Hi Mkuu,
Kwanza kabisa natanguliza salamu zangu kwa wingi sana.
Pili napenda kuwasimlia jambo wadau na kuwauliza swali nisikie wanasemaje, ni hivi;
Rafiki yangu wa karibu sana wa hapa mji wa jirani, Isabella aliniomba kuwafundisha wanafunzi wimbo wa kiswahili, maana yeye Isabella ni mwalimu wa shule ya msingi.
Kwanza kabisa natanguliza salamu zangu kwa wingi sana.
Pili napenda kuwasimlia jambo wadau na kuwauliza swali nisikie wanasemaje, ni hivi;
Rafiki yangu wa karibu sana wa hapa mji wa jirani, Isabella aliniomba kuwafundisha wanafunzi wimbo wa kiswahili, maana yeye Isabella ni mwalimu wa shule ya msingi.
Yeye Isabella anapenda sana lugha ya kiswahili, maneno mawili mtatu nimemfundisha anayajua sana, hivyo basi aliomba niwafundishe wanafunzi wake ambao wamemaliza shule ya msingi darasa la tano, ili kwenye sherehe yao ya kuwaaga waje waimbe wimbo huo wa kiswahili.
Sasa tupo karibu na kumaliza mafunzo hayo, juzi tukapata nafasi kidogo ya kupumzika, wakati tukiwa kwenye mapumziko hayo, mwalimu Isabella akaniomba niweze kuongea na wanafunzi hao mambo mbalimbali ya Tanzania na Afrika kwa ujumla, story zikaanza kama kawaida, mara ukafika wakazi wa kuulizwa maswali, hapo ndipo kichekesho kinakuja na kukosa nguvu kabisaaa!!!, maana mara za kwanza kwanza nilipofika nchini hapa nilikuwa nakasirika sana na maswali ya hawa jamaa kwa ujumla, kama vile kwenu kuna vitanda vya kulalia, au kuna boga za majani???....na bla bla bla nyingiiiii.....!!!!
Lakini baada ya kuzoea na kuona kila mara Televisheni zao zinaonyesha mbuga za wanyama tu! na sehemu mbaya tu zenye maisha magumu tu! Ndipo niligundua si tatizo lao, ni kutokujua hasa kwa wale ambao hawajasafiri kabisa, hata kutoka nje tu ya mji yao ni vigumu sana kuelewa kama na sisi waafrika tuna mambo mazuri, tena mazuri kushinda wao.
Sasa mwanafunzi mmoja aliniuliza swali ambalo, ilibidi kucheka tu....hata wenzake ilikuwa ni vicheko mpaka basi, mimi mwenyewe sikutegemea kabisa swali kama hili, aliniuliza hivi;
Nilimwuliza swali Babu yangu kuhusu Afrika, kwanini Afrika ni maskini, hasa watoto wanahangaika sana?
Sasa mwanafunzi mmoja aliniuliza swali ambalo, ilibidi kucheka tu....hata wenzake ilikuwa ni vicheko mpaka basi, mimi mwenyewe sikutegemea kabisa swali kama hili, aliniuliza hivi;
Nilimwuliza swali Babu yangu kuhusu Afrika, kwanini Afrika ni maskini, hasa watoto wanahangaika sana?
Babu alinijibu; Waafrika maskini kwasababu hawapendi kufanya kazi, wanapenda raha tu! Hukaa chini ya miti ya minazi, wakisubiri nazi zidondoke ili waokote.
Eti ni kweli jambo hili???
Mimi nilishindwa kujibu....
pia aibu kwangu,
hata kwa mwalimu na wanafunzi wenzake.
Sasa wadau, je nyinyi mngelijibu vipi swali hili???
Sasa wadau, je nyinyi mngelijibu vipi swali hili???
