Polisi mkoani Arusha wakipakia mwili wa Mmoja wa watu waliouawa kwa tuhuma za ujambazi katika aeneo la Unga Limited Mjini ArushaNa Woinde Shizza, Arusha
JESHI la polisi mkoani Arusha limewauwa kwa kuwapiga risasi watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi baada ya kupata taarifa za kufanya uhalifu wa kupora mishara kutoka moja ya kiwanda kikubwa mjini hapa.
Watu hao waliuwawa majira ya saa tano eneo la unga limited baada ya kurushiana risasi na askali wa jeshi la polisi ambao waliwashinda nguvu na kufanikiwa kuwauwa majambazi hao.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo Japhet Lukumai alisema kuwa majamazi hao wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Corolla walisimamishwa na askali hao ambapo walikataa kusimama na kuanza kuwarushia risasi askali hao.
Lukumai alisema baada ya kurushiwa risasi askali polisi waliwajibu ndipo walipofakisha kuwa uwa majambazi hao baada ya majibizano ya muda murefu.
Kwa upande wa Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Basilio Matei alisema kuwa wananchi wasamaria wema walitoa taarifa polisi na ndipo askari wake walipo anza kuwafatilia majambazi hao.
Alisema kuwa mara baada ya majambazi hao kugundua kuwa wanafatiliwa ndipo waliporusha risasi juu na kuanza kushambuliwa na askari adi polisi walipo wauwa.
Matei aliwataja watu hao kuwa ni Erick Masawe na Michael Raphaeli wote wakazi manispaa ya Arusha.
Matei alisema kuwa baada ya kuuwawa watu hao walisachiwa na kukutwa na bunduki aina ya shotgun ilikuwa imekatwa mtutu leseni ya udereva ya Masawe,na funguo za pikipiki aina ya Toyo T974 BFZ ambayo ilitafutwa na kukamatwa.
Kamanda aliongeza kuwa kwa uchunguzi waliofanya wamebaini kuwa majambazi hao walishawahi kufugwa kwa makosa ya wizi wa roba na wametoka magereza hivi karibuni
Matei alisema miili ya marehemu hao imeifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti kwenye hospitali ya mkoa wa Arusha Mountmeru ikisubiri kutambuliwa na ndugu zao.
Matei alitoa alimpongeza mwananchi ambaye ametoa taarifa hiyo na aliaidi kumzawadia na alitoa wito kwa wananchi waendelee kutoa taarifa za majambazi ili waweze kuthibitiwa.


wana aki ya binadamu wako wapi?
ReplyDeleteAjari kazini
ReplyDeletekuwauwa majambazi kwa mtizamo wangu ni kitu kinachowezekena na kinafanyika katika nchi karibu zote duniani sana sana pale majambazi wanapoonekana kuhatarisha maisha ya watu. Kutokana na maelezo ya mwandishi wa habari hii, Polisi walifanya kosa la kimsingi la kujaribu kuwasimamisha watu wenye silaha. Polisi ilibidi wawafuatilie kwa muda mrefu mpaka hawa jamaa wajisalimishe. Ni ngumu kujua kama kweli walikuwa ni majambazi maana mashahidi wote ni marehemu. Na hata ushahidi wa polisi kudhibitisha kwamba jamaa hawa ni majambazi ni batili kwani hawapo kuthibitisha. kama ni finger prints kuwa ushahidi, inawezekana polisi wamejihudumia kutoka kwa miili ya watuhumiwa. Kwa nyumbani polisi kukusimamisha unajiuliza mara mbili maana hata nao badhi yao ni majambazi pia.
