Naelewa watanzania wote kwa ujumla (Tanganyika & Zanzibar) wameshaingia kwenye mchakato wa kinyanganyiro cha uongozi wa nafasi mbali mbali za siasa kuna jambo moja nadhani tumelifumbia macho na
hatuoni wala hatulizungumzii ningependa kuliweka wazi labda ni wazo
langu au ni la wengi lakini halijazungumziwa kwa undani.
Rais wa Jamhuri ya muungano amevunja Bunge letu tukufu, kwa kitendo
hicho alichopewa na kwa mamlaka yake kikatiba tunapata maana moja
kubwa.
hatuoni wala hatulizungumzii ningependa kuliweka wazi labda ni wazo
langu au ni la wengi lakini halijazungumziwa kwa undani.
Rais wa Jamhuri ya muungano amevunja Bunge letu tukufu, kwa kitendo
hicho alichopewa na kwa mamlaka yake kikatiba tunapata maana moja
kubwa.
1)Tanzania kwa ujumla haina wabunge, walikuwapo ukomo wao umetimia kwa
bunge kuvunjwa na mheshimiwa Rais J Kikwete ijumaa iliyopita.
2)katiba inasema ili kiongozi awe waziri ni lazima awe mbunge.
kwa kifupi tu na kwa maelezo ya hapo juu na kwa tafsiri nyepesi ni
kuwa baraza la mawaziri limevunjika pale Rais anapovunja Bunge.
Serikali kwa uwelewa wangu sasa hivi inaongozwa na makatibu wakuu
wakiwa ndio watendaji wakuu kwenye muundo wa serikali.
makatibu ndio utawala mkuu na wa mwisho kwenye utumishi wa umma.
hapo ndipo utata unapokuja kwenye kichwa changu nikiomba watanzania
wenzangu labda wanisaidie kutafsiri.
kama serikali kwa sasa inaendeshwa na makatibu wakuu,
kwanini
1.)mawaziri wa baraza lilivunjika kwa mujibu wa katiba wanaendelea
kutumia mali za wizara (umma) mfano magari na nyumba za serikali? je
katiba inawaruhusu kufuja mali hizi wakati wao sio mawaziri tena
(baada ya bunge kunvunjwa)
2.) kwanini wanalipwa mishahara na marupurupu kinyume na katiba wakati
ikijulikana wazi kuwa ukomo wao umefika pale Rais alipovunja bunge. je
huu sio uhujumu uchumi na kujilimbikizia mali kwa njia isiyo ya halali
(uhalalishwaji wake ni pale kuwa alikuwa waziri kabla ya bunge
kuvunjwa)
3.) Ikizingatiwa kuwa anapata yote hayo na kutumia mali ya serikali
kinyume na sheria je anakuwa havunji kanuni za uchaguzi kuwa anatumia
mali za serikali kwa sasa kufanyia kampeni za kisiasa hapa napata
utata ningeomba tafsiri sahihi.na mwisho mwanasiasa wa namna hiyo kwa
utashi wangu anakuwa na upendeleo (advantage) kuliko wagombea ubunge
wa jimbo alilokuwa analiwakisha je hii ni sahihi? na je sheria
inatafsiri nini hapa.
kwa hayo machache nadhani ni wabunge wachache ama wote waliokuwa
mawaziri watakuwa na upendeleo na makosa ya kuvunja sheria ili
kujihakikishia kurudi kwenye ubunge. je hii hi sahihi na je huu sio
upotezaji wa fedha za umma kwa hawa wachache.? mwisho kabisa nadhani
muheshimiwa Rais anapolivunja bunge huwa anawashukuru kwa kumsaidia
kuliendeleza taifa na kuwapa mafao yao kama sheria inavyosema. je
akiwashtaki watakuwa wanaonewa?