Mdau Baraka wa Chibiriti
Cesena, Italy


WEYE CHIBIRITI VIPI TENA?YAANI UNASHINDWA KUJIBU HILO SWALI HADI ULILETE HAPA?ANYWAY THAT'S A LITTLE KID AND SHE/HE DID ASK THE QN COZ THE GRANDFATHER HAD TOLD HER/HIM SO AND HAD BELIEVED THAT,BUT YOU HAD A CHANCE TO PROVE TO HER/HIM THAT WHOEVER TOLD HER THAT WAS WRONG BUT COZ YOU COULD NOT THEN THE LITTLE KID AND ALL THOSE PRESENT IN THE CLASSROOM WILL BELIEVE WHAT THE CHILD HAD SAID IS TRUE.I LIVE IN A FOREIGN COUNTRY AND THESE QNS COMES ALL THE TIME BUT ITS UP TO US TO EDUCATE THESE PEOPLE BY TELLING THEM THE TRUTH AS WE ALL KNOW THAT THE INTERNATIONAL MEDIA ONLY SHOW BAD STAFFS ABOUT AFRICA THEY NEVER SHOW GOOD THINGS AND THEY DO THAT FOR A REASON.MR CHIBILITI,NEXT TIME YOU DONT LET ALL THE TZNS LOOK DUMB,YOU COULD HAVE SAID SOMETHING,THOSE KIDS AND ALL THE FOREIGN COUNTRIES HAVE BEEN BRAIN WASHED ABOUT AFRICA TO BELIEVE THAT IN AFRICA IS REALLY PITTY SO GO BACK TO THOSE KIDS AND SAY SOMETHING,YOU GREW UP IN TANZANIA AND SO YOU KNOW THE FACTS,YOU INDEED KNOW THAT PEOPLE DONT SIT UNDER THE COCONUT TREE TO WAIT FOR COCONUT TO FALL OFF,COMON CHIBILITI ARE YOU KIDING ME?
ReplyDeleteMDAU,CA-USA
hivi chibiriti mbona mambo yako kama ya ki paulo kamau?
ReplyDeleteCHIBILITI EVEN HOWEVER YOU WERE NOT EDUCATED BUT YOU SHALL ANSWER ALL QUESTIONS ACCORDINGLY WITHOUT HESITATED ANYTHING YOU SHOWS YOUR WEAKNESSES ANY TIME YOU HAS ANSWERED THE CHILDRENS OF FORM FIVE THE QUESTIONS IS ASKED BY THEM. IF YOU DOES NOT KNOW WHY HOW COMES YOU WENT THERE TO ANSWER THE QUESTIONS. YOU CAME HERE TO MICHUZI TO ASKED US TO HELPED YOU SMALL THINGS. YOU LOOKED JUST UN EDUCATED LIKE THEMSELF. GO TO SCHOOL AND CAME UP BACK TO ANSWER SIMPLIFY QUESTION OF CHILDRENS OF ITALY FORM 5 KIDS. I AM SO SORRY CHIBILITI YOU ASTONISHED ME AT ALL.
ReplyDeletehuyo babu yake naye hazimtoshi, hayo maswali yasiyo na kichwa wala miguu ni karibia dunia nzima nje ya africa, hapa kuna mwenzangu mmoja alifurahi sana kupata nafasi ya kuongea na mwafrika, akauliza kama huku kuna benki, cha ajabu aliniuliza hivi nyie huwa mnakula, na mkila mnakula nini.huyu sio mtoto, ni kijana amemaliza chuo kikuu.ni vizuri kurekebisha yale wanayoyaamini sisi tukiwa wajumbe kama wale wa kusadikika,tuwaweke sawa.
ReplyDeleteIkiwa Misri wanaweza kupanda viazi mbatata (mviringo) ktk ardhi ya jangwa iliyojaa mawe, kwa nini nchi kama Tanzania, Uganda, Kenya wanakufa kwa njaa huku wana ardhi iliyo na rutuba, mvua kibao, Maziwa Victoria, Tanganyika n.k!
ReplyDeleteJibu rahisi ni kuwa Watu wa Afrika ya Mashariki ni 'wavivu wa kufikiria'
Mdau
Alexandria.
DAMN PETER LITO....WHATEVER THE NAME IS,YOUR ENGLISH IS SO SLUGGISH AND MAKES ME SICK TO MY STOMACH.IF YOU DAMN KNOW THAT YOU CAN NOT EXPRESS YOURSELF CONFIDENTLY IN ENGLISH THEN WHY WOULD YOU OPT TO,YOU MAKE PEOPLE FEEL DIZZY WHEN READING THAT BROKEN ENGLISH,SHAME ON YOU
ReplyDeleteHuyo mtoto hana kosa kwa vile kila kinachoonyeshwa huku ni watu masikini, watoto wana njaa, na watu awanaomba omba tu njiani. na pia kila anayekuja huku ni kuja kuomba na akija anakuja na zile picha na nguo mbaya ili wamwonee huruma...Who are we going to blame here? Twasira tuipeleke wenyewe halafu leo tulalamike.
ReplyDeleteMimimwanafunzi mkubwa chuo kikuu aliniuliza kama kwetu tuna nyumba za kawaida watu kuishi kwa vile alisikia ni jugle people tunaishi kwenye mashimo...Mtu mzima na amesoma huyo..kesho atawaambia nini watoto wake?