ReplyDeleteWeka yote pembeni, Let's assume these guys were criminals! once the criminals have been gunned down, their bodies should be handled with respect like any other deceased person. Hii habari inaonekana kila pahala duniani, hivyo ni lazima polisi wetu wafundishwe kuheshimu utu na pale utu unapochukuliwa bali wafundishwe kuheshimu maiti. Yangu ni hayo. So sad to see this rather disturbing photo. Ningeomba bwana Michuzi uiondoe tafadhali
Ankal yani picha hii imeniuma sana kila nikiitazama polisi wetu hawana utu kabisa wala hawajui thamani ya raia hii ni aibu hatukatai jambazi ila anahaki yake kama binaadam ubebaji gani wa mwili wa narehemu.shame on youu we polisi ulo beba mwili wa marehem . honeypie
ReplyDeleteasiefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu mnajidai nini kuwaonea huruma? kwenye hilo tukio la wizi wa mishahara ni lazima damu isiyo na hatia ingemwajika then nyie nyie ndo mngeanza kulaani kwa kishindo safi sana jeshi la polisi ueni wote hata wao wanaua watu ovyo juzi mbezi wameua wafanyabiashara wawili dawa ni kubastisha hhivyo vichwa shwain kabisa wametoka jela juzi juzi ina maana hawajakoma walikuwa wanapiga watu roba wametoka jela wameamua kushika mtutu next time si wangekuja na bomu kabisa? sioni huruma ng'ooo? na kwa upande wa magari ya kubebea wagonjwa bongo hayapoa kabsaa labda hospitali binafsi mara nyingi ajali zinapotokea yanakujaga hayo malandrover ya mwaka arobaini na saba hakuna cha nesi wala nini huwa yankujaga na mapolisi kwa hilo inatia kinyaa sana na aibu kumuweka majeruhi au marehemu kwenye gari kama hio kwa dar ni fashion manake yamejazana kweli ikitokea ajali yanawahi eneo la tukio utadhani yenyewe ndio zima moto!
ReplyDeleteHAWAHITAJI KUHESHIMIWA..NINYI MNAOSEMA MAJAMBAZI YAHESHIMIWE MNA MAANA GANI? POLISI NAWAPA PONGEZI SANA..YOTE MLIYOYAFANYA NI HAKI TUPU. NINYI MNAOLALAMIKA MNATAKA HAO WABEBWE KIVIPI? HAWAHITAJI HESHIMA WALA KUHESHIMIWA...JE MAJAMBAZI YANAPOVAMIA MBONA YANAUA NA KUBAKA..JE MNATAKA KUSEMA YANAUA NA KUBAKA KWA USTAARABU? ACHENI UNAFIKI..WANASTAHILI HIVYO KWA MATENDO WALIYOYAFANYA, POLISI MMEFANYA KAZI NZURI SANA..PONGEZI.
ReplyDeleteIts a war between raia, polisi na majambazi ambapo majambazi yameshapoteza utu kwa kuua watu ovyo na hata kuua polisi kama wangeweza.
ReplyDeleteSo its all abt hate kwamba iri ni riuaji rikubwa-tupa huko.
May be they are wrong ila HATE ndio sababu.
huyo jamaa wa Fri Jun 25, 10:20:00 PM,kwanza hiyo lafudhi yake tu inaonesha jinsi gani alivyokuwa na roho ya kutu, kasema "yanakujaga na mapolisi" sasa ndo lugha gani hiyo.Kila mwananchi huwa anamchango wake na ndio maana adhabu ya kifo huwa inapingwa!
ReplyDeleteYes, dawa ya moto ni moto. atakeyeishi kwa upanga naye atamalizwa kwa upanga. P Mollel. Arusha.
ReplyDeleteNinyi mnaowaurumia majambazi, bora muwaurumiye waliouawa na majambazi na jamaaa zao
ReplyDeleteMichuzi utakuja kuua watu, unaweka pidha za watu wamekufa! Inawezekana huyo ni mtoto, ndugu, mume, kaka wa mtu mwingine ambaye anaweza akamuona amekufa na kupatwa na BP naye kufa!
