplaining haitasaidia kama wahusika hawaambiwi...Uzuri wa huku kuna competition ukiona huyu hafai unahamishia biashara yako kwingine...Ni heri ulipe hela nyingi lakini roho yako iwe safi kuliko kulipa cheap ticket na ndio hizo stops kibao....na pia kama hamna passenger bill of right ndio hivyo...
ReplyDeleteJapo unamalalamishi hapa kosa ulilofanya ni kujumuisha Taifa nzima hata wale ambao hawahusiki.
ReplyDeleteSasa je tukusaidie vipi kama siyo uchochezi unaleta hapa?
Unahaki ya kulalamika ila kwa lugha yako inaonesha wewe ni mzushi.
Biashara ni biashara hivyo kuwa wazi na ulalamikie kampuni na siyo kusema Wakenya hivi na vile...
Kwani Wakenya wote wana hisa kwenye hiyo Kampuni?
Uzushi na uzalendo ni vitu viwili tofauti mdau unayejiita "Mdau Mzalendo"... Uliyoandika hapo juu siyo uzalendo ni uzushi na uchochezi kwani ni kosa kujumulisha watu na kuwashutumu kwa pamoja.
ReplyDeleteJe unahaki gani kuwajumulisha Wakenya wote kama siyo uzushi na kuwa na nia ya uchochezi? Na je hauoni kwamba wewe na huyo anayejiita "Kamau Mkenya" ambaye uraia wake chimbuko lake ni hapa kwenye blogu ya MICHUZI wote ndugu moja kwa kuwa na sifa ya UCHOCHEZI? Hilo ni swali la kutafakari...
Kama tatizo haujaridhishwa na huduma basi hatua muhimu ni kutoa malalamiko kuhusu kampuni na siyo nchi kwa ujumla. Hivyo zungumzia Kampuni na siyo watu kwa pamoja japo unauhuru wa kuongea kwani unachangia mgongano badala ya kuleta uelewano.
Toa ajenda nyingine hii uliotoa ni uzushi na uchochezi kwa kutumia kigezo cha uzalendo.
Mdau Mkenya
mhhh inatisha ila tufanyeje sasa!!!wakenya nao!!!hata katari pale wanatabia hiyohiyo wahudumu wakikenya wakiwaona wabongo basi hata lugha wanajifanya hawajui ili kukusumvbua tu!!daa!zat is too much!!
ReplyDeletehuyo mattaka kazi kama hana tena maana wafanyakazi wote ATC walisimamishwa kama siyo kufukuzwa, sasa na yeye si alikuwa mfanyakazi wa ATC au? anyway hizo ndege wachana nazo kama vipi toka kigali na basi hadi bk the chukua ndege au meli hadi mwanza chukua ndege hadi dar.kama unataka mengine bukoba na mwanza ni karibu sana na hao wakwe zetu kama si watani zetu.
ReplyDeleteUtter crap!How come we dont "hear" anyone; Tanzanians included complaining about the long waits in Amsterdam or the fact that KLM is a major carrier(and dominates) to most of European and African destinations?Are you aware that Tanzania does NOT have its own National Carrier?who would you blame huh?I advise you to use your energy in more productive arguments like taking the Tanzanian government to task:why it CANNOT sustain its own carrier...THEN and ONLY then you COULD possibly start an argument on this podium.!
ReplyDeletebadala ya kuishukuru kq kwa kututoa kimasomaso wana afrika mashariki unalaumu?? wewe mwendawazimu kweli.
ReplyDeletehalafu unafanya hasti jenerolaizesheni! ati wakenya?!
iulize serikali yako kwanini ilishindwa kuendesha ndege - unafikiri ndege ni daladala kwamba ikichomoka na abiria mmoja itapakia wengine njiani?
afterall hujalazimishwa kupanda hiyo - kuna fly 540, turkish air na shared charter.
fanya uchunguzi kwanini delai zinatokea, kisha toa ushauri ili kuleta maendeleo ya usafiri wa anga hapa ea. ET haituhusu, KQ ndio ya EA.
kuweni wapenda maendeleo wazalendo wa AfriMash.
SAFI SANA SISI NI TAIFA LA WALALAMIKAJI KILA KUKICHA, HATUTAKI KUFANYA KAZI BALI KWETU KULALAMIKA NI DILI, SAFI SANA.
ReplyDeleteKama huduma mbovu panda ndege nyengine, biashara yao ikisha kwenda kombo watafunga hiyo route na itakuwa imekula kwao.
ReplyDeleteAnzisha ndege yako itakayopuruka Afrika Mashariki nzima kuanzia Dar hadi Juba ambayo haitachelewesha safari zozote,kuwa na tiketi za bei nafuu uone kama utaweza kuhimili ushindani katika sekta hiyo!Nyoo!
ReplyDeleteTanzania tumefulia..............wewe hadi toilet papers tunaimport shame on us.............
ReplyDeletePole mdau kwa yaliyokukumba mimi kilio changu ni kwa hawa watu wa KLM
ReplyDeletenilimiss flight Dublin Airport Airlingus wakati nakata tiketi sikuambia kuwa Air Lingus itana deal na KLM, WAkati mimi natafuta mlango wa KLM ni check in naambiwa umechelewa kucheck in hivyo inabidi uwapigie Office za KLM Holland nawapigia Holland naambiwa office zitafunguliwa saa 3.00 a.m.
hapo ni saa 10 alfajiri any way nikasubiri mpaka kwenye saa tatu niakapiga simu nikaambiwa KLM hawapo responsible na abiria kumiss flight, fine nikata kuclaim wa change date au compensation wakakataa nakudai Ticket is invalid.
Sasa angalia huo usumbufu wakati nanunua ticket sikuambiwa hayo yoote matatizo yamenikumba kila mtu ananiruka, nacho taka niseme nikuwa mashirika ya ndege haswa KLM,Kenya Airways hawako intergrity for their passengers wao wakisha uza ticket tu ngoma unayo
Precision Air nao vipi?
ReplyDeleteMtalalamika sana lakini kama mkulima kala mbegu tusishangae kunyanyasika kwenye mashirika ya ndege nje. Tumieni kura zenu Oktoba kuweka watu kwenye ofisi za utumishi wa umma ambao hawatasaini mikataba ya kuwaumizeni walipa kodi wao.