
Angalizo: Soma ukiwa kwenye Foleni ndefu ya Magari,
na shiriki kwenye utatuzi wa tatizo hili.
na shiriki kwenye utatuzi wa tatizo hili.
Hoja ya Msongamano Mkubwa wa Magari
(Traffic Jam) jijini Dar-es-salaam
Kwanza Sheria ya Usalama barabarani, Sheria hii ni nzuri sana lakini nasita kusema kwamba utekelezaji wake sio makini. Unaweza kupata mshangao kidogo labda nianze na hili !
Kwanza Sheria ya Usalama barabarani, Sheria hii ni nzuri sana lakini nasita kusema kwamba utekelezaji wake sio makini. Unaweza kupata mshangao kidogo labda nianze na hili !
Sio Kila gari linalotembea Dar-es-salaam ni Gari, Sina takwimu sahihi za idadi ya magari dar, lakini wasiwasi wangu wa kwanza ni hali ya Magari yaliyo dar, labda tujiulize maswali yafuatayo
1) Ni mara ngapi umekutana na Gari limeharibika katikati ya Barabara, Ni magari mangapi hayana Insurance lakini yanatembea barabarani, ni Magari mangapi hayana Road licence na yanatembea barabarani, ni madereva wangapi hawana leseni na ni wangapi wanazo leseni za mitaani na wanaendesha magari kila siku dar na ni magari mangapi yamekaguliwa kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani Dar kuangalia hali ya Matairi, Honi, Taa, Engine nk.
Ukijiuliza maswali yote haya sina shaka unaweza kuona kama sheria ya usalama barabarani haifuatwi na walio wengi dar, lakini serikali kila kukicha inaendelea kuwalipa wafanyakazi ambao wana jukumu la msingi la kuhakikisha sheria hii inafuatwa.
Ni mara ngapi walio na makosa kama hayo niliyoonyesha hapo juu hukamatwa na polisi wetu na kutoa kitu kidogo na kuachiwa, kwa nini tusiige mfano wa nchi za wenzetu mfano mzuri tuu Rwanda ambao Polisi huwezi kumkuta anafanya mazungumzo na dereva, na wako strictly baada ya kumkamata aliyevunja sheria ya barabarani moja kwa moja hupelekwa kituoni na hatua kali huchukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kulipa faini kali inayowezesha kuboresha barabara.
Hatuoni kwamba tukiwa makini katika hili kila magari 2 kati 10 au pengine zaidi yatabaki nyumbani na hivyo lupunguza msongamano wa Magari ambayo sio Magari yanayotembea Dar?
Tuendelee na swala la Sheria ya Usalama barabarani na sasa ivi tuangalie pikipiki na Mikokoteni. ni mara ngapi tumekuta mikokoteni au pikipiki katikati ya mji zimepakia mizigo? Kwa jiji kama la Dar nadhani tunatakiwa kuwa na limitation ya aina ya chombo cha usafiri na eneo husika, sidhani kama tunahitaji kuliona gari la tani kadhaa city centre??
Sidhani kama tunahitaji kuwa na mikokoteni inayobeba ndizi na mikaa city centre au pikipiki zinazobeba kuku??
Ushauri wangu kwa Jiji na Manispaa ni vizuri tukachukua hatua za haraka sasa ivi na kuweza kuweka sheria ndogo za usimamizi wa Jiji na Manispaa yetu, nadhani haya yako kwenye uwezo wetu.
ICT Ambassador De Africa,
Sesil C. Latemba
sesil7c@yahoo.com
+255 713 335480
.....itaendelea kesho
Mdau hapo umechungulia umeona mbali ongera kwa hilo, ili tatizo lipo ndani ya uwezo wetu kama serikali imeona askari wetu wameshindwa kusimamia sheria zetu waunde kikosi maalum cha usamamiaji wa sheria za barabarani waende ktk nchi zinazofuata mfumo wa sheria na wapewe mafunzo ya kutosha kwa muda kama wa miezi 6 halafu waingie mtaani, kwa kuanzia hata kikosi cha watu kama 150 kinatosha. Dar itabadilika tatizo kubwa hivi sasa ni hizi hongo zinaanzia wizarani hadi kwa yule anayepewa lindo mtaani. MBONA INAWEZEKANA HATUHITAJI ASKARI WOTE WALE MTAANI.....