ReplyDeletePili, hii globu ni ya kila mtu, nina watoto wawili wadogo wanaipenda sana, hivyo vitu kama hivyi sio vizuri kuweka public.
Tatu, Ningekuomba wewe kama mwandishi wa habari uweze kutumia ujuzi wako wa kufundisha jamii pamoja na hao Polisi, ndio jamaa huyo ni jambazi ila at the same time ana haki yake. Please jaribu kukemea issue kama hizi. Bila ya watu kama wewe Tanzania haiwezi kuendelea na tunahitaji mchango wako ndg Michuzi.
All People, Bandits inclusive, are innocent until proven guilty (by Courts of Law).
ReplyDeleteKwa kweli hamna anayewapenda majambazi haswa ukizingatia kuwa wao wenyewe ni 'wanyama', yaani hawana utu wala huruma hata kidogo, na wala wakija kuvamia hawabagui, yaani watadhuru ama kuua wote, hata vitoto vichanga visivyo na hatia.
Ila, hiyo haimaanishi kuwa polisi / walinda amani katika ku-deal na hao majambazi ndio nao waaue back. Tukifanya hivyo, who will note the difference (I mean, what is the difference) kati ya hao majambazi na polisi? Nadhani mbele ya watu, wote watakuwa wanaonekana kama 'wanyama' na wasiojali utu wa binadamu.
Polisi wangeweza wakawapiga hao 'majambazi' shaba ya mguuni au sehemu nyingine yoyote ile (lakini nadhani hasa mguuni) kwa lengo la kuwa-slow down hao majambazi ili wawakamate - yaani lengo lisingekuwa kuwauwa hao majambazi.
Nadhani watu kama hao wakikamatwa wakiwa hai huwa wanakuwa na 'thamani' zaidi, kwani ushahidi (maelezo) unaweza kupatikana kutoka kwao ambao unaweza kupelekea hata pengine kukamatwa kwa kundi zima, au kupelekea kwa hiyo deal kuwa solved vizuri zaidi, tofauti na wakipatikana wakiwa wamekufa.
Hivyo nadhani inabidi kuwe na tofauti kati ya majambazi na polisi (kwa namna ambayo polisi wanawa-handle majambazi vs. Majambazi wanavyo ua ua hovyo raia), kwani polisi wengi wameenda shule ama kupitia mafunzo, hivyo wao wengi wao wamestaarabika kuliko majambazi, na tunawategemea wafuate taratibu (kamata jambazi, ikizidi sana shaba ya nguu, then rumande, then mahakamani, mahakama iamue kesi kwa ushahidi)- JAPO NI NGUMU MAANA MAJAMBAZI WANAKERA! HAWANA UTU KABISA HAWA MAJAMBAZI, YAANI SIO WATU KABISA! ILA TUJITAHIDI HIVYO HIVYO KU-DEAL NAO KIUTU.
NYINYI NYOTE HAMJAWAHI KUVAMIWA NDIYO MAANA MNAONA HURUMA AU NA NYINYI NI HAOHAO MAJAMBAZI,
ReplyDeleteMI NAONA POA TU KUFANYIWA HIVYO MAANA WAO WAKIKUVAMIA HAWANA SALIAMTUME, TENA NA MAPANGA BORA HATA WAO WANAPIGWA RISASI MOJA WAMEVUTA WEWE NA JAMAA ZAKO MNAUGUZA MAJERAHA YA MAPANGA NA UNAWEZA USIPONE HAPOHAPO WAMEKUIBIA YAANI MAJAMBAZI NI BORA WAFANYIWE HIVYO TU!!
