Marehemu Hajra Kassu Aloo

Familia ya Kikeke na Kassu Aloo , inatoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani kwa misaada yao ya kiroho, hali na mali wakati wa kumuuguza, kifo na hatimaye mazishi ya mpendwa Mama yetu, HAJRA KASSU ALOO ambaye alifariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tarehe 24.06.2010 sawa na mwezi 11 Rajabu na kuzikwa tarehe 27.06.2010 sawa na mwezi 14 Rajabu Kenya makaburi ya Pasua, Moshi.

Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa Madaktari wa Emergency MNH Dk Alwyn Mziray, Dk Faith Ringo, Dk Henry Joseph na Dk Mpoki wa ICU MNH na wauguzi wa Hospitali ya Muhimbili ICU na Madaktari wa Regency ,KCMC, Mtakatifu Joseph ya Moshi, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) na watumishi wote wa Mfuko , Uongozi na wafanyakazi wote wa BBC idhaa ya Kiswahili, J Ray McDermott, Jumuiya ya Watanzania waishio Houston Texas na Kikundi cha akina mama cha Tumaini Jema cha Matete Kimara Bucha.

Kwa kuwa sio rahisi kumshukuru kila mmoja peke yake, tunaomba mzipokee shukrani zetu kwa namna ya pekee na Mwenyezi Mungu awajaalie kila la kheri kwa upendo wenu.

Khityma (AROBAINI) itafanyika nyumbani kwa marehemu Hajra Kassu siku ya Jumamosi tarehe 31.07. 2010 (Mwezi 19 Shabani) Uwanja wa sabasaba, Moshi mjini kuanzia saa 4 asubuhi.
Karibuni sana.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati
Wana Familia ya Kikeke na Kassu Aloo

INNA LILAH WA INNA ILLAHI RAJIUUN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...