ReplyDeleteNdugu yenu MOLE...
TANDIKA
ahhh kaka hapo umeongea mimi niko uingereza, sasa umechukua fomu ya angalau ubunge? kwa sababu wewe unatufaa! nakubaliana na kila kitu ulichoongea, lakini yuko wapi wa kubadilisha? ndo maana mimi nimeamua kujichimbia nchi za watu, nafikiri tukiwa watano tu kama wewe na tukapewa nafasi jiji au nchi nzima itabadilika, asante.
ReplyDeleteNDUGU LATEMBA NINA WASIWASI NA UPEO WA ELIMU YAKO, KWA SABABU TULITEGEMEA UNGETOA SABABU ZA MSINGI NA ZENYE UPEO!! LEO UMEINGILIA KAZI ZA ASKARI WA USALAMA BARABARANI UNAONYESHA KUWA SI WAAMINIFU NA KAZI ZAO,NA PIA NI WALA RUSHWA!!HAWA NDUGU ZETU KAZI ZAO WANAZIFANYA KWA UMAKINI TENA WA HALI YA JUU, UKITAKA TAKWIMU TEMBELEA MAKAO MAKUU YAO UTAPEWA DATA ZOTE ZA KILA SIKU MAGARI MANGAPI YAMEKIUKA SHERIA NA WAMETOZWA KIASI GANI NK,TATIZO SS WANANCHI TUNAPENDA DEZO HATUJAPATA ELIMU YA KUTOSHA KUISAIDIA NCHI YETU TUNAPAENDA KUIIBIA KWANI USHURU HATULIPI IPASAVYO TUNAMRUBUNI AFISA AKUACHIE USILIPE KWA KUMPA KITU KIDOGO,UNAENDESHA GARI BILA LESENI UKIKAMATWA UNAHONGA ZAIDI YA BEI YA LESENI,KWA UJINGA WAKO,TUNAJIRUDISHA NYUMA WENYEWE LEO ASKARI WAKIKAKAA BARABARANI KUZIKAGUA GARI MOJA MOJA TUTAANZA KUPIGA KELELE TUNACHELEWESHWA KAZINI NK,AU UNAKWEPA UNAPITA VICHOCHORONI,UMEME UNAIIBIA TANESCO,MAJI UNAIBA, USHURU UNAKWEPA KULIPA HIVI UNATEGEMEA NINI?MAMBO ULIYOYAZUNGUMZA YT NDIO YALIYOPO SASA KUNATAFUTWA MIKAKATI MIPYA,MBADALA KUZIDISHA MAFANIKIO, MAANA SIKU HIZI HUKUTI MAGARI MITUMBA KAMA ZAMANI MAANA GARI ZAIDI YA MIAKA 10 UNATOZWA UCHAKAVU,MAGARI MAKUBWA HAYARUHUSIWI KUINGIA MJINI MCHANA HIYO IPO, VIBAJAJI HAVIRUHUSIWI MJINI KATI, VIPANYA MWISHO NJE YA MJI NK, UNGEELEZA MANTIKI WEWE UNAJARIBU KUTAKA KUJIONYESHA KUWA UPO NA TUMEKUONA, TATIZO FAMILIA MOJA INA MAGARI ZAIDI YA MOJA MIKAKATI MIPYA NI HIYO 1>FLYOVER,
ReplyDelete2>MAGARI MAKUBWA KUBEBA ABIRIA KUPUNGUZA VIPANYA3>NJIA ZA TRENI MAJINI NK,KUKIWA NA USAFIRI WA UHAKIKA KUINGIA NA KUTOKA MJINI WEWE MTU WA BOKO AU KIBAMBA AU MBAGALA GARI UNAIACHA UBUNGO,AU MWENGE UNAPANDA BASI KUBWA AU TRENI UNAINGIA MJINI KATI UKITOKA KAZINI UNAIKUTA GARI YAKO PALE UNARUDI KWAKO. LAKINI FLYOVER ITASAIDIA KUONDOA HII KERO.JIJI LA DAR NDIO MAENDELEO YA TZ NA NI KIUNGO CHA BIASHARA ZOTE NA BANDARI YA UHAKIKA PIA. DODOMA NI MAKAO MAKUU YA SERIKALI, DAR NI MAKAO MAKUU YA UZALISHAJI NA MAENDELEO.TZ YA LEO SI YA JANA TUMEANZA KUTEMBEA KWA KASI
Mbona unazidi kutoka nje ya mada.Kichwa cha habari "Hoja ya Msongamano Mkubwa wa Magari
ReplyDelete(Traffic Jam) jijini Dar-es-salaam" hakiendani na yale uliyoyaandika leo.Suala la vyombo husika kutafuta magari mabovu au yanayokiuka sheria za usalama barabarani na kuyaweka kando hakuwezi kuondoa foleni Dar es Salaam.Jiulize ,Kama hakuna magari mabovu au yaliyokiuka sheria za barabara inamaana magari yote yatakuwa barabarani na hata ukiyapata magari mabovu ni machache mno hakuna yadi ya magari inayouza magari mabovu.