Mnaotete kuuwawa majambazi au na nyie ndio wale wale nini(Majambazi)?mmeshaelezwa kuwa walijibizana risasi na polisi,sasa hapo mlitegemea nini?acheni use....e
ReplyDeleteanon 01:06:00 we ndio ndio nyang'au kweli usijidai we ni malaika wa mapambio hivyo una huruma sanaa! ndiyo na roho kutu kama wewe unajidai nini hapa hayo ni majambazi yalikuwa yanarushiana risasi na mapolisi, je ingetokea mapolisi wamekufa ingekuaje?? sifagilii ushuz hata siku moja hawakujifunza jela hiyo ndio haki yao, hata kama ni ndugu yako ulia mbali , kwani hujaona mtoto anaua familia nzima anachinja baba anabaka mama anaua ina maana mijangili kama hiyo haina huruma hata chembe adhabu yao ni moto tuuu, safi sana mapolisi kazi nzuri, kuhusu hayo malandrover ya zamani kubeba majeruhi au marehemu nilisema magari hayo huwa yanakuja na mapolisi eneo la tukio badala ya gari la wagonjwa, sasa hapo hukuelewa nini wewe? usiniletee vuvuzela lako halina mlio
ReplyDeletemdau
TIKRIT
NYIE MNAOTOA KOMENTI ZA KUWAHURUMIA MAJAMBAZI NANYI PIA NI MAJAMBAZI AU MNAFAIDIKA NA UJAMBAZI KWA NJIA MOJA AMA NYINGINE,, HIVI HAMJUI KUWA IMEANDIKWA JINO KWA JINO AU HAMJAWAHI VAMIWA NA HATA MWIZI TU AFU AKAKUTISHIA UPANGA!!! KAMA HAMJAJIARISHIA.. VILEVILE HAMUWAJUI MAJAMBAZI WA ARUSHA WANAUA RAIA KAMA KUKU,ETI MNAUULIZA HAKI ZA BINADAMU,NYOOOO
ReplyDeleteMI NAWAPONGEZA SANA POLISI TENA KAZI YAO NI VERY RISK,ENDELEENI HIVYO HIVYO HAKUNA HAJA YA KUJAZA MAJAMBAZI GEREZANI,WAULIENI MBALI,HAWANA HURUMA HAOO.. SAFI SANA MAAFANDE WANGU
halafu wewe unayetetea haki za binadamu NENDA KWENYE MSIBA WA MTU ALIYEULIWA NA JAMBAZI HALAFU WAAMBIE WAFIWA KUWA YULE JAMBAZI ANA HAKI ZA BINADAMU,AFU UONE KAMA HAUJAGEUKA KITOWEO.!!!!!!!
ReplyDeleteHAKI ZA BINADAMU!!???????
Ankal mi nina hasira na majambazi yaani natamani hata walioko mahabusu watolewe afu wapigwe risasi hadharani. majambazi hawana huruma jamni!!!!!!! wote wnaowatetea ni washirika wao,we fikiria pesa ilivyo ngumu bongo afu jitu linakuvamia linakuibia,linabaka afu linaua!!!!!!!bora polisi waendelee hivyo hivyo tuu
ReplyDeleteNAWAPONGEZA SANA POLISI,KAZI YENU NI NGUMU NA WAKATI MWINGINE INAHATARISHA MAISHA YENU PIA.BUT NAWAOMBEA KWA M. MUNGU AZIDI KUWAPIGANIA NA KUWALINDA ZAIDI ILI MUENDELEE KUTULINDA SISI RAIA WEMA WA NCHI HII.