Asante kaka michuzi.
from
Boss
-----------------
Angalizo: Globu ya Jamii imefuatilia hoja hii kwa Mwanasheria Mkuu na jibu liko njiani laja wakati wowotw kuanzia sasa. Tufanye subira wadau
-Michuzi
MICHUZI HUNA SABABU YA KUTUAMBIA TUFANYE SUBIRA KWA VILE MWANASHERIA MKUU ATAKUJA NA JIBU KWANI KUNA HOJA YA KUCHANGIA HAPA REGARLESS MAJIBU YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YATAKAVYOKUJA. WENYE UELEWA NA LOGIC WATUPE MCHANGAO WAO HATUNA SABABU YA KUSUBIRI JIBU KUTOKA KWA MWANASHERIA MKUU HATA MAJIBU YAKE PIA YATAJADILIWA KUTOKANA NA UELEWA TOFAUTI WA WATU NA HUO NDIO UTAWALA BORA WA WAZI NA HAKI SAWA NA DEMOKRASIA NCHI NI YETU SOTE NA LAZIMA TUCHANGIE MAWAZO KWA FAIDA YETU SOTE. KIMSINGI KUNA HOJA NZITO YA KUCHANGIA KIUFUNDI. MIMI KWA MTAZAMO WANGU MDOGO HAWASITAHILI KUFANYA HIVYO. WALITAKIWA WAONDOKE KWENYE MADARAKA NA HATA KWENYE NYUMBA ZA SERIKALI UNLESS KATIBA SHERIA MAMA YA NCHI INASEMA VINGINEVYO JUU YA HILI.
ReplyDeleteMIMI KAMA MSOMI WA MUZMBE WA CHUO KIKUU CHA KULE MOLOGOLO AMBAYE NIMEBOBEA KATIKA MASWALA YA UATWALA KUTOMA MASTERS YA CANADA NA MBA YA WOLSTRTI NA KEMPINSIKI YA KILIMANJALO HOTEL I SAY ASK THAT THIS IS CORRUPT OF GOVENRMENT OF TANZANIA. I AM NOT IS PRESIDENT OF ALL DHE PEOPLE, BUT I WAS IN MUZUMBE AND HE WAS GETING IN DGREE OF ECONOMY AND WANTS ALL TANZANIA TO BE DEVELOPMENT. DONT LET MINISTER TO LEAVE MASAKI AND CAMPAINGS CCM TO BE PRESIDENT AGAIN. SO RIZIWANI, DR. JOHN MASHAKA AND PROF SHAYO WAS THE PREDISENT OF 2015 OF TANZANIA, WE HAS TO ZIMBABWE AND BECOMES KOMREDI MUGABE OR TO SOMALIA AND MUJAHEEDEN TO LEAVE TANZNAIA OF CORRUPTY. WE LOVED THE PATRIO ADN THE COUNTRY LIKE NYERERE AND THIS IS NOT GOOD, FOR THE MINISTER TO BECOME MORE POWER IN GOVERNMENT AND LEAVE THE OFFICE, SO I GO TO NBA OF MEMPHIS WITH HIS HIGHNESS HASHEEM THABEET AND WOLSTRIT OF AMELIKA OF NABII YOHANA MASHAKA AND BECOMES THE PRESIDENT OF TANZNAIA WITH RIZINWANI AT STATE HOUSI OF IKULU YA KIVUKONI.I SEE WE BECOME LOST IN THE SEA IF WE LEAVE PARLIAMENT OF DODOMA AND BECOMES POWERFUL AND MZEE WA VIJISENTI AND ROSTAM AZIZIZMA AND MZEE LOWASSANA OF MONDULI SHINYANGA SO I SAY THIS IS CORRUPTY TOO MUCH OF TANZANIA
ReplyDeletePETER NALITOLELA
US Blogger)
ReplyDeleteWatu wenye hela kama mimi waingekumbwa na matatizo kama haya, wala wananchi wasingepoteza hela zao za kodi kuwaudumuia
Hawa mawaziri ni wezi wa kutupwa. Mimi naweka tayari jopo la mawakili kuwafungulia mashtaka hawa wezi bwana. Lazima washtakiwe, kwa nini waweke magari ya umma majumbani mwao? Hawa ni wezi
Kikwete angenipa kazi, wala asingekuwa na wasiwasi wa kuibiwa. Mimi nina hela za kutosha, mshahara wangu ni Trillioni 7 kwa mwaka, sasa nitawaibia nini watanzaia?
