Na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii, Arusha

Mtu mmoja aliyejulika kwa jina la Ritha Mrema (48) mkazi wa njiro amefariki dunia mara baada ya kupigwa risasi na mfanyakazi wake wa ndani katika paji la uso.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi wa mkoani hapa Basilio Matei wakati akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa tukio hilo lilitokea June 17 majira ya usiku katika eneo la Njiro Block F ambapo ambapo mtuhumiwa Omary Ally (18) alimpiga risasi tajiri yake ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Njiro.

Kamanda amesema kuwa wakati walipokuwa wakimuhoji mtuhumiwa alisema kuwa ilikuwa ni majira ya usiku katika nyumbani kwao walisikia kishindo cha wezi wakivunja ili kuaingia ndani, ndipo marehemu akaignia ndani na kuchukua bastola na kumpa mfanyakazi wake huyo wa ndani aitumie.

Alisema kuwa mara baada ya kukabithiwa kijana huyo wakati alipokuwa ana jiandaa kwa ajili ya kukabiliana na wezi hao ndipo alipo jikuta amempiga tajiri yake .

"kijana huyu alikuwa hajui kutumia silaha. Sasa mara baada ya kukabidhiwa na tajiri bastola hiyo wakati akiikoki badala ya kuwageuzia wale wezi alikosea na kumgeuzia tajiri yake na kumpiga katika paji la uso"alisema Kamanda Matei.

Basilio alisema kuwa wakati tukio hilo likitokea mume wa marehemu alikuwa hayupo na ilisemekana kuwa alikuwa amesafiri kibiashara kwenda nje ya nchi na alimuachia mkewe silaha hiyo kwa ajili kujilinda.
Alisema kumuachia mtu silaha unayomiliki kihalali ni kinyume cha sheria ya umiliki wa silaha kutokana na mwanamke huyo kutokuwa na ujuzi pamoja na leseni ya kutumia silaha hiyo.

Aidha kamanda alisema mtuhumiwa mpaka sasa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi hapo uchunguzi utakapo kamilika na kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu shitaka, bila shaka la kuua bila kukusudia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2010

    Masikini kijana wawatu, alikuwa tayari kufa kwa ajili ya tajiri na mali yake, sasa yuko lupango. Poleni wafiwa, huu ujambazi utakuja kwisha lini???????. Maisha Bongo ni mashaka makubwa!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2010

    inasikitisha halafu inachekesha

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2010

    Hapo mpuuzi kuliko wote ni huyo mume wa mama mwenye nyumba. Utamuachiaje mkeo asiyejua kutumia silaha bunduki ukijua fika kuwa ni hatari sana. Pia kuna uwezekano kuwa njama imetendeka hapo kati ya mume wa mama na huyo kijana na mama akawa alishaelezwa kuwa ukishindwa kuitumia ampatie kijana na kijana akafanya alichoelekezwa. kama ni hivyo basi huu mkakati ulikuwa ni kabambe. Naamini Tanzania wako wanandoa wengi wanapoteza maisha kwa kuuawa na wenzi wao na jamii hujua kuwa ni bahati mbaya kumbe hakuna kitu kama hicho. Huyo kiaja abanwe sana tu atasema kama alitumika kukamilisha mpango mzima. Njia ya muongo ni fupi, ukweli utajiweka wazi tu iwapo vyombo husika vitafuatilia kwa makini na kutopokea rushwa.Pia yawezekana ni bahati mbaya! Poleni sana wafiwa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2010

    Mdau wa tatu, TUPO PAMOJA! You had in mind what I exactly had in mind, that is, CONSPIRACY THEORY! Kabsaaa! No question about it! Ila tu kwa kweli uchunguzi ufanyike, I might be wrong, I am only human. Sikutaka kuongea kwanza maana sikutaka kuonekana kwamba nina kiherehere kama mbuzi wa shughuli. Maana duh!

    Mi baada ya kuisoma hiyo 'story' I was like, mmmhh! Kilichonijia akilini ni kuwa huyo baba alikula njama kumuua mke wake, kutumia 'aiders and abetters'. Kabsaa! Watu naona sasa wameamua kuacha zile za kuzibana pumzi usiku na asubuhi kupiga mayowe, baada ya kushtukiwa, na badala yake 'wanabuni' mbinu nyingine, kama hizi!