ReplyDeleteAMEN
Wewe mdau wa Sat Jun 26, 07:40:00 AM, pole kusikia ulishavamiwa na majambazi na pole kusikia hawana cha msalia mtume japo bado hupo una hata mikono ya kuandika na macho ya kiona unachokiandika na hata ubongo japo kidogo wa kutafakari. Kwa ufupi ushukuru una uhai. Kati ya wote walioandika hapa hakuna anayewatetea majambazi na matendo yao, kinacholalamikiwa hapa ni kutohshimu maiti maana ukikuta mwili wa aliyekuwa mtenda mema umelala sambamba na mwili wa aliyekuwa jambazi na mtenda maovu uwezi tofautisha na miili hii itapewa heshima sawa bila kujali. Hiki ndicho kinatakiwa na wala si ombi kwa serikali bali ni haki za msingi. Vitani unapompiga risasi adui yako na kumuua, uendi kutemea mate maiti japo nia yake kabla hajafa ilikuwa ni kukuua. Unapokamata mateka wa kivita, unalazimika uwatendee haki japo nia yao ilikuwa ni kukuua wewe na wananchi/familia yako. Jambazi ni adui yako mkubwa pale akiwa na uhai na ameshikilia silaha lakini pia na wewe ni adui yake mkubwa ukiwa umeshikilia silaha au if you are holding onto a vital information such as where the money is n.k and hence costing him the valuable escaping time na mbaya zaidi akihisi umemjua. Kwa hiyo siri ya kuwapona majambazi ni "avoid being a hero as much as you possibly can" Kwa wenzetu wazungu ndo maana usikii sana story za majambazi kukata watu mapanga kwani wao awachelewi kutoa information ili waachiwe uzima wao. In the west ni jamii za watu from the third world background ndo tunaongeza namba za statistics, maana nakumbuka mimi binafsi nilivamiwa na majambazi wakijaribu kuninyanganya chain yangu, wanilinipa kipondo si mchezo japo hata mimi nilifight back only afterwards kukumbuka kwamba ilikuwa gold chain fake. Mpaka sasa some 8 years on bado nina makovu, kisa I wanted to be a hero and to a few silly ones including myself I was a hero.
ReplyDeleteUjumbe wa msingi hapa heshimuni miili ya marehemus.
MIMI NI MKAZI WA ARUSHA NA KUNA JAMAA AMBAYE NI MJASIRIAMALI AMBAYE AMEKATWA VIDOLE VYOTE NA PANGA NA MAJAMBAZI TO BE HONEST NINGETAMANI KWELI HUYO JAMAA ANGEKUWA MMOJA WA WALE MAJAMBAZI WALIOMVAMIA. UJAMBAZI UMEZIDI SANA ARUSHA NA WAKIUAWA NI POA SANA TU!!! MIMI KWA KITENDO WALICHOKIFANYA HAWASTAHILI HESHIMA. HESHIMA YA NINI SASA NA UMESHAAMBIWA WALIKUWA WANARUSHIANA RISASI NA MAPOLISI SASA UNATAKA MAPOLISI NDO WANGEUAWA...? FUCK THEM ALL CRIMALS...NA NYIE MLIOKO ULAYA MNAOJIDAI MNAJUA HAKI ZA BINADAM RUDINI NYUMBANI MUONE CHA MOTO..FUCK YOU TOO!! NIMEKASIRIKA SANA
ReplyDeleteJamani maiti inatakiwa iheshimiwe sio kuibeba kama mzoga wa nguruwe. Utu gani huu hata kama ni jambazi utu wake unatakiwa uheshimiwe. Wizara ya mambo ya ndani bila shaka mmeona vijana wenu wanavyokosa Utu sasa wapelekeni darasani wakajifunze haki za binadamu.
ReplyDeletemmh yaani nyinyi mnawaonea huruma majambazi nahisi siyo wazima na! labda siku moja wakiingia makwenu ndiyo mtajua jambazi ni mtu gani, mimi naona bora tuweke sheria za kiarabu za kukatwa mikono, kuibiwa kunauma sana asikwambie mtu.