Mzee kikwete, US Blogger for Economic Minister 2010. Mimi msomi, hela ninazo na heshima nitailetea Tanzania kwenye anga za kimataifa. Hachana na hao wakina wezi wanaodandia hela za walipa kodi
Dr. US Blogger
Economics Department
Oxford Univesrsity
acha uchungu, uhuru tulishapata
ReplyDeleteKwanza nipende kumshukuru sana Bwana Boss kwa hoja yake ya msingi mno. Hii ni moja tu ya mambo ambayo yanaoyesha wazi kabisa kuwa katiba yetu inahitaji kubadishwa kabisa na sio kurekebishwa. Ukiangalia kwa karibu zaidi utaonakuwa hata mawaziri wako kisiasa mno kuliko kiutendeaji ndio maana hata maendeleo yanazidi kuzorota siku hadi siku. Kwa mtazamo wangu kungekuwa hakuna haja ya kuwa na waziri kabisa badala yake tutawa na makatibu wa wizira tu.Ambao wanateuliwa na rais na kwenda kuijieleza uwezo wao wanafasi walizochanguliwa mbele ya bunge kabla ya wabunge kuwapitisha kwa kupiga kura au kutowapitisha.
ReplyDeleteHapa bwana michuzi wala huhitaji kwenda kwa mwanasheria juu ya hoja ya Boss. Inajieleza vya kutosha. Waliokuwa mawaziri sio mawaziri tena pale bunge lilipo vunjwa. Na kama wanaendelea kutumia mali za serikali na kama mawaziri hio ni kinyume cha sheria. Utaona tatizo la kuwa na bunge bubu. Issue kama hii ilitakiwa iwe imeshatolewa macho na wabunge miaka mingi sana iliyopita lakini kwasababu tunawabunge wanaokwenda bungeni kwasababu tu ya majina yao au kwasababu tu rais ameonelea ni vema kuwa wawe wabunge ndio maana unakuta mambo kama haya hayajawahi kuzungumziwa bunge hata siku moja.
Issue nyingine yakuogopesha ni hawa wabunge wanaongia bunge kwa gia ya viti maalumu. Jamani hawa watu wanawawakilisha sehemu fulani ya jamii inakuwaje ambaye ni mbunge wa sehemu hio asishughulike na na maswala yote ya wananchi wa jimbo lake ili kusiwepo hawa wanaojiita wabunge wa viti maalumu? Kwa mfano eti kuna mbunge wa Vijana je hawavijana wanakaa kwenye majimbo tofauti na ya wabunge wengine? Tunajua serikali inagharamika kiasi gani kwa kila seat moja ya mbunge wakuteuliwa au mbunge wa viti maalumu? Hebu watanzania tujaribu kujiuliza maswali kama haya jamani.
Kuna mambo mengi sana yakutisha juu ya system nzima ya nchi yetu amabayo yakiongelewa kwa makini na kufanyiwa kazi bila kujali ubinafsi itasaidia sana kuendeleza nchi yetu badala ya kukaa na kuwaendeleza hawa wachache.
Swala jingi ni hii tabia tuliojiwekea ya kuliita bunge la tanzania "BUNGE TUKUFU" Jamani hvi tunajua maana ya neno TUKUFU? au UTUKUFU? Sijui kama ni katiba inayosema kuwa bunge liitwe bunge tukufu au ni mambo tu ya mazoea. lakini vyovyote vile bunge haliwezi kuwa tukufu. Utufuku ni mambo yanayohusu imani zaidi kuliko siasa. Kwahio kwa msingi sio sahihi kuliita bunge tukufu. Kama ambavyo mzee ruksa alianzisha kuwa yeye aitwe mtukufu rais. Hii nayo haikuwa sahihi kabisa. Tunashukuru waliofuatia baada yake walilikomesha hili kimya kimya.
Bunge limetumia neno hili TUKUFU kujikinga na maovu mengine yote wanayofanya wabunge kufikia mahali wanajiona kuwa wako juu ya sheria na sheria nyingine wao haziwahusu. Mtu ukimhoji mbunge unatishiwa kuwa umelikosea bunge. Imefikia mahali eti wanabunge hawaruhusiwi kuchunguzwa kwenye kesi za rushwa na takukuru. Wana hoji kama ni sawa kwa wao kuhojiwa na takukuru. Jamani kwani wabunge wao sio rai wa kawaida ambao wanatakiwa kufuata sheria zote za nchi hii?
Bwana Michuzi yako mambo mengi sana yanatakiwa kufanyiwa kazi tungeomba wewe kama mwandishi wa habari wa serikali uhakikishe hoja nzito kama hizi haziishii tu kwenye blog ya jamii isipokuwa zinafika kwenye magazeti katika kurasa za mbele hasa kipindi nyeti kama hiki cha kuelekea uchaguzi. wagombea wanaweza kuuliza maswali kama haya.