    Issues:

    1. Je, hii ni mara ya ngapi kwa huyu baba kusafiri - be it kwenda nje ya nchi ama mikoani?

    2. Je, kila akisafiri huwa alikuwa anamuachia huyo mama hiyo silaha kwa ajili ya kujihami ama hii ndio ilikuwa mara ya kwanza? Kama ilikuwa ndio mara ya kwanza, kwa nini aliamua kumuachia hiyo silaha?

    3. Kuhusiana na hao wezi waliokuwa wamekuja kuiba ama kuvamia, huyo baba alijuaje juaje kuwa watakuja mpaka amuachie huyo mkewe silaha, NA KWELI WAKAJA! Mmmmh! Hapa kuna kitu hapa. Hao wezi, huyo baba, na hao wezi, wote wasekwe lupango, mpaka watajane!

    4. Hiyo 'story' nani aliyeipika? Ni huyo kijana ama mashuhuda? Maana marehemu tayari alikuwa ameshakufa! Halafu, mbona hiyo story imekaa kumtetea huyo kijana zaidi? Huyo mumewe ana lipi la kusema kuhusiana na hilo? Ama yee ndie aliyemfundisha huyo kijana cha kusema? Halafu, ilikuwaje kuwaje mpaka silaha akailekeza kwa marehemu? Alimfananisha na hao wezi ama?

    5. Huyo baba is equally liable for the death of his wife kwa uzembe wake wa kuwaachia watu wasio na vibali wala ujuzi wa kutumia silaha, silaha ili wajihami. To me he is the root cause cha hicho kifo. Yeye awe charged kwa murder, na si Manslaughter!

    Huyo kijana na hao wezi ni aiders na abbtters. Muuaji mwenyewe ni huyo baba huyo. Ila I am only human, and can be wrong. Ila huyo kijana abanwe nanihii mpaka aongee, ila imsimbane sana. Na huyo baba nae asekwe lupango please kwa murder.

    MAREHEMU NA APUMZIKE KWA AMANI. DAMU YAKE NA ISIPOTEE BURE.

    Nawahurumia hao watoto wa marehemu, maana mama kaenda, baba mwenyewe ndio huyo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2010

    Mnasikia mabwaba maafande, hao watu wahusika na hicho kifo, yaani huyo kijana na huyo baba, wahojiwe katika vyumba tofauti na maafande tofauti kwa wakati mmoja, vyumba vya mahojiano viwe mbali mbali ili wasisikilizane, halafu wapigwe maswali sawa, nina uhakika majibu yatatofautiana tu, na ukweli utajulikana tu, hapo kwa jinsi ilivyokaa kaa hapo, kuna namna! There is something fishy about it! I SMELL A RAT!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2010

    Mabwana Maafande, samahani, na si Mabwaba maafande. Typing error.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2010

    Wadau hapo juu mko sahihi sana kuna watu wanawachukia sana wake zao!!!!! Kwa vyovyote huyo mama alikuwa hajui kutumia siraha!!! Lakini pia msisahau kuwa kuna wanawake waoga sana hawawezi kumeet na wezi face to face!!!!! So sad jamani!!! Mume atashitakiwa ikigundulika mke hakuwa na kibali cha kutumia siraha!!! Polisi arusha wamezidiwa nguvu na wezi!!! Mji hauna Amani kabisa huo ukiamka salama unaomba mungu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2010

    Sounds fishy to me...Hata kama hujui kutumia silaha huwezi kujeuka nyuma ukampiga mtu aliyekupa hiyo silaha...Duh CSI fanyeni kazi mpaka kieleweke.....Unajuaje huyo kijana aliwaambia hao watu mzee hayupo? ...haya mambo mimi siyaamini siye tukiwa wadogo baba akiwa anasafiri ndio waizi wanakuja na tulikua hatutangazi kabisa ...kumbe deal alikua nayo mlinzi wa nyumba na waizi.....

    Wasimwachie akijifanya mjinga lazima aseme ilikuaje kujeuka na kumpiga mtu kwanza kwenye paji cha uso? Na ilikua umbali gani ana kwa ana au la?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 20, 2010

    Toeni pole na acheni pumba hapa za kujifanya mnaangalia sana tv.
    Ni bahati mbaya period.
    Mibichwa tu na ushamba wenu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 20, 2010

    Wewe mdau wa Sun Jun 20, 12:18:00 AM, Umekosa hoja. Wewe hujatoa hoja unahimiza wenzio na uchunguzi una nafasi yake wengine hapa ni taaluma yao hivyo hoja zao zinaweza saidia kupata ufumbuzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...