Na Ripota wa Mahakama
wa Globu ya Jamii
Hatima ya kuwapo au kutokuwapo kwa mgombe binafsi nchini, imebakia mikononi mwa bunge baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania kubainisha kuwa suala hilo linapaswa kuamuliwa na Bunge na si Mahakama.
Maamuzi hayo ambayo ni ya Jopo la majaji saba wa Mahakama ya Rufani Tanzania, likiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Augustino Ramadhani yametengua uamuzi wa kuwapo kwa mgombea binafsi nchini ambao ulitolewa hapo awali na mahakama kuu, baada ya kukubaliana na hoja za Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikil, zilizotaka kuwapo kwa mgombea binafsi nchini.
Jaji Ramadhani asubuhi ya leo alisoma hukumu dhidi ya kesi hiyo, hukumu ambayo imeufuta uamuzi wa kuwapo kwa mgombewa binafsi hivyo kurudisha suala hilo bungeni.
Katika maamuzi ya jopo hilo kuhusiana na rufani hiyo iliyofunguliwa na Serikali, mahakama hiyo imesema kuwa hoja ya mgombea binafsi ni ya kisiasa zaidi na si sheria.
Jaji Ramadhani alisema kuwa kutokana na ukweli huo, mahakama kama makahakama inasimamia sheria hivyo haiwezi kutolea maamuzi suala hilo ambalo kwa upande
mwingine linagusa katiba.
Aliongeza kuwa Bunge ndilo lenye mamlaka ya kufanya marekebisho ya kikatiba, hivyo iwapo katiba itakuwa inahitaji marekebisho inawajibika kufanya hivyo.
Kutokana na hilo, Jaji Mkuu amesema kuwa mahakama haina mamlaka ya kutengua kilichopo katika katikba, hivyo sula la mgombea binafsi linafaa kushughurikiwa na bunge.
Lakini kwa upande wa Mch. Mtikila ambaye alifika mahakamani hapo kusikiliza uamuzi huo, akiwa nje ya mahakama aliifanananisha hukumu hiyo na hukumu ya kisiasa na kusema kuwa haikuwa ya kisheria.
Akizungumza na wanahabari, Mtikila alisema kwamba mahakama hiyo hakikutenda haki na kwamba maamuzi ya mwanzo ya kuruhusu mgombea binafsi ndio yaliyokuwa ya haki.
Awali katika rufani hiyo Serikali ilidai kuwa Mahakama Kuu ilikosea kwa kujipa mamlaka ya kutoa uamuzi wa kuwapo kwa mgombea binafsi nchini.
Katika hilo Serikali ilidai kuwa mahakama kuu ilifanya makosa kwa kujipa mamlaka yakutengua vifungu vya katiba ya nchi.
Mbali na sababu hiyo Serikali ilidai kuwa mahakama hiyo ilijipachika mamlaka ya kibunge ya kutunga sheria.
Hiyo ni ilikuwa ni Rufani ya pili kufunguliwa na serikali kuhusiana na hoja hiyo ya mgombea bianafsi, kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2007 Serikali ilikata rufani dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu ikidai kuwa mahakama hiyo ilikosea kisheria kutafsiri ibara ya 21(1)(c), 39(1)(c) (b) na 69(1)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lakini rufani hiyo ya mwanzo ilitupwa na Mahakama ya Rufani, baada ya mahakama hiyo kukubaliana na hoja ya kuwapo kwa mgombea binafsi.
Mei 2006, mahakama Kuu ilitoa maamuzi ya kuwapo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi ambapo mahakama hiyo ilisema kuwa maamuzi hayo yanatokana na katiba ya nchi ambayo inatoa haki hiyo.
Maamuzi hayo yaliweka wazi kuwa kila mwananchi ana haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi.
Pia maamuzi hayo yalibahinisha kuwa Katiba haiweki masharti kuwa hilo lifanyike kwa mtu kujiunga na chama fulani na kwamba hilo limewekwa wazi katika katiba.
Kwa mara ya kwanza Mtikila aliwahi kushinda kesi kama hiyo mnamo mwaka 1993, ushindi ambao ulitokana na maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
Pamoja na maamuzi hayo yaliyomfanya Mtikila kuibuka kidedea, Bunge lilishindwa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi.
Kwa kuwa kuna utata katika katiba yetu, Bunge ambalo ndilo mwakilishi wa wananchi, litatunga sheria ya kuwepo au kutokuwepo huyo mgombea binafsi. Hilo ni bora zaidi kuliko maamuzi kufanywa na Mtikila au Mahakama! hata hivyo ni usumbufu tu wa mtikila, Muda wote lazima atafute visababu vya kuonekana kwenye TV!
ReplyDeleteBaada ya uamuzi wa shauri hili kuzungushwa kwa muda mrefu watu wenye kuijua vizuri nchi hii walijua kinachoendelea na maamuzi yatakuwaje. Udumu "Uhuru wa mahakama"
ReplyDeleteKhaaaa hawa nao????!!!! kwani sheria zinasemaje? Hawawezi kuangalia sheria na kujua kama zinaruhusu au la? na kama kulikua na upenyo hawakujua kuwa kuna miaka watu watahitaji kufanya hili basi wawamwachie independent people wenye hela zao mwaka huu then wakae vikao na kutafakari hili jambo huko mbeleni na jinsi wanavyoona linawezekana TZ?
ReplyDeleteUkiachia bunge sasa hivi mpaka lianze kuangalia si uchaguzi utakua umepita?
Ndio hivyo kama hamuupdate sheria za nchi kwenda na wakati wenye akili watawachallenge mpaka mkome.
I can't believe wanashindwa kuangalia sheria na kusema kutokana na katiba yetu kifungu hiki haikubali au inakubali full stop. Na kama haikuwapo basi ni kuwa nchi haikatai hilo...
Bongo kweli tambarare
sikutegemea kuwa mahakama ya rufaa chini ya majaji saba ingetoka na majibu kama haya. hii ni siasa kabisa kuliko ukweli wenyewe. Ee mungu ibaliki Tanzania na watu wake.
ReplyDeleteWe mtoa maoni 10.59 na 8.08 msiwe kama watoto wadogo unalilia kitu unataka saa hiyo hiyo. Bunge kazi yake ni kutunga sheria sheria zilizopo haziruhusu mgombea binafsi sasa unataka mahakama iamue awepo mgombea binafsi iende kinyume na katiba. Yaani mahakama kazi yake sio kuiharibu katiba bali ni kutimiza yale yalioandikwa kwenye katiba. Msifanye mambo haraka haraka mkaonekana hamfikiri jamani. This is pretty simple mbona. Katiba yetu ina matatizo na chombo kile kile kilichounda katiba hicho hicho kinatakiwa kubadilisha. Kumbukeni jinsi tulivyopata mfumo wa vyama vingi. wananchi walitoa maoni yao and then the process ikaendelea. Mtindo wakubadilisha katiba ndio huo huo msifanye mambo kienyeji. Usilaumu kitu usichojua bwana aha!!
ReplyDelete