Naomba nimsaidie mdau kidogo:
ReplyDelete- Kuvunja Bunge siyo sawa na kuvunja baraza la mawaziri kwani Bunge linakosa rasmi tarehe 20 Augusti. Hivyo kama kuna jambo linatokea sasa hivi kuitaji Bunge, Rais anaweza kuita Bunge la wabunge wote waliokuwepo wakati huu. Hivyo, siyo sahihi kufikiria kuwa kwa vile Bunge limevunjwa basi mawaziri hawapo, la hasha. Mawaziri wote wanapoteza nafasi zao wanapopoteza Ubunge ambao hadi hivi sasa bado wanao hadi Augusti 20. Kwa hiyo hoja zozote za matumizi ya ofisi za Uwaziri zinatakiwa zije baada ya siku hiyo.
-Mawaziri bado ni mawaziri kwani bado ni wabunge hadi tarehe 20 Augusti ambapo kampeni mpya inapoanza na wao ndiyo wanapoteza uwaziri na Ubunge wao.
- Hata Wabunge wakipoteza nafasi zao itakapofika August 20 na kuna jambo la kitaifa limetokea kati ya wakati huo na Uchaguzi Mkuu Rais anaweza kumteua mtu yeyote kati ya hao kuwa Waziri.
-
Michuzi nasikia Rais mtarajiwa Dr waukweli amepokelewa vizuri sana huko kwao,mbona habari hii haujatupatia au blog ya jamii haina wawakilishi huko AR,
ReplyDeleteHoja ya maana sana.
ReplyDeleteAsante mdau kwa kuleta hii hoja.
Ankal asante kwa kupeleka hii hoja kwa Mwanasheria Mkuu.
(US Blogger)
Haya ni matatizo ya katiba kutungwa na "Special interest" The leadership elites. Wanaangalia masilahi yao tu mpaka wana sahau mambo muhimu. Katiba inampa rais uwezo wa kuvunja bunge na bunge linapewa uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani kwa rais.
ReplyDeleteGap hapa ni kwamba, kama mna rais kichaa anaweza subiri kipindi hiki ambacho bunge halipo kufanya mambo ya ajabu kabisa bila kuwa na hofu ya kuwajibishwa.
Kama waziri ni lazima awe mbunge ni dhahiri kuwa mawaziri hakuna kikatiba na kwa maana hiyo hatuna baraza la mawaziri kwa sasa, gap jingine hili
Nchi nyingi sana hakuna suala la kuvunja bunge, kinachofanyika ni kwamba ubunge wa mbunge aliyepo madarakani unaisha tu baada ya uchaguzi kufanyika, mshindi kupatikana na mshindi huyo kuapishwa bungeni.
Tanzania hatuna katiba tuna sheria za kulinda masilahi ya watawala tu.
tunajua jibu linakuja na tunalilijua tayari. Katika nchi isiyo heshimu katiba tutambiwa wana haki zote mpaka serikali mpya itakapoundwa
ReplyDeleteBWANA ANKAL, SWALI LA MSINGI LIMEULIZWA NA WADAU WACHANGIE HOJA. SWALI LANGU AU HOJA YANGU KWA WADAU, JE RAIS NAE ANA MAMLAKA GANI YA KUENDELEA KUKAA IKULU, IKIWA UCHAGUZI BADO HAUJAFANYIKA?. JAMANI EHEEE, RAIS KAVUNJA BUNGE TU HAJAVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI, WENZETU HUWA WANASEMA TUPO KWENYE TRANSITION PERIOD-KIPINDI CHA MPITO. TUSIANGALIE TU MAWAZIRI, THE ALL SYSTEM. WADAU MPOOOO.
ReplyDeleteSHUKRAN, ANKLA!!!!
ndugu zangu naomba tuwe tunatumia kiswashili katika kutoa maoni yetu.. au kama tunatumia kugha tofauti mfano kiingereza basi kiwefasaha.. mfano. I AM NOT IS PRESIDENT OF ALL DHE PEOPLE,....SO RIZIWANI, DR. JOHN MASHAKA AND PROF SHAYO WAS THE PREDISENT OF 2015 OF TANZANIA, WE HAS TO ZIMBABWE AND BECOMES KOMREDI MUGABE OR TO SOMALIA AND MUJAHEEDEN TO LEAVE TANZNAIA OF CORRUPTY. yaani hakieleweki kitu gani kinazungumziwa..tujivunie kujua kiswahili na hata kiingereza kama tunakijua basi tukiandike fasaha.. huu ni mtazamo wangu tu...
ReplyDelete