ReplyDeleteAnkal mimi niko hapa arusha. ni wiki hii hii tumemzika kijana mmoja aliyepigwa risasi dukani kwake karibu na msikiti wa ijumaa ambaye ameacha watoto wanne, wa mwisho akiwa na miezi sita tu. pia majambazi hayo yalimuua mama mmoja mpita njia. Je hao wanaouliwa na majambazi hawana haki? Pili, hilo tukio la unga limited ambako majambazi hayo mawili yaliuawa na polisi jasiri lilitokea hadharani mchana kweupe! kila aliyeona tukio hilo ametoa ushuhuda kuwa majambazi hayo ndiyo yaliyoanza kutupa risasi. sasa mlitaka polisi wafanye nini? well done to the police this time around. wewe unayesema kuwa 'everyone is innocent until proven guilty' ni sawa. lakini kama wewe ni jambazi na mimi ni polisi ukianza kunirushia risasi, i promise you i'll riddle your f****** body with bullets. Nyinyi majambazi wote na ma-sympathisers wa majambazi mnaotoa maoni yenu hapa, kwanza heshimuni sheria, maisha na uhai wa watu wengine mkitaka sheria na watu wengine raia wema wawaheshimu na waheshimu haki zenu. Sawa? Ukisoma historia ya ulaya na marekani utaona ilikuwa ni ya ukatili na umwagaji damu lakini nchi hizo za USA na zile za Europe zimeweza kuendelea BAADA YA RAIA WEMA KUWASHINDA MAJAMBAZI NA KUWAFANYA MAJAMBAZI WAWAOGOPE RAIA WEMA NA SIYO THE OTHER WAY ROUND. Mimi kama nina silaha nyumbani, nikiingiliwa nyumbani na majambazi yenye silaha ambo yanataka kuidhuru familia yangu sitasita hata sekunde moja kuitumia silaha hiyo ili kuwapa majambazi hayo "a one-way ticket to hell!" Katika sheria ya nchi zote, "self-defence is justified". (said the late Lord Denning, one of the 20th century greatest legal luminary who helped shape not only UK's legal system but the law in most Eu countries kutokana na kutilia mkazo due process na kuanisha limitations zake). Kwa kifupi nyinyi majambazi na wapambe wenu hapa juu mnaomboleza vifo vya hayo majambazi, karibuni A-town, tunawasubiri kuwapa mnachostahili kama mtaamua kuishi kwa upanga!
ReplyDeleteNimesoma maoni ya wadau na kuyatafakali sana. Nimegundua kuwa wengi wa wachangiaji kwenye hii mada, ama wako nje ya nchi au hawaelewi kinachoendelea nchini. Kwa kifupi, POLICE kama walinzi wa amani, wanajitahidi sana kuweza amani kwa kila mtu na mahala popote. Lakini mambo mengi sana yanakwamisha utendaji wa kazi zao mpaka baada ya tunawaona kama hawafanyi kazi. Moja ya vikwazo hivyo ni uwezo wa kifedha pia na utaratibu wa kisheria hapa nchini. Utakuta wengi wa hawa vijana (majambazi) wana mtandao wenye watu wa pesa kubwa. Ukimkamata leo, kesho unaweza pishana naye mitaani akiwa huru na kejeli kibao. lakini mbaya zaidi ni kwamba watu hawa ukiwapeleka mahakani, kesi inaweza chukua miaka minne au zaidi, ili kuwakatisha tamaa police na walihusika na huo ujambazi. Mwishowe mtuhumi anaachiwa huru. Sasa basi, kwa issue kama hii ya Arusha inawezekana kabisa POLICE walikuwa wanajua njama zote in advance na inawezekana kabisa police walisha-interact sana na hawa jamaa. Ili kumaliza udhia na kuweka heshima, njia rahisi ni kuwa-eliminate kabisa. Tunatambua kuwa kila mtu ana haki ya kutambuliwa ubinadamu wake na utu wake, lakini wewe mwenyewe usipoutambua utu wako, unadhani nani atayekujali?! Hawa walikuwa ready kuua. Kama wangekuwa ready kukamatwa wasingepiga risasi juu. Walikuwa wanamtishia nani? Na je police wangeingia kichwa kichwa si nao wangeuwawa?! Mimi nadhani tukemee mfumo mzima wa kisheria wa nchi yote. Pia tukemee wale wanaopenda kuvuna wasichopanda tena kwa gharama ya damu za wenzao. Watu wengi sana wamejeruhiwa au hata kuuwawa kabisa ati kwa sababu walikuwa wanatetea mali zao zisiibiwe na majambazi. Je, hao majambazi kuna haja ya kulia lia na kudai kuwa wanastahili haki duniani?