Ungewaambia watoto wako maskini kwa vile hatubelieve on birth control na mpaka sas hivi tunaamini kuwa the more babues you have the richer you are hata kama huna hela ya kuwatunza...Serious...tukae chini tujiulize ni kwanini watu wanakua wanazaa tu bila ya kujua watatunzaje hao watoto wao???mimi namsupport huyo mtoto kwa swali lake na nahitaji jibu....
jibu ni rahisi sana mwambie barabara za tanzania ni nyembamba badala ya kuzitanua kwanza, wao wameweka sheria ya marufuku magari kutanua. sio wavivu, wanafanyakazi ila kinyumenyume na kwa roho mbaya
ReplyDeleteJamani tuwe wakweli na tusiwe wavivu wa kufikiri katika masuala muhimu yanayohusu mustakabali wetu kama waafrika na hasa kama watanzania. mtoto kawasilisha mawazo ya babu yake vizuri. Hivi nani anabisha leo kuwa watanzania wengi ni wavivu wa kufanyakazi na kufikiri pia? nani hajui kama viongozi wetu wanaugonjwa huo pia? mimi kwa mtazamo wangu babu naposema waafrika wanasubiri nazi zianguke waokote hakuwa na maana ya nazi hizi tunazopata tui jamani. Ana maana tunasubiri misaada hata ya nguo za ndani zilizotumika zinazouzwa kwetu kama mitumba. Hatuwezi kujenga njia ya treni iendayo kasi Dar hadi tupate msaada wa wafadhili. Rejea bajeti ya mwaka huu, baadaya ya wafadhili kugoma kusaidia bajeti kutokana na wizi wa fedha zao, nchi imehaha kupunguza majeti. Hamuoni kuwa huo ni ugonjwa unaohitaji tuwekwe sisi sote kwenye chumba cha wagonjwa mahututi au vichaa sorry, wagonjwa wa kufikiri tuwekwe mirembe? Inauma sana jamani. miaka 48ya uhuru lakini uhuru wa kutembea mitaani bila kucharazwa viboko na wakoloni, lakini uhuru wa kufikiri hatuna ndugu zangu. Mtoto yuko sahihi, wengi wetu ni wavivu, na tunahitaji wakoloni wa kijerumani waje kututawala tena watushikishe adabu. NI WAVIVU KWA KWELI.
ReplyDeletejibu lake kweli 90% hasa ya vijana wa tz mpaka leo wanakaa chini ya minazi aka maskani kusubiri nazi zianguke nazi zenyewe mtu apite wapige mizinga, jibu lake kweli
ReplyDeleteHahaha Cgibi wa Chibiriti mbona JIBU HAPO LILIKUWA NI RAHISI UNGEMWAMBIA HUYO DOGO KUWA WA AFRICA SIO WAVIVU HAWAJAKAA PALE CHINI YA MTI KUSUBIRI NAZI IANGUKE BALI WANASUBIRI BABU ZAKO WARUDISHE MALI WALIZOCHUKUWA LONGTIME MAANA WALISEMA WATARUDISHA HAHAAHAHAAA LOL! KAAAZI KWELI 2,
ReplyDeleteKUNA MTU ALIKWENDA KUSOMA HUKO ULAYA ENZI HIZO, SASA HAWA JAMAA TENA NI MWANACHUO MWENZIE (UNIVERSITY) AKAMUULIZA KWENU AFRICA NASIKIA MNAISHI KWENYE MITI? YULE JAMAA AKAMJIBU NDIO HALAFU KUNA MTII MKUUUUBWA NDIO BALOZI WENU ANAISHI HAPO JAMAA (MZUNGU)AKASTUKA HAIWEZEKANI M'AFRIKA AKAMUULIZA HAIWEZEKANI VIPI SASA WAKATI AFRIKA YOOTE HAKUNA NYUMBA TUNAISHI KWENYE MITI YEYE NYUMBA ATAPATA WAPI, MZUNGU IKABIDI AFANYE UTAFITI MWENYEWE NA KUGUNDUA HALA HALISI ILIVYO NA MPAKA HIVI ANAISHI AFRICA. SASA CHIBIRITI HUYO MTOTO MUELEZE UKWELI WA UMASIKINI WETU HIIHIHIIIIII IT'S FUNNY HAH! -
kufakunoga
Jibu lilipaswa kuwa ndio ni kweli hata balozi wao nae analala kibandani, na pia huwa tunagombea nae nazi pindi zidondokapo
ReplyDeleteUngemtemea kohozi huyo mtoto we chiribiti.