Ndugu yangu unapoweka kichwa cha habari inabidi kiendane na kile unachokizungumzia na kujua hilo si lazima uwe mwandishi wa habari.
Tatizo la msongamano wa magari jijini Dar es Salaam linasababishwa na vitu vifuatavyo;
1.Ofisi nyingi za serikali na mashirika mbalimbali kujazana sehemu moja(katikati ya jiji) hii inasababisha wafanyakazi na wananchi kuelekea eneo moja during peak hours
2.Barabara za kuingia barabara kuu(feeder roads) nyingi ni mbovu kiasi wenye magari wanaogopa kupitisha magari yao huko wakiogopa kuyaharibu.
3.Kukosekana kwa barabara za lami zinazounganisha wilaya kupitia nje ya mji(mf.kutoka Kibamba au Mbezi hadi Gongo la Mboto bila kupitia Ubungo na Tazara au Mbagala hadi uwanja wa ndege bila kupita Tazara au Tegeta hadi Gongo la Mboto bila kupita Mwenge)
4.Kukosekana Traffic lights madhubuti barabarani.
5.Kukosekana kwa Satellites Town(miji midogo) ambako huduma zote ikiwemo mabenki,masoko n.k kuwa huko.Mf.Soko la kariakoo lisiwepo pale bali yaanzishwe masoko kama hilo katika maeneo ya kila Wilaya mf.Tegeta,Gongo la Mboto,Temeke
5.Kukosekana kwa usafiri madhubuti wa abiria.mf.badala ya kuwa na vipanya yawepo mabasi ya abiria 100.Kukosekana kwa usafiri wa treni za abiria jijini,kukosekana kwa usafiri wa boti.Mf toka feri hadi kunduchi
Ukiangalia sababu hizo unapata utatuzi(solution) wa kila moja.Ni yangu ni hayo tu yanayohusu tatizo la "Msongamano wa Magari Jijini Dar es Salaam"
Wako mtanzania,
Nicholas,Netherlands
Asante kwa ujumbe lakini kiswahili chako, mmmmh! wewe pamoja na anon wa Thu Jul 22, 09:30:00 AM kutoka TANDIKA, Nini maana ya ONGERA? SEma HONGERA, jifunze kutumia H badala ya i, unapotosha kiswahili kama huwezi acha Mnaudhi.
ReplyDeleteWe embasado wa ICT hapo mwisho umeandika ......ni vizuri tukachukua hatua za haraka sasa ivi na kuweza.... NINI maana ya sasa IVI, HUoni aibu na kiswahili chako?
Sijuwi tatizo ni nini,
Brother Kamau akiponda Mnamuona eti bishoo anatuonea.
Mdau.
MwanaFA na AY wamekuambieni msije mjini lakini nyinyi bado mwaja tu...
ReplyDeleteSafisheni kwanza City Center yale magari yanayopaki pembeni mwa barabara ndiyo mwanzo ya msongamano wote...
Wera weraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!
ReplyDeleteWizi mtupu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!