Angalizo: Soma ukiwa kwenye Foleni ndefu ya Magari,
na shiriki kwenye utatuzi wa tatizo hili.

Hoja ya Msongamano Mkubwa wa Magari
(Traffic Jam) jijini Dar-es-salaam


Swala la Vituo vya daladala, Hapa naomba niwalaumu sana sana madesign na maengeer wa barabara zetu, kweli hamkututendea haki, vituo vya daladala ni vidogo sana kiasi ambacho madereva wote wa daladala husimama katikati ya barabara wakishusha na kupakia abiria, badala ya kuwalaumu madreva wa daladala nadhani tungeanza na swala la kurekebisha vituo vyetu.

Mimi nakijua kituo cha Mapipa na Ubungo walau ndivyo unavyoweza kusema ni vituo vya daladala, labda tungefikiria kuvipunguza viwe vichache lakini viwe vikubwa, Kituo cha daladala kiwezeshe gari kuingia kabisa ndani na kushusha na kupakia abiria bila kusababisha karaha kwa wengine, wenzangu tunaopita barabara ya Sinza uzuri hata hivyo vituo vyenyewe havipo, inakulazimu umsubiri dreva wa daladala mpaka atakapo amua kuondoka ndipo na wewe upite, hii ni kero tena kubwa sana.

Traffic wa Buguruni na Tazara wanajitahidi sana kuvuta magari lakini standi ya Buguruni Chama daladala zote ziko barabarani, walau Mwenge kituo cha kwenda Tegeta baada ya mataa traffic wameamua kukiua, sio siri inakera sana sana, Wenzangu wa Mbezi ya Kimara stand ni ndogo sana sana, magari hayawezi kuingia na kushusha abiria na kuondoka, hivyo husimama barabarani na kusababisha msongamano isiyo na msingi, Nashauri kabla ya Fly over tupanue vituo vyote vya daladala halafu sheria ya usalama barabarani iwe makini na adhabu kali itolewe kwa atakaye shusha au kupakia abiria katikati ya barabara.

Kuna kero nyingine ya msongamano ambayo inachangiwa na mikusanyiko ya watu isiyo ya Lazima, me naomba nizungumzie Soko la Jioni Ubungo stand ya Daladala, Je waliotengeneza plan ya hiyo stand walisema kutakuwa na soko pembeni?

Ubungo stand ya daladala ni kero hususani wakati wa jioni, wenye magari hupaki barabarani na kufanya shopping ya Nyanya na Vitunguu, ili hali traffic anayeongoza magari anashindwa kuyavuta kutokea mjini, hali kadhalika Daladala husimama katikati ya barabara kama kawaida, sasa ivi ubungo jioni kumejaa vibaka wanakwapua watu simu, wakina mama pochi na site mirror kwa magari yanayokwenda nje ya nchi ( Hususani Harier na Lexus).

Nimeshuhudia mwenyewe mara tatu sehemu ya Darajani vibaka waking’oa site mirror ya gari mpya zilizokuwa zinaendeshwa kwenda nchi za jirani, hivi hao wageni wanapata picha gani kwa nchi yetu? Lakini hali hii tunaikaribisha wenyewe kwa kuruhusu soko lisilo halali Ubungo linalokusanya watu wengi wasio na lazima.

ICT Ambassador De Africa,
Sesil C. Latemba
sesil7c@yahoo.com
+255 713 335480
.....itaendelea kesho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2010

    ANGALAU LEO UMEONGEA KITU CHA KUELEWEKA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2010

    MAONI YA MATUMIZI YA LUGHA: Aidha andika kwa kiswahili fasaha, au weka maneno ya kiingereza ambayo huna hakika na tafsiri yake kwa kutumia "inverted commas". Kwa mfano, neno "Site mirror" ulilotumia si sahihi. Kwa kiingereza fasaha ni "Side mirror".

    Mdau,
    Afrika ya Kusini

    ReplyDelete
  3. Mdau "Afrika ya Kusini" Cha muhimu hapa ni ujumbe. inategemea mtu amekulia wapi na kasome wapi. Huu si wakati wa kufundishana kiswaili au kiingereza. Mada kuu hapa ni Msongamano mkubwa wa Magari jiji la Dar es Salaam. Hii hdiyo naomba wadu tuchangie.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2010

    Haya maneno yanakosewa sana na watu hata wale tunaodhani wanaelewa.

    Site mirror badala ya Side Mirror.

    na

    Nitaku-deep badala ya Nitaku-beep, halafu hii imekaa kama tusi vile ;-)

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2010

    Nimependezwa sana na Mawazo ya Mtoa hoja hapo juu, Suala la spelling Mistake aliyotoa Mdau wa Africa ya kusini naona ameishiwa Point kwani amefuata vitu Vidogo ambavyo havina manufaa makubwa kwa Tatizo lililopo!
    Mimi naongezea Ushauri ufuatao,
    . Katika barabara yoyote kuna kitu kinaitwa full time design Capacity je Tanroad wanafanya utafiti kugundua capacity ya barabara Zetu? Kwa upande wangu Naona Capacity ya Junctions Nyingi ni Below 40%, Nivigumu kuamini ila ndio Hali Halisi kwa hiyo cha kuzingatia ni kufanya utafity kugundua Chanzo cha hilo tatizo na kupata mtu wa kulisimamia na kurudisha capacity ya barabara zetu (Intersections)
    .Kwa observation yangu nimegundua Tatizo Biashara Nyingi bila mpangilio barabarani,
    .Watu kuwa na uzembe na kutokuheshimu muda, Say design speed ya intersection ambako kwa asilimia kubwa watu huenda taratibu sana!
    .Mashimo katikati ya makutano, Kama ilivyo ubungo,

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2010

    Hilo la mashimo kwenye makutano ya barabara, ambalo umegusia mdau hapo juu nalo linachangia sana foleni kiukweli. Mfano mzuri ni makutano ya barabara ya Kilwa na Mandela (Uhasibu- TIA), yaani ni panakera hadi basi. Hizi barabara nadhani ziko chini ya Tanroads (niko radhi kusahihishwa), sijui hawazioni, ama fungu lilishatafunwa ama si kipaumbele kwao maana wazee wa Ma STK, SU, DFP n.k sio maeneo yao huko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...