Mkuu wa taasisi ya NANDO'S ya marekani Bw. Kingsley Holgate akiwa na mbunge wa jimbo la moshi mjini Philemoni Ndesamburo baada ya kumkabidhi vyandarua 500 kwa ajili ya hospitali, zahanati na vituo vya afya katika manispaa hiyo.
Mkuu wa taasisi ya NONDO'S ya marekani Bw. Kingsley Holgate akimkabidhi Mbunge wa jimbo la moshi mjini Mh. Philemoni Ndesamburo vyandarua 500 kwa ajili ya hospitali,zahanati na vituo vya afya katika manipaa hiyo. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.
TAASISI isiyo ya kiserikali ya NANDO’S ya nchini Marekani imemkabidhi mbunge wa jimbo la Moshi mjini Mh. Philemon Ndesamburo msaada wa vyandarua 500 vitakavyotolewa kwa hospitali,zahanati na vituo vya afya katika manispaa hiyo.

Msaada huo unafutia ombi la alilowasilishia Mh. Ndesamburo kupitia ofisi yake iliyopo Afrika kusini kwa taasisi hiyo inayoendesha mapambano dhidi ya malaria duniani ambayo iliahidi kusaidia.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mkuu wa taasisi hiyo Kingsley Holgate alisema hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kudhibiti ugonjwa wa malaria unaozikumba nchi mbali mbali barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Vyandarua hivyo 500 vimekabidhiwa na mkuu wa taasisi hiyo, Bw. Kingsley Holgate, ambapo unakuwa sehemu ya msaada ulitolewa katika nchi 13 za Afrika, zilizotembelewa na taasisi hiyo.

Kwa upande wake mh Ndesamburo, mbali na shukurani alisema utagawanywa katika hospitali hizo pamoja na zile zinazomilikiwa na taasisi za dini, ili kusaidia mpango mzima wa kukabiliana na tatizo sugu la ugonjwa wa malaria.

Ugonjwa wa malaria unaongoza kwa kuangamiza mamilioni ya watu ulimwenguni, ambapo jitihada mbali mbali zimekuwa zikifanywa kuutokomeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2010

    He! huyu ni santa claus ametuletea zawadi kabla ya krismas. Tunashukuru sana.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2010

    Hivi ni kweli hatuwezi hata kutengeneza vyandarua na mpaka tupewe misaada ya vyandarua? Kwanini tusibadilishe kiwanda kimoja tuu cha pombe na kukifanya kitengeneze cha/kiandarua? baadhi yetu tunaona aibu kwamba vyandarua pia lazima viwe vya misaada.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2010

    YALEEE YALEEEEEE YA MUSA

    MIDEVU KAMA HIYO AKIWEKA MUISLAM BASI ATAAMBIWA AL QAIDA

    HAPO WAOSHA VINYWA MTASEMAJE?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2010

    kwa niaba ya watanzania tunashukuru kwa huo msaada lakini hicho kichaka cha ndevu daah kinatisha. ndio hapo wazungu wanaponifurahishaga wahanaga complications

    ReplyDelete
  5. TototunduJune 09, 2010

    Huyu father christmas ndio nini kugawa zawadi mwezi wa 6?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2010

    LOl....thats a huge mustachee

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2010

    jamani tukiachana na mustch wake,ana wazo zuri la kupambana na maralia na ndio maana ameziangalia zaidi hospitali na zahanati,kule watu wanateseka sana.lakini inabidi tujisikie aibu kupewa msaada wa vyandarua,kuna kipindi raisi wa marekani alikuja na kutembelea kiwanda kule arusha,kwani kiwanda tunacho kimoja tu?..hizo jitihada za serikali za kupambana na maralia kwa nini viwanda visiwepo vya kutosha,yaani kila kitu msaada,tanzania tunakosa viongozi wanaoijua na kuiweza management.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2010

    Duh! Wadau mmeniwahi! I wanted to say just that! Kuwa, Christmas CAME EARLY this year! Maana huyo Nando's ni Santa Claus tosha! Petit Papa Noël (Father Christmas)haswaa.

    Tunashukuru kwa vyandarua.

    Merry Christmas Everybody!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 10, 2010

    DOH SILI TENA NANDOS-MADEVU MACHAFU KISHENZI HALAFU HATA HAOGI KISHA ANATULISHA KUKU NDIO MAANA WANAKUA WATAMU WATAMU SIO

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 10, 2010

    JAMANI JAMANI WATANZANIA TUAMKE!!!!

    HAWA WANGEKUWA NA NIA NZURI YA KUONDOA MALERIA SI WANGEMWANGIA DAWA MADIBWI YOTE KUUA MZALIWA YA MBU.

    WE UNAPEWA VYANDARUA VYENYE DAWA YA KUKAA MIAKA MITANO, MBUA AKIGUSA TU ANAKUFA..HIZI CHEMICAL ZINAUKALI KIASI GANI ?? HEBU TUFIKILI. MTU ANYAYELALIA HIYO NET NAKUVUTA HEWA KILA SIKU ANAATHILIKA KIASI GANI ??? NANI ANAJUA HIZO CHEMICALS ZINA NINI???
    MTOTO ATAKAYEZALIWA NA MAMA ANYETUMIA HIZ NET ANATHILIKA KIASI GANI ??

    JAMANI, HAKUNA MSAADA UNOTOLEWA BILA KUMAANISHA, HAWA WAZUNGU SIWA KUAMINI KIASI HIZO JAMANI !! WANALAO JAMBO KATIKA KIZAZI CHETU.

    USA KWENYE WALIFANYA KAMPENI YA KUUA MAZALIA YA MBU, NDO MBU WAKAISHA SIO KUTUMIA VYANDALIA VYA DAWA KAMA WANAVYO TUDANGANYA !!

    NAAMINI MABILION YA BUSH ANGEYAPELEKA KUUA MAZALIA YA MBU YANGETUSAIDI SANA, SIO KUNUNUA VYANDARUA VINVYOISHA NA KUTUACHIA MADHALA, NA VIKIISHA JE WATUTUPA TENA?? HAPA KUNA KITU WATANZANIA TUAMKEEEEEE !!!


    INANIUMA SANA,

    MTANZANIA HALISI

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 10, 2010

    merry christmas ho ho ho wadau wote

    kutokua na viongozi wenye kujali matumbo yao ndo ivi!!ilhali tunaweza kuua mazalia ya mbu kutokomeza malaria Tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...