Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh. Margaret Sitta pamoja na watu wengine tisa amekamatwa na kikosi cha kuzuia na kupambana na rushwa nchini Tanzania, TAKUKURU, huko mkoani Tabora baada ya upekuzi wa mikoba ndani ya gari lake kukutwa na zaidi ya shilingi milioni moja za Kitanzania, bahasha za khakhi zaidi ya mia moja, simu saba aina ya NOKIA na vitu vingine.
Inasadikika vitu hivyo vingepewa baadhi ya wajumbe ambao wangepiga kura katika uchaguzi wa wagombea Ubunge viti maalumu uliofanyika mkoani humo leo.
Inasadikika vitu hivyo vingepewa baadhi ya wajumbe ambao wangepiga kura katika uchaguzi wa wagombea Ubunge viti maalumu uliofanyika mkoani humo leo.
Mbona mi sielewi jamani uchaguzi si ni October?, au viti maalum huwa vipo bila kutegemea idadi ya watakaoshinda uchaguzi mkuu?, kama ni hivyo basi October ni upuuzi mtupu huu wa sasa ndiyo uchaguzi mkuu fulstoop
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteHivi ccm walivyoshikia bango hili suala la gharama za uchaguzi hawakuwa wakifahamu kuwa wao ndiyo wahusika wakuu?Mwaka huu wataumbuana kweli,haya sisi yetu macho tu.
ReplyDeleteMbona magazeti mengine yanaripoti kuwa takukuru haijamkamata mama Sitta per se akitoa hongo hiyo?
ReplyDeleteTakukuru, namna gani hii???!!! Aaah!
huyu ndiye kada michuzi bwana kaweka post chiniiii ili tusiione na kucomment
ReplyDeleteJamani, kwani kuwa na hela na bahasha kwenye gari ni kosa? Lakini wasije kuwa wanatupiga changa la macho kwa wale walio against mtandao na wanamtandao wakawa safe, hii ni kuchafuliana tu wala hakuna lolote, tunajua kuwa wote wanatoa rushwa in one way or anaother nani hatoi huko? wasitudanganye, watanzania sasa ujinga basi.
ReplyDeleteTAKUKURU mlijuaje kama mama sitta anakwenda kutoa rushwa? mlipiga ramli au mmetumwa na kambi nyingine kumharibia. Kuweni na subira mpaka mpate ushahidi wa kosa alilotenda mtuhumiwa ndio mumkamate na kumuanika katika vyombo vya habari, simu 7, shilingi milioni 1 na bahasha kadhaa za kakhi ni vitu vidogo sana. TAKUKURU msipoangalia mwaka huu mtalipa fidia kwa kumchafulia mtu sifa yake na kumvunjia hadhi.
ReplyDeleteJamani kufanya kampeni si kunaitaji kutumia pesa! Sasa watu wanakusaidia kufanya kampeni watazunguka sehemu mbalimbali vipi wasipokuwa na fungu la usafiri? NA pasipo kuwa na simu kwaajili ya masiliano je watu waandikiane barua wakati wa kampeni. Hii Tukuruku sasa ina chuki binafsi na haki haitatendeka inavyoelekea hasa kwa wale wagombea targeted. Inabidi chombo hicho kifanye kazi kwa umakini sana la sivyo uchaguzi huu utakuwa sio wa haki na unaweza kuleta vurugu msipokuwa waangalifu.
ReplyDeleteMDAU USA
SASA HAO "TUKUNYEMA" WATUELEZE NA SISI TUNAOISHI NJE TUKIJA TANZANIA TUNARUHUSIWA BAHASHA NGAPI KWA KILA MTU NA HELA KIASI GANI?PIA SIMU NGAPI?KWANI TUSIJE TUKASUKUMIWA RUSHWA JAPOKUWA HATUTAKI UONGOZI NA UCHAGUZI UMEKWISHA HII KASHESHE YA TUKUTUKU IMENIKUMBUSHA ILE KESI YA JAMAA MMOJA ZENJ ALIYEKUWA LUPANGO MIAKA KUMI KWA KESI YA MAUAJI BAADA YA MIAKA MITANO KUTUMIKIA AKATOKEA WAKILI WA KIDOSI WA KUJITOLEA KUTOKA DAR,SIKU YA KESI MAHAKAMANI WAKILI AKAKUTA USHAHIDI ULIOKUWEPO NA ULIOMFUNGA YULE JAMAA ILIKUWA NI KISU NA MIKONO YAKE ILIKUWA NA DAMU NA JAMAA ALIYEULIWA ALIKUWA AMECHINJWA YULE WAKILI AKAWAULIZA WAENDESHA MASHTAKA MLIPIMA HIYO DAMU MKAHAKIKISHA KUWA ILIKUWA NI YA BINADAMU NA BLOOD GROUP NI YA HUYO MAREHEMU JAWABU IKAWA HAPANA.
ReplyDeleteWAKILI AKAMWAMBIA JAJI NAOMBA MAHAKAMA IMUOMBE RADHI MSHTAKIWA NA KUMUACHIA HURU MARA MOJA KWA KUWA SIKU HIYO ILIKUWA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA KOSA LAKE ALIAMUAMUA KUCHINJA KUKU ILI AFURAHI NA FAMILIA YAKE BAHATI MBAYA IKAMKUTA HII BALAA.
JAJI ALIRIDHIKA NA UTETEZI NA YULE JAMAA AKADUNDA,SASA MIMI SIJUI KAMA YULE JAMAA KAUA AU HAKUUWA LAKINI SHERIA NDIO HIYO KAZI KWAO HAO TUKUNYEMA AU TUKURURU.
MDAU.
TIBET.