ReplyDeleteKumbuka pia, wasemaji wakubwa wa haki za binadamu Duniani ndiyo hao hao waliomnyonga SADDAM HUSSEIN live kule Baghdad. Kati yenu nyie sikumsikia hata mmoja akilaani na kukemea watu hawa!
PICHA YA HAPO JUU INAONYESHA JINSI VYOMBA VYA DOLA VISIVYOJALI HAKI ZA BINADAMU. INAPOTOKEA MAJIBIZANO YA RISASI NA WAHALIFU NI KAWAIDA BAADHI KUPOTEZA MAISHA NA HAPO SI 100 NI WAHALIFU MPAKA SHERIA IFUATE MKONDO.
ReplyDeleteNIKIACHA HILO ,LA KUSIKITISHA NA KUTISHA JINSI POLISI WALIVYOCHUKUA MWILI WA ALIYEUAWA KUINGIZWA GARINI NI AIBU TUPU. HAKI ZA BINADAMU NI SIFURI. KAMA SERIKALI HAINA PESA WATUOMBE TUCHANGIE KUNUNUA MACHELA YA KUCHUKULIA MAITI BADALA YA HALI KAMA ILIVYO INAVYOTIA AIBU TUPU.
SIJUI LINI TUTAELIMNIKA, MAANA SUALA KAMA HILO SI SHAURI YA DARASA, KWANI NI INFORMAL EDUCATION, AU COMMONSENSE TU INAHITAJIKA HAPA.
LABDA TUNAHITAJI KUFUNGA SAFARI KWENDA KUTEMBELEA NCHI MBALIMBALI KAMA WAKUU WETU KUJIFUNZA HILO JUU YA HAKI ZA BINADAMU KITU AMBACHO HAKITALETA MABADILIKO. KWANI MANABII TUNAO ILA TU HATUWASIKII KWA MAANA HIYO HATA AKIFUFUKA MFU HATUTAMSIKIA KAMA MISAHAFU ISEMAVYO.
sio kama nasi ni majambazi la hasha. acheni roho mbaya nyie hata kama jambazi ndo umninginizie hivyoooo? acheni roho mbaya tunajua majambazi ni adui ya jamii yetu kuturudisha kila siku lakini kuna haki yake kama binaaadam basi ingekuwa hivyo tusinge wazika tuwatupe majalalani yaani nyie wote mnao furahia hiyo picha kwa kuninginizwa huyo kijana. mnamatatizo ya kufikiria. ingekuwa ndugu yako ungefurahia??? aninginizwe au ndo nyie mapolisi mlio ninginiza mnatetea hoja zenu?? honeypie
ReplyDeleteyani hapa ndo tunaona kabisa sisi watanzania jinsi gani akili zenu zile ndefu na walio na akili fupi. yaani eti mnafurahia na kushabikia mtu kuninginizwa eti kisa jambazi?? hastahili kuonewa huruma wala kusitiriwa kisa anaua na kuvamia na kubaka ???? mtu ameshakufa msitiri haijalishi huyu ni jambazi au nani yaani nyie wote mnao shabikia udhalilishaji wa maiti hiyo kuninginizwa bongo zenu zina mushkeli
ReplyDeletetena mnamatatizo jaribuni kukua kiakili
japo mna miiili mikubwa
honeypie
Laiti kama hayo majambazi yasingelianza kufyatua risasi bado yangelikuwa hai. Chaguo letu ni simple: Ama raia wema tuwashinde washenzi majambazi au wao watutawale kwa hofu katika nyoyo zetu kama ilivyokuwa Kenya. Sam.
ReplyDelete