ReplyDeletePole kaka, kwa kweli hilo swali gumu tena ni ghafla,na kwa Ulaya kumdanganya mtoto ni kosa, kwahiyo nadhani ulipata kigugumizi cha ghafla ikabidi uanze kucheka tu, kuonyesha ugumu wa shwali kila mtu aliyechangia hapa hamna aliyetoa jibu kwa fasaha, pia hili swali halina jibu la fasaha, kila jibu linaweza kuwa sawa au si sawa ila ni jinsi wewe utakavyojibu.
ReplyDeleteMimi nadhani swali hili linahitaji jibu refu kidoga ambalo linahitaji mchanganuo wa kijamii, kisiasa na kiuchumi. Jibu linatakiwa kuanza na kutafsiri swali kama alivyofanya mchangiaji hapo juu, maana ya kusubiri nazi ni 'misaada'. Kwanini kwa sababu viongozi wetu siyo waaminifu katika kutekeleza sera zao na niwafujajaji wa mali. Hali hii inafanya kurudisha nyuma maendeleo, maana kwa mfano kama mkulima hawezi kuuza mazao kwa bei mzuri, hii inamanisha mwaka mwingine hataweza kulima kabisa, na hali hii inachangiwa pia na masoka ya kimataifa yakiwemo ya huko ulaya ambayo hali ya mkulima ni bora kuliko afrika, kwa mfano wao wanatoa subsidies kwa wakulima wao, hivyo mazao ya Afrika hayana ubora na kama yanaubora ni ghali kuliko hayo ya Ulaya. kwa upande mwingine utawala bora unasababisha vita kwenye nchi nyingine, hivyo watu hawawezi kufanya shughuli zao za kiuchumi kama inavyopaswa, mwishowe wanakuwa maskini.Ndiyo maana babu kasema wanakaa chini ya mnazi kusbiri zidondoke. Ila unawezaongeza kwa kusema watu wa afrika wanafanya kazi sana kushinda hata Ulaya maana muda wanaotumia kufanya kazi kwa zana hafifu ni mwingi, kama watawezeshwa basi wanaweza kufanya maajabu, ila serikali zinaongozwa na walafi ambao ndiyo hao babu yako kanamanisha waafrika wanapenda raha, ila hawa watu ni wachache tena ni viongozi wa siasa tu. Mapinduzi yanaendelea na itafika siku Afrika itakuwa kama hapa, maana hata Ulaya ilipitia hali hii kabla ya kufika hapo ambapo hao watoto wamezaliwa na kukuta kila kitu kipo, waambie sisi ndo tupo kwenye mchakato wa kujenga Afrika ili baadae watu wasikae tena chini yaminazi.
Nadhani ukijaribu kumjibu kwa aina hii wanaweza juwa kuwa maendeleo ni process na kuwa Afrika inaendelea, ingawa wao Ulaya wametupita kwa kila kitu. Waambie wakija Afrika watashangaa. Pia usione aibu kuwakumbusha ukoloni, maana wakati wa ukoloni sisi waafrika tulikuwa tunafanya kazi zao na wao walikuwa wanajenga nchi zao. Na wajuwe kuwa Ulaya imeaanza kushamili tangu karne ya 15, ni miaka miasita sasa , wakati Afrika inamiaka 50 tu tangu kupata uhuru. Waambie kipindi cha ukoloni walibomoa misingi yetu yote ya maaendeleo na kuingiza mtindo wao wa maendelea. Kwa sasa inakuwa ngumu maana maendeleo yanatafsiriwa kuwa na kitu cha kutoka Ulaya. Hilo ndo tatizo linalowafanya watu wakae chini ya minazi. I did this and worked alot, influenced many white friends to have interest in Africa and see or help.
Chitu
Asanteni sana wadau kwa michango yenu mizuri ya kulijibu swali hili, ambalo kwangu kwakweli lilikuwa gumu na lakushitukiza. Kweli kama walivyosema mdau, hata mimi nakubalana kwamba Babu ya huyo mtoto alikuwa akimaanisha sana ,misaada kwa ujumla. Mimi binafsi sikuweza kumjibu palepale huyo mtoto, maana darasa zima liliagusha kicheko tuuu...hata mimi nikabaki nacheka tu! Lakini hali halisi ndo hiyo, maana hata Mwalimu Nyerere alikuwa akiongea sana kuhusu swala la Afrika kuwa tuna mawazo tegemezi sana, mjomba akipata uwezo basi ndugu wote wanataka wakakae kwake hata bila yakufanya kazi, na watu wana uwezo wa kufanya kazi kabisa...lakini basi mimi sisemi mengi zaidi, ila nawashukuru sana kwa kunipa mwanga mzuri wa kujibu hili swali; na mimi kesho tu nitamjibu kweli swali lake. Asanteni sana!
ReplyDeleteBaraka wa Chibiriti.